Thursday, November 21, 2024

NCHI ZA UKANDA WA MAZIWA MAKUU KUKUTANA ANGOLA KUJADILI HALI YA AMANI NA USALAMA

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Afrika, katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Ellen Maduhu akifuatilia kikao cha Waratibu wa Kitaifa cha Jumuiya ya Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) kilichokuwa kikiendelea jijini Luanda Angola tarehe 21 Novemba 2024. 

Watendaji na Viongozi wa sekta mbalimbali kutoka Nchi wanachama wa Jumuiya ya Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) wanatarajiwa kukutana jijini Luanda, Angola kujadili kuhusu hali ya amani na usalama katika ukanda huo kwenye mkutano utakaofanyika tarehe 24 Novemba 2024.

Mkutano huo utakao husisha Mawaziri wa Mambo ya Nje kutoka nchi Wanachama wa ICGLR unalenga kujadili na kutatua changamoto za amani na usalama katika eneo la ukanda huo hususan nchi za Jamhuri ya Sudani, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). 

Mbali na hayo mkutano huo utajadili suala la kumpata Mwenyekiti ajaye atakayeongoza Jumuiya hiyo kwa kipindi cha miaka miwili ijayo baada ya wa sasa Angola kumaliza muda wake, na kupendekeza Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya kufuatia ya wasasa kumaliza kipindi chake cha kuhudumu.

Maandalizi ya mkutano huo yalianza tarehe 11 Novemba 2024 kwa vikao mbalimbali katika ngazi ya wataalamu ikiwemo wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, Wataalamu wa masuala ya jinsia, wataalamu wa masuala ya fedha, Mawaziri wa Ulinzi na Waratibu wa Kitaifa kutoka nchi wanachama waliokutana leo tarehe 21 Novemba 2024. 

Akizungumza kwenye ufunguzi wa kikao cha Waratibu wa Kitaifa, Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya ICGLR Balozi Jao Samuel Caholo ameeleza kuwa licha ya jitihada jinazoendelea na mafanikio yaliyopatikana katika kurejesha na kudumisha hali ya amani na usalama kwenye ukanda wa maziwa Makuu, bado juhudi zaidi zinahitajika kutoka nchi wanachama ili kupata suluhu ya kudumu dhidi ya migogoro hiyo. 

Balozi Caholo ameongeza kusema kuwa suala la kulinda amani na usalama katika ukanda wa maziwa makuu ni muhimu kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya wananchi wa ukanda huo. 

Kadhalika, emetoa wito kwa nchi wanachama kupitia Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Angola kuongeza juhudi katika kushughulia hali ya kuzorota kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi za DRC na Rwanda na Burundi na Rwanda. 

“Amani na usalama katika ukanda wetu unategemea zaidi utayari na juhudi zetu wenyewe katika kutafuta suluhu ya changamoto zinazotukabili, hivyo ni mtarajio ya wengi kuwa mkutano huu muhimu utasaidia kufikia malengo ya kuwa na ukanda wenye amani ya kudumu kwa mustakabali mwema wa kizazi chetu na kijacho” Alieleza Balozi Caholo. 

Vilevile, mkutano huo utapokea na kujadili taarifa ya hali ya utendaji wa Sekretarieti ya IGCLR kwa kuangazia ufanisi wa maeneo mbalimbali ikiwemo mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2024, hali ya utoaji michango ya nchi wanachama, rasilimali watu na hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mpango mkakati wa mwaka 2022 -2026.

Katika hutua nyingine kikao hicho cha Waratibu wa Kitaifa kilichofanyika leo tarehe 21, kimetoa pole kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufatia maafaa yaliyotokana na kuporomoka kwa jengo yaliyotokea hivi karibuni katika eneo la Kariakoo, jijini Dar es Salaa. 

Aidha mkutano huo umetoa pongezi kwa Serikali ya Tanzania chini ya Uongozi wa Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuchuka hatua za haraka katika kushugulikia janga hilo ikiwemo kuokoa watu walioangukiwa na jengo na kutoa huduma muhimu ikiwemo matibabu kwa majeruhi. 

Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo ngazi ya Waratibu wa Kitafa umeongozwa Bi. Ellen Maduhu, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Afrika, katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 

ICGLR yenye makao makuu yake jijini Bujumbura, Burundi ilianzishwa mwaka 2007, na ina jumla ya Nchi Wanachama 12, ambao ni Angola, Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Kongo, DRC, Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, Sudan, Tanzania, Uganda na Zambia.
Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya ICGLR Balozi Jao Samuel Caholo akizungumza kwenye ufunguzi kikao cha Waratibu wa Kitaifa ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa Waziri wa Mambo ya Nje (RIMC) wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) unaotarajiwa kufanyika tarehe 24 Novemba 2024 jijini Luanda, Angola.
Kikao cha Waratibu wa Kitaifa cha ICGLR kikiendelea jijini Luanda, Angola
Meza Kuu wakiongoza Kikao cha Waratibu wa Kitaifa cha ICGLR kikiendelea jijini Luanda, Angola. 
Picha ya pamoja

kurugenzi Msaidizi wa Idara ya Afrika, katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Ellen Maduhu akifuatilia kikao cha Waratibu wa Kitaifa cha Jumuiya ya Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) kilichokuwa kikiendelea jijini Luanda Angola tarehe 21 Novemba 2024.

