Friday, May 6, 2022

TANZANIA YASHIRIKI MAONESHO YA KILIMO YA MACFRUT 2022 ITALIA

Katika jitihada za kutekeleza Diplomasia ya Uchumi kwa vitendo, Tanzania kwa mara ya kwanza imeshiriki katika maonesho ya kimataifa ya kilimo yanayojulikana kama MACFRUT FIERA yanayoendelea mjini Rimini, nchini Italia.

Maonesho hayo yanawakutanisha wazalishaji, wanunuzi na wauzaji wa bidhaa za kilimo cha mbogamboga na matunda, ufugaji wa kuku na mashine za kisasa zinazotumika katika kilimo. 

Akifungua maonesho hayo, Waziri wa Kilimo wa Italia, Mhe. Stefano Patuanelli, alisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika sekta ya kilimo ikiwa ni pamoja na matumizi ya teknolojia ya kisasa katika kilimo ili kuongeza tija katika uzalishaji na usalama wa chakula. 

Ubalozi wa Tanzania nchini Italia kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo umevutia ushiriki wa sekta binafsi katika maonesho hayo ambayo tunda la mwaka huu ni parachichi. 

Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, aliwasihi wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchini humo kuja kuwekeza Tanzania katika sekta ya kilimo na sekta nyinginezo.

“Nawahakikishia kuwa Tanzania imeboresha mazingira ya uwekezaji kwa kupunguza kero zilizokuwa hapo awali na kwamba, Watanzania wapo tayari kuwapokea,” alisema Balozi Kombo. 

Maonesho ya MACFRUT hufanyika kila mwaka. Awamu inayofuata ya maonesho (MACFRUT FIERA 2023) itafanyika mwezi Mei, 2023 katika mji wa Rimini. 

Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na washiriki kutoka Angola waliotembelea banda la Tanzania katika maonesho ya MACFRUT

Maafisa kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Italia wakizungumza na baadhi ya washiriki waliotembelea banda la Tanzania katika maonesho ya a MACFRUT 

Washiriki kutoka Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja naBalozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo kwenye maonesho ya MACFRUT katika mji wa Rimini, Italia

Naibu Waziri Mkuu wa Uganda na mgeni rasmi katika kongamano maalum kwa ajili ya Afrika, Mhe. Rebecca Kadaga (katikati mwenye barakoa) akiungana na viongozi wengine kukata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa maonesho hayo uliofanyika tarehe 4 Mei 2022


Thursday, May 5, 2022

BALOZI SOKOINE ASHIRIKI MKUTANO WA MAKATIBU WAKUU SADC

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine ameshiriki Mkutano wa Kamati ya Kudumu katika ngazi ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) uliofanyika leo kwa njia ya mtandao.

Balozi Sokoine ameshiriki mkutano huo akiwa katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa SADC unaotarajiwa kufanyika kwa njia ya mtandao tarehe 6 Mei 2022. 

Pamoja na masuala mengine, Makatibu Wakuu wamejadili athari za mafuriko yaliyotokea katika Ukanda wa SADC kwa kipindi cha Januari hadi Aprili 2022.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akishiriki Mkutano wa Kamati ya Kudumu katika ngazi ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) uliofanyika leo kwa njia ya mtandao katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akishiriki Mkutano wa Kamati ya Kudumu katika ngazi ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) uliofanyika leo kwa njia ya mtandao katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo  ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Balozi Agnes Kayola.  



BALOZI MUSHY AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO KWA RAIS AUSTRIA

Balozi wa Tanzania nchini Austria, Mhe. Celestine Joseph Mushy, amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Austria, Mhe. Alexander Van der Bellen, leo tarehe 05 Mei 2022

Januari 2022, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan alimteua Balozi Mushy kuwa Balozi wa Tanzania nchini Austria. 

Balozi wa Tanzania nchini Austria, Mhe. Celestine Joseph Mushy akiwasilisha  Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Austria, Mhe. Alexander Van der Bellen

Balozi wa Tanzania nchini Austria, Mhe. Celestine Joseph Mushy akiwasilisha  Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Austria, Mhe. Alexander Van der Bellen

Rais wa Jamhuri ya Austria, Mhe. Alexander Van der Bellen akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Austria, Mhe. Celestine Joseph Mushy 

Rais wa Jamhuri ya Austria, Mhe. Alexander Van der Bellen akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Austria, Mhe. Celestine Joseph Mushy mara baada ya kupokea Hati za Utambulisho za Balozi Mushy



WAZIRI MULAMULA APOKEA NAKALA ZA HATI YA UTAMBULISHO YA BALOZI WA MTEULE WA ETHIOPIA NCHINI

 

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akipokea Nakala ya Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Ethiopia nchini Mhe. Sibru Mamo Kedida alipofika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam  kujitambulisha baada ya kuwasili nchini  

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akionesha Nakala ya Hati za Utambulisho alizopokea kutoka kwa Balozi Mteule wa Ethiopia nchini Mhe. Sibru Mamo Kedida alipofika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam  kujitambulisha baada ya kuwasili  nchini

