Monday, April 27, 2015

Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC waanza jijini Harare

Waziri wa Mambo ya Nje wa Zimbabwe, Mhe, Simbarashe Mumbengegwi akifungua Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unaojadili Mkakati na Mwongozo wa kuelekea Maendeleo ya Viwanda katika Kanda ya SADC. Mhe. Mumbengegwi amefungua mkutano huo jijini Harare, Zimbabwe  huku akiwa na huzuni kubwa kufuatia taarifa ya kifo cha Bregedia Jenereli Hashim Mbita ambaye alitoa mchango mkubwa katika ukombozi  wa nchi za Kusini mwa Afrika. Mhe. Mumbengegwi aliwaomba wajumbe wote wa mkutano kusimama ili kumuombea dua Bregedia Hashim Mbita.



Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Abdallah Kigoda (Mb) wa katikati akiomba dua kumkumbuka Brigedia Hashim Mbita. Kulia kwa Mhe, Kigoda ni Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Nchemba (Mb) na kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb) nao pia wakimuombea dua Brigedia Mbita.

Meza kuu nayo ikimtakia kheri Brigedia Hashim Mbita.

Katibu Mtendaji wa SADC, Bi. Stergomena Tax akitoa hotuba kwa Baraza la Mawaziri wa SADC.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Zimbabwe, Mhe. Simbarashe Mumbengegwi akitoa hotuba ya ufunguzi ya Mkutano wa Baraza la Mawziri wa SADC.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Zimbabwe akiangalia hotuba aliyekabidhiwa na Katibu Mtendaji wa SADC, Bi. Tax mara baada ya kuwasilishwa na Katibu Mtendaji huyo mbele ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC

Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Nchemba (Mb); Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda (Mb); Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb) wakiwa na Mawaziri wa nchi nyingine katika Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC.


Picha ya pamoja ya Baraza la Mawaziri wa SADC.




Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda (katikati), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (kulia) na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Nchemba wakiwa katika kikao cha maandalizi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC jijini Harare, Zimbabwe. 

Mhe. Kigoda akiendesha kikao hicho cha maandalizi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Bw. Musa Uledi wa kwanza kushoto akitoa maelezo kwa Waheshimiwa Mawaziri juu ya agenda zitakazojadiliwa katika Mkutano wa Mawaziri wa SADC.

Makatibu Wakuu wakiwa katika kikao cha maandalizi. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha.

Wataalamu mbalimbali wakiwa katika kikao cha maandalizi.

Na. Mwandishi wa Wizara ya Mambo ya Nje.

Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wameanza kikao cha siku mbili jijini Harare, Zimbabwe leo kufanya matayarisho ya Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya hiyo, utakaofanyika hapo tarehe 29 Aprili, 2015.

Kikao cha Mawaziri, kinachoongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Zimbabwe, Mhe. Dkt. Simbarashe Mumbengegwi, kinatayarisha agenda ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi, ambao utajikita kwenye Mpango Mkakati wa Maendeleo ya Viwanda wa nchi za SADC. Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal, anatarajiwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kwenye mkutano huo, utakaofanyika chini ya Mwenyekiti wa SADC, Rais Robert Mugabe.



Katika kikao cha Mawaziri, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe, anawakilishwa na Naibu wake, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim, ambaye aliwasili Harare jana. Washiriki wengine ni Waziri wa  Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda, Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Nchemba, Naibu waziri wa Uchukuzi, Mhe. Dkt. Charles Tizeba na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Gerson Lwenge.



Mbali na mkakati wa maendeleo ya viwanda na mpango wa utekelezaji wake, Mawaziri watajadili Mpango wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Miundombinu na uanzishwaji wa Soko Huria la Utatu baina ya nchi za SADC, EAC na COMESA.

Kikao cha Mawaziri kilitanguliwa na Kikao cha Maafisa Waandamizi, kilichosimamiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajab Gamaha na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Bw. Musa Uledi.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

 

Simu: 255-22-2114615, 211906-12
Barua pepe: nje@nje.go.tz
Barua pepe: gcu@nje.go.tz

Nukushi: 255-22-2116600

              

 



           20 KIVUKONI FRONT,
   P.O. BOX 9000,
       11466 DAR ES SALAAM, 
                                    Tanzania.

 


Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemteua Balozi Rajabu Hassan Gamaha kuwa Balozi wa Tanzania nchini Burundi.

