Tuesday, October 6, 2015

Makamu wa Rais aongoza waombolezaji kifo cha kaka wa Waziri Membe

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha wageni muda mfupi baada ya kuwasili nyumbani kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe (Mb) kumpa pole kufuatia kifo cha kaka yake Waziri Membe, Bw. Simon Kamillius Membe aliyefariki dunia siku chache zilizopita huko nchini India. 
Makamu wa Rais akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu, nyumbani kwa waziri Membe leo tarehe 06-10-2015.
Makamu wa Rais akiwapa pole familia ya Marehemu Simon Kamillius Membe aliyefariki dunia siku chache zilizopita huko nchini India. 
 Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe.Benjamin Mkapa akisaini kitabu cha wageni muda mfupi baada ya kuwasili nyumbani kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe (Mb) kumpa pole kufuatia kifo cha kaka yake Waziri Membe, Bw. Simon Kamillius Membe aliyefariki dunia siku chache zilizopita huko nchini India. 

 Rais Mstaafu Mhe.Benjamin Mkapa akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu, nyumbani kwa waziri Membe leo tarehe 06-10-2015.
 Rais Mstaafu Mhe.Benjamin Mkapa akiwapa pole familia ya Marehemu Simon Kamillius Membe aliyefariki dunia siku chache zilizopita huko nchini India.

Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa marehemu.

Mama Salma akiwapa pole familia ya marehemu.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi akisaini kitabu cha wageni muda mfupi baada ya kuwasili nyumbani kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe (Mb.), kumpa pole kufuatia kifo cha kaka yake Waziri Membe, Bw. Simon Kamillius Membe aliyefariki dunia siku chache zilizopita huko nchini India.

Dkt. Reginald Mengi akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu, nyumbani kwa Waziri Membe leo tarehe 06-10-2015.
 Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi, akiwapa pole familia ya marehemu.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe (Mb.), akitoa heshima zake za mwisho kwa marehemu kaka yake, Simon Membe.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu Bw. Omar Mahita naye akitoa heshima za mwisho kwa Marehemu.
 Balozi wa Tanzania nchini DRC - Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo -, Balozi Anthony Cheche akitoa heshima zake za mwisho .
 Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu, nyumbani kwa Waziri Membe leo tarehe 06-10-2015.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga, akitoa heshima zake za mwisho kwa Marehemu, leo tarehe 06-10-2015.
 Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. James Lugaganya, akitoa heshima zake za mwisho kwa Marehemu, leo tarehe 06-10-2015.
 Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Joachim Utaru, akitoa heshima zake za mwisho kwa Marehemu, leo tarehe 06-10-2015.
 Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Nigel Msangi,akitoa heshima zake za mwisho kwa Marehemu, leo tarehe 06-10-2015.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, wakitoa heshima zao za mwisho kwa Marehemu, leo tarehe 06-10-2015.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe (Mb), akiwaongoza waombolezaji kuingia kanisani, tayari kwa Misa ya kumuombea Marehemu.
 Baadhi ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, wakiwa wamesimama wakati mwili wa Marehemu unaingizwa kanisani, St. Peters jijini Dar es Salaam.
 Mwili wa Marehemu ukiingizwa kanisani.
Misa ikiendelea. 
 Kiongozi wa Misa akiendelea na Maombezi kwa Marehemu. 
Misa ikiendelea. 
 Misa ikiendelea
 Muongozaji wa shughuli, Richard Kasesela akiendelea na matangazo.
 Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango na Mwakilishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. James Lugaganya, akitoa salamu za rambirambi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje.
 Balozi wa Zimbabwe hapa nchini Mhe. Edzai Chimonyo, akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Mabalozi wote wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.
Mapadri walioongoza misa hiyo. 
 Mwakilishi wa Familia ya Marehemu akitoa neno la shukrani.
 Balozi wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hapa nchini na mkuu wa Mabalozi wote wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, Mhe. Juma Khalifan Mpango, akitoa heshima za mwisho kwa Marehemu.
 Naibu  Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angela Kairuki akitoa heshima zake za mwisho kwa Marehemu.
Mwili wa Marehemu ukiingizwa kwenye gari,tayari kwa safari ya kwenda kijijini kwa Marehemu Rondo, Mkoani Lindi tayari kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika kesho Jumatano, tarehe 07.10.2015.
==============================
PICHA NA REUBEN MCHOME.

Monday, October 5, 2015

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
 


Simu: 255-22-2114615, 211906-12
Barua pepe: nje@nje.go.tz
Barua pepe: gcu@nje.go.tz
Tovuti : www.foreign.go.tz     

Nukushi: 255-22-2116600

              

 

 
         20 KIVUKONI FRONT
P.O. BOX 9000,
      11466 DAR ES SALAAM, 
               Tanzania.

  


Taarifa zaidi ya Mahujaji kutoka Tanzania huko Saudi Arabia

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa masikitiko makubwa imepokea jina la Bw. Khamis Juma Shamte hujaji kutoka Tanzania aliyefariki dunia kufuatia tukio la mkanyagano wa Mahujaji lililotokea eneo la Mina, Makkah tarehe 24 Septemba, 2015. Kifo cha Bw. Shamte kinafanya idadi ya vifo vya Watanzania kufuatia tukio hilo kufikia watu nane (8) hadi sasa.

Aidha, Wizara imepokea jina la Bi Hawa Amrani Khamis aliyekuwa amepotea tangu siku ya ajali hiyo ambaye amepatikana akiwa mzima na aliweza kuungana na Mahujaji wengine na kurejea nyumbani tarehe 02 Oktoba, 2015.

Vile vile orodha ya majina ya majeruhi wote wa ajali ambao bado wapo hospitali imetolewa. Hadi sasa kuna Mahujaji wanne (4) wa Tanzania ambao wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali mbalimbali za Saudi Arabia na hali zao zinaendelea vizuri. Mahujaji hao ni Bi. Hidaya Mchomvu, Bi. Mahjabin Taslim Khan na Bw. Ahmed Abdalla Jusab. Pia, kuna mgonjwa mmoja ambaye aliugua tangu alipowasili Madina akitokea nchini anayeitwa Mustafa Ali Mchira ambaye bado amelazwa katika Hospitali ya Ansari Madina katika chumba cha wagonjwa mahututi. Bw. Mchira hakujeruhiwa kwenye ajali ya mkanyagano.

Hadi kufikia tarehe 03 Oktoba, 2015, Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia kwa kushirikiana na Tanzania Hajj Mission na Vikundi vilivyopoteza Mahujaji umefanikiwa kupata majina ya Watanzania 32 ambao bado hawajapatikana. Orodha ya Majina na Vikundi vyao ni kama ifuatavyo:-

 KIKUNDI CHA KHIDMAT ISLAMIYA

1.  Abdul Iddi Hussein
2.  Awadh Saleh Magram
3.  Burhan Nzori Matata
4.  Yussuf Ismail Yussuf
5.  Saleh Mussa Said
6.  Adam Abdul Adam
7.  Archelous Anatory Rutayulungwa
8.  Farida Khatun Abdulghani
9.  Rashida Adam Abdul
10.              Hamida Ilyas Ibrahim
11.              Rehema Ausi Rubbaga
12.              Faiza Ahmed Omari
13.              Khadija Abdulkhalik Said
14.              Shabinamu Ismail Dinmohammed
15.              Salama Rajabu Mwamba
16.              Johari Mkesafiri Mwijage

KIKUNDI CHA TCDO

17.              Alwiya Sharrif Abdallah
18.              Hafsa Sharrif Saleh Abdallah

KIKUNDI CHA AHLU DAAWA

19.              Masoud Juma
20.              Issa Amiri Faki
21.              Juma Jecha Dabu
22.              Nassor Mohammed Hemed
23.              Mohammed Awadh Namongo
24.              Juma Yussuf Bajuka
25.              Said Habibu Ferej
26.              Khadija Hamad
27.              Rahma Salim
28.              Hadija Abdallah Sefu
29.              Farida Khamis
30.              Nuru Omar Karama
31.              Laila Manunga
32.              Saida Awadh

Zoezi la kuwatambua Mahujaji wa Tanzania ambao bado hawajaonekana linaendelea. Serikali ya Saudi Arabia imetoa picha nyingine zipatazo elfu moja (1,000) kwa ajili ya kuangalia Mahujaji waliofariki dunia katika ajali hiyo.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam

05 Oktoba, 2015

Friday, October 2, 2015

Press Release

H.E Park Geun-hye, President of the Republic of Korea

PRESS RELEASE

H.E. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a congratulatory message to H.E. PARK Geun-hye, President of the Republic of Korea. The message reads as follows:

Her Excellency PARK, Geun-hye,
President of the Republic of Korea,
Seoul,

Your Excellency,

On behalf of the Government and the people of the United Republic of Tanzania and indeed on my own behalf, I would like to convey my warm congratulations to you and through you, to the Government of the Republic of Korea on the auspicious occasion of celebrating your country’s 70th anniversary of the National Day.  

The government of Tanzania highly values the ties, which exist with the Government of the Republic of Korea, and is ready to maintain and enhance the relations in a bid to benefit the peoples of the two countries. Together, we have built bridges between our two nations in every conceivable field, from education, health, infrastructure and commerce and trade. It is therefore vital that we continue to work together so as to contribute to the efforts of making the world a better place to live.

Please accept, Your Excellency, my best wishes for your continued good health, progress and prosperity of the people of the Republic of Korea”.

Issued by: The Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, Dar es Salaam

2nd October, 2015

Balozi Marmo Afanya ziara ya Kikazi Mjini Hamburg

Mhe. Philip S. Marmo,Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani (Kushoto) akiwa kwenye kikao na Mhe.Wolfgang Schmidt, Naibu Waziri anaye shughulikia masuala ya Umoja wa Ulaya na Mambo ya Nje wa jimbo la Hamburg. Mkutano huo ulifanyika siku ya tarehe 29 Septemba,2015 kwenye ofisi Mhe.Schmdit mjini Hamburg.Mhe.Balozi Marmo alikuwa mjini Hamburg kwa ziara ya kikazi.
Mhe. Philip S. Marmo,Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani (wa kwanza kushoto) kwenye mazungumzo na Mhe.Vladimir Vladimirovich Golitsyn, Rais wa "International Tribunal for the Law of the Sea" aliyevaa tai ya zambarau (kulia) na Bi. Petra Hammelmann (katikati) Balozi wa Heshima wa Tanzania wa mji wa Hamburg. Mazungumzo hayo yalifanyika kwenye ofisi ya Mhe.Golitsyn siku ya tarehe 29 Septemba, 2015 mjini Hamburg.
Balozi Filip Marmo (wa pili kulia) akiwa katika Kaburi la Malika Salma Emily Ruete Binti binti wa Sultani Said Said wa Zanzibar ambaye alikuwa Mzanzibar wa KWanza kuja Hamburg mwaka 1866 na kuolewa na Mfanyabiashara wa Kijerumani. 

Thursday, October 1, 2015

Katibu Mkuu Nje azungumza na watumishi wa Ubalozi wa Tanzania NY

Balozi Liberata Mulamula, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania Jijini New York, Marekani. 


Balozi Mulamula akiwa kwenye picha ya pamoja na maofisa wa Ubalozi wa Tanzania New York wakiongozwa na  Balozi Tuvako Manongi, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa (wa pili kushoto) na Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi, Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa (wa kwanza ksuhoto). Wengine kwenye ujumbe wa Balozi Mulamula kutoka Makao Makuu ni Balozi Celestine Mushy, Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa (wa kwanza kulia) na Bi. Mindi Kasiga, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Mambo ya Nje (wa kwanza kushoto mstari wa juu).

Mkutano ukiendelea.

Wednesday, September 30, 2015

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA


 
Simu: 255-22-2114615, 211906-12
Barua pepe: nje@nje.go.tz
Barua pepe: gcu@nje.go.tz

Nukushi: 255-22-2116600

              

 

    
20 KIVUKONI FRONT,P.O. BOX 9000,
       11466 DAR ES SALAAM, 
                                    Tanzania.


Taarifa zaidi ya Mahujaji kutoka Tanzania huko Saudi Arabia

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa masikitiko makubwa imepokea majina mengine mawili ya  Mahujaji kutoka Tanzania waliofariki dunia kufuatia tukio la mkanyagano wa Mahujaji lililotokea eneo la Mina, Makkah tarehe 24 Septemba, 2015 na kupelekea vifo vya Watanzania kufuatia tukio hilo kufikia watu saba (7) hadi sasa.

