Timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Nje Sports) leo terehe 22 Aprili 2023, imeingia dimbani kucheza dhidi ya mpinzani wake timu ya Wizara ya Mambo ya Ndani, kwenye mchezo uliochezwa katika uwanja wa Sekondari ya Morogoro kuanzia majira ya saa 3.00 asubuhi.
Katika mchezo huo Nje Sports imepoteza kwa goli 1-0, lililofungwa katika dakika ya 37 ya kipindi cha pili (katika mashindano haya ya Mei Mosi mpira wa miguu unachezwa kwa dakika 60 badala 90 kama ilivyozoeleka) na kudumu hadi mwisho wa mchezo.
Hata hivyo licha ya kupoteza mchezo huo mbele ya Maafande, Nje Sports inasongo mbele kucheza hatua ya timu 16 bora ambazo zimefuzu katika hatua ya makundi baada ya kujikusanyia alama 7 katika kundi C, na kuwa miongozi mwa timu nne zilizofuzu katika kundi hilo.
Kundi C lilijumuisha timu sita ambazo ni Wizara ya Ulinzi ambayo imejikusanyia alama 12 (kinala wa kundi), Wizara ya Fedha na Mipango –Hazina FC alama 10 (nafasi ya pili), Wizara ya Mambo ya Ndani alama 9 (nafasi ya tatu) Nje Sports alama 9 (nafasi ya nne) 21st Century alama 5 (nafasi ya 5) Ushirika alama 0 (nafasi ya 6)
Akizungumza muda mfupi baada ya mchezo huo Mwalimu wa Nje Sports Bw. Shaaban ameushukuru Uongozi wa Wizara kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa kikosi chake, ambao umewezesha kufunzu hatua ya 16 bora. Vilevile ametoa pongezi kwa wachezaji na uongozi wa timu kwa kufuzu hatua inayofuata katika mashindano hayo ya kuelekea Kilele cha Maadhimisho Mei Mosi yanaoyondelea mjini Morogoro.
Nje Sports inatarajiwa kushuka tena dimbani kucheza dhidi ya Mamlaka ya Pato Tanzania (TRA) siku ya Jumapili tarehe 23 Aprili 2023 saa 10.00 jioni.
Mechi ikiendelea |
Penati ikipigwa kuelekea lango Nje Sports. Penati hiyo haikufanikiwa kutengeneza goli baada ya kudakwa na kipa mahiri wa Nje FC. |
Mlinzi mahiri wa Nje Sports Bw. Abbas Abdallah shuti lililoelekezwa langoni kwake. |
Mchezaji wa Nje FC akiwatoka walinzi wa timu ya Wizara ya Mambo ya Ndani kwenye mechi iliyochezwa katika uwanja wa Morogoro Sekondari. |
Baadhi ya wachezaji wa Nje Sports wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mchezo wao dhidi ya Wizara ya Mambo ya Ndani |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.