Balozi Gamaha anachukua nafasi ya Balozi Dkt. Mwasi Nzagi ambaye amestaafu kwa mujibu wa sheria.

Kabla ya uteuzi huo Balozi Gamaha alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Uteuzi huo unaanza mara moja.

-Mwisho-
Imetolewa na:
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam
27 Aprili 2015

PRESS RELEASE

H.E. Ram Baran Yadav, President of Nepal

PRESS RELEASE

H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a condolence message to H.E. Ram Baran Yadav, President of the Democratic Republic of Nepal following a tragic earthquake that rocked Nepal on Saturday 25 April 2015.

The message reads as follows:

“H.E. Ram Baran Yadav,
President of the Federal Democratic Republic of Nepal,
KATHMANDU

I have learnt with profound shock and deep sorrow the sad news of a 7.8 magnitude earthquake that hit Nepal on Saturday, 25 April 2015 claiming at least 1,800 lives and devastating buildings and centuries old temples.

The tragedy is not only for the loved ones of those who perished but also for all the Nepali people and their friends. As a country therefore, our thought and prayers are with the people of Nepal in this time of grief.

On behalf of the Government and the People of the United Republic of Tanzania and on my own behalf, I offer deep condolences to the victims of the powerful earthquake and also sincere sympathies to the injured and families of the victims.

Please accept, Your Excellency, the assurances of my highest consideration”.

ISSUED BY: THE MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS AND INTERNATIONAL COOPERATION, DAR ES SALAAM

27TH APRIL, 2015



Saturday, April 25, 2015

Waziri Membe apokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka Mabalozi Wateule wa Urusi na Algeria

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb), akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Urusi nchini Tanzania, Mhe. Yuri Fedorovich Popov.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb). akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Urusi mara baada ya kupokea Nakala za Hati za Utambulisho. Katika mazungumzo hayo pamoja na mambo mengine, Mhe. Waziri aliishukuru Serikali ya Urusi kwa misaada inayotoa kwa Tanzania katika sekta mbalimbali kama vile elimu. Wawili hao pia waliafikiana  umuhimu wa kukuza na kuimarisha zaidi ushirikiano kati ya Tanzania na Urusi.
Mazungumzo yanaendelea.
Waziri Membe akiagana na Balozi Mteule wa Urusi nchini Tanzania.
Waziri Membe katikati akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mteule wa Urusi. Wakwanza kulia ni Balozi Joseph Sokoine, Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kutoka kushoto ni maafisa wa Ubalozi wa Urusi nchini Tanzania.

============================================

BALOZI MTEULE WA ALGERIA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb), akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Algeria nchini Tanzania, Mhe.Saad Belabed.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Algeria nchini Tanzania. Katika mazungumzo hayo, Mhe. Membe alieleza kuwa zaidi ya miaka 50 sasa Tanzania na Algeria zimekuwa katika uhusiano na ushirikiano mzuri wa nchi na nchi na hata katika ngazi ya Kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.
Mazungumzo yakiendelea
Mazungumzo yanaendelea huku Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (wa kwanza kushoto), Bi. Zuhura Bundala na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga wakinukuu mazungumzo hayo.
Waziri Membe akiagana na Balozi Mteule wa Algeria nchini Tanzania baada ya kupokea Nakala za Hati za Utambulisho.

Picha na Reginald Philip.


Waziri Membe akutana na Rais wa Comoro, ahudhuria hafla ya Muungano Moroni

Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania akiwa kwenye mazungumzo na Dkt. Ikililou Dhoinine, Rais wa Visiwa vya Komoro, alipomtembelea Ikulu nchini humo. Katikati ni Afisa Ubalozi Mwadini Jabir, Mkuu wa Utawala Ubalozi wa Tanzania Moroni, na pia alikua mkalimani wakati wa mazungumzo hayo.

Serikali za Tanzania na Komoro zimekubaliana kuimarisha sekta ya uchukuzi na miundombinu ili kurahisisha usafirishaji wa watu na bidhaa za biashara na chakula baina ya nchi hizo mbili.

