Monday, June 1, 2015

Balozi Mulamula akabidhiwa rasmi Ofisi

Katibu Mkuu Mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,  Balozi Liberata Mulamula akikabidhiwa rasmi Ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo  Balozi John Haule. Kabla ya uteuzi huo Balozi Mulamula alikuwa Balozi  wa Tanzania nchini Marekani na Mhe.  Haule kwa sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya. Makabidhiano hayo yalifanyika Wizarani leo tarehe 01 Juni, 2015.
Balozi Mulamula akizungumza huku Naibu Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya, (kulia kwa Balozi Mulamula), Mhasibu Mkuu Bw. Paul Kabale (wa tatu kutoka kushoto), Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Mambo ya Nje, Bw. Mathias Abisai na Afisa Habari wa Mambo ya Nje Bw. Ally Kondo
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bw. Nigel Msangi (wa kwanza kulia), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga (wa pili kutoka kulia), Mkurugenzi Idara ya Sera na Mipango Bw. James Lugaganya na  Balozi Haule wakimsikiliza Balozi Mulamula  (hayupo pichani)
Katibu Mkuu, Balozi Mulamula akiwa kwenye Mkutano na baadhi ya Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo mara baada ya kukabidhiwa rasmi Ofisi na Balozi Haule.


Picha na Reginald Philip

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.