Friday, May 3, 2024

BALOZI SHAIBU AONGOZA WATUMISHI WA WIZARA KUTEMBELEA MAMLAKA YA NGORONGORO

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Balozi Said Shaibu Mussa leo tarehe 03 Mei 2024 amewaongoza Watumishi wa Wizara kutembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) ikiwa ni utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje inayoweka msisitizo katika Diplomasia ya Uchumi.


Akizungumza alipowasili  Mamlaka ya Ngorongoro, Balozi Mussa amesema Wafanyakazi hao waliokuwa  jijini Arusha kushiriki Mkutano wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara uliofanyika tarehe 02 Mei 2024, wametumia fursa hiyo kutembelea na kujionea kwa macho eneo hilo  ambalo ni la kipekee duniani ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan za kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania kupitia njia mbalimbali ikiwemo filamu ya Tanzania: The Royal Tour.


Kadhalika, amesema Wizara kama mdau wa sekta ya utalii nchini imetumia mkutano wa Baraza Kama fursa kwa kuwapa Wafanyakazi nafasi ya kufanya utalii wa ndani, ili kujifunza na kujenga uwezo wa kutangaza kivutio hicho na vingine vingi kikamilifu kutokana na kujionea kwa macho na kupata kwa undani taarifa muhimu kuhusu vivutio hivyo.


"Si vyema unapomwambia mtu kuhusu kitu fulani wakati wewe mwenyewe hukijui au hujafika, kwani tunaamini kwamba kuona ni kuamini. Hivyo tupo hapa kujifunza na kuwafunza wengine kuhusu utalii wa ndani na tusiwaambie tu wageni kuhusu eneo hili wakati sisi wenyewe hatulijui" amesema Balozi Mussa.

Kadhalika amepongeza jitihada za Mhe. Rais Dkt Samia za kutangaza utalii hususan kupitia filamu ya The Royal Tour na kusema matunda yake yameonekana kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya watalii kutoka ndani na nje ya nchi wanaotembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

"Filamu ya Royal Tour iliyoongozwa na Mhe. Rais Samia haikutoa matokeo kwa watu wa nje tu bali imetoa matokeo, mvuto na ushawishi hata kwa wananchi wa ndani wakiwemo Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki tunaunga mkono na tunatekeleza kile ambacho Mhe. Rais amekianza na kimeleta ushawishi mkubwa kwa watu kutembelea nchini", amesema Balozi Mussa.


Balozi Mussa ametumia wasaa huo kutoa wito kwa wananchi wa Tanzania na wageni kutembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ili kujionea wanyama wakubwa watano maarufu kama "The Big Five" wanaopatikana katika Hifadhi hiyo kama Simba, Tembo, Chui, Nyati na Faru.


Kwa upande wake, Afisa Utalii wa Mamlaka ya Ngorongoro, Bw. Orgoo Mauyai amesema Ngorongoro ni ya kipeee na tofauti na hifadhi nyingine duniani kutokana na binadamu na wanyamapori kuishi pamoja na Mamlaka hiyo ni urithi wa dunia chini ya Shirika la Elimu na Utamaduni la  Umoja wa Mataifa (UNESCO) na ameipongeza Wizara kwa kuitembelea Mamlaka hiyo.


Pia amewahimiza Wafanyakazi wa Wizara hiyo na Watanzania kwa ujumla kuendelea kupiga kura ili Hifadhi ya Mamlaka ya Ngorongoro itetee ushindi wake wa nafasi ya kwanza ya kuwa Kituo Kinachoongoza Kuvutia Watalii Afrika iliyoupata mwaka 2023 kwa kupiga kura kupitia Tovuti ya utalii ya www.worldtravelawards.com. Ili kuwa mshindi wa kipengele hicho kwa mwaka 2024.


Nao Wafanyakazi wa Wizara waliopata fursa ya kushiriki ziara hiyo wameupongeza Uongozi wa Wizara hiyo kwa kuwawezesha kutembelea hifadhi hiyo kwani imewawezesha kufahamu mambo mengi yenye manufaa katika utekelezaji wa majukumu yao na katika maisha yao kwa ujumla.