Haya yamesemwa kwenye mazungumzo baina ya Mhe. Dkt. Ikililou Dhoinine, Rais wa Visiwa vya Komoro, na Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, ambapo Mhe. Membe alimpelekea salamu za Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwenye mazungumzo yao walisisitiza ushirikiano wa nchi hizi mbili hususan kwenye eneo la biashara na uchukuzi. Rais Dhoinine alielezea jinsi sekta ya usafiri wa anga ilivyoathirika kutokana na mgogoro nchini Yemen na kwamba ndege za shirika la ndege la nchi hiyo kwenda Comoro na nchi nyingine duniani zimesitishwa. Rais huyo aliongeza kuwa, tegemeo kubwa la wananchi wake hivi sasa ni Tanzania kupitia shirika lake la ndege ATC ambalo kwa sasa linafanya safari nchini humo mara tatu kwa wiki.

“Ni dhahiri wananchi wetu hutegemea sana usafiri wa anga kwa ajili ya kusafirisha bidhaa mbalimbali hata chakula, na hivyo shirika moja la ndege likiacha safari zake Comoro, tunaathirika sana” alisema Rais Dhoinine.

Kwa upande wa Tanzania, Mhe. Membe ambaye alifuatana na Mhe. Christopher Chiiza, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayehusika na masuala ya uwekezaji na uwezeshaji, alisema kuwa pindi shirika la ndege la Tanzania litakapoimarika, ndege zake zitakwenda Comoro kila siku ya wiki, kulinganisha na hali ilivyo sasa.

Aliongeza kuwa bidhaa za chakula na biashara ambazo zinaingia Comoro kutoka nchi za Pakistan, Ufaransa na Ukraine, kama vile mchele, sukari na simenti pia zinapatikana nchini Tanzania. Hivyo ni wakati muafaka sasa kwa nchi hizo kuainisha maeneo muhimu ya ushirikiano ili wananchi wake wanufaike.

Mwaka 2014, Serikali za Tanzania na Comoro zilisaini mkataba wa ushirikiano (General Cooperation Agreement) baina ya nchi na nchi, wakati wa ziara ya Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Comoro.

Kufuatia mazungumzo hayo, Mhe. Membe alimthibitishia Rais Dhoinine azma ya Serikali ya Tanzania ya kuanzisha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (Joint Permanent Commission) ambayo itaharakisha na kusimamia utekelezaji wa miradi yote ya uhusiano baina ya Tanzania na Comoro.

Baada ya mazungumzo hayo yaliyofanyikia kwenye Ikulu ya Rais jijini Moroni, Waziri Membe alihudhuria hafla ya siku ya taifa ya Tanzania, Muungano Day, iliyofanyikia nyumbani kwa Mhe. Chabaka Kilumanga, Balozi wa Tanzania nchini Comoro tarehe 23 Aprili 2015, kama sehemu ya Kongamano la Biashara baina ya Tanzania na Komoro.

Akihutubia jumuiya ya wanadiplomasia na wajumbe wa kongamano la biashara waliohudhuria hafla hiyo, Mhe. Membe aliweka msisitizo kwa sekta binafsi za nchi hizi kubuni mbinu za kuimarisha sekta za usafiri, utalii na uchukuzi ili kuneemeka na ushirikiano unaosimamiwa na Serikali za nchi hizo.

“Ni matumaini yangu kuwa uhusiano mzuri wa Serikali zetu utasaidia  na kukuza uhusiano wa biashara na sekta binafsi na hatimaye kuimarisha zaidi uhusiano wa watu wetu” alisema Waziri Membe.

Mhe. Membe alikua nchini Comoro kwa ziara ya siku moja ambapo alihudhuria Kongamano la Biashara na kutembelea fukwe za bahari za visiwa hivyo.

MWISHO.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
25 Aprili 2015



Ujumbe wa Mhe. Membe kwenye mazungumzo na  Mhe. Dkt. Ikililou Dhoinine, Rais wa Visiwa vya Komoro

Friday, April 24, 2015

Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Ushirikiano kati ya Asia na Afrika wamalizika nchini Indonesia