Wednesday, November 20, 2024

ANNE MAKINDA LAUNCHES SADC ELECTORAL OBSERVATION MISSION FOR NAMIBIA'S UPCOMING GENERAL ELECTIONS

The Head of the Southern African Development Community (SADC) Electoral Observation Mission (SEOM), Hon. Anne Makinda, has officially launched the SADC Mission to observe the upcoming General elections in the Republic of Namibia, scheduled for November 27, 2024.

The SADC-SEOM was officially launched in Windhoek, Namibia, on November 20, 2024.

The Head of Mission Hon Makinda was accompanied members of the Troika of the Organ on Politics, Defence, and Security Affairs from the Republics of Malawi, Zambia, and the Chair United Republic of Tanzania as well as representatives from the SADC Electoral Advisory Council and the SADC Secretariat.

Other attendees at the ceremony included heads of diplomatic missions, government officials, representatives from the Electoral Commission of Namibia, political parts, religious organizations, civil society groups, other international election observation missions, SADC election observers, and members of the media.

In her keynote address, Hon. Makinda expressed gratitude to the people of Namibia for their ongoing commitment to the democratic process and emphasized the significance of the upcoming elections in furthering democratic governance in the country.

“SADC observes elections not as a one-time event, but as part of a long-term cycle aimed at consolidating democracy and ensuring that elections are free, fair, transparent, and credible,” she stated.

Hon Makinda also said the SEOM, comprising 65 observers from eight SADC Member States (Eswatini, Botswana, Malawi, Mozambique, South Africa, Zambia, Zimbabwe, and Tanzania) will monitor various key aspects of the election, from voter registration and the functioning of the Electoral Commission of Namibia (ECN), neutrality of security forces and the accessibility of polling stations.

She said SEOM will also assess the broader political and security environment, ensuring that the conditions are conducive to peaceful and democratic elections.

Adding that  SADC Observers will be deployed across all 14 regions of Namibia to ensure comprehensive coverage of the electoral process.

The Head of SEOM emphasized that SADC’s role in election observation is far from superficial, highlighting that the mission follows a comprehensive and systematic approach, which includes monitoring election-day procedures, evaluating the legal framework, electoral management, and post-election processes.
"We do not simply observe for a few days, issue a statement, and leave; our mission is part of an ongoing effort to learn from past experiences and strengthen electoral systems for the benefit of citizens across the region." Hon. Makinda emphasized.

She said SEOM will assess Namibia’s elections based on the Revised SADC Principles and Guidelines Governing Democratic Elections (2021), which emphasize citizen participation, human rights, transparency, and fairness, and aim to ensure the integrity of the electoral process by preventing fraud, political violence, and the misuse of state resources.

The mission builds on earlier assessments by the SADC Electoral Advisory Council (SEAC) in 2023 and 2024, which reviewed Namibia’s political environment, legal framework, voter registration, ECN readiness, and provisions for election security and media coverage.

She highlighted Namibia’s strong tradition of peaceful elections, noting that the country’s transition from apartheid to independence has made it a model of peace and democracy in Southern Africa.

“Namibia has set an example for the region with its peaceful and tolerant elections, and it is essential that this tradition continues for the long-term stability of the country,” she said.


The SEOM will continue to monitor the election process closely, with a preliminary statement of observations to be released on November 29, 2024, at 11:00 am.

On behalf of Her Excellency Dr. Samia Suluhu Hassan, President of the United Republic of Tanzania and Chairperson of the SADC Organ on Politics, Defence, and Security Cooperation, Hon. Makinda urged all registered Namibian voters to participate peacefully in the elections on November 27, 2024, and called for post-election peace and respect for the results.

"This election is a critical moment for Namibia and the Southern African region, and we urge all citizens to exercise their right to vote, contribute to strengthening democracy, and ensure that the elections are peaceful, orderly, with results respected by all." Hon Makinda reiterated.

The presence of the SADC Electoral Observation Mission in Namibia underscores the region’s commitment to upholding democratic principles and electoral integrity, with SADC’s role in supporting free and fair elections being crucial to advancing peace, security, and regional integration.

 

Tuesday, November 19, 2024

BALOZI YAKUBU APOKEA UJUMBE MAALUM WA RAIS SAMIA KUTOKA KWA RAIS WA COMORO


Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Mhe. Saidi Yakubu amekutana na kuzungumza na Rais wa Comoro Mheshimiwa Azali Assoumani na kupokea ujumbe maalum wa Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoka kwa Rais  Azali Assoumani alipokutana naye jijini  Moroni.