"Nimefurahi kuwa hapa leo. Nimejionea kwa macho uzuri wa hifadhi hii napongeza viongozi waliofanikisha hili kwani tumejifunza mengi" alisema Bi. Lilian Mushi. 

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaibu Mussa akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye geti la kuingia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ambapo amewaongoza Wafanyakazi wa Wizara  leo tarehe 03 Mei 2024 kutembelea Mamlaka hiyo ikiwa ni utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje inayoweka msisitizo katika Diplomasia ya Uchumi. Wafanyakazi hao waliokuwa  jijini Arusha kushiriki Mkutano wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara uliofanyika tarehe 02 Mei 2024, walitumia fursa hiyo kutembelea na kujionea kwa macho eneo hilo la kipekee duniani

Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashiriki, Bi. Chiku Kiguhe akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye geti la kuingia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Anayesuhudia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara,  Balozi Mussa

Afisa Maliasili wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Bw. Orgoo Mauyai akitoa ufafanuzi kuhusu Hifadhi hiyo ambayo aliielezea kama ya kipekee kwa vile ni makazi kwa binadamu na wanyama

Balozi Mussa na Wafanyakazi wa Wizara wakimsikiliza Afisa Maliasili Bw. Mauyai akitoa ufafanuzi kuhusu Mamalaka ya Hifadhi ya Ngorongoro

Maelezo yakiendelea

Wafanyakazi wakisikiliza maelezo kuhusu Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro

Sehemu nyingine ya Wafanayakzi wa Wizara

Wafanayakazi wa Wizara wakisikiliza maelezo kuhusu Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
Sehemu nyingine ya Wafanyakazi wa Wizara
Maelezo yakitolewa
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, Balozi Mussa (wa pili kushoto) akiwa pamoja na wenyeji wake alipowasili katika geti la kuingia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Kushoto ni Afisa Maliasili, Bw. Orgoo Mauyai na Wafanyakazi wengine wa Mamlaka hiyo
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, Balozi Mussa akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Wizara mara baada ya kuwasili katika geti la kuingia  Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kujionea kivutio hicho cha utalii ili kuwa mabalozi wazuri wa kukitangaza ndani na nje ya Tanzania
Wafanyakazi wa Wizara wakipata picha kufurahia ziara hiyo
Wafanyakazi wa Wizara katika picha
Msafara wa Magari ya Utalii yaliyobeba wafanyakazi wa Wizara kuelekea Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, Balozi Mussa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine wa Wizara na Wafanyakazi walipowasili kwenye sehemu maalum ya kuonesha bonde la Ngorongoro
Picha ya pamoja



Wafanyakazi wa Wizara wakipata picha za bonde la Ngorongoro linaloonekana kwa mbali

Picha ya pamoja

Naibu Katibu Mkuu, Balozi Mussa akiangalia wanyama mbalimbali baada ya kuwasili katika bonde la Ngorongoro. Anayechukua tukio ni Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bi. Chiku Kiguhe

Ziara katika bonde la Ngorongoro ikiendelea

Tembo ambaye ni mmoja wa wanyama mashuhuri watano wanaojulikana kama The Big Five akiwa Ngorongoro

Viboko nao wanapatikana Ngorongoro

Pundamilia

Tembo

Simba ambaye ni mmoja wa wanyama mashuhuri watano wanaojulikana kama The Big Five akiwa Ngorongoro


Ziara ikiendelea katika bonde la Ngorongoro














 

MAWAZIRI EAC WAAZIMIA KUONGEZA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA AFYA


Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akichangia mada kwenye Mkutano wa 24 wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Afya wa Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dar es Salaam, Mei 3, 2024.

Mawaziri wanaosimamia Sekta ya Afya katika Nchi Wanachama wa Jumuiya Afrika Mashariki wameweka mikakati na kukubaliana kuongeza ushirikiano zaidi katika kuboresha utoaji wa huduma katika sekta hiyo.

Azma hiyo imefikiwa leo tarehe 3 Mei 2024 kwenye Mkutano wa Kawaida wa 24 wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Afya wa Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dar es Dar es Salaam.

Mawaziri hao wamekutana kupitia na maboresho ya mikakati itakayosaidia kutatua changamoto zinazo changia kuzorota kwa ustawi wa sekta ya afya katika Jumuiya.