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uratibu na Mahusiano, Mhe. Dkt. Mary Nagu akihutubia Mkutano wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Ushirikiano kati ya Asia na Afrika uliofanyika mjini Jakarta, Indonesia tarehe 23 Aprili, 2015. Waziri Nagu aliongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo.
Mhe. Dkt. Nagu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Tanzania ulioshiriki mkutano wa  Wakuu wa Nchi wanachama wa Ushirikiano kati ya Asia na Afrika uliofanyika mjini Jakarta, Indonesia tarehe 23 Aprili, 2015. Kulia kwa Mhe. Dkt. Nagu ni Balozi wa Tanzania nchini Indonesia mwenye makazi yake nchini Malaysia, Mhe. Ponari Mlima, Kushoto kwa Dkt. Nagu ni Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki. Kulia ni Afisa wa Ubalozi wa Tanzania Indonesia mwenye makazi nchini Malaysia na kushoto ni Afisa Mambo ya Nje, Bw. Khatibu Makenga.
Mhe. Dkt. Nagu akiwa na viongozi wengine kutoka frika na Asia akishiriki matembezi ya kuadhimisha miaka 60 ya ushirikiano wa Asia  na Afrika
Matembezi yakiendelea.
==================================
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Asia na Afrika umemalizika leo hapa jijini Jakarta, Indonesia kwa kushuhudia kupitishwa  maazimio muhimu matatu ambayo ni kudumisha ushirikiano miongoni kwa nchi wanachama katika masuala ya ustawi wa amani, kuimarisha Mkakati Mpya wa Ubia kati ya Asia na Afrika na Azimio la Palestina.

Mkutano huo pia uliadhimisha miaka 60 ya Ushirikiano baina ya nchi za Asia na Afrika pamoja na miaka 10 ya Mkakati Mpya wa Ubia wa Pamoja kati ya nchi za Asia na Afrika (commemoration of the 60th Anniversary of the Asian-African Conference and the 10th Anniversary of the New Asia-Africa Strategic Partnership).

Lengo la maazimio hayo ni kuongeza ushirikiano zaidi kwa kuzileta pamoja nchi wanachama katika kushughulika changamoto wanazokabiliwa nazo kama vile ukosefu wa amani, ubaguzi wa rangi, matabaka katika jamii, ukosefu wa chakula, ukosefu wa ajira, biashara haramu ya kusafirisha binadamu, ugaidi, biashara isiyo na usawa, uharamia, ujangili pamoja na mengineyo.

Katika hotuba fupi zilizotolewa na nchi wanachama, nyingi zimeunga mkono suala la taifa la Palestina kupata uhuru wake, kuendelea kushinikiza mageuzi katika Umoja wa Mataifa hususan katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kuweka mazingira mazuri ya kuwezesha ushirikiano wa kiuchumi baina ya Afrika na Asia kwa kuimarisha miundombinu  kama vile viwanja vya ndege, njia za mawasiliano, uzalishaji wa nishati ya kutosha, ujenzi wa reli na barabara pamoja kuweka masharti rahisi katika kufanya biashara.

Masuala mengine ni kuachana na utegemezi wa Mashirika ya fedha ya kimataifa ambayo hayana mifumo yenye usawa, kuzuia uhalifu wa aina mbalimbali, kuongeza ajira na elimu kwa vijana na mengineyo.

Aidha, kwa msukumo sawa na ule unaofanywa na nchi wanachama katika kuisemea Palestina ipate uhuru wake, nchi hizo pia zimeombwa ziweke nguvu sawa na hiyo katika kufanikisha upatikani wa uhuru wa nchi ya Sahara Magharibi.

Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka Asia na Afrika ambapo upande wa Asia alikuwepo Mwenyeji wa Mkutano Rais wa Indonesia, Mfalme wa Jordan, Rais wa China, Rais wa Vietnam, Rais wa Iran,  Rais wa Myanmar, Waziri Mkuu wa Japan, Waziri Mkuu wa Thailand, Waziri Mkuu wa Singapore, Waziri Mkuu wa Bangladesh, Waziri Mkuu wa Malaysia na wawakilishi wa viongozi wakuu kutoka mataifa mengine ya Asia katika ngazi ya Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri na Mabalozi. 

Kwa upande wa Afrika alikuwepo Rais wa Zimbabwe na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Mfalme wa Swaziland, Rais wa Madagascar, Rais Siera Leone, Makamu wa Rais wa Afrika ya Kusini na wawakilishi wa viongozi wakuu wa Nchi za Afrika katika ngazi ya Mawaziri na Mabalozi.  Tanzania iliwakilishwa na Mhe. Dkt. Mary Nagu (Mb), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Uratibu na Mahusiano.

