Wednesday, November 24, 2021

BALOZI MULAMULA : WEKENI UTARATIBU WA KUSHUGHULIKIA DIASPORA

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine (kushoto) akizungumza wakati wa kikao kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kulia) na Mabalozi wa Tanzania nje ya nchi, katikati ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk. Kikao hicho kilifanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa njia ya mtandao

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kulia)  akizungumza wakati wa kikao na  Mabalozi wa Tanzania nje ya nchi kilichofanyika jijini Dar es Salaam kwa njia ya mtandao.


Kiongozi wa mabalozi wa Tanzania nje ya nchi ambaye pia ni Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi Mhe. Irene Kasianju (katikati) akizungumza katika kikao cha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula na Mabalozi wa Tanzania nje ya nchi kilichofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa njia ya mtandao, kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma Rajab na kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Naimi Aziz.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Diaspora Bi Tagie Mwakawago (kushoto) akizungumza juu ya mfumo wa kielektroniki wa kuwasajili Diaspora katika kikao cha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula na Mabalozi wa Tanzania nje ya nchi kilichofanyika jijini Dar es Salaam kwa njia ya mtandao.
Baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Wizara walioshiriki katika kikao cha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula na Mabalozi wa Tanzania nje ya nchi kilichofanyika jijini Dar es Salaam kwa njia ya mtandao wakifuatilia kikao hicho.



 


 

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) amewataka Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania Nje ya Nchi kuweka utaratibu wa kushughulikia masuala ya Diaspora katika meneo yao ya uwakilishi.

Balozi Mulamula ametoa agizo hilo Jijini Dar es Salaam alipozungumza na mabalozi hao kwa njia ya mtandao kwa lengo la kuwakumbusha na kuwapa tarifa juu ya utendaji kazi wa Wizara na mambo mengine yanayojiri nchini.

 ‘‘Anzisheni utaratibu wa kushughulikia masuala ya Diapora katika maeneo yenu ya uwakilishi, ikiwemo kuratibu mikutano ya mara kwa mara hata kama ni kwa njia ya mtandao’’ amesema Balozi Mulamula.

Waziri Mulamula pia amewataka mabalozi  kuratibu mikutano ya mara kwa mara na diaspora hata kama ni kwa njia ya mtandao ikiwa ni harakati za kuwaweka pamoja na kuwajumuisha katika mipango na harakati za kuiletea nchi maendeleo kupitia Watanzania hao wanaoishi nje ya nchi.

Amewaelekeza mabalozi pia kuhakikisha kuwa wanawatambua Diaspora wa Tanzania duniani kote na kuwawekea mazingira mazuri ya kuwawezesha kuchangia katika maendeleo na uchumi wa taifa.

 

Waziri Mulamula ameongeza kuwa, Wizara inatambua umuhimu wa Diaspora na kuthamini mchango wao katika maendeleo ya Taifa ndiyo maana  imeamua kuingiza masuala ya Diapora katika  Sera mpya ya Mambo ya Nje.

“Wizara tumehakikisha kuwa masuala ya Diapora yanakuwa sehemu ya Sera ya Mambo ya Nje hii ni kutokana na mchango wa Diapora kwa maendeleo ya Taifa,” amesema Waziri Mulamula.

 

Balozi mulamula ameongeza kuwa Serikali inalifanyia kazi ombi la Diaspora la kupatiwa hadhi maalum na kuutaka uongozi wa Wizara kuongeza jitihada za kuleta mfumo wa kielektroniki wa kuwasajili Diaspora wote duniani ili kuweza kupata tarifa muhimu na takwimu sahihi.

 

Katika kikao hicho Waziri Mulamula aliwaelezea mabalozi hao juu ya maandalizi ya Serikali katika kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara, utengenezaji wa Sera mpya ya Mambo ya Nje, uanzishwaji wa Idara mpya ya Diplomacia ya uchumi ambayo itakuwa kiungo katika ya wizara, Balozi za Tanzania Nje na Idara na Balozi zetu taasisi nyingine za Umma na Sekta binafsi ili kufanikisha azma ya Serikali katika kutekeleza Diplomasia ya Uchumi na hivyo kujiletea maendeleo.