Sambamba na kufikia azma hiyo Mawaziri hao wamekubaliana kufanya kazi kwa pamoja ili kuimarisha mifumo na miundombinu ya utoaji wa huduma za afya ikiwemo uimarishaji wa maabara, maboresho ya programu mbalimbali za afya, maboresho ya mafunzo kwa wataalam wa afya, maboresha ya sera za afya, utafiti na ufuatiliaji.

Vilevile wamejadili na kuweka mikakati mahsusi ya kukabiliana na ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo kisukari na shinikizo la juu la damu. Mikakati hiyo ni pamoja na kuwashauri na kuwahamasisha wananchi uzingatiaji wa mlo kamili, kufanya mazoezi na kuacha au kupunguza matumizi ya pombe. 

Akizungumza katika mkutano huo Waziri wa Afya nchini Mhe. Ummy Mwalimu ameeleza kuwa Tanzania inaendelea na utekelezaji wa mikakati hiyo, ambapo amebainisha kuwa katika suala la uhamasishaji wa ufanyaji mazoezi Serikali imechukua hatua ya kufunga daraja la Tanzanite la jijini Dar es Salaam kwa kila Jumamosi ili kuruhusu wananchi kufanya mazoezi katika daraja hilo. 

Mbali na hayo Mawaziri hao wamejadili kuhusu namna ya kukabliana na changamoto mbalimbali zinazochangia kuzorota kwa sekta hiyo katika Jumuiya. Wametaja changamoto hizo kuwa ni Mabaliko ya Tabia Nchi, uhaba wa fedha za kuendesha programu na miradi mbalimbali ya afya, milipuko ya magonjwa, kuzuka kwa vita na mapigano kwenye baadhi ya maeneo katika Jumuiya, uhaba wa wataalam na miundombinu isiyotosheleza mahitaji ikiwemo vituo vya afya na vifaa tiba. 

Katika kukabiliana na changamoto hizo wamepitisha mikakati ya kukabiliana nazo ikiwemo kuimarisha mfumo wa ununuzi wa dawa kwa pamoja, kupitisha mpango mkakati wa pamoja wa masuala ya afya wa Jumuiya kwa mwaka 2024/2030, kuimarisha ufuatiliaji na utambuzi wa wagonjwa, kukamilisha na kuwasilisha andiko la kuomba fedha za kukabiliana na majanga, kuimarisha afua za kinga ili kutokomeza malaria katika Jumuiya na kuendelea kusimamia Vyuo Vikuu vya Afya ili viendelee kutoa elimu bora ndani ya Jumuiya. 

Mkutano huo uliofanyika kwa siku tano kuanzia terehe 29 Aprili hadi tarehe 3 Mei 2024 uliaanza katika Ngazi ya Wataalam ambapo pamoja na masuala mengine walikufanya tathimini ya utekelezaji wa maagizo na makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa 23 wa Baraza hilo. Tarehe 2 Aprili 2024 uliendelea katika Ngazi ya Makatibu Wakuu na kuhitimishwa na Mkutano wa Mawaziri tarehe 3 Mei 2024.
Mawaziri na Makatibu Wakuu wanaosimamia Sekta ya Afya katika nchi Wanachama wa Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja
Makatibu Wakuu wanaosimamia Sekta ya Afya na Elimu katika nchi Wanachama wa Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja
Sehemu ya Ujumbe wa Tanzania wakifuatilia Mkutano wa 24 wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Afya wa Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dar es Salaam, Mei 3, 2024.

Bi. Judith Ngoda Afisa Uchumi Mkuu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akifuatilia Mkutano wa 24 wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Afya la Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea jijini Dar es Salaam, Mei 3, 2024.
Mkutano wa 24 wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Afya wa Afrika Mashariki ukiendelea 

Thursday, May 2, 2024

BALOZI MBAROUK AFUNGUA MKUTANO WA NNE WA BARAZA LA WAFANYAKAZI LA WIZARA

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amefungua Mkutano wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara uliofanyika jijini Arusha.



Akifungua Mkutano huo, Mhe. Balozi Mbarouk amewasihi  Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuendelea kubuni maeneo ya kimkakati ya ushirikiano ambayo yatakuza na kuendeleza ushawishi wa Tanzania katika majukwaa ya Kikanda na Kimataifa.