Akizungumza na Balozi Yakubu baada ya kumkabidhi ujumbe huo maalum wa Rais Samia Mhe. Rais Azali Assoumani ameelezea kuridhishwa kwake na ushirikiano wa sekta za biashara na kijamii uliopo kati ya Tanzania na Comoro.

Mhe. Rais Azali pia alimueleza Balozi Yakubu kuwa amekutana na Marais wa Tanzania, Hayati Ali Hassan Mwinyi; Hayati Benjamin Mkapa; Mhe. Jakaya Kikwete; Hayati John Magufuli na sasa Rais Samia Suluhu Hassan na wote wameonesha upendo mkubwa kwa Comoro na anafurahi sasa kampuni za Tanzania zinakwenda kuwekeza Comoro.

Kwa upande wake, Mhe. Balozi Yakubu amemshukuru Mhe. Rais Azali kwa ushirikiano anaoupata kutoka kwa mamlaka mbalimbali nchini Comoro na hivyo kurahisisha utendaji kazi wake na kumueleza namna uwekezaji na biashara kati ya Tanzania na Comoro unavyoimarika katika siku za hivi karibuni.

BALOZI MBUNDI AFANYA MAZUNGUMZO NA MKUU WA USHIRIKIANO WA KIKANDA WA UJERUMANI

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi amekutana kwa mazungumzo na Mkuu wa Ushirikiano wa Kikanda wa Ujerumani, Bi. Julia Kronberg katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 19 Novemba, 2024.

Mazungumzo ya viongozi hao yalijikita katika kuimarisha ushirikiano wa maendeleo katika eneo la biashara, ujenzi wa miundo mbinu, afya, kujenga uwezo wa rasilimali watu, kuwainua wanawake na vijana kiuchumi.

Aidha, katika mazungumzo hayo Balozi Mbundi ameeleza kuwa Tanzania na Ujerumani zimekuwa zikishirikiana kwa karibu katika miradi ya maendeleo ambapo Shirika la Maendeleo la Ujerumani la GIZ limekuwa likichangia shughuli mbalimbali nchini na katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

‘’ Ushirikiano uliopo ni ishara ya kuendelea kukua kwa Jumuiya imara ya Afrika Mashariki kwakuwa ushirikiano huo kwasasa unatimiza miaka 20 tangu uanzishwe na umewezesha kutekelezwa kwa miradi yenye mafanikiao kupitia utaratibu maalum uliowekwa na pande zote mbili’’, alieleza Balozi Mbundi.

Pamoja na masuala mengine Balozi Mbundi ameainisha maeneo yanayohitaji usaidizi katika Jumuiya hiyo. Ameyataja maeneo hayo kuwa ni pamoja na kuwawezesha vijana katika shughuli za kilimo, kujenga uwezo kwa sekta binafsi ili kuwapa uelewa juu ya utafutaji  wa masoko na usafirishaji wa bidhaa za biashara, utunzaji wa mazingira, matumizi ya nishati safi,  na kuongeza thamani ya bidhaa za biashara kama vile ngozi.

Naye, Bi. Julia Kronberg amesisitiza kuwa GIZ kwa kushirikiana na Benki ya Dunia inaendelea kukuza na kuimarisha ushirikiano wake na EAC kwa kufadhili miradi mbalimbali katika ukanda huo.

‘’GIZ inashirikiana na Baraza la Biashara Tanzania  ambapo imekuwa ikipata fursa ya kukutana na sekta binafsi katika ukanda wa EAC na kuwawezesha wafanyabiashara wadogo wanaofanya biashara mipakani’’, alisema Bi.  Julia.

Pia, ameeleza kuwa GIZ kwa upande mwingine imewekeza kwa kiasi kikubwa katika kusaidia jitihada za kuimarisha huduma za sekta ya afya katika ukanda wa EAC na imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na Umoja wa Ulaya ili kuweka nguvu ya pamoja katika kusukuma maendeleo ya Ukanda wa Afrika Mashariki.

 

Sunday, November 17, 2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasili jijini Rio de Janeiro, Brazil

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasili jijini Rio de Janeiro, Brazil leo 16 Novemba, 2024 tayari kwa kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Kundi la G20 kufuatia mualiko wa Rais wa Brazil, Mhe. Luiz Inácio Lula da Silva.


Ajenda kuu za mkutano huu ni pamoja na Ushirikishwaji wa jamii katika mapambano dhidi ya njaa na umaskini; Mabadiliko ya nishati sambamba na kukuza maendeleo endelevu katika nyanja za uchumi, jamii, na mazingira; na Mageuzi ya mifumo ya kiutawala katika taasisi za kimataifa.


