Picha ya pamoja |
Monday, March 28, 2022
TANZANIA, LIECHTENSTEIN KUWEKEZA KATIKA KILIMO HAI
Na Mwandishi wetu, Dar
Tanzania na Liechtenstein zimekubaliana kuweka mpango mkakati wa kuwekeza katika kilimo hai na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo katika mikoa ya Morogogo na Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam wakati alipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Liechtenstein Mhe. Dominique Hasler ambaye yuko nchi kwa ziara ya kikazi.
Katika mazungumzo hayo viongozi hao wamekubalia kuangazia maeneo mapya ya ushirikiano katika sekta za Utalii, Viwanda, na Elimu, hususan kumuendeleza mtoto wa kike katika masomo ya sayansi na teknolojia.
“Tumekubaliana mara baada ya ziara yake tuweze kuangazia namna gani tunaweza kudumisha na kuendeleza maeneo mapya ya ushirikiano baina yetu kwa maslahi ya Tanzania na Liechtenstein,” Amesema balozi Mulamula.
Nae Waziri wa Mambo ya Nje wa Liechtenstein Mhe. Dominique Hasler amesema Liechtenstein ina uhusiano imara na wa siku nyingi, na tumekuwa tukisaidia miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo hapa nchini Tanzania hivyo kuja kwetu hap ani kuja kuiona miradi hiyo na kutuwezesha kujadiliana kwa pamoja ni namna gani tunaweza kuendele kushirikiana katika miradi hiyo.
"Katika kikao changu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania tumejadili mambo mbalimbali ya ushirikiano baina ya nchi zetu, lakini kubwa kabisa tumekubaliana kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano," Amesema Waziri Hasler.
Waziri Hasler akiwa nchini atatembelea miradi mbalimbali ya kilimo hai inayotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Tanzania na Liechtenstein kupitia Sustainable Agriculture Tanzania (SAT) katika mkoa wa Morogoro na Dodoma.
Mjumbe aliyeambatana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Liechtenstein Mhe. Dominique Hasler akifafanua jambo wakati wa kikao |
Friday, March 25, 2022
NGORONGORO YAIKUTANASHA SERIKALI NA MABALOZI, WAKUU WA MASHIRIKA YA KIMATAIFA NA WADAU WA MAENDELEO
Na Waandishi Wetu, Dar
*Yasema inazingatia Haki za Binadamu na kuwawezesha wale watakaoondoka kwa hiyari katika maeneo hayo
Serikali imesema haitamzuia mtu yeyote anayetaka kuondoka kwa hiyari katika eneo la Ngorongoro kwenda kuishi popote nchini na kuwataka wadau wengine kutowazuia wanaotaka kuondoka katika eneo hilo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Damasi Ndumbaro ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Mabalozi, Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa na Wadau wa Maendeleo kuhusu mpango wa serikali wa kutafuta suluhu ya kudumu katika eneo la Ngorongoro na Loliondo na kuongeza kuwa itawawezesha wale wote wanaotaka kuondoka kwa hiyari katika maeneo hayo.
Dkt. Ndumbaro amewaeleza Mabalozi hao kuwa mpaka sasa jumla ya kaya 164 sawa na watu 915 wamejiandikisha kuondoka Ngorongoro kwa hiyari na kwenda kuishi katika maeneo mbadala watakayopewa na Serikali ikiwa ni pamoja na kuwajengea nyumba ama kuwalipa fidia.
Waziri Ndumbaro ameongeza kuwa Serikali imeamua kuchukua hatua hiyo ili kuzipatia ufumbuzi changamoto zilizojitokeza katika eneo la Ngorongoro ikiwa ni kuongeza kwa binadamu kutoka 8000 mwaka 1959 hadi kufikia 110,000 kwa sasa ikiambatana na ongezeko la mifugo kutoka mifugo 200,000 mwaka 1959 hadi kufikia mifugo 1,000,000 kwa sasa jambo linaloathiri ikolojia na uhifadhi, maendeleo ya utalii na maendeleo ya jamii ya wanaoishi Ngorongoro.
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiwa ameambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Fatma Rajabu amesema dhumuni la kuwaita Mabalozi hao pamoja na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa ni katika jitihada zinazofanywa na Serikali kuhakikisha Mabalozi na wadau wa Maendeleo wanapata taarifa sahihi kuhusu suala la Ngorongoro na Loliondo kutokana na kugubikwa na upotoshaji.
Ameongeza kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeweka utaratibu wa kuzikutanisha Wizara za kisekta na Mabalozi, Wakuu wa Masharika ya Kimataifa na Wadau wa Maendeleo mara moja kila baada ya miezi 3 lengo likiwa ni kutoa fursa kwa Serikali kutoa ufafanuzi wa masuala mtambuka ya serikali na kuruhusu majadiliano yanayosaidia wadau hao kuwa na taarifa sahihi pamoja na kuwa na uelewa wa pamoja.
Akichangia mjadala huo, Balozi wa Ujerumani nchini, Mhe. Regina Hess ameunga mkono jitihada za Serikali za kulinda uhifadhi na mazingira katika eneo la Ngorongoro ili kukabiliana na athari zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Damasi Ndumbaro akiongea na Mabalozi, Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa na Wadau wa Maendeleo (hawapo pichani) Jijini Dar es Salaam |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiongea na Mabalozi, Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa na Wadau wa Maendeleo (hawapo pichani) Jijini Dar es Salaam |
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma Rajab akiongea na Mabalozi, Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa na Wadau wa Maendeleo Jijini Dar es Salaam |
Balozi wa Denmark nchini, Mhe. Mette Norgaard Spandet akitoa maoni yake wakati wa mjadala kuhusu jitihada za Serikali za kulinda uhifadhi na mazingira katika eneo la Ngorongoro |
Balozi wa Ujerumani nchini, Mhe. Regina Hess akichangia mjadala kuhusu jitihada za Serikali za kulinda uhifadhi na mazingira katika eneo la Ngorongoro |
Balozi wa Uingereza nchini, Mhe. David Concar akichangia mjadala kuhusu jitihada za Serikali za kulinda uhifadhi na mazingira katika eneo la Ngorongoro |
Sehemu ya Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa pamoja na Wadau wa Maendeleo wakifuatilia mkutano |
Sehemu ya Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa pamoja na Wadau wa Maendeleo wakifuatilia mkutano |
Mawaziri, Makatibu Wakuu, Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa pamoja na Wadau wa Maendeleo katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza mkutano wao leo Jijini Dar es Salaam |
MKUTANO WA 15 WA BARAZA LA KISEKTA LA KILIMO NA USALAMA WA CHAKULA WAHITIMISHWA JIJINI DAR ES SALAAM
Mawaziri walioshiriki Mkutano wa 15 wa Baraza la Kisekta la Kilimo na Usalama wa Chakula la Jumuiya ya Afrika Mashariki wakisaini ripoti ya Mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam. |
Sehemu ya Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia Mkutano wa 15 wa Baraza la Kisekta la Kilimo na Usalama wa Chakula la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliokuwa uliofanyika jijini Dar es Salaam. |
Thursday, March 24, 2022
WAZIRI MULAMULA AMUAGA BALOZI WA UGANDA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akionge na Mabalozi (wastaafu) katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam |
Wednesday, March 23, 2022
WAZIRI MULAMULA AFUNGUA MKUTANO WA WANAWAKE KATIKA DIPLOMASIA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akifungua Mkutano wa Women in Diplomacy uliofanyika jijini Dar es Salaam |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akifurahia jambo wakati akizungumza na Balozi Gertrude Mongela kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Women in Diplomacy |
TANZANIA YAFAFANUA MSIMAMO WAKE KUHUSU MGOGORO WA URUSI NA UKRAINE
Na Mwandishi Wetu, Dar
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa ufafanuzi kuhusu sababu ya kupiga kura ya kutofungamana na upande wowote katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu mgogoro unaoendelea kati ya Urusi na Ukraine huku ikisisitiza pande zote mbili kutafuta suluhu katika meza ya mazungumzo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) ametoa ufafanuzi huo wakati akifanya mahojiano na mojawapo ya vyombo vya Habari kutoka China na kuongeza kuwa Sera ya Tanzania kuhusu namna ya kutatua changamoto za migogoro inapojitokeza ni kwa kutumia njia za kidiplomasia.
Balozi Mulamula amesisitiza kuwa Sera ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haijabadilika tangu uhuru na kuongeza kuwa Tanzania inaamini hakuna mgogoro ambao hauwezi kutatulika hasa panapokuwepo na utashi na nia njema ya kumaliza mgogoro na kwamba njia ya kidiplomasia ndio chaguo sahihi kwa Tanzania kuhusu namna bora ya kumaliza mgogoro kati ya Urusi na Ukraine.
