Wednesday, July 26, 2017

Tanzania calls for immediate solution on Diplomatic crisis in Gulf Countries


PRESS STATEMENT

Tanzania calls for immediate solution on Diplomatic crisis in Gulf Countries

The united Republic of Tanzania is supporting the initiatives taken by the Amir of Kuwait HH Sheikh Sabah Al-Jaber Al-Sabah’s mediation efforts to address the Gulf crisis and the exploration of possible solution methods.

The diplomatic crisis began in June 5th 2017 when Saudi Arabia, United Arab Emirates, Bahrain, and Egypt abruptly cut off diplomatic relations with Qatar by withdrawing ambassadors and imposing trade and travel bans.

Tanzania call for unity and stability of the Gulf region and it emphasis that a solution should be found within the framework of the Gulf Cooperation Council and in that regards, it joins and support the initiative of the State of Kuwait that called for the crisis to be resolved through peaceful negotiations.

We therefore, appeal to the Gulf Nations to quickly resolve their disputes in peaceful and diplomatic manner.


Issued by Government Communication Unit, Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation

26 July, 2017

Hafla ya kumuaga Balozi wa Israeli nchini Mhe. Yahel Vilan

  
 Balozi Innocent Shiyo Mkurugenzi wa Idara ya Afrika akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Balozi Augustine Mahiga kwenye hafla ya kumuaga Balozi wa Israel Nchini aliyemaliza muda wake Mhe. Yahel Vilan,  tarehe 22 Julai,2017-  Hyatt, Dar es salaam.


Balozi Innocent Shiyo akimkabidhi zawadi Mhe.Balozi Yahel Vilan kwa niaba ya Mhe. Waziri Mahiga katika hafla hiyo.

Balozi Innocent Shiyo na Balozi Vilan pamoja na wageni wengine wakiwa katika hafla hiyo.

Tuesday, July 25, 2017

Balozi Mahiga apokea Nakala za Hati za Utambulisho za Mabalozi Watatu


Balozi Mteule wa Jamhuri ya Indonesia

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Jamhuri ya Indonesia nchini Tanzania, Mhe. Prof. Ratlan Pardede ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Jamhuri ya Indonesia nchini Tanzania, Mhe. Prof. Ratlan Pardede. Katika mazungumzo hayo, Mhe. Waziri aliisifu Indonesia kwa hatua ya maendeleo iliyofikia katika nyanja mbalimbali ikiwemo sekta ya kilimo na kuelezea matumaini yake kuwa ujio wa Mhe. Balozi utasaidia kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na Indonesia yatakayosaidia Tanzania kujifunza kutokana na maendeleo ya Indonesia.
 
Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia mazungumzo hayo. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Autralasia, Bi Justa Nyange, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Bi. Mindi Kasiga na Afisa Dawati, Bw. Emannuel Luangisa

 Mwakilishi wa Papa, Tanzania


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Mwakilishi Mteule wa Papa nchini Tanzania, Mhashamu Marek Solczynski ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika mazungumzo na Mwakilishi Mteule wa Papa nchini Tanzania, Mhashamu Marek Solczynski.
Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia mazungumzo hayo. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bi Mary Matari, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Bi. Mindi Kasiga na Afisa Dawati, Bw. Ceaser Waitara.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Mwakilishi Mteule wa Papa nchini Tanzania, Mhashamu Marek Solczynski mara baada ya kuwasili Wizarani kwa ajili ya kuwasilisha Nakala za  Hati za Utambulisho.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akibusu pete ya Mwakilishi Mteule wa Papa nchini Tanzania, Mhashamu Marek Solczynski kabla ya kupokea Nakala za  Hati za Utambulisho.


Balozi Mteule wa Ujerumani
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Shirikisho la Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Dkt. Detlef Wachter ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Shirikisho la Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Dkt. Detlef Wachter. Katika mazungumzo hayo, Mhe. Waziri aliishukuru Ujerumani kwa msaada mkubwa inaotoa kwa Tanzania, hususan katika kulinda rasilimali ikiwemo hifadhi za Taifa na kusisitiza umuhimu wa makampuni makubwa ya Kijerumani kuja kuwekeza nchini.

Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia mazungumzo hayo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Itifaki, Bi. Grace Martin, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Bi. Mindi Kasiga na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bi Mary Matari.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi Mteule wa Shirikisho la Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Dkt. Detlef Wachter mara baada ya kuwasili Wizarani kwa ajili ya kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho.

Picha ya pamoja.

