Thursday, January 27, 2022

MKUTANO WA 19 WA MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE WA AFRIKA NA NORDIC KUFANYIKA JUNI 2022 FINLAND


Na Mwandishi Wetu, Dar

Mkutano wa 19 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika na nchi za Nordic unatarajiwa kufanyika mwezi Juni 2022 nchini Finland.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Finland nchini Mhe. Riitta Swan leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Katika kuendeleza na kuimarisho ushirikiano wa nchi hizo mbili viongozi hao wamependekeza kufanikisha ziara ya Mhe. Waziri Mulamula nchini Finland pamoja na ushiriki wake katika mkutano wa 19 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Nordic utakaofanyika nchini Finland mwezi Juni 2022. 

Katika mazungumzo ya viongozi hao, Balozi Mulamula amemhakikishia Balozi Swan kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana kwa karibu na Finland katika kuhakikisha Mataifa hayo yanashirikiana kijamiii, kisiasa na kiuchumi.

"Finland amekuwa mdau Mkubwa wa Maendeleo hapa nchini kwetu hasa katika sekta ya fedha hususan katika masuala ya kodi, mazingira, tehama, uongozi pamoja na uwezeshaji wa wanawake........pia tumekubaliana kuendeleza ushirikiano wetu kwa Maendeleo endelevu," amesema Balozi Mulamula.

Katika tukio jingine, Waziri Mulamula amekutana kwa mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Stanbink Tanzania Bw. Kevin Wingfield
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula katika mazungumzo na Balozi wa Finland nchini Mhe. Riitta Swan leo katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiteta jambo na  Balozi wa Finland nchini Mhe. Riitta Swan pamoja na Afisa kutoka Ubalozi wa Finland nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Balozi wa Finland nchini Mhe. Riitta Swan, wengine ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Afrika Mashariki Balozi Swahiba Mndeme, Bi. Kisa Mwaseba Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje pamoja na Afisa kutoka Ubalozi wa Finland 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Stanbink Tanzania Bw. Kevin Wingfield yaliyofanyika katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam



TANZANIA NA INDIA KUONGEZA MAENEO YA USHIRIKIANO

Na Mwandishi wetu, Dar

Tanzania na India zimeahidi kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano katika kuhakikisha maendeleo endelevu kwa maslahi mapana ya pande zote mbili.

Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula wakati akihutubia sherehe za maadhimisho ya 73 ya Jamhuri ya India jana jioni Jijini Dar es Salaam.

Tanzania na India zimedhamiria kufanya kazi kwa karibu katika kutafuta njia bora ya kufungua fursa mpya na kuimarisha fursa mpya za biashara na uwekezaji zilizopo kati ya nchi hizo.

“Kuanza kwa safari za ndege za moja kwa moja kutoka Dar es Salaam hadi Mumbai kwa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) na kufunguliwa kwa soko la parachichi nchini India ni miongoni mwa hatua zilizochukuliwa ili kuimarisha na kukuza uhusiano wetu katika sekta za biashara na uwekuzaji pamoja na utalii kati ya India na Tanzania,” Amesema Balozi Mulamula. 

Pamoja na mambo mengine, Balozi Mulamula ameongeza kuwa Tanzania na India kwa sasa zimeanzisha ushirikiano katika usambazaji wa nishati, ujenzi wa miundombinu na Kilimo. Matarajio ya kuimarisha ushirikiano unaoendelea kati ya nchi hizi mbili ni mazuri na yanatia matumaini. 

“Uwekezaji wa India pamoja na idadi ya Wahindi wanaotembelea Tanzania kwa madhumuni ya kuwekeza katika sekta za madini, utalii, viwanda, kilimo, usindikaji wa mazao ya kilimo, nishati, usafirishaji, ujenzi, huduma za fedha na maendeleo ya rasilimali watu unaendelea kuongezeka kwa kasi,” amesema Balozi Mulamula.

Kwa upande wake, Balozi wa India nchini, Mhe. Binaya Srikanta Pradhan amesema kuwa Tanzania imekuwa na uhusiano mzuri na India ambapo uhusiano huo umekuwa ni chachu ya maendeleo kwa mataifa yote mawili na umepelekea kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano.

“Ushirikiano na mshikamano uliopo baaina ya mataifa yetu mawili umekuwa chachu ya maendeleo na lengo la ushirikiano wetu yetu ni kukuza uchumi wetu,” amesema Balozi Pradhan 

Aidha, Balozi Pradhan amebainisha kuwa Tanzania itaendelea kuwa ya kipekee kwa taifa la India kutokana na mshikamano ambao umepelekea mataifa haya kufanya biashara, uwekezaji, kujenga uwezo, ujenzi wa miundiombinu pamoja na maendeleo ya kiuchumi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akihutubia sherehe za maadhimisho ya 73 ya Jamhuri ya India jana jioni Jijini Dar es Salaam

Balozi wa India nchini, Mhe. Binaya Srikanta Pradhan akihutubia sherehe za maadhimisho ya 73 ya Jamhuri ya India jana jioni Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula. 

Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Kiongozi wa Mabalozi nchini ambaye pia ni Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini Mhe. Dkt. Ahmada El Badaoui Mohamed 

Sherehe za maadhimisho ya 73 ya Jamhuri ya India zikiendelea jana jioni Jijini Dar es Salaam

Balozi Mulamula na baadhi ya Mabalozi wakifuatilia sherehe za maadhimisho ya 73 ya Jamhuri ya India jana jioni Jijini Dar es Salaam

Sehemu ya Mabalozi wakifuatilia sherehe za maadhimisho ya 73 ya Jamhuri ya India jana jioni Jijini Dar es Salaam

Sherehe za maadhimisho ya 73 ya Jamhuri ya India jana jioni Jijini Dar es Salaam

Mabalozi na wageni waalikwa wakifuatilia sherehe za maadhimisho ya 73 ya Jamhuri ya India  

Sehemu ya Mabalozi wakifuatilia sherehe za maadhimisho ya 73 ya Jamhuri ya India  


Wednesday, January 26, 2022

TANZANIA, MOROCCO ZAKUBALIANA KUIMARISHA USHIRIKIANO

Tanzania na Morocco zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika nyanja za biashara na uwekezaji, elimu, utalii, uwezeshaji wa kiuchumi kwa wanawake na vijana.

Makubaliano hayo yamefikiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco Bw. Nasser Bourita walipofanya mkutano wa kwa njia ya mtandao. Balozi Mulamula ameshiriki katika mkutano huo akiwa katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

“Tumezungumzia masuala ya kuimarisha uhusiano wetu baina ya Tanzania na Morocco na tumepitia makubaliano yaliyofikiwa wakati wa ziara ya Mfalme wa Morocco alipotembelea Tanzania mwaka 2016 pamoja na kuangalia mikataba mbalimbali iliyotiwa saini wakati wa ziara ya Mfalme wa Morocco ……… laikini pia tumejadili umuhimu wa kuwa na tume ya pamoja ya ushirikiano,” Amesema Balozi Mulamula.

Katika mkutano huo, viongozi hao wamejadili na kukubaliana kuimarisha ushirikiano wa karibu katika sekta za biashara na uwekezaji, utalii, elimu hasa katika kuongeza idadi ya ufadhili wa masomo kwa watanzania kutoka wanafunzi 30 hadi 50.

“Morocco ni nchi inayopata watalii wengi, hivyo tumekubaliana kushirikian kwa karibu zaidi ili kuweza kupata uzoefu ni njia gani wanatumia katika kukuza sekta ya utalii,” ameongeza Balozi Mulamula.

Katika tukio jingine, Balozi Mulamula amekutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Oman nchini Dkt. Salim Saif Al Harbi katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. 

