Friday, June 26, 2015

Rais Kikwete atumia fursa ya maadhimisho ya Miaka miwili ya Papa Francis kuwa madarakani kuwaaga Maaskofu



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa Hotuba yake kwenye maadhimisho ya Siku ya kitaifa ya Taifa la Vatican pamoja na kuadhimisha miaka miwili ya Baba Mtakatifu, Papa Franci kuwa madaraki kwenye Ubalozi wa Vatican hapa nchini.  Rais Kikwete ameipongeza Vatican kwa kuwa na mahusiano mazuri na Tanzania, pia alitumia nafasi hiyo kuwaaga Maaskofu wote wa Tanzania walio kuwepo kwenye maadhimishi hayo ikiwa ni sherehe yake ya mwisho akiwa madarakani. maadhimisho hayo yalifanyika katika makazi ya Balozi wa Vatican hapa nchini Askofu Padilla tarehe 26.06.2015, na kuhudhuriwa na Waziri wa Mambo ya nje Bernard Membe (Mb.), Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuber Bin Ally na Muadhama Polycarp Kardinal Pengo, Mabalozi na maaskofu wa kanisa katoliki hapa nchini.  
Rais Kikwete akiendelea kuhutubia huku Waziri Membe na Askofu Padilla (Kushoto) wakifuatilia kwa makini hotuba hiyo.
Balozi wa Vatican Askofu Padilla naye akitoa hotuba yake katika maadhimisho hayo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Kamilius Membe (Mb.) akitoa salamu za pongezi ya maadhimisho ya miaka miwili ya Baba Mtakatifu, Papa Francis wakati wa maadhimisho hayo katika Ubalozi wa Vatican uliopo hapa nchini  
Viongozi mbalimbali wa Kidini, Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa nchini wakisikiliza kwa makini Hotuba zilizo kuwa zikitolewa na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Mwakilishi wa Baba Mtakatifu nchini Askofu Francisco Montecillo Padilla na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb.) hawapo pichani
Rais Kikwete(Kulia) akifanya akigonganisha Glasi na Muadhama Polycarp Kardinal Pengo (Wa kwanza kushoto) na Balozi wa Vatican Askofu Montecillo Padilla kama ishara ya kumtakia Baba Mtakatifu Afya njema na miasha marefu wakati wa maadhimisho hayo.

juu na chini: Rais Kikwete akigonganisha Glasi na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa nchini na Waziri Membe.
Waziri Membe akimtambulisha Kaimu Mkuu Mufti wa Tanzania Sheikh Ally (Kulia) kwa Balozi wa Vatican nchini Askofu Padilla
Waziri Membe (Katikati) akimtambulisha Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuber Bin Ally kwa Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Dianna Melrose 
Rais Kikwete (Wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Kamilius Membe (Wa kwanza kulia), Balozi wa Vatican nchini Askofu Padilla (Wa kwanza Kushoto) na Kaimu Mkuu Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuber Bin Ally 
Rais Kikwete akiagana na Maaskofu mara baada ya kumalizika kwa maadhimisho hiyo  
Waziri Membe (Kushoto) akizungumza jambo na Balozi Askofu Padilla
Waziri Membe naye akiagana na Maaskofu mara baada ya kumalizika kwa Maadhimisho hayo.

Picha na Reginald Philip






No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.