 

WAZIRI KOMBO AWASILI NCHINI ZIMBABWE KUHUÐHURIA MKUTANO WA DHARURA WA SADC


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe .Balozi Mahmoud Thabit Kombo amewasili Harare, Zimbabwe, tarehe 16 Novemba, 2024 kuhudhuria Mkutano wa Dharura wa Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) ambao unatarajiwa  kufanyika tarehe 17 - 19 November 2024.

Waziri Kombo amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mhe. IGP Mstaafu Simon Sirro.

Pia, Mhe. Kombo amekutana na Ujumbe wa Tanzania unaoshiriki mkutano huo na kupokea  taarifa ya maandalizi ya mkutano huo ambao unalenga kujadili masuala mbalimbali yanayohusu kanda hiyo hususan hali ya Ulinzi, Usalama na mikakati ya kutatua changamoto mbalimbali zinazoikumba kanda.

Aidha mkutano huo utatanguliwa na mkutano wa Kamati ya Makatibu wakuu wa SADC utakaofanyika tarehe 17 November 2024.

Saturday, November 16, 2024

MAAFISA MAMBO YA NJE WAFAIDIKA NA UZOEFU WA MABALOZI WASTAAFU


 Mafunzo ya siku tano kuhusu mawasiliano ya Kidiplomasia kwa watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki yamehitimishwa jijini Dodoma Novemba 15, 2024, huku watumishi wakitakiwa kutumia ujuzi waliopata kutoka kwa Mabalozi Wastaafu na Mahiri kuboresha utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Wakufunzi wa semina hiyo, walisisitiza umuhimu wa mafunzo yaliyotolewa kuzingatiwa na washiriki kwa kuwa mawasiliano ya kidiplomasia yanahusisha nchi na nchi, mashirika ya kikanda na kimataifa, hivyo ni jambo muhimu kwa sababu linagusa sura ya nchi. 

Mafunzo hayo yalilenga mbinu za kuandaa nyaraka za mawasiliano ya kidiplomaisa zenye ubora, matumizi sahihi ya lugha na kwa kuzingatia wakati, Mabalozi walibainisha kuwa, ili lengo hilo liweze kutimia, washiriki wametakiwa kuwa mbele ya muda kwa kufahamu yanayotokea duniani na kusoma vitabu na nyaraka nyingine ambazo zitawapa ujuzi wa aina mbalimbali ikiwemo utajiri wa misamiati.

Mabalozi walieendelea kwa kueleza kuwa utekelezaji wa majukumu utakaozingatia weledi utaifanya Wizara hiyo iendelee kuwa kiungo muhimu cha Serikali katika utekelezaji wa diplomasia ya uchumi na kuhimiza umuhimu wa diplomasia ya umma kuimarishwa ili wananchi waelewa nafasi nyeti ya Wizara katika kukuza uchumi wa nchi.

Kwa upande wao, washiriki wa mafuunzo hayo waliahidi kufanyia kazi masomo waliyoyapata ambayo kwa kiasi kikubwa yalikuwa kwa njia ya vitendo, ili nafasi ya Wizara katika nchi iendelee kuimarika kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma.

Mabalozi wastaafu walioendesha mafunzo hayo ni Balozi Bertha Semu-Somi; Balozi Mohammed Maundi; Balozi  Peter Kallaghe, Balozi Begum Taj; Balozi Tuvako Manongi na Bw. Khamisi Abdallah.

WAZIRI KOMBO APOKEA TAARIFA YA KAMATI MAALUM YA MAPITIO YA KITUO CHA DKT. SALIM AHMED SALIM


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo, (Mb), amepokea Taarifa ya  Kamati Maalum ya Wizara kuhusu mapitio ya kituo cha uhusiano wa kimataifa cha  Dkt. Salim Ahmed Salim cha Jijini Dar es Salaam. iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Balozi Khamis Sued Kagasheki. 

Katika Taarifa hiyo, Balozi Kagasheki aliwasilisha matokeo ya uchambuzi uliofanywa na Kamati na kuainisha mapungufu yaliyobainika kwenye maeneo mbalimbali na kutoa mapendekezo husika kuboresha Kituo hicho ili kikidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye katika nyanja za diplomasia na uhusiano wa Kimataifa.
Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo Mhe. Waziri Kombo aliishukuru Kamati hiyo kwa ufanisi, uzalendo, taaluma, ukweli na uwazi katika kutekeleza jukumu ililopewa.

Mhe Waziri alibainisha kuwa mapendekzo ya Kamati yatachangia kuboresha Kituo hicho na hivyo kufikia malengo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwanadiplomasia Namba Moja Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kukifanya Kituo hicho kuwa kituo cha umahiri, fikra na rejea katika kukuza wanadipolomasia wa Tanzania ili waweze kutoa mchango unaotarajiwa katika nyanja ya diplomasia na uhusiano wa kimataifa nchini na ukanda wa Afrika.