 

Aidha, amesema kuwa Serikali imekamilisha ufunguzi wa Konseli Kuu katika Mji wa Lubumbashi - Jamhuri ya Kimemokrasia ya Congo (DRC) na Guangzhou - Jamhuri ya Watu wa China pamoja na kuonesha nia ya kufungua Konseli Kuu katika Mji wa Shanghai na katika Jamhuri ya watu wa China.

 

 

Tuesday, November 23, 2021

WAZIRI MULAMULA AWASIHI MABALOZI KUUNGA MKONO JITIHADA ZA SERIKALI

Na Waandishi wetu, Dar

Serikali imetoa wito kwa mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa kuunga mkono juhudi za kusaidia upatikanaji wa chanjo ya Uviko 19 kwa Watanzania.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) alipokutana na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao pamoja na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa Jijini Dar es Salaam.

Waziri Mulamula amewasihi mabalozi hao kuendelea kuungana na Serikali katika jitihada za upatikanaji wa chanjo ya Uviko 19 ambapo amesema kuwa hadi sasa ni watanzania milioni 1.5 wamechanjwa

“Ninawaomba zaidi chanjo nyingine ili watanzania wote waweze kuchanja kwani mwamko wa kuchanja kwa sasa hapa nchini umekuwa mkubwa,” amesema Balozi Mulamula

Pia Waziri Mulamula amewahakikishia kuwa Tanzania inazingatia masula ya demokrasia, utawala bora, utawala wa sheria pamoja na kuheshimu haki za binadamu.

Kwa upande wake kiongozi wa Mabalozi nchini ambaye pia ni Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini Mhe. Dkt. Ahmada El Badaoui Mohamed amesema pamoja na mambo mengine, vikao hivyo vimekuwa na manufaa makubwa katika utekelezaji wa majukumu yao hapa nchini.

Nae Waziri wa uchumi wa buluu Zanzibar Mhe. Abdalla Hussein Kombo amesema katika mkutano huo, wamejadili agenda ya uchumi wa buluu ambayo ina vipaumbele vitano ambavyo ni uvuvi na utamaduni, utalii, usafirishaji, usimamizi wa bahari pamoja na nishati.

“Tumewaeleza wenzetu mabalozi vipaumbele vyetu vya uchumi wa buluu na wameonesha nia ya kushirikiana na sisi katika kuendeleza agenda yetu ya Uchumi wa buluu,” amesema Mhe. Kombo 

“Pia tumewaeleza kuwa tumemaliza kupitia sera yetu ya uchumi wa buluu na sasa tumeshatekelez mpango wa utekelezaji na sasa tunataka tuone namna gani sisi na wao tunaweza kuanza kuitekeleza agenda yetu ya uchumi wa buluu,” ameongeza Mhe. Kombo

Mkutano huo umehudhuriwa pia na Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba (Mb), Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) na Naibu Waziri wa Madini Mhe. Prof. Shukrani Manya pamoja na Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiongea na mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wanaoziwakilisha nchi na Taasisi zao hapa nchini katika kikao cha pamoja kilichofanyika Jijini Dar es Salaam


Kiongozi wa Mabalozi nchini ambaye pia ni Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini Mhe. Dkt. Ahmada El Badaoui Mohamed akiongea na mabalozi (hawapo pichani) katika kikao cha pamoja kilichoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akiongea na Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wanaoziwakilisha nchi na Taasisi zao hapa nchini katika kikao cha pamoja kilichofanyika Jijini Dar es Salaam


Sehemu ya Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ulioshiriki katika kikao cha pamoja kati ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi na Taasisi zao hapa nchini na Uongozi wa Wizara 

Sehemu ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi na Taasisi zao hapa nchini wakifuatilia kikao  


Sehemu ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi na Taasisi zao hapa nchini wakifuatilia kikao  


Sehemu ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi na Taasisi zao hapa nchini wakifuatilia kikao  



 

BALOZI FATMA AFUNGUA MADHIMISHO WIKI YA VYAKULA VYA KIITALIANO

 Na Mwandishi wetu, Dar

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab amefungua Maadhimisho ya Wiki ya Dunia ya vyakula vya Kiitaliano (World Week of Italian Cuisine).

Akifungua maadhimisho hayo jana jioni Jijini Dar es Salaam, Balozi Fatma amesema kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Italia katika kuhakikisha uhusiano uliopo baina yake unaendele kuimarika na kuwasihi kutumia maadhimisho hayo pamoja na mambo mengine, kutangaza vivutio vya utalii hapa nchini.

“Italia imekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na Serikali yetu katika nyanja mbalimbali ikiwemo utalii, elimu, biashara na uwekezaji………..naomba niwahakikishie tutaendelea kushirikiana ili kukuza maendeleo kwa maslahi ya pande zote mbili,” amesema Balozi Fatma

Balozi Fatma ameongeza kuwa Italia imekuwa mstari wa mbele katika sekta ya utalii na kuwasihi kutumia madhimisho hayo pia kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo Tanzania.

Kwa upande wake Balozi wa Italia nchini, Mhe. Marco Lombardi amesema Italia itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kudumisha na kuendeleza ushirikiano wake wa muda mrefu.

“Kupitia maadhimisho haya naamini kuwa yatakuwa chachu ya kuhamasisha upikaji wa vyakula mbalimbali vizuri ambavyo kwa namna moja au nyingine vitatoa ajira kwa watanzania pamoja na kuongeza fursa za utalii hapa nchini,” amesema Balozi Lombardi.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab akisalimiana na Balozi wa Italia hapa nchini, Mhe. Marco Lombardi mara baada ya kuwasili kwenye makazi ya Balozi kwa ajili ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Dunia ya vyakula vya Kiitaliano (WORLD Week of Italian Cuisine) Jijini Dar es Salaam


Balozi wa Italia hapa nchini, Mhe. Marco Lombardi akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab katika Maadhimisho ya Wiki ya Dunia ya vyakula vya Kiitaliano (WORLD Week of Italian Cuisine) Jijini Dar es Salaam


Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Nabil Hajlaoui akisalimiana na Balozi wa Italia hapa nchini, Mhe. Marco Lombardi pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Swahiba Mndeme.


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab akisalimiana na Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini Mhe. Dkt. Ahmada El Badaoui Mohamed


Balozi wa Italia hapa nchini, Mhe. Marco Lombardi akiteta jambo na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Nabil Hajlaoui katika Maadhimisho ya Wiki ya Dunia ya vyakula vya Kiitaliano (WORLD Week of Italian Cuisine) Jijini Dar es Salaam


Balozi wa Finland hapa nchini, Mhe. Riitta Swan akiteta jambo na Balozi wa Marekani nchini Mhe. Dk. Donald Wright katika Maadhimisho ya Wiki ya Dunia ya vyakula vya Kiitaliano


Sehemu ya Mabalozi pamoja na wananchi waliojitokeza katika Maadhimisho ya Wiki ya Dunia ya vyakula vya Kiitaliano jijini Dar es Salaam


Balozi wa Italia hapa nchini, Mhe. Marco Lombardi akihutubia Mabalozi pamoja na wananchi waliojitokeza katika Maadhimisho ya Wiki ya Dunia ya vyakula vya Kiitaliano jijini Dar es Salaam


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab akiwasilisha hotuba yake kwa mabalozi na wananchi (hawapo pichani) wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Dunia ya vyakula vya Kiitaliano


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab akiteta jambo na Balozi wa Finland hapa nchini Mhe. Riitta Swan


Balozi wa Canada nchini Mhe. Pamela O'Donnell akiteta jambo na Balozi wa Marekani hapa nchini Mhe. Dkt. Donald Wright



 

Monday, November 22, 2021

Wafanyabiashara wa Nyama wa Oman Kuzuru Tanzania

Wafanyabiashara maarufu nchini Oman wanatarajiwa kufanya ziara nchini tarehe 25 Novemba 2025 kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kupata eneo mkoani Tanga la kukusanyia mifugo hai ya kusafirisha Oman kupitia bandari ya Tanga.