Mazungumzo ya viongozi hao yamelenga kujadilia masuala mbalimbali ya kuendeleza na kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya Serikali ya Tanzania na Oman.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akishiriki mkutano wake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco Bw. Nasser Bourita. Mkutano huo umefanyika kwa njia ya mtandao.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akifuatilia mkutano 
Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco Bw. Nasser Bourita akimsikiliza Balozi Mulamula (hayupo pichani) katika mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akimueleza jambo Kaimu Balozi wa Oman nchini Dkt. Salim Saif Al Harbi walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Kikao baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula na Kaimu Balozi wa Oman nchini Dkt. Salim Saif Al Harbi kikiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam



HOTUBA YA WAZIRI MULAMULA KWENYE DIPLOMATIC SHERRY PARTY IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

BOFYA HAPA KUSIKILIZA HOTUBA YA MHE. WAZIRI MULAMULA KWENYE DIPLOMATIC SHERRY PARTY ILIYOFANYIKA TAREHE 24 JANUARI 2022, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM


Tuesday, January 25, 2022

HABARI PICHA DIPLOMATIC SHERRY PARTY IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana aliwaalika Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa katika Sherehe za Mwaka Mpya 2022 kwa Mabalozi (Diplomatic Sherry Party) Ikulu – Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, katika sherehe hizo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alisema Sera Mpya ya Mambo ya Nje itaendelea kuzingatia Diplomasia ya Uchumi na kuakisi maendeleo mapya kama vile uchumi wa bluu, mabadiliko ya tabianchi, uchumi wa kidigitali pamoja kukuza lugha ya Kiswahili kama lugha ya kidiplomasiana kibiashara. 

Awali, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula aliwahakikishia Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na Waakilishi wa Mashirika ya Kimataifa kuwa Tanzania chini ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuimarisha uhusiano wake kila wakati. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongea na Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa katika Sherehe za Mwaka Mpya 2022 kwa Mabalozi (Diplomatic Sherry Party) Ikulu – Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akitoa hotuba yake wakati wa Sherehe za Mwaka Mpya 2022 kwa Mabalozi (Diplomatic Sherry Party) Ikulu – Dar es Salaam

Kiongozi wa Mabalozi nchini ambaye pia ni Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini Mhe. Dkt. Ahmada El Badaoui Mohamed akihutubia wakati wa Sherehe za Mwaka Mpya 2022 kwa Mabalozi (Diplomatic Sherry Party) Ikulu – Dar es Salaam

Sehemu ya Uongozi wa Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ukifuatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa Sherehe za Mwaka Mpya 2022 kwa Mabalozi (Diplomatic Sherry Party) Ikulu – Dar es Salaam

Baadhi ya Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa wakiwa katika  Sherehe za Mwaka Mpya 2022 kwa Mabalozi (Diplomatic Sherry Party) Ikulu – Dar es Salaam

Baadhi ya Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa wakiwa katika  Sherehe za Mwaka Mpya 2022 kwa Mabalozi (Diplomatic Sherry Party) Ikulu – Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Finland hapa nchini Mhe. Riitta Swan wakati wa Sherehe za Mwaka Mpya 2022 kwa Mabalozi (Diplomatic Sherry Party) 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi mbalimbali katika Sherehe za Mwaka Mpya 2022 kwa Mabalozi (Diplomatic Sherry Party) 






Saturday, January 22, 2022

BALOZI MULAMULA AFANYA MKUTANO KWA NJIA YA SIMU NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA SWEDEN

 Na Mwandishi wetu, Dar

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) amefanya mkutano kwa njia ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden Mhe. Ann Linde katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Viongozi hao pamoja na mambo mengine, wamejadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Sweden ikiwemo vipaumbele vya pande zote mbili kuelekea Mkutano wa Wakuu wa Nchi baina ya nchi za Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika (European Union - African Union Summit) uliopangwa kufanyika tarehe 17 – 18 Februari 2022.

Katika tukio jingine, Balozi Mulamula amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Somalia nchini Mhe. Zahra Ali Hassan katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam ambapo mazungumzo yao yamelenga kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Somalia
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akizungumza kwa njia ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden Mhe. Ann Linde

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akizungumza kwa njia ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden Mhe. Ann Linde. wengine ni Maafisa waandamizi Wizarani Bw. Charles Mbando na Bi. Agnes Kiama. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Balozi wa Somalia nchini Mhe. Zahra Ali Hassan katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula na Balozi wa Somalia nchini Mhe. Zahra Ali Hassan yakiendelea


Friday, January 21, 2022

BALOZI MULAMULA APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO UNHCR, UNFPA

Na Mwandishi wetu, Dar

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) amepokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Bibi. Mahoua Parums pamoja na Mwakilishi Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu (UNFPA) Bw. Mark Bryan Schreiner katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Balozi Mulamula amewaeleza Bibi. Parums na Bw. Schreiner kuwa UNHCR na UNFPA zimekuwa na mchango mkubwa kwa kuiunga mkono Serikali ya Tanzania katika kushughulikia masuala ya wakimbizi pamoja na kukuza maendeleo.

“Tumekubaliana na UNHCR kuendelea kushirikiana kwa karibu pamoja na Wizara ya Mambo ya Ndani katika mchakato wa kurudisha wakimbizi wa Burundi nchini kwao kusudi hali ya Burundi iendelee kutengamaa kwani kurudi kwa wakimbizi hao kutachangia maendeleo ya Burundi,” amesema Balozi Mulamula.

Balozi Mulamula ameongeza kuwa itakumbukwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye alipofanya ziara ya kitaifa hapa nchini Oktoba 2021 alitoa rai ya wakimbizi wa Burundi warudi nchini kwao ili kuweza kuchangia maendeleo ya Taifa hilo.  

Pia Balozi Mulamula ameongeza kuwa Mwakilishwa wa UNFPA amekuja wakati muafaka ambapo Serikali inatarajia kuanza zoezi la Sensa mwezi Augusti 2022 na hivyo kutoa rai kwa Shirika hilo kuwashirikisha na kuwawezesha vijana na wanawake wa kitanzania katika maendeleo ya teknolojia.  

“Rai yangu kwao ni kuwahusisha vijana na wanaweke kwani UNFPA mbali na kushughulika na idadi ya watu wana program ya kuwashirikisha na kuwawezesha vijana ni vyema washirikiane kwa pamoja na Mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa kwa maendeleo ya pande zote mbili,” Amesema Balozi Mulamula.

Kwa upande wake Mwakilishi wa UNHCR Bibi. Parums ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuwapokea na kuwalinda wakimbizi kwa muda mrefu.

“Tumekubaliana kushirikiana kwa pamoja na Serikali katika kuwalinda na kuwasaidia wakimbizi na kuwapatia baadhi ya mahitaji muhimu……tunaomba tuendeleze ushirikiano huu kwa maendeleo yetu,” amesema Bibi. Mahoua.

Nae Mwakilishi wa UNFPA, Bw. Schreiner amesema UNFPA itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha kuwa inasonga mbele kimaendeleo ikiwa ni pamoja na kusaidia katika zoezi la Sensa linalotarajiwa kufanyika Augosti 2022 ili kuiwezesha Tanzania kupata takwimu sahihi kuhusu idadi ya watu na kuiwezesha kusonga mbele kimaendeleo.

Katika tukio jingine, Waziri Mulamula amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Bibi. Sarah Gordon-Gibson.

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadiliana masuala mbalimbali ya kuendeleza na kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya Serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania na WFP.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Bibi. Mahoua Parums katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mwakilishi Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu (UNFPA) Bw. Mark Bryan Schreiner katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mwakilishi wa UNHCR, Bibi. Mahoua Parums akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula 

Kikao baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Mwakilishi wa UNHCR, Bibi. Mahoua Parums kikiendelea 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimueleza jambo Mwakilishi wa UNFPA Bw. Mark Bryan Schreiner katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam



Mwakilishi wa UNFPA Bw. Mark Bryan Schreiner akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Bibi. Sarah Gordon-Gibson 

FURSA ZA AJIRA


 

WAZIRI MULAMULA AZISISITIZA BALOZI KUTUMIA FURSA ZINAZOPATIKA KWA MASLAHI YA TAIFA

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Liberata Mulamula ameyasema hayo alipozungumza na watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uganda tarehe 20 Januari 2022.