Aidha, Wakuu wa Nchi na wawakilishi wa Bara la Asia na Afrika walipata fursa ya kuutembelea mji wa kihistoria wa Bandung ikiwa ni kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya Mkutano wa kwanza wa ushirikiano kati ya Asia na Afrika. Mkutano wa kwanza wa Wakuu wa Nchi wa Afrika na Asia ulifanyikia katika mji wa Bandung mwaka 1955 ambapo wakuu wa nchi na wawakilishi kutoka nchi 29 zikiwemo nchi saba kutoka Afrika walihudhuria.

Nchi kutoka Afrika zilikuwa ni Algeria, Misri, Ethiopia, Ghana, Liberia, Libya na Sudan ambazo kwa pamoja na zile za Asia walitoka na maazimio kumi katika mkutano huo ikiwa ni pamoja na kuheshimu haki za binadamu kama ambavyo Umoja wa Mataifa unataka, kuheshimu uhuru wan chi na mipaka yake, kutambua usawa wa kimatabaka na nchi, kutoingilia kati masuala ya ndani ya nchi nyingine, kuheshimu haki za kila mtu na mengineyo.


IMETOLEWA NA:  WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM
24 APRILI, 2015




Naibu Waziri wa Mambo ya Nje akutana kwa mazungumzo na CEO wa Standard Chartered nchini

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akimkaribisha Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini Bi. Liz Lloyd alipomtembelea Wizarani kwa ajili ya mazungumzo na Mhe. Maalim. 
Mhe. Maalim akimtambulisha kwa Bi. Llyoid Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya. 
Mhe. Dkt.  Maalim akizungumza na Bi. Lloyd
Ujumbe alioambatana nao Bi. Lloyd wakifuatilia mazungumzo.
Bi. Lloyd nae alipata wasaa wa kuchangia hoja wakati wa mazungumzo na Dkt.  Maalim 
Balozi  Yahya (kushoto) akiwa na Katibu wa Naibu Waziri Bw. Adam Isara wakisikiliza mazungumzo kati ya Dkt. Maalim na Bi. Lloyd (hawapo pichani)
Mazungumzo yakiendelea.


Picha na Reginald Kisaka.

Membe awahimiza Watanzania kuchangamkia fursa Comoro


Mhe. Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania akihutubia Kongomano la Biashara baina ya Tanzania na Comoro jijini Moroni Alhamis tarehe 23 Aprili 2015



Membe awahimiza Watanzania kuchangamkia fursa za kibiashara na kuwekeza katika Visiwa vya Comoro

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.)  amewahimiza wafanyabiashara wa Tanzania kuchangamkia fursa za biashara na uwekezaji Visiwani Comoro kwani uhusiano baina ya nchi hizi mbili umeimarika.

Mhe. Membe alitoa kauli hiyo wakati akilihutubia Kongamano la Biashara baina ya Tanzania na Comoro lililoandaliwa na Balozi za Tanzania na Comoro kwa kushirikiana na sekta binafsi za nchi hizo mbili jijini Moroni, Comoro tarehe 23 Aprili, 2015.

 “Watanzania tunathaminiwa sana hapa kutokana na mchango wetu mwaka 2008 tulipokikomboa Kisiwa cha Anjouan kutoka kwa Kanali Bacar. Sasa Serikali ya Umoja wa Visiwa vya Comoro imeimarika na uhusiano wetu umeshamiri. Wanatukaribisha sisi kwanza kushirikiana kibiashara, tuchangamkie fursa hii” alisema Waziri Membe.


Vilevile,  Mhe. Membe alisifu jitihada za ofisi za ubalozi wa nchi hizi mbili kwa kuitikia wito wa kuimarisha uhusiano wa kibiashara kwa kuandaa kongamano hilo la kihistoria.

“Rais Kikwete alipofanya ziara yake hapa mwaka 2014, aliahidi kukuza uhusiano wetu na kutoa wito wa kushirikiana kibiashara kwa manufaa ya nchi zetu. Nawapongeza sana Balozi Kilumanga na Balozi Fakih kwa kushirikiana na sekta binafsi na kutekeleza hili kwa wakati”alisema Waziri Membe, ambaye aliongoza ujumbe wa Tanzania kwenye kongamano hilo.