Wafanyabiashara hao ambao ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Abu Suleiman Al-Darai Trading &Services, Bw.  Mohamed S. Aldarai; Afisa Mtendaji Mkuu wa Desert Cold Store LLC, Dkt. Munawar H. Pardhan; Mkurugenzi wa Desert Cold Store LLC, Bw. Aasim M. Pardhan na Mkurugenzi wa IKTIMAl Trading Company LLC, Bw. Salem Al Dighaishi awali walikuwa wanasafirisha nyama iliyogandishwa tani 240 kwa mwezi kutoka nchini walifanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Abdallah Kilima hivi karibuni kuhusu taratibu za utekelezaji wa biashara yao hiyo.

Mhe. Balozi aliwapongeza wafanyabiashara hao kwa kuonesha nia ya kufanya biashara na Tanzania kwani itasaidia kubadilisha urari wa biashara kati ya nchi hizi mbili ambao kwa sasa inaonesha Oman inauza zaidi nchini Tanzania. Aliwaahidi wafanyabiashara hao kuwa atawakutanisha na Mamlaka husika nchini Tanzania akiwemo Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Edwin Rutageruka ili kukamilisha taratibu husika. 

Wafanyabiashara hao walielezea malengo yao ya baadaye ni kufanyabiashara ya kusafirisha matunda kutoka nchini kwenda Oman na nchi nyingine za ghuba, jambo ambalo litasaidia wakulima wa Tanzania kupata soko na kuondoa uharibifu wa matunda yanayoharibika kwa kukosa soko.

Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Abdallah Kilima akiwa katika picha ya pamoja na wafanyabishara wa nyama. Kutoka kulia ni Bw. Salem Al Dighaishi - Mkurugenzi wa IKTIMAl Trading Company LLC; Bw. Mohamed S. Aldarai – Mkurugenzi Mwendeshaji wa Abu Suleiman Al-Darai Trading &Services; Dkt. Munawar H. Pardhan – Afisa Mtendaji Mkuu wa Desert Cold Store LLC; na Bw. Aasim M. Pardhan – Mkurugenzi wa Desert Cold Store LLC.

Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Abdallah Kilima akipokea zawadi kutoka kwa Bw. Mohamed S. Aldarai, kiongozi wa ujumbe wa wafanyabiashara ya Nyama nchini Oman. Kushoto ni Bw. Tahir Bakar Khamis – Mkuu wa Utawala, Ubalozi wa Tanzania Oman.

Saturday, November 20, 2021

TAARIFA YA MAFANIKIO YA MIAKA 60 YA UHURU WA TANZANIA BARA


TAARIFA YA MHESHIMIWA BALOZI LIBERATA MULAMULA (MB), WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MAFANIKIO YA MIAKA 60 YA UHURU WA TANZANIA BARA 

TAREHE 20 NOVEMBA, 2021, DODOMA 

BOFYA HAPA KUTAZAMA VIDEO YA  MHESHIMIWA BALOZI LIBERATA MULAMULA (MB) KUHUSU MAFANIKIO YA MIAKA 60 YA UHURU WA TANZANIA BARA 

Friday, November 19, 2021

WAZIRI MULAMULA AZIHAKIKIKISHIA USHIRIKIANO TAASISI ZA KIMATAIFA ZENYE MAKAZI YAKE NCHINI


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb.) amezihakikishia ushirikiano taasisi za kimataifa zenye makazi yake hapa nchini pamoja na kuzitaka kutekeleza kwa tija malengo mahsusi ya taasisi hizo kuwepo nchini Tanzania.

Hayo yamesemwa na Waziri Mulamula alipokutana na Msajili wa Mahakama ya Kimataifa ya Kesi Masalia za iliyokuwa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) na Mauaji ya Halaiki ya iliyokuwa Yugoslavia ya Zamani (ICTY) – (IRMCT) Bw. Abubaccar Tambadou alipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma tarehe 19 Novemba 2021.

"Tanzania ikiwa nchi mwenyeji wa mahakama unayoiongoza tutaendelea kutoka ushirikiano ili kuwawezesha kusimamia majukumu yenu kwa ufanisi na kuhakikisha lengo lilokusudiwa la mahakama hii kumaliza kesi zilizobaki pamoja na kuwa kituo cha kumbukumbu kwa kesi hizo linatimia" alisema Mhe. Mulamula.

Waziri Mulamula aliongeza kwa kusema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kuthamini heshima ya kuwa mwenyeji wa Taasisi hiyo na kwamba inaendelea kusimamia uhuru na haki za mahakama nchini kama ilivyosaini katika makubaliano mbalimbali ya kimataifa na anakaribisha mashirika mengine ya Kimataifa kuja kujenga nchini kwa kuwa ni mahali salama kuishi na kiutendaji. 

Pia ametumia fursa ya mazungumzo hayo kuwakaribisha watanzania na wageni wanaofanya tafiti kuhusiana na taasisi hiyo na nyingine za kimataifa zinazohusiana kwa namna moja au nyingine kiutendaji na mahakama ya IRMCT kuja kwa ajili ya kufanikisha tafiti zao.

Bw. Abubacaar amefanya ziara hiyo kwa ajili ya kujitambulisha kufuatia kuteuliwa kwake hivi karibuni kuwa Msajili wa Mahakama hiyo, ambapo pamoja na mambo mengine alipata nafasi ya kueleza majukumu ya Mahakama sambambamba na maboresho ya kiutendaji yanayotarajiwa kufanywa na mahakama hiyo.

“Mahakama inashukuru kwa ushirikiano unaoendelea kutolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na itaendelea kutoa taarifa za mara kwa mara pale inapobidi ili kuiwezesha nchi mwenyeji kuwa na uelewa wa pamoja na mahakama kiutendaji” alieleza Bw. Abubaccar

Wataalamu wengine walioshiriki katika mazungumzo hayo ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab, Mkurugenzi Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Caroline Chipeta, Mkuu wa Utawala wa Mahakama ya IRMCT, Bw. David Falces, na Mwanasheria kutoka IRMCT, Bi. Tully Mwaipopo.

Mwaka 2010 Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, lilipitisha Azimio nambari 1966 la kuanzisha Mfumo wa Kimataifa utakaomalizia mashauri ya Masalia kwa iliyokuwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ya Rwanda (ICTR) yaliyotokea mwaka 1994 na Mauaji ya Halaiki yaliyotokea katika iliyokuwa Yugoslavia ya Zamani (ICTY). Katika azimio hilo Baraza kuu lilibainisha wazi kwamba Arusha itakuwa Makao Makuu ya tawi hilo jipya la IRMCT na The Hague kuwa makao makuu ya Tawi Jingine.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa katika mazungumzo na Msajili wa Mahakama ya Kimataifa ya Kesi Masalia za Mauaji ya Kimbari (IRMCT) Bw. Abubacarr Tambadou jijini Dodoma. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) akimsikiliza Msajili wa Mahakama ya Kimataifa ya Kesi Masalia za Mauaji ya Kimbari Bw. Abubacarr Tambadou walipokutana kwa mazungumzo jijini Dodoma. 
Mazungumzo yakiendelea
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) na Msajili wa Mahakama ya Kimataifa ya Kesi Masalia za Mauaji ya Kimbari Bw. Abubacarr Tambadou wakiwa katika picha ya pamoja.

 

Kutoka kusho; Mwanasheria wa IRMCT Bi. Tully Mwaipopo, Mkuu wa Utawala wa Mahakama ya IRMCT Bw. David Falces, Msajili wa IRMCT Bw. Abubacarr Tambadou, Waziri Mhe. Balozi Liberata Mulamula, Naibu Katibu Mkuu Balozi Fatma Rajab, na Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria Balozi Caroline Chipeta katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazungumzo.