Monday, June 1, 2015

WAZIRI MEMBE AWASIHI WATANZANIA KUTOCHAGUA VIONGOZI WANAOSAKA UONGOZI KWA KUTOA RUSHWA

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe.Bernard Membe (Mb) akimkabidhi Bi. Shamim Khan tuzo ya heshima ya kujishughulisha na kazi za kijamii hapa Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe.Bernard Membe akipokea tuzo maalumu kutoka kwa Sheikh Ismail Mohamed wakati wa tamasha la kwanza la Kaswida lililofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa na kudhaminiwa na Kampuni ya Dira ya Mtanzania. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe.Bernard Membe  akizungumza katika tamasha hilo la kwanza Qaswida, lililofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa,Mh Membe amewataka Watanzania kusubiri kwa hamu siku ya kutangaza nia ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu,

Alisema siku hiyo ya Juni 6, wananchi wasikilize nini anataka kuifanya nchi iweze kuondoka ilipo ikiwemo kuendelea kudumisha amani na utulivu uliopo. “Mkae tayari siku hiyo, naamini uongozi mzuri wa nchi ni ule wa kudumisha amani na utulivu na ili nchi iweze kusonga mbele, maadili kwa viongozi ni muhimu,” alisema Waziri Membe.

Mhe.Membe alitumia nafasi hiyo kuwasihi Watanzania kuacha kuchagua viongozi ambao kwa nje, wanajinadi  wana dini, lakini matendo hayaendani na maadili ya  dini zao. Alisema ili mtu aweze kuaminika kuwa ana dini, jamii ifuatilie katika madhehebu yao, hivyo amewasihi wasichague viongozi wanaosaka uongozi kwa kutoa rushwa.

“Msikubali kuwa na viongozi ambao kwa nje, wanaojinadi kuwa na dini kinyume na matendo yao, lazima mchague wenye hofu ya Mungu ambayo husisitizwa na dini zote,” Alisema uongozi wa heshima ni ule unaochukia rushwa ambayo ni adui wa haki, hivyo amewataka wananchi kuwaogopa wapenda rushwa kama ukoma. 
Baadhi ya Washiriki waliohudhuria tamasha hilo.
Baadhi ya Washiriki waliofika kwenye tamasha hilo la kwanza la Qaswida.
Baadhi ya Washiriki waliofika kwenye tamasha hilo la kwanza la Qaswida.
Mmoja wa washiriki wa tamasha la Qaswida kutoka Madrasa ya Nur-Pugu,Samiu Mussa akighani Qaswida mbele ya wageni waalikwa mbalimbali (hawapo pichani) waliofika kwenye tamasha hilo,lililodhaminiwa na kampuni ya Dira  ya Mtanzania
Kikundhi cha Qaswida kiitwacho Iqhyau wakighani Qaswida ya maadili
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe.Bernard Membe (Mb) akipokelewa na wenyeji wake alipokuwa akiwasili katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa,kwa ajili ya kushiriki tamasha la kwanza la Qaswida
Mkurugenzi wa Kampuni ya Ulamaa Qaswida Promotions ambao ndio waandaji wa tamasha la kwanza la Qaswida,Ustaadh Jumanne Ligopora akimkaribisha mgeni rasmi  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe.Bernard Membe 
Sheikh Ismail Mohamed akizungumza jambo na Waziri Membe wakati wa tamasha la kwanza la Qaswida lililofanyika jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na Kampuni ya Dira ya Mtanzania.
Waimbaji wa Qaswida kutoka kikundi cha Muumini cha Buguruni jijini Dar es Salaam wakiimba kwenye tamasha la kwanza la Kaswida lililofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa. Tamasha hilo lilidhaminiwa na Kampuni ya Dira ya Mtanzania.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.