“Nichukue fursa hii kuwasihi kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia weledi na ubunifu, muendelee kubuni maeneo ya kimkakati ya ushirikiano ili kuimarisha uhusiano wa uwili, kikanda na Kimataifa kuendeleza ushawishi wa Tanzania katika majukwaa ya kimataifa,” alisisitiza Balozi Mbarouk.


Amesema Wizara inaandelea na kazi ya uandaaji wa Mkakati wa Kitaifa wa utekelezaji wa  Diplomasia ya Uchumi ambao kukamilika kwake kutachochea ufanisi na kuleta tija katika kukuza Ushirikiano wa kiuchumi na kijamii katika ngazi ya uwili, kikanda na kimataifa.

 


Amewataka wafanyakazi wa Wizara kuimarisha ushirikiano, uhusiano na maelewano miongoni mwao huku wakiendelea kufanya kazi kwa weledi, ujuzi wa hali ya juu ili kuleta tija na ufanisi kwa taifa.



Pia amewapongeza wajumbe wa Baraza kwa kazi nzuri ya kuwawakilisha wafanyakazi wengine katika Baraza hilo.



Awali akizungumza kwenye mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo amesema Wizara itaendelea kushughulikia changamoto mbalimbali za Wafanyakazi na kuboresha mazingira ya kazi ili kuhakikisha utekelezaji wa majukumu ya Wizara unakamilishwa kwa tija na ufanisi.

 


Naye Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Wizara, Bi Pili Sukwa ameawaasa Watumishi wa Wizara kuendelea kutii sheria, kanuni  taratibu na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Viongozi wa Wizara na Serikali kwa ujumla ili kwa pamoja kufikia malengo tarajiwa.



Mkutano huo, pamoja na mambo mengine umepokea taarifa mbalimbali za utekelezaji wa majukumu ya Wizara pamoja na kupokea na kujadili Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kabla ya kuwasilishwa kwenye Bunge la Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania.


Naibu Waziri wa Mambo na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) akifungua Mkutano wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara lililofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 02 Mei, 2024

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi na Mwenyekiti wa Baraza   Baraza la Wafanyakazi la Wizara, Dkt. Samwel Shelukindo  akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza hilo lililofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 02 Mei, 2024

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anyeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi akizungumza wakati wa Mkutano wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara uliofanyika jijini AICC jijini Arusha tarehe 02 Mei 2024


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaibu Mussa  akichangia jambo wakati wa Mkutano wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara uliofanyika jijini Arusha tarehe 02 Mei 2024

Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Chiku Kiguhe akiwasilisha taarifa kuhusu masuala ya Utawala kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wakati wa Mkutano wa Nne wa Baraza hilo uliofanyika AICC jijini Arusha tarehe 02 Mei 2024

Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara wakifuatilia mkutano huo katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 02 Mei, 2024

Mjumbe wa Mkutano wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara Bw. Emmanuel Mwasabwite akichangia kitu wakati wa mkutano huo katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 02 Mei, 2024


Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara wakifuatilia mkutano huo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 02 Mei 2024
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara wakifuatilia mkutano huo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 02 Mei, 2024

Meza Kuu wakifuatilia Mkutano wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara wakifuatilia mkutano huo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 02 Mei, 2024

Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara wakifuatilia mkutano huo katika  Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 02 Mei, 2024

Sekretarieti ya Mkutano wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara wakinukuu masuala mbalimbali yaliyojadiliwa katika mkutano wa nne wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 02 Mei, 2024

Mgeni rasmi ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (wa tano kushoto walioketi) pamoja na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo (wa nne kushoto walioketi) wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Mkutano wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara  baada ya ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 02 Mei 2024  



 

Tuesday, April 30, 2024

MAWAZIRI WA URATIBU WA SERA ZA MAMBO YA NJE EAC WAKUTANA DAR ES SALAAM

Mkutano wa 14 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Uratibu wa Sera za Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umefanyika leo tarehe 30 Aprili 2024 jijini Dar es Salaam. 

