Vice President of The United Republic of Tanzania (red tie), Dr. Mohamed Gharib Bilal with other delegates observe a minute of silence in honor of Brigadier Mbita during SADC Summit in Harare. |
Wednesday, April 29, 2015
SADC Stops for Mbita
SADC Heads Of State adopt Industrilization Strategy
Vice President of The United Republic of Tanzania, H.E Dr. Mohamed Gharib Bilal (R) represented President Jakaya Mrisho Kikwete at Summit. |
Part of Heads of State and Government who attended the Summit follow up the opening statement. Right is the President of South Africa, H.E Jacob Zuma |
A Cultural group entertains the Heads of State and Government and other delegates in the Conference hall. |
Heads of state of the Southern African Development Community (SADC) today adopted an Industrial Development Strategy to leverage the region's resources for sustainable development The strategic plan and roadmap was developed by a Ministerial Task Force mandated by the Heads of State last August.
It is a three-phase programme emphasizing efficient use of resources, value edition, diversification and competitiveness to propel the region into a high tech industrial entity by 2063.
The summit directed secretariat to compile the requisite budget and the Ministerial Council to prepare implementation plan. The Heads of State also approved revision of the Indicative Regional Development Plan, which now gives industrial development top priority.Development of infrastructure, including energy, water, roads and railways and ICT is ranked second while peace and security is third, followed by social services.
The President of the United Republic of Tanzania, H.E. Jakaya Kikwete, was represented by the Vice-President, Dr. Mohamed Gharib Bilal at the Summit, which was attended for the first time by newly elected Presidents Edgar Lungu of Zambia, Philip Nyusi of Mozambique, Hage Geingob of Namibia and Lesotho Prime Minister Pakalitha Mosisili.
The Summit chaired by Zimbabwe President Robert Mugabe was also attended by the President South Africa , Jacob Zuma, King Mswati of Swaziland and Mauritius Prime Minister Anerood Jugnauth.
The Heads of State and Government Further endorsed a plan to inaugurate the tripartite Free Trade Area (FTA) combining the SADC, EAC and COMESA blocks in June.
They agreed that the creation of a continental FTA earlier scheduled for 2017 be pushed back to 2020.
In her remarks to the Summit, the SADC Executive Secretary, Dr. Stergomena Lawrence Tax, said the Industrial Development Plan would boost the region's gross product and income per capital.
Chairman Mugabe said member states should brace to finance the plan because western countries were unlikely to help. "Those who benefit from our underdevelopment cannot be expected to help us," he said.
He lamented that although SADC countries ranked highly in global mineral and agricultural output, more than two thirds of their population was below the poverty line.
President Mugabe formerly handed over the Regional Peace Training Centre (RPRC) facility to Dr. Tax as part of the Summit opening ceremony.
The facility for the training of military personnel, police and civilians has been donated to SADC by the Zimbabwe government.
Afrika yamuaga Marehemu Brigedia Generali Hashim Mbita
Waziri Membe akimpa pole Mjane wa Marehemu Brigedia Generali Hashim Mbita, Mama Ngeme Mbita. |
Mhe. Membe akimpa pole mmoja wa watoto wa Marehemu Brigedia Generali Hashim Mbita wakati wa shughuli za kitaifa za kuaga mwili zilizofanyika katika Viwanja vya Lugalo |
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Mhe. Mama Netumbo Nandi Ndaitwah akiwa ameongozana na Balozi wa Namibia hapa nchini, Mhe.....kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Brigedia Generali Hashim Mbita wakati wa shughuli za kitaifa za kumuaga zilizofanyika katika Viwanja vya Lugalo. |
Mhe. Mama Netumbo Nandi Ndaitwah akimpa pole Mjane wa Marehemu Brigedia Generali Hashim Mbita, Mama Ngeme Mbita. |
Baadhi ya Wawakilishi wa Serikali ya Msumbiji nao wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Marehemu Generali Hashim Mbita |
Waziri wa Ulinzi wa Zimbabwe, Mhe. S. Sekeramayi (kulia) akiwa pamoja na Mkuu wa Majeshi wa Zimbabwe, Valarios Sibanda (mwenye sare za jeshi) pamoja na Balozi wa Zimbabwe hapa nchini, Mhe. Edzai Chimonyo (katikati) akiwa na Wawakilishi wengine wakitoa heshima zao za mwisho |
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya nae akitoa heshima zake za mwisho huku akiwa ameongozana Katibu Mwenezi wa CCM, Bw. Nape Nnauye. |
Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. John Haule akiwa ameonozana na Balozi Celestine Mushy, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kutoa heshima zao za mwisho. |
Kiongozi wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini ambaye pia ni Balozi wa DRC, Mhe. Juma Halfan Mpango akitoa mkono wa pole kwa watoto wa Marehemu Brigedia Generali Hashim Mbita |
Balozi wa Zambia hapa nchini, Mhe. Judith Kapijimpango nae akitoa pole kwa wafiwa |
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga nae akitoa mkono wa pole kwa wafiwa............Matukio mengine kwenye shughuli za kuaga mwili wa Marehemu Balozi Mbita |
Waziri Membe akisaini Kitabu cha Maombolezo |
Sehemu ya Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa yaliyopo hapa nchini wakishiriki shughuli za kuaga mwili wa Marehemu Brigedia Generali Hashim Mbita |
Mwakilishi wa Serikali ya Msumbiji ambaye ni Mwakilishi wa Kamati Kuu wa FRELIMO, Bw. Zaimundo Domingos Pachinuapa akitoa salamu za rambirambi za Serikali hiyo wakati wa shughuli za kitaifa za kuaga mwili wa Marehemu Brigedia Generali Hashim Mbita |
Mwakilishi wa Serikali ya Afrika Kusini ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Nomaindia Mfeketo akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya serkali yake. |
Sehemu ya waombolezaji wakifuatilia matukio |
Waziri Membe akiwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Mhe. Mama Netumbo Nandi Ndaitwah wakifuatialia hotuba mbalimbali wakati wa shughuli za kumuaga Marehemu Brigedia Generali Hashim Mbita |
Viongozi wa Skauti hapa nchini nao walikuwepo kumuaga Brigedia Generali Hashim Mbita |
|
Waziri Membe akisalimiana na Mkuu wa Majeshi, Generali Davis Mwamunyange |
Jeneza lililobeba mwili wa Marehemu Brigedia Generali Hashim Mbita likiwa limebebwa na Wanajeshi Picha na Reginald Philip ==============================
SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA MHE. BERNARD
MEMBE,
WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO
WA KIMATAIFA
WAKATI WA SHUGHULI ZA KUMUAGA MAREHEMU
BRIGEDIA JENERALI HASHIM MBITA, TAREHE 29 APRILI, 2015
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu;
Mheshimiwa
Benjamin William Mkapa;
Rais Mstaafu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mheshimiwa
Mizengo Peter Pinda (Mb)
Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mama Ngeme Mbita
Mke wa Marehemu;
Watoto wa Marehemu;
Wanafamilia;
Mheshimiwa Hussein Mwinyi
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa;
Jenerali Davis Mwamunyange
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi;
Mheshimiwa
Abdulrahman Kinana
Katibu Mkuu wa
CCM;
Viongozi Mbalimbali mliopo hapa;
Mabalozi;
Waombolezaji;
Mabibi na Mabwana;
Nianze
kwa kutoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa na Serikali kwa ujumla. Kifo cha Brigedia Jenerali
Hashim Mbita ni msiba mkubwa sio kwetu tu hapa Tanzania, lakini pia kwa nchi za
Kusini mwa Jangwa la Sahara na bara lote la Afrika.
Nimelazimika kusimama na
kuzungumza mbele yenu kwa kuwa pamoja na heshima kubwa aliyoipata kama mwanajeshi
na nafasi zingine kubwa alizowahi kushika, lakini pia Mheshimiwa Hashim Mbita alitumikia Taifa lake kama Balozi
wetu katika jiji la Harare nchini Zimbabwe kuanzia mwaka 2003 hadi mwaka 2006.
Kama
ilivyoelezwa, Mheshimiwa Mbita atakumbukwa zaidi kama Katibu Mtendaji wa Nchi
za Mstari wa Mbele (Frontline States) kwa miaka 22 akiwa nguzo muhimu katika
harakati za kupinga ukoloni na kupigania Uhuru kwa nchi kadhaa za Kusini mwa
Afrika. Iliyokuwa OAU na kwa ridhaa ya Mwalimu Julius Nyerere, Ofisi za nchi za
mstari wa mbele ziliweka makao makuu hapa Dar es Salaam ambapo Jenerali Mbita
aliitumikia kati ya mwaka 1972 hadi hadi mwaka 1994.
Ni harakati hizi hizi ndio ambazo zimepelekea
Mhe. Mbita kupatiwa tuzo ya “Medali ya Sir Seretse Khama”, tuzo ya Umoja wa
Afrika ya “Son of Africa” na pia “The Royal Order of Munhumutapa” iliyotolewa
na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe mwaka 2014.
Ingawaje
Mhe. Mbita ametutoka lakini Mawazo na uzoefu wake utabaki nasi daima. Kupitia
SADC, “The Hashim Mbita Project” ambayo imeandika na kuhifadhi uzoefu, fikra na
kazi zake itakuwa ni hazina kubwa ya Mwanajeshi, Mpigania Uhuru na
Mwanadiplomasia Mtanzania. Ameiletea heshima nchi yetu na huyu ni Mkombozi wa
kweli wa kupigwa mfano.
Tunajivunia
utu wake na ndio maana leo, pamoja nasi tunafutwa mchozi na wenzetu. Naomba
kuwatambulisha kwenu.