Mhe. Waziri pia aliainisha utayari wa Wizara katika kutekeleza mapendekezo ya Kamati ili kukifanya Kituo hicho kiakisi taswira na  kuenzi kazi na mchango mkubwa wa Mwanadiplomasia Nguli nchini Balozi Dkt. Salim Ahmed Salim alizofanya na kuutoa katika diplomasia ya Tanzania, Bara la Afrika, Umoja wa Mataifa na ulimwenguni kwa ujumla. 

Balozi Kombo aliwahakikishia wajumbe wa Kamati hiyo kuwa, Wizara chini ya uongozi wake itaandaa mpango kazi wa kutekeleza mapendekezo yao kwa kuaza na maandalizi ya Mfumo wa Kisheria ambao utakamilika mapema ili kuleta mageuzi ya kweli.

Kamati hiyo iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ina wajumbe sita ikiongozwa na Balozi Khamis Sued Kagasheki kama Mwenyekiti, wajumbe wengine ni Balozi Dkt. Ramadhan Kitwana Dau; Balozi Dkt. Salim Othman Hamad; Profesa Marcellina Mvula Chijoriga; Bw. Kadari Lincoln Singo na CPA. Asumpta Marcel Muna ilianza utekelezaji wa Majukumu yake Mwezi Aprili, 2024.

Kamati hiyo ilianisha masuala yanayopaswa kufanyiwa kazi kuwa ni umuhimu wa kuweka mfumo mpya wa kisheria na umiliki wa Kituo; Malengo, Programu za Mafunzo na  Wadau wa Kituo. Aidha, mapendekezo mengine yaligusa Uhusiano kati ya Wizara Mama na Kituo; Uongozi, Ajira na Maendeleo ya Watumishi; Mfumo wa Bajeti na Utawala; Miundombinu na Mazingira ya Kujifunzia na Kufundishia. 

Mengine ni Kuimarisha Ushirikiano na Ubia (partnerships) baina ya Kituo wadau wengine ndani na nje; Mpango  wa Biashara wa Kituo (Business Model ) utakoondoa utegemezi wa Serikali na kuboresha muundo wa Wizara Mama na Kada ya Maafisa Mambo ya Nje na Kada Nyingine.

 

NAIBU WAZIRI LONDO ASHIRIKI MKUTANO WA 45 WA SCTIFI


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikiq masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Dennis L. Londo ameshiriki Mkutano wa 45 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji la Afrika Mashariki (SCTIFI) uliofanyika tarehe 15 Novemba, 2024 jijini Arusha.

Aidha, Mawaziri wengine waliohudhuria Mkuyano huo ni pamoja na Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb.);Waziri wa Viwanda na Biashara  na Mhe. Shaban Omary; Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar.

Mkutano huo ambao madhumuni yake ni kujadili namna bora ya kuboresha na kuweka mazingira mazuri ya biashara baina ya Nchi wanachama wa EAC, pia umejadili taarifa ya wataalamu kuhusu masuala mbalimbali yenye maslahi kwa Taifa ikiwemo masuala ya Forodha, Biashara, Viwango na Uzalishaji wa Bidhaa, Uwekezaji na Ushindani.


Friday, November 15, 2024

MAAFISA MAMBO YA NJE WAFAIDIKA NA UZOEFU WA MABALOZI WASTAAFU


Mafunzo ya siku tano kuhusu mawasiliano ya Kidiplomasia kwa watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki yamehitimishwa jijini Dodoma Novemba 15, 2024, huku watumishi wakitakiwa kutumia ujuzi waliopata kutoka kwa Mabalozi Wastaafu na Mahiri kuboresha utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

 
Wakufunzi wa semina hiyo, walisisitiza umuhimu wa mafunzo yaliyotolewa kuzingatiwa na washiriki kwa kuwa mawasiliano ya kidiplomasia yanahusisha nchi na nchi, mashirika ya kikanda na kimataifa, hivyo ni jambo muhimu kwa sababu linagusa sura ya nchi. 

Mafunzo hayo yalilenga mbinu za kuandaa nyaraka za mawasiliano ya kidiplomaisa zenye ubora, matumizi sahihi ya lugha na kwa kuzingatia wakati, Mabalozi walibainisha kuwa, ili lengo hilo liweze kutimia, washiriki wametakiwa kuwa mbele ya muda kwa kufahamu yanayotokea duniani na kusoma vitabu na nyaraka nyingine ambazo zitawapa ujuzi wa aina mbalimbali ikiwemo utajiri wa misamiati.

Mabalozi walieendelea kwa kueleza kuwa utekelezaji wa majukumu utakaozingatia weledi utaifanya Wizara hiyo iendelee kuwa kiungo muhimu cha Serikali katika utekelezaji wa diplomasia ya uchumi na kuhimiza umuhimu wa diplomasia ya umma kuimarishwa ili wananchi waelewa nafasi nyeti ya Wizara katika kukuza uchumi wa nchi.