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiangalia Nakala ya Hati za Utambulisho alizopokea kutoka kwa Balozi Mteule wa Ethiopia nchini Mhe. Sibru Mamo Kedida alipofika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam  kujitambulisha baada ya kuwasili nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Balozi Mteule wa Ethiopia nchini Mhe. Sibru Mamo Kedida alipofika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam  kujitambulisha baada ya kuwasili nchini

Balozi Mteule wa Ethiopia nchini Mhe. Sibru Mamo Kedida akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula alipofika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam  kujitambulisha baada ya kuwasili nchini

Mazungumzo yakiendelea

Mazungumzo yakiendelea

Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiongozwa na Mkuu wa Itifaki nchini Balozi Yusuph Mndolwa (wa kwanza kushoto) ulioambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula  hayupo pichani ukifuatilia mazungumzo kati wa Balozi Mulamula na Balozi Mteule wa Ethiopia nchini alipofika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kuwasilisha nakala ya Hati za Utambulisho

Balozi Mteule wa Ethiopia nchini Mhe. Sibru Mamo Kedida akimkabidhi zawadi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula alipofika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kukabidhi nkala ya Hti za Utambulisho baada ya kuwasili nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (wa pili kulia) akiwa na Balozi Mteule wa Ethiopia nchini Mhe. Sibru Mamo Kedida (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja baada ya kukabidhi Nakala ya Hati za Utambulisho alipofika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam  kujitambulisha baada ya kuwasili nchini. wa kwanza kulia ni Mkuu wa Itifaki nchini Balozi Yusuph Mndolwa na wa kwanza kushoto ni ofisa Ubalozi wa Ethiopiaa nchini Bw. Mulato.




Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) amepokea nakala ya Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Ethiopia nchini Mhe. Shibru Mamo Kedida leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Baada ya kupokea nakala ya hati hizo viongozi hao walipata fursa ya kuzungumza ambapo Balozi Mulamula alimhakikishia Balozi Mteule ushirikiano wa hali ya juu kumuwezesha Balozi huyo kutekeleza majukumu yake ya kibalozi hapa nchini na kuhakikisha uhusiano kati ya Tanzania na Ethiopia unaendelea kuimarika.

‘‘Unaona timu yangu niliyoambatana nayo hapa, nichukue nafasi hii kukuhakikishia kuwa Wizara itakupa ushirikiano wote utakaouhitaji katika kutekeleza majukumu yako, saa 24 milango yetu iko wazi, tunataka uhusiano kati ya nchi zetu uzidi kuimarika,’’ alisema Balozi Mulamula.

Balozi Mulamula amesema Tanzania imefarijika kupata balozi mpya baada ya Balozi wa awali kumaliza muda wake wa uwakilishi, na kuongeza kuwa kitendo hicho ni ishara ya uhusiano mzuri na urafiki uliopo baina ya Tanzania na Ethiopia.

Naye Balozi Mteule wa Ethiopia Mhe. Sibru Mamo Kedida amemshukuru Waziri Mulamula  kwa jinsi alivyompokea na kuelezea uhusiano kati ya Tanzania na Ethiopia ulivo mzuri na kuahidi kuwa atahakikisha uhusiano huo unazidi kukua na kuimarika.

“Ethiopia na Tanzania zimekuwa katika uhusiano mzuri sana  kidiplomasia, nchi zzetu zimekuwa na lengo moja, nitahakikisha uhusiano kati ya nchi hizi unaimarika na hata kufikia nchi hizi Tanzania na Ethiopia zinashirikiana kufanya biashara na uwekezaji kwa maslahi ya pande mbili,” amesema Mhe. Balozi Kedida

 

 

BALOZI MBAROUK AMPOKEA KATIBU MKUU JUMUIYA YA MADOLA ZANZIBAR

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amempokea Katibu Mkuu Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland alipowasili Zanzibar katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.

Mhe. Scotland yupo nchini kwa ziara maalumu ya kukutana na kumfahamisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan maudhui ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Madola unaotarajiwa kufanyika nchini Rwanda mwezi Juni 2022.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akimpokea Katibu Mkuu Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Zanzibar  

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akimkaribisha Katibu Mkuu Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Zanzibar  

Katibu Mkuu Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Zanzibar 

Mazungumzo baina ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk na Katibu Mkuu Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland yakiendelea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Zanzibar 





Wednesday, May 4, 2022

SHEHENA YA KWANZA YA PARACHICHI KUTOKA TANZANIA YAWASILI NCHINI INDIA

Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa Mbega leo tarehe 04 Mei 2022 amepokea kwa mara ya kwanza shehena ya matunda aina ya Parachichi kutoka Tanzania ikiwa ni mwendelezo wa juhudi za Ubalozi huo za kutafuta masoko ya bidhaa za mazao ya mbogamboga na matunda nchini India.