Mkutano huo wa ngazi ya Mawaziri umepokea taarifa ya utekelezaji wa maelekezo na maazimio yaliyofikiwa katika Mikutano iliyotangulia ya Baraza hilo katika Sekta ya Uratibu wa Sera za Nje, iliyowasilishwa baada ya Mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu uliofanyika tarehe 27 Aprili 2024.

Mbali na kupokea taarifa hiyo Mawaziri hao pia wamejadili mapendekezo ya maeneo ambayo Nchi Wanachama zinaweza kuwa na msimamo wa pamoja katika majukwaa ya kimataifa, utoaji wa hadhi maalum ya uangalizi kwa kamisheni na mashirika ya kimataifa, Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Uratibu wa Sera za Nje na suala la kuwa mwakilishi wa Jumuiya katika Umoja wa Afrika. 

Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo uliohudhiriwa na Nchi zote Wanachama wa Jumuiya, umeongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato.

Aidha Mkutano huo ulifuatiwa na Mkutano wa 12 wa Pamoja wa Mabaraza ya Kisekta ya Mawaziri wa Ushirikiano katika Ulinzi, Mambo ya Ndani na Uratibu wa Sera za Mambo ya Nje.

Akifungua Mkutano huo uliohusisha sekta tatu Naibu Katibu Mkuu, Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki anayesimamia miundombinu, uzalishaji, jamii na siasa Bw. Andrea Ariik Malueth, ameeleza kuwa mkutano huo pamoja na masuala mengine una jukumu kubwa la kuhakikisha unalinda misingi, uhuru na kuimarisha ulinzi na usalama katika Jumuiya. 

Hali kadhalika Mkutano huo ngazi ya Mawaziri ulikuwa makhususi kwa ajili ya kupokea na kujadili taarifa iliyowasilishwa kwao na mkutano ngazi ya Makatibu Wakuu wanaosimamia masuala ya Ulinzi, Mambo ya Ndani na Sera za Mambo za Nje katika nchi Wanachama.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato achangia mada kwenye Mkutano wa 14 wa Baraza la Kisekta Mawaziri wa Uratibu wa Sera za Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dar es Salaam, 30 Aprili 2024
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax akichangia mada kwenye Mkutano wa 12 wa Pamoja wa Mabaraza ya Kisekta ya Mawaziri wa Ushirikiano katika Ulinzi, Mambo ya Ndani na Uratibu wa Sera za Mambo ya Nje wa EAC uliofanyika jijini Dar es Salaam, 30 Aprili 2024
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayesimamia masuala ya EAC Mhe. Stephen Byabato akichangia mada kwenye Mkutano wa 14 wa Baraza la Kisekta Mawaziri wa Uratibu wa Sera za Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dar es Salaam. Pamoja naye ni Katibu Mkuu, Balozi Stephen Mbundi (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama Bi. Mwanamridu Amity Jumaa (kulia).
Mkutano wa 14 wa Baraza la Kisekta Mawaziri wa Uratibu wa Sera za Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ukiendelea
Meza kuu wakiongoza Mkutano
Sehemu ya ujumbe wa Tanzania wakifuatilia Mkutano wa 12 wa Pamoja wa Mabaraza ya Kisekta ya Mawaziri wa Ushirikiano katika Ulinzi, Mambo ya Ndani na Uratibu wa Sera za Mambo ya Nje wa EAC uliokuwa ukiendelea jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya washiriki wakifuatilia Mkutano wa 12 wa Pamoja wa Mabaraza ya Kisekta ya Mawaziri wa Ushirikiano katika Ulinzi, Mambo ya Ndani na Uratibu wa Sera za Mambo ya Nje wa EAC uliokuwa ukiendelea jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya ujumbe wa Tanzania wakifuatilia Mkutano wa 12 wa Pamoja wa Mabaraza ya Kisekta ya Mawaziri wa Ushirikiano katika Ulinzi, Mambo ya Ndani na Uratibu wa Sera za Mambo ya Nje wa EAC uliokuwa ukiendelea jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya washiriki wakifuatilia Mkutano wa 12 wa Pamoja wa Mabaraza ya Kisekta ya Mawaziri wa Ushirikiano katika Ulinzi, Mambo ya Ndani na Uratibu wa Sera za Mambo ya Nje wa EAC uliokuwa ukiendelea jijini Dar es Salaam.