Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe. Begum Taj akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Prof. Mlacha mara baada ya kuwasili chuoni hapo kwa ziara maalum.
Balozi wa Tanzania nchini Uswisi, Mhe. Modest Mero akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Prof. Mlacha mara baada ya kuwasili chuoni hapo kwa ziara maalum.
Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma akiwaongoza Mabalozi wa Tanzania na Maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mara baada ya kuwasili chuoni hapo kwa ziara maalum.
Mabalozi wa Tanzania wakisikiliza kwa makini historia fupi ya Chuo hicho kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Chuo Prof. Mlacha muda mfupi baada ya kuwasili chuoni hapo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambaye pia alikuwa Mkuu wa Msafara wa ziara ya Mabalozi, Bi. Mindi Kasiga akizungumza machache kuwakaribisha Waheshimiwa Mabalozi kuanza kikao na uongozi wa chuo hicho.
Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, Mhe.Tuvako Manongi akichangia jambo katika mkutano huo.
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mhe.Peter Kalaghe naye akitoa mchango wake wakati wa mkutano huo.
Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. John Kijazi akichangia mada wakati wa mkutano huo. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Mhe.Radhia Msuya na kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Mhe.Philip Marmo
Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu Dodoma Prof. Mlacha ( aliyesimama mbele)akizungumza wakati wa kikao chake na Mabalozi wa Tanzania walipotembelea chuoni hapo.
Afisa Habari wa Chuo Kikuu cha Dodoma(aliyenyoosha mkono) akitoa maelezo wakati wa ziara fupi ya kuzunguka Chuo hicho huku Waheshimiwa Mabalozi wakiangalia kwa makini maeneo ya chuo hicho.
Balozi Tanzania nchini Uganda, Mhe. Ladislaus Komba (kulia) na Mhe.Anthony Cheche wakiangalia mazingira na majengo ya aina yake ya chuo hicho kama yanavyoonekana kwa mbali.
Picha ya Pamoja.
===============
Picha na Reuben Mchome na Reginald Philip.