 

Akizungumza na Naibu Mwenyekiti wa Bandari ya Jawalarlal Nehru ya mjini Mumbai, Bw. Unmesh Sharad Wagh mara baada ya kupokea shehena hiyo, Balozi Mbega ameishukuru Serikali ya India kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania kwenye sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo na kwa pamoja na Bw. Wagh walikubaliana kushirikiana katika sekta ya uchukuzi hususan katika kubadilishana ujuzi kwenye masuala ya Bandari.

 

Katika maelezo yake Balozi Mbega amesema kuwa, wafanyabiashara wa India wamehamasika kutokana na juhudi za uhamasishaji zinazofanywa nchini humo na Ubalozi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa hapa nchini na sasa wapo tayari kuanza kuingiza matunda aina ya Nanasi na Embe kutoka Tanzania.

 

“Huu ni mwendelezo wa juhudi za Ubalozi kwa kushirikiana na Serikali na TAHA wa kuendelea kutafuta masoko ya bidhaa za mazao ya mbogamboga na matunda nchini India. Wafanyabiashara wa India wamehamasika na sasa wanakamilisha taratibu za kuanza kuingiza nanasi na embe za Tanzania nchini India, amesema Balozi Mbega.  

 

Pia, Balozi Mbega amekishukuru Chama cha Wakulima wa Mbogamboga na Matunda Tanzania (TAHA) kwa ushirikiano wao uliofanikisha shehena hiyo ya Parachihci kuwasili India salama.

 

Shehena hiyo ya kwanza ya parachichi  imewasili nchini India kupitia Bandari yaJawalar Nehru ya mjini Mumbai kwa ushirikiano kati ya Kampuni ya IG Fruits ya India na Kampuni ya Avoafrica ya Makambako mkoani Iringa.

Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa Mbega (kushoto mwenye miwani myeusi) akikata utepe wakati wa mapokezi rasmi ya Kontena lenye matunda aina ya Parachcihi kutoka Tanzania lililowasili nchini humo tarehe 04 Mei 2022 kupitia Bandari ya Jawalar Nehru ya mjini Mumbai. Kontena hilo la Parachichi limewasili nchini humo kwa ushirikiano kati ya Kampuni ya IG Fruits ya India na Kampuni ya Avoafri ya Makambako mkoani Iringa. 

Balozi Anisa (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa bandari ya Mumbai baada ya kupokea na kufungua Kontena lenye Parachichi kutoka Tanzania
Picha ya pamoja
Balozi Anisa akiwa kwenye mazungumzo na Naibu Mwenyekiti wa Bandari ya Jawaharlal Nehru ya Mumbai, Bw. Unmesh Sharad Wagh baada ya kupokea matunda hayo ya parachichi  kutoka Tanzania. Katika mazungumzao yao walikubaliana kushirikiana katika kubadilishana ujuzi kati ya Tanzania na India kwenye masuala ya Bandari 

 

Monday, May 2, 2022

WAZIRI MULAMULA AFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU WA USALAMA WA TAIFA WA INDIA


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula amefanya mazungumzo na Naibu Mshauri wa Usalama wa Taifa wa India Mhe. Vikram Misri jijini Dar es Salaam. 


Mazungumzo yao yalijikita kujalidi masuala mbalimbali kuhusu ulinzi na usalama katika ngazi ya Kitaifa, Kanda na Kimataifa kama vile changamato za wahamiaji haramu, ushafirishaji haramu wa binadamu, ugaidi na uharamia. 

Waziri Mulamula amemweleza Mhe. Misri kuwa hali ya usalama ndani ya nchi na kwenye mipaka ya nchi yetu ni salama na tumekuwa tukiendelea kushirikiana vizuri na nchi jirani zinazotuzunguka na Jumuiya za kikanda katika kutatua changamoto mbalimbali kama vile usafirishaji haramu wa binadamu, uharamia na masuala ya ugaidi. 

Naibu Mshauri wa Usalama wa Taifa wa India Mheshimiwa Balozi Vikram kwa upande wake ameeleza kuridhishwa kwake na namna Serikali ya Tanzania inavyoshiriki kutatua na kukabiliana na changamoto za ulinzi na usalama katika ngazi ya Taifa, Kikanda na Kimataifa. Vilevile aliongeza kusema kuwa Serikali ya India itaendelea kushirikiana na Tanzania katika eneo la ulinzi na usalama.

Naibu Mshauri wa Usalama wa Taifa wa India H.E Amb. Vikram Misri yupo nchini kwa ziara ya kikazi ambapo anatarajia kuonana na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Mazungumzo yakiendelea
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa katika mazungumzo na Naibu Mshauri wa Usalama wa Taifa wa India Mhe. Vikram Misri yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula Naibu Mshauri wa Usalama wa Taifa wa India Mhe. Vikram Misri wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka India na Watendaji wa Wizara
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula na Naibu Mshauri wa Usalama wa Taifa wa India Mhe. Vikram Misri wakisalimiana walikutana kwa mazungumzo jijini Dar es Salaam