Kwa upande wake, Rais wa Visiwa vya Comoro, Mhe. Ikililou Dhoinine alisema kuwa yeye na Serikali yake wanathamini mchango mkubwa wa Tanzania kwa watu wa Comoro na hivyo atahakikisha uhusiano wetu unakua kwenye nyanja zote, Serikalini, sekta binafsi na hata baina ya watu wa nchi zote mbili.

Aidha, baada ya ufunguzi rasmi wa kongamano hilo, wafanyabiashara wa Tanzania walikutanishwa na wenzao wa Comoro kwenye makundi madogo madogo ili kuibua changamoto zinazokwaza biashara baina ya nchi hizo. Mikutano hiyo inatarajiwa kuibua njia bora zaidi ya kuwezesha biashara baina yao na kuimarisha uhusiano baina ya watu wake.

Akiwa jijini Moroni, Mhe. Membe alipata fursa ya kutembelea fukwe za bahari ambazo ni vivutio vikubwa vya utalii kwenye nchi hiyo ya visiwa akiwa na mwenyeji wake Mhe. Dkt. Alanrif Said Hussane, Waziri wa Mambo ya Nje wa Visiwa vya Comoro.

Serikali ya Tanzania ilifungua ofisi zake za ubalozi mwaka 2013 ambapo inawakilishwa nchini humo na Mhe. Chabaka Kilumanga, Balozi wa Tanzania, mwenye makazi yake Moroni. Kwa upande wa Serikali ya Comoro ilifungua Ubalozi wake nchini Tanzania mwaka 2014 na inawakilishwa na Mhe. Ahamed El Badaoui Mohamed Fakih Balozi wa Comoro mwenye makazi yake Dar es salaam.

Kongamano hilo la siku mbili lililofunguliwa na Mhe. Ikililou Dhoinine, Rais wa Visiwa vya Comoro, lilifanyika kwenye ukumbi wa bunge jijini Moroni, mojawapo ya visiwa vitatu vinavyounda Umoja wa Visiwa vya Comoro, na kuhudhuriwa na wafanyabiashara takriban mia moja kutoka Tanzania. Visiwa vingine vinavyounda umoja huo wa Comoro ni Ngazija (Grand Comoro), Anjouan na Moheli huku mji mkuu ukiwa Moroni.

-Mwisho-

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

Sehemu ya Wafanyabiashara waliohudhuria Kongamano hilo wakimsikiliza Mhe. Membe 

 Picha ya meza kuu ya viongozi wa Tanzania na Comoro,

katikati ni Rais wa Visiwa vya Comoro Mhe. Dk. Ikililou Dhoinine, 
akiwa na Mhe. Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa 
Kimataifa wa Tanzania na Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania kwenye 
Kongomano la Biashara wakifuatilia ufunguzi.

 Rais wa Visiwa vya Comoro Mhe. Dk. Ikililou Dhoinine, akizungumza na Mhe. Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania wakati wa ufunguzi rasmi wa Kongamano la BIashara baina ya Tanzania na Comoro tarehe 23 Aprili 2015 Moroni.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje amuaga Mwakilishi wa FAO nchini

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akimkaribisha Mwakilishi wa Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (F.A.O) nchini Bi. Diana E. Tempelman alipomtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi wa Shirika hilo hapa nchini. 
Mhe. Dkt. Mahadhi akizungumza na Bi. Diana kwa kumpongeza kwa uwakilishi wake mzuri wa Shirika la FAO hapa nchini
Bi. Diana nae akitoa neno la shukrani kwa Naibu Waziri kwa Ushirikiano mzuri aliokuwa akiupata kutoka Wizarani wakati wote akiwa hapa nchini.  

Picha na Reginald Philip

Wednesday, April 22, 2015

Waziri Membe azungumza na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa UN eneo la Maziwa Makuu

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), akizungumza na Mwakilishi  Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye Ukanda wa Maziwa Makuu, Bw.  Said Djinnit walipokutana kwa mazungumzo tarehe 22 Aprili, 2015. Katika mazungumzo yao waligusia masuala ya usalama katika Ukanda huo hususan hali ilivyo nchini DRC.
Waziri Membe akimweleza jambo Bw. Said Djinnit (katikati) huku Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilshi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Bw. Alvaro Rodriguez akisikiliza kwa makini.
Waziri Membe (kulia) akiagana na Bw. Said Djinnit mara baada ya kumaliza mazungumzo yao


Picha na Reginald Philip