· Kutoka Namibia, Mheshimiwa
Netumbo Nandi Ndaitwah, Naibu Waziri Mkuu na pia Waziri wa Mambo ya Nje.
· Uwakilishi kutoka
Zimbabwe, Mheshimiwa Dr. Sydney Selelamayi, Waziri wa Ulinzi na Ujumbe wake.
· Uwakilishi kutoka
Afrika Kusini, Mheshimiwa Nomaindia Mfeketo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa
Afrika Kusini.
· Kutoka Msumbiji, Mheshimiwa
Raimundos Domingos Pachinuapa, Mwakilishi wa Kamati Kuu wa FRELIMO.
Tunashukuru
kwa kuweza kujumuika nasi katika msiba huu.
Kwa
heshima na taadhima, tunatoa pole kwa familia na Watanzania wote. Mwenyezi
Mungu ailaze roho ya Marehemu Mheshimwa Balozi Brigedia Jenerali Hashim Mbita mahala Pema Peponi.
Amina!
|
Tuesday, April 28, 2015
Rais Kikwete amkaribisha Rais Clinton (Mstaafu) Ikulu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameambatana na Rais Mstaafu wa Marekani Mhe. Bill Clinton mara baada ya kuwasili Ikulu, na kufanya mazungumzo naye. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb.), ambaye pia alishiriki mazungumzo hayo. Rais Clinton yupo nchini kwa ziara binafsi ya siku tatu. |
Rais Kikwete akiwa katika Mazungumzo na Mhe. Clinton. Wa kwanza kulia ni waziri wa Mambo ya Nje na Ushikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard K. Membe ambaye alishiriki kwenye mazungumzo hayo pamoja na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mhe. Dkt. Seif Suleiman Rashid (hayupo pichani) |
Waziri wa Mambo ya Nje akiwa katika picha ya pamoja na Rais Mstaafu wa Marekani Mhe. Bill Clinton, Ikulu Dar es salaam, leo tarehe 28 Aprili 2015. |
Picha na Reginald Philip
Waziri Membe apokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Japan.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Bernard K. Membe (Mb) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Japan hapa nchini Mhe.Masaharu Yoshida. Hafla hiyo fupi ilifanyika Wizarani tarehe 28 Aprili, 2015
Balozi Mteule wa Japan hapa nchini Mhe.Masaharu Yoshida akimsikiliza kwa makini Waziri Membe muda mfupi baada ya kukabidhi nakala zake za hati za utambulisho.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Bw.Nathaniel Kaaya (mwenye tai nyekundu) kwa pamoja na Bw.Thobias Makoba, Katibu wa Waziri na Afisa kutoka Ubalozi wa Japan hapa nchini wakifuatilia mazungumzo kati ya Waziri Membe na Balozi Yoshida (hawapo pichani)
Kikao kikiendelea.
Waziri Membe akifafanua jambo kwa Balozi Yoshida huku Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Bi.Mindi Kasiga (kulia) akinukuu mazungumzo hayo.
Mhe. Yoshida nae akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho huku Mhe. Waziri Membe na Maafisa wakimsikiliza kwa makini.
Waziri Membe akifurahia jambo na mgeni wake Balozi Mteule wa Japan Mhe. Yoshida.
Waziri Membe akiagana na Balozi Mteule wa Japan hapa nchini Mhe. Yoshida mara baada ya kukabidhi nakala zake za hati za utambulisho.
Picha na Reuben Mchome.
Waziri Membe amuenzi Marehemu Brigedia Generali Hashim Mbita
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisaini Kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha Bregedia Generali Hashim Mbita, kilichotokea hivi karibuni katika Hospitali ya Lugalo Jijini Dar es Salaam. Marehemu Brigedia Generali Mbita aliwahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zambabwe pia atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa kwenye harakati za ukombozi Barani Afrika. |
Waziri Membe akimpa pole Mjane wa Marehemu Bregedia Generali Mbita, Bi. Ngeme Mbita |
Mhe. Membe akimpa pole mtoto wa Marehemu Brigedia Generali Mbita Bi. Sheilla Mbitta |
Waziri Membe akizungumza na wafiwa |
Waziri Membe akisalimiana na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini mara baada ya kuwasili kwenye Msiba wa Brigedia Generali Hashim Mbita |
Waziri Membe akisalimiana na aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zuberi Zitto Kabwe walipokutana kwenye msiba wa Brigenida Generali Mbita |
Waziri Membe akiwa amejumuika na Waombolezaji wengine kwenye msiba wa Brigedia Generali Mbitta nyumbani kwake Chang'ombe Jijini Dar es Salaam |
Waziri Membe akizungumza na waandishi wa Habari juu ya kifo cha Brigedia Generali Mbita. Waziri Membe alimwelezea Balozi Mbita kama kiongozi makini na mwadilifu na pia alikuwa mwanaharakati mahiri ambaye alihakikisha Bara lote la Afrika linakuwa huru.
Picha na Reginald Philip
|
Subscribe to:
Posts (Atom)