“Sisi msimamo wetu na Sera yetu na msingi wetu wa Sera yetu ya Mambo ya Nje ni kutofungamana na pande zozote, hivyo kutokupiga kura ni kuonesha msimamo wa Tanzania,” amesema Balozi Mulamula
Alipoulizwa endapo Tanzania imeathirika na vita inayoendelea kati ya Urusi na Ukraine, Balozi Mulamula amesema madhara yanayotokana na vita hiyo yanajionesha dhahiri huku akitaja baadhi ya madhara hayo kwa baadhi ya wanafunzi wa kitanzania waliokuwa wanasoma nchini Urusi kukatisha masomo yao na kurejea nchini wakisubiria vita kumalizika pamoja na ongezeko la bei ya petroli na gesi duniani.
Kutokana na vita inayoendelea kati ya Ukraine na Urusi Tanzania ililazimika kuwaondoa raia wake nchini Ukraine hususan wanafunzi takribani 300 waliokuwa wakisomea masuala ya udaktari nchini humo
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akihojiwa na mmoja wa waandishi wa habari kutoka China |
Tuesday, March 22, 2022
MKUTANO WA 15 WA BARAZA LA KISEKTA LA KILIMO NA USALAMA WA CHAKULA KUFANYIKA DAR ES SALAAM
Meza kuu wakifuatilia Mkutano wa 15 wa Baraza la Kisekta la Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea katika Hoteli ya Four Points jijini Dar es Salaam. |
Mkutano wa 15 wa Baraza la Kisekta la Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ukiendelea katika Hoteli ya Four Points jijini Dar es Salaam |
Monday, March 21, 2022
TANZANIA, EU ZAKUTANA KUJADILI EPA
Na Mwandishi wetu, Dar
Serikali ya Tanzania
imekutana na Umoja wa Ulaya (EU) kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Mkataba
wa Ushirikiano wa Kiuchumi (EPA) kati ya Umoja huo na Tanzania.
Akiongea wakati wa kikao
cha wataalamu kutoka Tanzania na EU kilichofanyika Jijini Dar es Salaam, Katibu
Mkuu wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Prof. Godius Kahyarara amesema kikao
hicho kinalenga kujadili makubaliano yaliyokwama awali kutokana na Tanzania
kutokuwa tayari kuridhia baadhi vipengele vilivyomo kwenye mkataba huo.
Prof. Kahyarara amesema Tanzania
haikukubaliana na baadhi ya vipengele vya mkabata wa EPA na kuona kuwa ni
vigumu kuingia katika makubaliano ya mkataba huo kabla ya kurekebisha vipengele
hivyo.
“Tumekaa na wataalamu wetu
na wenyewe wamekuja na wataalamu wao, tutapitia kipengele kimoja baada ya kingine
na tunaamini tutafika mwisho na kama tulivyo waambia wenzetu wa EU tunaona
faida ya kufanya biashara na wao kwa maslahi ya pande zote mbili,” amesema
Prof. Kahyarara
Kwa upande wake Balozi wa
Umoja wa Ulaya nchini Mhe. Manfredo Fanti amesema majadiliano hayo yanalenga
kuangalia vipengele vya mkataba ambavyo Tanzania ilionesha mashaka katika kikao kilichopita ili kuvipatia ufumbuzi
na kusonga mbele kwa pamoja hasa ikizingatiwa kuwa Tanzania sasa inatoa kipaumbele
katika utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi.
“Itakumbukwa kuwa Tanzania
inatekeleza diplomasia ya uchumi na wawekezaji kutoka Umoja wa Ulaya wanania ya
kuja kuwekeza Tanzania na Afrika Mashariki, hivyo tukikamilisha majadiliano
haya itakuwa ni jambo lenye maslahi kwa pande zote,” Amesema Balozi Fanti.
Kikao cha leo kinatokana
na mazungumzo ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan aliyafanya alipokuwa katika ziara ya kikazi nchini Ubelgiji ambapo
alikutana na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Ulaya, Bw. Charles Michael mwezi
Februari 2022.
Balozi wa Umoja wa Ulaya
nchini Mhe. Manfredo Fanti akiongea na washiriki wa kikao (hawapo pichani), kulia
ni Katibu Mkuu wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Prof. Godius Kahyarara katika
kikao kilichofanyika Jijini Dar es Salaam
Balozi wa Umoja wa Ulaya
nchini Mhe. Manfredo Fanti akiongea na washiriki wa kikao, kulia ni Katibu Mkuu
wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Prof. Godius Kahyarara katika kikao
kilichofanyika Jijini Dar es Salaam
Kikao kikiendelea Washiriki kutoka Tanzania na Umoja wa Ulaya wakiwa katika picha ya pamoja