Waziri Mulamula alikutana na watumishi wa Ubalozi huo alipokuwa nchini Uganda kwa ziara ya siku mbili ambapo, pamoja na mambo mengine alishiriki Mkutano wa Nne wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) uliomalizika tarehe 19 Januari 2022.

“Balozi zilizopo mipakani zina fursa nyingi kiuchumi hivyo, ni muhimu  kufanya Vikao vya Ujiraini Mwema na kuendelea kuhuisha mipango kazi kila inapohitajika kufanya hivyo kwa lengo la kutatuta changamoto na kuainisha maeneo mapya ya ushirikiano”, alisema Waziri Mulamula.

Pia, akaeleza Wizara inaendelea kuboresha mazingira ya kazi na kuhakikisha Balozi zote zinakuwa na Rasilimali zinazojitosheleza kuwezesha majukumu ya kisekta kutekelezwa kwa tija.

Vilevile akahimiza umuhimu wa kuongeza kasi ya kuzitangaza shughuli zinazofanyika sambamba na fursa mbalimbali zinazopatikana katika nchi hiyo hususani shughuli za kiuchumi ili ziweze kunufaisha wananchi na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wa Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Aziz Mlima alieleza kuwa Ubalozi ulifanikisha kikao cha ujirani mwema kilichofanyika kati ya Tanzania na Uganda, mwaka 2017 mjini Bukoba, Kagera.

Pia, kufuatia kupungua kwa masharti ya ugonjwa wa UVIKO- 19, Ubalozi unaendelea kuratibu shughuli nyingine zenye lengo la kuhakikisha Diplomasia ya uchumi na Diplomasia ya Umma inatekelezeka kikamilifu.

Kadhalika, Waziri Mulamula alitumia ziara hiyo kutembelea mali za Ubalozi huo ikiwemo majengo na viwanja, ambapo alipata ufafanuzi juu ya maboresho yanayotarajiwa kufanyika pamoja na uanzishaji wa miradi mipya katika maeneo hayo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula ( kati) akipokea maelezo kutoka kwa Balozi wa Tanzania Nchini Uganda, Mhe. Dkt. Aziz Mlima ( kulia ) tarehe 20 Januari 2022 jijini Kampala, Uganda. Kushoto ni maafisa wa Ubalozi huo.


Wednesday, January 19, 2022

WAZIRI MULAMULA AFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA UGANDA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Mhe. Jen. Jeje Odongo tarehe 19 Januari jijini Kampala, Uganda.
Viongozi hao walijadili masuala ya ushirikiano wa kidiplomasia hususani Diplomasia Uchumi kwa maslahi ya mataifa yao.

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Uganda na Tanzania wakiwa na Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Aziz Mlima (wa kwanza kushoto), Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Mhe. Richard Kabonelo (wa kwanza kulia) pamoja na maafisa kutoka nchi hizo wakifuatilia majadiliano.

Mhe. Waziri Mulamula akikabidhi zawadi kwa Mhe. Waziri Odongo

Picha ya Pamoja Waheshimiwa Mawaziri na Mabalozi wa Tanzania na Uganda.

 

MKUTANO WA NNE WA TUME YA KUDUMU YA PAMOJA (JPC) KATI YA TANZANIA NA UGANDA UMEMALIZIKA JIJINI KAMPALA, UGANDA

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania na Uganda walifungua Mkutano wa Nne wa Tume ya Kudumu ya Pamoja kati ya nchi hizo mbili unaofanyika leo tarehe 19 Januari 2022 jijini Kampala, Uganda.

Mkutano huu wa siku moja ulitanguliwa na Mkutano Ngazi ya Wataalamu uliofanyika tarehe 17 Januari 2022 na kufuatiwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu uliofanyika tarehe 18 Januari 2022.

Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano huu unaongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb.) ambaye ameambatana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.), Naibu Waziri wa  Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Mhandisi Geodfrey Kasekenya(Mb.), Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe (Mb.), Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Antony Mavunde (Mb.) na Naibu Waziri Wizara ya Nishati, Mhe. Steven Byabato (Mb.).

