Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb), ametembelea na kujionea namna ujenzi
wa jengo la Wizara katika mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma unavyoendelea.
Katika ziara hiyo ya ukaguzi Mhe. Dkt. Tax
amemtaka mkandarasi wa ujenzi wa jengo hilo kuongeza kasi ili ujenzi ukamilike
kwa wakati.
“Nimetembelea hapa, nimejionea kazi ilipofika,
kazi bado ni kubwa inabidi muongeze bidii zaidi ili Mungu akijaalia mwezi
Oktoba mwaka huu badala ya Desemba ujenzi uwe umekamilika na tuone tunajipanga
namna gani,” amesema Dkt. Tax.
Amesema Wizara ina uhitaji mkubwa wa jengo hilo
kwa kuwa watumishi wametawanyika katika maeneo matatu tofauti na inakuwa ngumu kukutana kwa haraka pale inapobidi.
Amesema kukamilika kwa jengo Hilo kutatoa ahueni
kwa watumishi wa wizara na kuwawezesha kuwa sehemu moja na hivyo kurahisisha
utendaji kazi wa Wizara.
Katika ziara hiyo Mhe. Waziri Dkt. Tax
aliambatana na Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk, Katibu Mkuu Balozi Joseph Sokoine na watendaji
wengine wa Wizara.
Ujenzi wa jengo la Wizara ulianza mwezi Januari
2022 na unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba 2023. Ujenzi huo utagharimu kiasi
cha Shilingi bilioni 22.9 ambazo
zimetolewa na Serikali ili kuziwezesha Wizara na Taasisi za Serikali kuwa na
majengo ya kudumu katika mji wa Serikali.
Ujenzi huo unafanywa na Umoja wa makampuni ya
Sole works na mshauri elekezi ambaye ni Chuo Kikuu cha Ardhi.
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisaini kitabu cha wageni alipowasili kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma tarehe 07 Januari 2023 |
|
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akisaini kitabu cha wageni akiwa ameambatana na Mhe. Dkt. Tax kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma tarehe 07 Januari 2023 |
|
Mhe. Dkt. Tax akizungumza na wakandarasi wa jengo la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alipofika kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo ambapo aliwahimiza kuongeza kasi ya ujenzi wa jengo hilo. |
|
Mhe. Dkt. Tax akizungumza na wakandarasi wa jengo la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alipofika kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo ambapo aliwahimiza kuongeza kasi ya ujenzi wa jengo hilo. |
|
Sehemu ya Wakurugenzi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wamsikiliza Mhe. Dkt. Tax wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara katika Mji wa Serijkali Mtumba |
|
Sehemu ya Wakurugenzi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wamsikiliza Mhe. Dkt. Tax wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara katika Mji wa Serijkali Mtumba
Sehemu ya Wakandarasi wanaosimamia ujenzi wa Jengo la Wizara wakimsikiliza Mhe. Dkt. Tax alipotembelea jengo la Wizara kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi |
|
Mkandarasi anayesimamia ujenzi wa Jengo la Wizara akitoa maelezo kuhusu hatua mbalimbali zilizofikiwa katika ujenzi wa jengo hilo ambapo kwa sasa limekamilika kwa asilimia 55. |
|
Mkandarasi wa Jengo la Wizara akifafanua jambo kwa Mhe. Dkt. Tax kuhusu hatua mbalimbali za ujenzi wa jengo hilo kwa kuonesha picha |
|
Mhandisi wa Wizara, Bw. John Kiswaga naye akitoa ufafanuzi kwa Mhe. Waziri Tax kuhusu maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara |
|
Mhe. Balozi Mbarouk akiangalia sampuli ya fremu za milango na kusisitiza ujenzi huo uzingatie ubora wa hali ya juu wa vifaa vyote vitakavyotumika kama, mbao, vigae na marumaru. |
|
Mhe. Balozi Mbarouk akisisitiza jambo kwa wakandarasi kabla ya kuanza ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara |
|
Mhe. Dkt. Tax kwa pamoja na Mhe. Balozi Mbarouk wakiingia kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara lililopo katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma |
|
Mhe. Dkt. Tax akipanda ngazi kuelekea ghorofa za juu za jengo hilo ili kukagua maendeleo ya ujenzi |
|
Mhe. Dkt. Tax akimsikiliza Mkandarasi wa Wizara, Bw. Kiswaga wakati akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya ujenzi wa jengo la Wizara |
|
Mhe. Dkt. Tax akitoa maelekezo kwa wakandarasi na kuwataka kuongeza kasi na kuzingatia ubora na viwango katika ujenzi wa jengo la Wizara |
|
Mwonekano wa jengo la Wizara linaloendelea kujengwa katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma |