Monday, June 22, 2015

Rais Kikwete aongea na Watanzania wanaoishi India

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Watanznia wanaoishi India katika Hotel ya Taj Palace jijini Delhi. Rais Kikwete aliwaeleza mambo ya maendeleo yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya nne ikiwemo ujenzi wa miundombinu kama vile barabara, maji, umeme na uboreshaji wa bandari ya Dar es Salaam. Aidha, aliwambia mipango iliyopo ya kujenga bandari ya Bagamoyo na reli ya kati ya kisasa. Aliwaeleza pia hali ya kisiasa, hususan maandalizi ya uchguzi mkuu ambapo zoezi la kuchukua fomu za kuwania nafasi ya Rais linaendelea.

Baadhi ya Watanzania waliohudhuria mkutano wa Rais Kikwete

Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe (Mb) kulia na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb) nao waliongozana na Rais Kikwete katika mkutano na Watanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekzaji Tanzania (TIC), Bi. Juliet Kairuki akitoa ufafanuzi wa masuala ya uwekezaji kwa Watanzania wanaoishi India.

Dada wa Kitanzania ambaye kwa sasa ni mwanafunzi wa Shahada ya Uzamili ya masuala ya Teknolojia ya Kilimo nchini India akimuuliza swali Rais Kikwete. Dada huyo alitaka kujua Serikali imejipngaje kuhakikisha kuwa mazao yanayolimwa nchini Tanzania yanasindikwa kabla ya kusafirishwa nje ya nchi. Rais Kikwete alieleza kuwa katika awamu ya pili ya mpango wa maendeleo wa mwaka 2025 ambao unaanza kutekelezwa mwaka 2015/2016 unalenga maendeleo ya viwanda. 

Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na watoto wa wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini India.
Rais Kikwete (kushoto) akiwa pamoja na Balozi wa Tanzania nchini India, Me. Mhandisi John Kijazi


Mama Salma Kikwete (katikati) akiwa na baadhi ya Watanzania wanawake wanaoishi India.

 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.