Majina ya Mahujaji hao ni Bw. Athumani Mateso Chaulana na Bw. Ahmed Said Bawazir ambao kupitia picha zao wametambulika kuwa wamefariki dunia.

Aidha, Wizara imepokea majina mapya 19 ya Mahujaji kutoka Tanzania ambao bado hawajaonekana. Itakumbukuwa kuwa tarehe 29 Septemba, 2015 Wizara ilitoa taarifa za kupatikana kwa majina 18 ya Mahujaji wa Tanzania ambao ni kati ya 50  ambao bado hawajaonekana. Kupatikana kwa majina hayo kunafanya idadi ya Mahujaji waliopotea na majina yao kutambulika kufikia 37.

Orodha ya majina mapya 19 ya Mahujaji wa Tanzania ambao mpaka sasa bado hawajaonekana ni kama ifuatavyo:-

1.  Juma Bajuka
2.  Masoud Juma
3.  Issa Amir Faki
4.  Juma Jecha Dabu
5.  Nassor Mohammed Hemed
6.  Mohamed Awadh Namongo
7.  Juma Bakula
8.  Said Habib
9.  Hamis Juma Shamte
10.              Khadija Hamad
11.              Rahma Salim
12.              Hadija Abdallah Sefu
13.              Farida Khamis
14.              Laila Manunga
15.              Bi. Hawa Amrani Khamis
16.              Saida Awadhi
17.              Maimuna Seleman Ruwaly
18.              Jalia Kassim Mashule
19.              Nuru Omar Karama

Mbali na taarifa za kupatikana kwa majina hayo, Wizara imepokea taarifa ya kuonekana Mahujaji saba wakiwa hai. Mahujaji hao ni:-

1.  Ali Abdulrahman (Abidina)
2.  Abdallah Hassan Pande
3.  Suleiman Ali Kidogoli
4.  Mohammed Salum
5.  Mwadini Hassan
6.  Habiba Ramadhan Ali (Maulana)
7.  Ramadhan Muhsin

Ubalozi kwa kushirikiana na Tanzania Hajj Mission na Vikundi vya Mahujaji unaendelea na juhudi za kuwatambua Mahujaji wengine wa Tanzania ambao hawajaonekana kwa kutembelea katika hospitali zilizohifadhi maiti na kulaza majeruhi wa ajali hiyo ikiwa ni pamoja na kuhakiki picha za mahujaji waliofariki ili kubaini Mahujaji kutoka Tanzania.

Wizara inapenda kufafanua kuwa, orodha inayotolewa si kamili kwa maana kwamba inaweza kuongezeka kwa vile baadhi ya majina ya Mahujaji yaliwayowasilishwa Ubalozini na ndugu wa mahujaji waliopotea hayamo katika orodha hii. Pia Ubalozi unaendelea kuwasiliana na vikundi vilivyopeleka Mahujaji ili kuweza kupata taarifa kamili na sahihi ya jumla ya Mahujaji wote ambao hawaonekani.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam
30 Septemba, 2015


Mkurugenzi wa Asia na Australasia na Balozi wa India wajadili maandalizi ya India- Africa Summit

Mkurugenzi wa Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki (kulia) akiwa katika mazungumzo na Balozi wa India nchini, Mhe. Sandeep Arya. Mazungumzo yao yalihusu pamoja na mambo mengine, ushiriki wa Serikali ya Tanzania katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Kiafrika na India utakaofanyika jijini New Delhi, India tarehe 26 - 29 Oktoba 2015.

Mazungumzo kati ya Balozi wa India na Balozi Kairuki yanaendelea. Wengine katika picha, kulia ni Bw. Emmanuel Luangisa, Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kushoto ni Afisa wa Ubalozi wa India wakifuatilia mazungumzo hayo.


Balozi wa India nchini, Mhe.Sandeep  Arya akiagana na Balozi Kairuki mara baada ya kukamilisha mazunguzmo yao yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.