Mkutano na vyombo vya Habari kuhusu Uhusiano kati ya Tanzania na Kenya


Taarifa ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania na Kenya kuhusu utekelezaji wa maamuzi ya Wakuu wa Nchi Mhe. Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania na Mhe. Rais Uhuru Kenyatta wa Jamhuri Kenya
  
Ndugu waandishi wa habari, mtakumbuka kuwa tarehe 28 Juni, 2017 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitoa taarifa kwa umma kuhusu vikwazo vya kibiashara ambavyo nchi ya Kenya iliweka katika baadhi ya bidhaa kwa kipindi cha hivi karibuni. Katika taarifa ile, Serikali ya Tanzania ilibainisha dhamira yake ya kufanya mazungumzo na Serikali ya Kenya kwa lengo la kumaliza tofauti hizo za kibiashara baina ya nchi hizi mbili kwa kuzingatia taratibu za kibiashara tulizokubaliana katika Jumuiya yetu ya Afrika ya Mashariki.
Bidhaa za Tanzania ambazo ziliwekewa vikwazo na nchi ya Kenya ni unga wa ngano pamoja na gesi ya kupikia (LPG). Aidha, juhudi za awali za Serikali ya Tanzania kuona vikwazo hivyo vinaondelewa na Serikali ya Kenya kwa wakati hazikuzaa matunda. Hali hiyo ilipelekea Serikali ya Tanzania nayo kuchukua hatua.
Kwa kuzingatia mahusiano mazuri ya kindugu yaliyopo kati ya nchi zetu mbili na kwa kujali manufaa mapana ya Jumuiya yetu ya Afrika Mashariki, Viongozi Wakuu wa nchi hizi mbili Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta, Rais wa Jamhuri ya Kenya walizungumza na kukubaliana kuondoleana vikwazo hivyo maramoja, Vikwazo hivyo ni;
1.     Serikali ya Kenya kuondoa vikwazo kwa bidhaa za unga wa ngano na gesi ya kupikia (LPG) kutoka Tanzania.

2.     Serikali ya Tanzania kuondoa vikwazo kwa bidhaa za maziwa zinazozalishwa nchini Kenya.

3.     Serikali za Kenya na Tanzania kuondeleana vikwazo vyovyote vile ambavyo vinaweza kuathiri biashara ya bidhaa na huduma kati ya nchi zetu mbili.

4.     Sigara ni kati ya mambo yaliyojadiliwa. Hata hiyo utekelezaji wake utafuata taratibu za ndani
Hivyo, Viongozi Wakuu wa nchi zetu mbili waliwaelekeza Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi wa Tanzania na Kenya, Mhe. Dkt. Augustine Philip Mahiga (Mb) na Dkt. Amina Mohammed, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Kenya kuutarifu umma kwamba pande zote mbili zimekubaliana kumaliza tofauti hizo za kibiashara zilizojitokeza hapo awali.
Katika kutekeleza hilo, Mhe. Waziri Dkt. Amina Mohamed alimwalika Mhe.Waziri Dkt. Mahiga nchini Kenya tarehe 23 Julai, 2017 ambapo walifanya Mkutano wa Pamoja na waandishi wa habari kuutangaza uamuzi wa Viongozi Wakuu wa Kenya na Tanzania kuondoleana vikwazo hivyo maramoja.

Kufuatia makubaliano haya ya pamoja kati ya nchi hizi majirani ambazo ni waasisi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, pia, tunapenda kutaarifu kwamba Mataifa haya mawili yamekubaliana kuunda Tume ya Pamoja ambayo itakuwa na jukumu la kuepusha tofauti za kibiashara kati ya Tanzania na Kenya pamoja na kutolea ufumbuzi changamoto za kibiashara kati ya nchi hizi mbili pindi zinapojitokeza. Tume hii itaongozwa na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania na Kenya na kujumuisha Mawaziri wanaohusika na masuala yaJumuiya ya Afrika Mashariki, Biashara, Fedha, Mambo ya Ndani ya Nchi, Kilimo, Uchukuzi na Utalii wa nchi zote mbili.
Vilevile, Mawaziri hawa wataunda mfumo wa kupeana taarifa mara kwa mara kuhusu masuala yenye changamoto za kibiashara kwa lengo la kuepusha kujirudia kwa tofauti kama hizi. Ni matarajio yetu kuwa uamuzi huu wa pamoja utakuza zaidi mahusiano ya kibiashara baina ya nchi hizi mbili. Aidha, tunapenda kuwashukuru wafanyabiashara wa nchi zetu mbili kwa uvumulivu.


MASWALI NA MAJIBU BAADA YA TAARIFA YA MSINGI
SWALI:  Je ni kwa nini Kenya waliweka vikwazo hivyo hapo awali?
JIBU: Sababu za awali zilizotolewa na Serikali ya Kenya zilidai kwamba bidhaa hizo hazikidhi viwango vya ubora wa kimataifa. Hata hivyo, Wataalamu wa Tanzania wameihakikishia Kenya kuwa bidhaa za unga wa ngano kutoka Tanzania zina ubora  unaokubalika Kimataifa na huuzwa nchi nyingine za Jumuiya ya afrika Mashariki na Afrika ya Kati. Halikadhalika bidhaa ya gesi ya kupikia (LPG) inakidhi viwango vya ubora vya Kimataifa
.
SWALI: Nini msimamo wa Serikali ya Tanzania kuhusu tuhuma za baadhi ya wanasiasa wa Kenya na baadhi ya vyombo vya habari kuhusu Tanzania kuingilia uchaguzi wa Kenya.
JIBU: Tuhuma hizi hazina ukweli wowote, na hata nilipokuwa  nchini Kenya juzi niliona zimeripotiwa tena na vyombo vya habari vya Kenya. Naomba nikanushe tena kwa mara nyingine, kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, haijawahi, na wala haifikirii kuingilia maswala ya ndani ya nchi nyingine tunazoshirikiana nazo ikiwemo maswala ya uchaguzi. Hatujawahi kuingilia uchanguzi wa Kenya na hututegemei kufanya hivyo kwenye uchaguzi huu na chaguzi nyingine zozote. Naomba waandishi wa habari, kabla ya kuandika taarifa hizi, wazihakiki mara mbili, na watutafute kutoa ufafanuzi kabla ya kuwapelekea wananchi taarifa hizi za kupotosha. Natoa rai, tuwe waangalifu na walaghai wa nje  wanaotaka kutugombanisha. Nichukue pia fursa hii kuwatakia wananchi wa Kenya uchaguzi mwema wa amani na huru.
SWALI:  Je ni kwanini Tanzania inaonekana kuweka vizingiti vingi vya kibiashara ikilinganishwa na nchi nyingine kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na Afrika ya kati kwenye siku za hivi karibuni? Je hii haitakwaza ukuaji wetu wa uchumi kama nchi?
JIBU: Hapana, hata kidogo. Serikali ya Tanzania inaendelea kuweka mazingira wezeshi ya biashara ili kuwezesha uchumi wa nchi kukua na kuendelea, kutokana na biashara ndani ya bara la Afrika na hususan ukanda wetu wa Afrika Mashariki na Kati. Tanzania kwa siku za hivi karibuni chini ya uongozi wa Rais wa Awamu ya Tano, Mhe. John Joseph Pombe Magufuli, imefanya mageuzi makubwa kwenye taasisi zetu za bandari na ushuru yaani TRA. Hatua hizi zinalenga kwenye kuziba mianya iliyokuwepo huko nyuma ambayo ilisababisha ukusanywaji hafifu wa mapato. Ni wazi sasa mambo yanaenda kwa uwazi zaidi na ushuru unatozwa na kukusanywa kwa wakati. Tuna hakika sasa changamoto hizi zimepungua na nchi jirani zitaendelea kufanya biashara na sisi bila vikwazo.

SWALI: Kabla ya kuunda hii kamati ya kutatua changamoto zilizojitokeza hivi karibuni, Jumuiya ya Afrika Mashariki imekua ikitatua vipi changamoto kama hizi za kibiashara hususan kwenye nchi zenye ushindani mkubwa kama Kenya na Tanzania?
JIBU: Jumuiya ya Afrika Mashariki imejiwekea misingi imara na muhimu ya kutatua changamoto pindi zinapojitokeza. Hivyo ukiacha jopo la wataalam wa Serikalini kuna Baraza la Mawaziri wa Biashara wa Jumuiya yetu ya Afrika Mashariki  ambao pia huweza kupendekeza ufumbuzi wa changamoto mbalimbali kwa wakuu wa nchi ili kutatua changamoto hizi. Lakini kutokana na ukaribu uliopo baina ya Tanzania na Kenya, hili la sasa tumelitatua kwa haraka na kwenda mbele zaidi kuunda tume ya mawaziri wa nchi zetu mbili ili huko baadae tuweze kutatua masuala kama haya mapema sana kabla ya kuathiri biashara kati ya nchi zetu mbili.
Ni dhahiri kwamba nchi zetu mbili ni jirani na tunalindwa na Itifaki za Jumuiya yetu ya Afrika Mashariki, lakini pia tuna ushindani kati yetu. Na ili tupate maendeleo ni lazima kuweka ushindani wenye tija kwa manufaa ya ukanda wetu na wananchi wetu. Japo kuwa Kenya ipo kwenye kundi la nchi zenye kipato cha kati, uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi kubwa na ni hali ya kawaida kwa changamoto kama hizi kujitokeza pindi nchi zinapokuwa katika ushindani wa kiuchumi.Kwa namna ya pekee naomba kusifu tena hekima za Viongozi wetu wa Juu kwa kutatua changamoto hizi kwa wakati.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam, 24 Julai, 2017





Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Balozi Augustine Mahiga wa kwanza kulia akitoa ufafanuzi kwenye mkutano na vyombo vya habari kuhusu utekelezaji wa maamuzi ya Wakuu wa Nchi Mhe. Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania na Mhe. Rais Uhuru Kenyatta wa Jamhuri ya Kenya katika masuala mbalimbali ya Uhusiano kati ya Tanzania na Kenya.
Anayefuata katika picha ni Balozi Innocent Shiyo Mkurugenzi Idara ya Afrika, kushoto kwake Bw.Peter Sang, Kaimu Balozi wa  Kenya Nchini, katika Ukumbi wa Mikutano wa JNICC, Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Julai, 2017

Sehemu ya waandishi wakiwa katika Mkutano huo.

Saturday, July 22, 2017

Wanaarusha wafurika katika amsha amsha ya kuchangamkia fursa za soko la EAC

Chuo cha Ufundi Arusha
Mgeni Rasmi ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega (kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (The Foundation for Civil Society-FCS), Bw. Francis Kiwanga alipowasili kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Ufundi Arusha kwa ajili ya kufungua kongamano la siku moja la kuhamasisha vijana kuchangamkia fursa za kibiashara katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kongamano hilo ambalo lilikuwa na kaulimbiu "Chungulia fursa Boda to Boda" liliandaliwa kwa ushirikiano baina ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, FCS na Clouds Media kwa udhamini wa Trademark East Africa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi, Bw. Francis Kiwanga akitoa neno la ukaribisho kwa wageni waalikwa ambapo pia alieleza sababu za kufanya kampeni ya kuwahamasisha vijana kuchangamkia fursa za EAC. Bw, Kiwanga alisema kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na FCS na Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam zimebaini kuwa wastani wa vijana asilimia 11 katika nchi za EAC hawana ajira na asilimia 59 hawana taarifa kuhusu fursa zilizopo katika Jumuiya hiyo. Hivyo, Kongamano hilo ni kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu fursa zilizopo ili vijana waweze kujiajiri.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega akisoma hotuba ya ufunguzi ambapo alisisitiza umuhimu wa vijana kung'amua fursa mbalimbali na kubuni bidhaa zitakazokidhi soko la EAC lenye watu zaidi ya 150.

Sehemu ya umati wa watu uliohudhuria kongamano hilo wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mgeni Rasmi.

Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha, Dkt. Richard Kaisi akitoa neno ambapo alihimiza vijana kujifunza elimu ya ufundi wa aina mbalimbali ili waweze kuwa wabunifu wazuri kutokana na teknolojia ya kisasa.

Mchumi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Justin Kisoka akitoa maelezo kuhusu sheria, kanuni na taratibu za kufuata endapo mtu anataka kufanya biashara katika nchi za Afrika Mashariki. Aidha, alisisitiza umuhimu wa vijana kujiunga katika vikundi ili iwe rahisi kupata huduma kama za mikopo.

Watu wa makundi mbalimbali walishiriki kongamano hilo wakiwemo watu wenye mahitaji maalum. Pichani mlemavu wa masikio akipatiwa tafsri kwa lugha ya alama wa masuala yanayojiri katika shughuli hiyo.

Huwezi kufanya biashara katika nchi za EAC bila ya kuwa na Hati halali ya kusafiria. Pichani ni Bw. Suleiman Masoud, Afisa wa Uhamiaji akitoa maelezo namna ya kupata Hati ya Kusafiria. 

Mlemavu wa macho akitoa maoni yake na kuuliza swali kwa watoa mada. Alidai kuwa taasisi za Serikali ndio zinakwamisha na kuwachelewesha Watanzania wasiweze kuchangamki ipasavyo fursa za EAC kutokana na ukiritimba usiokuwa na sababu.

Kama kawaida ujumbe ulifikishwa kwa njia tofauti. Pichani ni wasanii wa bendi ya Cocodo wakicheza wimbo wa kuhamasisha biashara za kuvuka mipaka.
Uwanja wa Sheikh Amri Abeid

Vijana walifuatwa katika maeneo yao mtaani ili kufikishiwa neno la kuwahamasisha kufanya biashara za kuvuka mipaka ndani ya EAC. Pichani ni Mtaalmu wa Masuala ya Afrika Mashariki kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Abel Maganya akiwahamasisha vijana wanaofanya biashara zao kando ya Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Sehemu ya watu waliohudhuria wakisikiliza neno kutoka kwa Bw. Maganya.

Hamasa kwa njia ya muziki
Soko la Mbauda
Bw. Kisoka akitoa neno. Alisisitiza vijana waondoe khofu na wajiunge katika vikundi na aSerikali ipo nyuma yao kuwaunga mkono.

Wafanyabiashara wa Soko la Mbauda wakisikiliza ujumbe kwa makini.

Binti huyo akitoa ujumbe kwa njia ya ngojera ili mradi watu wahamasike na kuona umuhimu wa kujikwmua kimaisha kwa kufanya biashara za kuvuka mipaka.

Kinanda na gitaa vilipigwa kwa ustadi mkubwa na kutoa ujumbe kwa Watanzania wasibweteke kwni fursa zipo lukuki ktika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki


Friday, July 21, 2017

Amsha amsha ya vijana kuchangamkia fursa za Soko la EAC yashika kasi

ROCK CITY MALL, MWANZA
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (The Foundation for Civil Society- FCS), Bw. Francis Kiwanga akitoa neno la ukaribisho kwa wageni waalikwa katika Kongamano la siku moja la kuwahamasisha vijana kuchangamkia fursa za Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Kongamano hilo lilifanyika kwenye ukumbi wa Rock City Mall jijini Mwanza tarehe 19 Julai 2017. 

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mhe. Mary  Onesmo Tesha ambaye alikuwa Mgeni Rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella akisoma hotuba ya ufunguzi kwenye kongmano la kuwhamasisha vijana kufanya biashara za kuvuka mipaka ya nchi za EAC. Mhe. Tesha aliwasihi vijana waondoe hofu na wajiunge katika vikundi ili waweza kufanya biashara kwa urahisi. Aliahidi kutoa milioni moja kwa kikundi kilichoundwa hapohapo kwa uratibu wa Mwkilishi wa Cloud Media, Bw. Samsonight Odera

Bi. Tesha akiendelea na hotuba yake.

Mchumi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw, Justin Kisoka akiwaeleza vijana wa Mwanza waliofurika kwenye ukumbi wa Rock City Mall sheria, kanuni na taratibu za kufuata kwa yeyote anayetaka kuanza biashara ya kuvuka mipaka ya nchi za EAC.

Mtaalamu wa Msauala ya EAC, Bw. Abel Maganya akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusu kufanya biashara ndani ya Jumuiya ya EAC ikiwemo namna ya kupata cheti cha uasili na hati za kusafiria.

Mbinu mbalimbali zilitumika kufikisha ujumbe wa umuhimu wa kufanya biashara katika nchi za EAC. Hapa vijana wa Vipaji Foundation wakionesha kwa kutumia igizo baaadhi ya bidhaa zinazoweza kuuzwa katika nchi za EAC.

Mjasiriamali aliyefanikiwa ambaye pia ni maaruku wa kutoa mihadhara ya mbinu za kufanya biashara, Bw. James Mwang'amba akiwasilisha mada kuhusu mbinu za kuanza biashara na kuiendesha hadi ikakua kubwa.

Sehemu ya umati wa watu walioshiriki kongamano.

BABATI, MANYARA
 Msafara ulipokuwa unatokea Mwanza kwenda Arusha, ulisimama kwa muda Babati na kuongea na Wanababati namna ya kufanya biashara katika nchi za EAC.

Mkazi wa Babati akiuliza swali ili apate ufafanuzi kabla ya kuanza kupeleka bidhaa zake nchini Kenya

Vijana wa Vipaji Foundation wakitoa somo kwa Wanababati kupitia sanaa. 

Wanababati wakisikiliza kwa makini ujumbe wa namna ya kufanya biashara ya kuvuka mipaka.