Kwa upande wao, washiriki wa mafuunzo hayo waliahidi kufanyia kazi masomo waliyoyapata ambayo kwa kiasi kikubwa yalikuwa kwa njia ya vitendo, ili nafasi ya Wizara katika nchi iendelee kuimarika kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma.

Mabalozi wastaafu walioendesha mafunzo hayo ni Balozi Bertha Semu-Somi; Balozi Mohammed Maundi; Balozi  Peter Kallaghe, Balozi Begum Taj; Balozi Tuvako Manongi na Bw. Khamisi Abdallah.


 

Thursday, November 14, 2024

NAIBU WAZIRI LONDO ASISITIZA NGUVU YA PAMOJA KATIKA KUYAFIKIA MAENDELEO ENDELEVU

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dennis Londo (Mb.) akishiriki Mkutano wa Kwanza wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika na Urusi uliofanyika tarehe 8 na 9 Novemba, 2024 jijini Sochi, Urusi. 


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Dennis Londo amesisitiza umuhimu wa nguvu ya pamoja katika kumaliza changamoto za kidunia na kuleta ustawi katika jamii ili kuyafikia maendeleo endelevu.

Msisitizo huo ameutoa alipokuwa akitoa salamu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo katika Mkutano wa Kwanza wa Mawaziri wa Mambo ya Nje kutoka nchi za Afrika na Shirikisho la Urusi uliofanyika tarehe 9 hadi 10 Novemba, 2024 mjini Sochi, Urusi na kuongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Shirikisho la Urusi, Mhe. Bogdanov Mikhail Leonidovich.

Pamoja na salamu hizo Mhe. Londo ameeleza kuwa Nchi za Afrika na Urusi zimekuwa na historia nzuri tangu enzi za harakati za ukombozi wa bara hilo ambapo nchi ya Urusi ilisaidia nchi mbalimbali barani Afika ili kupata Uhuru. Aidha, Ushirikiano huo umendelea kwa  kushirikiana katika kutatua  changamoto mbalimbali za kidunia ikiwemo kukosekana kwa amani, usawa na kutojitosheleza,  kadhalika kushirikiana   kutatua  migogoro ya kiuharifu, ugaidi na vita vinavyopelekea kupoteza maisha ya watu wake wasio na hatia. 

Vilevile, Mhe. Londo ameleza kuwa njaa, magonjwa ya kuambukiza na umasikini vimekuwa vihatarishi vya usalama kwa nchi hizo na hivyo ili kupata suluhisho la changamoto hizo unahitajika ushirikiano imara kutoka pande zote utakaoenda sambamba na maono ya pamoja ya kiongozi na kiutawala.

‘’ Mkutano huu unaweza kuweka mikakati ya utatuzi wa changamoto tunazopitia na kuidhihirishia dunia kuwa ushirikiano imara unaweza kumaliza changamoto za pamoja ambazo zimekuwa kikwazo katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu kwa ustawi wa maisha ya watu wetu na Taifa kwa ujumla’’, alisisitiza Mhe. Londo.

Pia, alieleza kuwa kufanikiwa kwa jitihada hizo za umoja na mshikamano kutapelekea kuelekeza nguvu ya pamoja katika maeneo ya kimkakati ya ushirikiano ikiwemo uwekezaji katika usalama wa chakula, biashara, ushirikiano wa kiuchumi, kushirikiana kumaliza ugaidi, kuimarisha sekta ya afya, ulinzi, na kujenga uwezo katika masuala ya kidijitali na teknolojia.

Pamoja na masuala mengine, Mhe. Londo ameeleza nia ya dhati ya Tanzania ya kushirikiana na Urusi na Afrika katika kukuza biashara na uwekezaji na kwamba katika miaka mitano iliyopita ushirikiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Urusi umekua kutoka dola za kimarekani 54,243,713 mwaka 2019 hadi dola za kimarekani 390,388,000 mwaka 2023.

Aidha, ameeleza kuwa kuwepo kwa utaratibu wa pamoja wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) umekuwa kichocheo cha kukuza biashara barani Afrika kwa kuondoa tozo, kukuza viwanda, kukuza biashara na uwekezaji ndani ya Afrika na kuleta ajira miongoni mwa vijana ambao ndio nguvu kazi ya nchi hizo. 

Urusi imekuwa ikisafirisha bidhaa zake barani Afrika mara 5 zaidi ya Afrika, na kwamba hii ni moja ya changamoto inayopelekea kushuka kwa maendeleo ya biashara na kiuchumi. Akasisitiza kuwa Urusi inaweza kuwekeza Afrika kupitia kampuni zake za biashara na uwekezaji ambazo zitasaidia kukuza viwanda vya uzalishaji vya Afrika, kuijengea Afrika uwezo katika masuala ya kiufundi na kuanzisha taasisi imara na zenye nguvu kibiashara.

