Friday, June 12, 2015

Watanzania wengine 13 warejea kutoka nchini Yemen

Kiongozi wa msafara wa Watanzania kumi na tatu waliorejea leo nchini wakitokea nchini Yemeni, Bw.Faiz Abdulsheikh Said akizungumza na Mwakilishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi.Asha Mkuja wakati wa mapokezi ya Watanzania hao walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa Shirika la Ndege la Qatar. Serikali imefanikiwa kuwarejesha nchini zaidi ya Watanzania 100  kutoka Yemen baada ya nchi hiyo kukumbwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe. Zoezi la kuwarejesha Watanzania hao linaratibiwa na kusimamiwa na Wizara kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Oman. Watanzania wengine 15 wanatarajiwa kuwasili nchini kesho tarehe 13 Juni, 2015.
Bi. Asha Mkuja akiendelea kupata maelezo kutoka kwa mmoja wa Watanzania hao Mzee Bader Saleh Omar kuhusu hali ilivyo nchini Yemen.
 Mazungumzo yakiendelea
 Mwakilishi wa Wizara ya Mambo ya Nje Bi.Asha akimsikiliza kwa makini mzee Bader, akimpa maelezo ya hali ilivyo huko Nchini Yemen.
 Watanzania hao wakijiandaa kuondoka ndani ya Uwanja wa Ndege baada ya kukamilisha taratibu zote.

Picha na Reuben Mchome

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.