Mkutano wa Nne umejadili na kutathimini masuala mbalimbali ya utekelezaji kwenye maeneo ya ushirikiano yaliyokubaliwa baina ya nchi hizi. Maeneo hayo ni pamoja na; Siasa na Diplomasia, Ulinzi na Usalama, Fedha na Uchumi, Nishati, Habari na Mawasiliano, Kilimo, Maendeleo na ujenzi wa Miundombinu, Elimu na Mafunzo, Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Utalii, Kilimo na Uvuvi, Maji na Mazingira, Afya na Elimu.

Akifungua Mkutano huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula ameishukuru Jamhuri ya Uganda kwa mapokezi mazuri ya kidugu na uratibu mzuri wa mkutano huo.

Pia, akaeleza imani aliyonayo kwa wajumbe wa mkutano huu ambao walijadili na kutoa maamuzi katika maeneo mbalimbali ya utekelezaji yaliyowasilishwa kwa ustawi wa mataifa haya, sambamba na kuanzisha maeneo mapya ya ushirikiano kupitia majadiliano hayo.

“Serikali zetu zimejikita katika kuhakikisha vikwazo vya biashara vinatatuliwa na hili linafanyika mara kwa mara katika ngazi zote za utekelezaji na maamuzi”, alisema Balozi Mulamula

Pia akafafanua kuwa kupitia ziara za viongozi wetu wakuu Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Yoweri Kaguta Museven, Rais wa Jamhuri ya Uganda changamoto na tozo mbalimbali za kibiashara zilitatuliwa ili kukuza na kuinua urali wa biashara baina ya Tanzania na Uganda.

Kwa upande wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Mhe. Jen. Jeje Odongo alieleza kuwa Mkutano huu utajadili na kufanya makubaliano katika sekta mbalimbali za ushirikiano zitakazosainiwa katika nyakati tofauti kwa lengo la kufungua maeneo mapya ya ushirikiano ili kuendelea kuimarisha ushirikiano na kutumia fursa zilizopo kwa manufaa ya wananchi wa Nchi hizi mbili.

Aidha, akafananua mkutano huu utajadili hali ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika nchi hizi mbili pamoja na mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) unaojengwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Reli hii ya kisasa (SGR) itapunguza adha za usafiri kwa Nchi za Afrika Mashariki sambamba na kuziunganisha nchi za ukanda huo na kupunguza gharama za kibiashara”, alisema Jen. Odongo.

Kwa pamoja viongozi hao walizitaka sekta zilizopo katika maeneo hayo ya ushirikiano kuhakikisha wanatekeleza na kutatua kwa wakati masuala yote ya kitendaji ili kuruhusu sekta hizo kustawi kiuchumi na kuinua maisha ya Wananchi.

====================================================================

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akihutubia katika ufunguzi wa Mkutano wa Nne wa Tume ya Kudumu ya Pamoja kati ya Tanzania na Uganda uliofanyika tarehe 19 Januari 2022 Kampala, Uganda.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Mhe. Jen. Jeje Odongo akihutubia katika ufunguzi wa Mkutano wa Nne wa Tume ya Kudumu ya Pamoja kati ya Tanzania na Uganda uliofanyika tarehe 19 Januari 2022 Kampala, Uganda.

Mhe. Waziri Mulamula pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Stergomena Tax wakifatilia majadiliano ya mkutano huo.

Mhe. Jen. Odongo, Mawaziri kutoka katika sekta za ushirikiano na ujumbe wa Wataalamu wakifuatilia majadiliano.

Kutoka kushoto Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Antony Mavunde na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Steven Byabato wakifuatilia Mkutano.

Kutoka kulia Naibu Waziri wa  Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Mhandisi Geodfrey Kasekenya na Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe wakifuatilia majadiliano.


Mawaziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Balozi Mulamula na Jen. Odongo wakionesha Hati za Muhtasari wa Makubaliano walizosaini mara baada ya kukamilisha majadiliano ya mkutano huo.
Picha ya Pamoja Mawaziri wa Mambo ya Nje,  Mhe. Balozi Mulamula na Jen. Odongo

Picha ya Pamoja Mawaziri  wa Mambo ya Nje na Mawaziri wengine wa kisekta walioshiriki kwenye majadiliano ya Mkutano huo.