Hata hivyo, inakadiriwa dola za kimarekani Trillion 3 katika soko huru la Afrika zinaweza kumaliza umasikini, kuleta usawa na kukuza uchumi na kuiweka Afrika katika ukuaji jumuishi na endelevu.

Pia aliishukuru Serikali ya Urusi kwa kauli yake ya kuendelea kuisaidia Afrika katika suala la kujenga uwezo kwenye biashara na teknolojia hususan katika sekta za uzalishaji ambazo zitaiwezesha Afrika kuzalisha bidhaa zenye ubora na zinazokidhi vigezo vya kimataifa.


 

NAIBU WAZIRI LONDO AKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA UBELGIJI

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Dennis Londo amekutana na kuzungumza na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo na Misaada ya Kibinadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Falme ya Ubelgiji Mhe. Heidy Rombouts. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.


Katika mazungumzo yao viongozi hao wamepongeza ushirikiano wa maendeleo uliopo kati ya Tanzania na Ubelgiji ambao tarehe 14 Novemba, 2024 umetimiza miaka 40 tangu kuanzishwa kwake.


Miaka 40 ya ushirikiano huo imeshuhudia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika nyanja mbalimbali za Elimu, Afya na Usafirishaji. Mhe. Londo pia ameishukuru Serikali ya Ubelgiji kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini na kutumia kikao hicho kuihakikishia Ubelgiji  dhamira na hatua za Serikali ya Tanzania kukamilisha miradi mikubwa ya kimkakati.


Mhe. Londo ametoa rai kwa Serikali ya Ubelgiji kuwekeza katika miradi mikubwa ya kimkakati inayoendelea kutekelezwa nchini.


Kwa upande wake Mhe. Rombouts ameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania na kuishukuru Tanzania kwa kuwa ndau mkubwa wa ushirikiano wa kimaendeleo.


Viongozi hao  wameahidi kuendelea kudumisha ushirikiano na kuzungumza mara kwa mara  katika masuala mbalimbali.
 

    Sunday, November 10, 2024

    Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SEOM) wakutana na Wakuu wa Misheni za Uangalizi wa Uchaguzi wa Kimataifa

    Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SEOM), Mheshimiwa Mohamed Chande Othman kwenye picha ya pamoja na Wakuu wa Misheni za Uangalizi wa Uchaguzi za Kimataifa za Umoja wa Afrika, Umoja wa Nchi Zinazozungumza Kifaransa pamoja na Jukwaa la Uangalizi wa Uchaguzi wa Kusini mwa Afrika



    Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SEOM), Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akiongoza kikao cha wadau pamoja na uongozi wa SEkretarieti ya SADC na Wajumbe wa SADC TROIKA na SEAC. 


    Viongozi wa Dini wakifanya mawasilisho ya hoja mbalimbali wakati wa mkutano wa pamoja na SEOM, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo.


    Mkuu wa Misheni  ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Umoja wa Afrika na msaidizi wake, wakifuatilia kwa karibu mawasilisho wakati wa Mkutano wa pamoja na SEOM

    Mkuu wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SEOM), Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akizungumza na Mwakilishi wa Wanataaluma kutoka Chuo Kikuu cha Mauritius ambaye naye aliwasilisha maoni yake juu ya mwenendo wa uchaguzi nchini humo. 


    Mhe. Lisa Simrique Singh, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Mauritius akifananua jambo kuhusu mchango wa ushirikiano wa kimataifa  kwenye michakato ya kidemokrasia nchini humo.



    Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia mikutano ya wadau.


    Mkuu wa Misheni  ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Umoja wa Nchi zinazozungumza Kifaransa akifuatilia mazungumzo kwenye kikao cha pamoja cha Misheni za Uangalizi wa Uchaguzi za Kimataifa.


    Friday, November 8, 2024

    MAWAZIRI EAC KUONGEZA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIPANGO NA MAKUBALIANO



    Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, IKULU Zanzibar Mhe. Ali Suleiman Ameir akifuatilia Mkutano wa 34 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango uliofanyika katika Makao Makuu ya Jumuiya jijini Arusha tarehe 8 Novemba 2024. 

    Mawaziri wanaosimamia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango katika Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wamekubaliana kuongeza kasi ya utekelezaji wa mipango, maagizo na makubaliano mbalimbali yaliyofikiwa katika Jumuiya.

    Hayo yamejiri katika Mkutano wa 34 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango uliofanyika leo tarehe 08 Novemba 2024 katika Makao Makuu ya Jumuiya jijini Arusha. 

    Miongoni mwa masuala hayo ni pamoja na utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo inahusisha vipengele mbalimbali ikiwemo uondoaji wa tozo na ada katika shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo usafirishaji, biashara na ajira. 

    Suala jingine ni la uondoaji wa vikwazo visivyo vya kiforodha katika biashara, ambapo licha ya kuripotiwa kuwa jumla ya vikwazo 274 vimeondolewa tangu mwaka 2007 wamekubaliana kuendelea kubaini vikwazo ambavyo havijafanyiwa kazi kikamilifu sambamba na uharakishwaji wake katika kuvitatua ili kuwarahishia wananchi katika Jumuiya kuendesha shughuli zao za kiuchumi kwa ufanisi na tija zaidi. 

    Agenda nyingine zilizojadiliwa katika mkutano huo ni; Taarifa ya Utekelezaji wa Utatu wa Pamoja wa COMESA-EAC-SADC, Maandalizi ya Mkakati wa Saba (7) wa Maendeleo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (2026/2027- 2030/31) na Hadidu za Rejea za Dira ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Mwaka 2050, taarifa ya maandalizi ya maadhimisho ya miaka 25 ya kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Mapitio ya Utekelezaji wa Mkakati wa Sita (6) wa Maendeleo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (2021/2022- 2025/26).

    Mkutano huo wa 34 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika kwa njia mseto (video na ana kwa ana) na kuhudhuriwa na Nchi Wanachama wote wa Jumuiya, ulitanguliwa na Mkutano wa ngazi ya Wataalamu uliofanyika tarehe 4-6 Novemba, 2024 na kufuatiwa na Makatibu Wakuu uliofanyika tarehe 7 Novemba 2024. 

    Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo umeongozwa na Mhe. Ali Suleiman Ameir, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, IKULU Zanzibar.
    Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki Balozi Stephen P. Mbundi akiongoza Mkutano wa 34 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango, Novemba 8, 2024


    Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia Mkutano wa 34 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango uliokuwa ukiendelea jijini Arusha.
    Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia Mkutano wa 34 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango uliokuwa ukiendelea jijini Arusha.
    Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia Mkutano wa 34 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango uliokuwa ukiendelea jijini Arusha.

    Sehemu ya ujumbe kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifuatilia Mkutano wa 34 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango uliofanyika katika Makao Makuu ya Jumuiya jijini Arusha tarehe 8 Novemba 2024. 

    TAARIFA KWA UMMA



     

    Thursday, November 7, 2024

    MAKATIBU WAKUU EAC WAKUTANA JIJINI ARUSHA

            Tanzania yaendelea kuaminiwa kuongoza mikutano ya Jumuiya
    Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki Balozi Stephen P. Mbundi akiongoza Mkutano wa 34 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango ngazi ya makatibu wakuu uliofanyika tarehe 7 Novemba 2024

    Makatibu Wakuu wanaosimamia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango katika Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wamekutana leo tarehe 7 Novemba 2024 jijini Arusha, ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa 34 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango unaotarajiwa kufanyika jijini humo tarehe 8 Novemba 2024.

    Mkutano huo umeongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki Balozi Stephen Mbundi ambaye aliteuliwa na Jamhuri ya Sudani Kusini kuongoza mkutano huo muhimu kwa niaba yao.

    Makatibu Wakuu hao umepitia na kupitisha agenda mbalimbali zitakazowasilishwa kwenye Mkutano wa 34 wa Baraza la Mawaziri, baada ya kupokea taarifa iliyowasilishwa kwao na Wataalamu waliokutana tarehe 4 - 6 Novemba 2024. 

    Taarifa ya Wataalamu iliyowasilishwa imeelezea hali na hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Viongozi Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya na masuala mbalimbali yaliyokubaliwa katika mikutano iliyopita. 

    Masuala hayo ni pamoja na utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki ikijumuisha taarifa ya uondoaji wa vikwazo visivyo vya kiforodha, Taarifa ya Utekelezaji wa Utatu wa Pamoja wa COMESA-EAC-SADC, Mapendekezo ya Vipaumbele vya Mpango na Bajeti ya Jumuiya kwa mwaka wa Fedha 2025/2026, Mapitio ya Utekelezaji wa Mkakati wa Sita (6) wa Maendeleo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (2021/2022- 2025/26) na Taarifa ya Maandalizi ya maadhimisho ya miaka 25 ya kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki. 
    Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayesimamia masuala ya Afrika Mashariki Balozi Stephen P. Mbundi akiongoza Mkutano wa 34 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango ngazi ya makatibu wakuu uliofanyika tarehe 7 Novemba 2024
    Mkutano ukiendelea
    Mkurugenzi wa Sera na Mipango katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Justin Kisoka akichangia kwenye Mkutano 34 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango unaofanyika jijini Arusha.

    Mkurugenzi wa Siasa, Ulinzi na Usalama Bi. Mwanamridu Amity Jumaa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akifuatilia Mkutano.
    Sehemu ya ujumbe wa Tanzania ukifuatilia Mkutano 34 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango unaofanyika jijini Arusha.
    Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathimini Bw. Haji Janabi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akifuatilia Mkutano.
    Sehemu ya ujumbe wa Tanzania ukifuatilia Mkutano 34 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango unaofanyika jijini Arusha.

    Mkutano ukiendelea