Monday, July 23, 2018
Sunday, July 22, 2018
Waziri Mkuu wa Korea atembelea NIDA na Hospitali ya Mnazi Mmoja
Mhe. Nak-Yon akiweka saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye kituo hicho. |
Maafisa wa vyombo vya Ulinzi na Usalama nchini wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yanaendelea kutolewa kwa mgeni rasmi. |
Juu na chini ni seemu ya ujumbe wa mhe. Nak-Yon pamoja na ujumbe kutoka Tanzania wakisikiliza maelezo yaliyokuwa yanatolewa. |
Mhe. Nak-Yon akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza ziara yake kwenye kituo hicho cha kuhifadhia kumbukumbu cha Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). |
*******Hospitali ya Mnazi Mmoja*******
Mhe. Jafo akimtambilisha kwa Waziri Mkuu, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema mara baada ya kuwasili hospitali ya Mnazi Mmoja. |
Mhe. Nak-Yon akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa Madaktari wa Mmnazi mmoja kuhusu matumizi ya kifaa cha maabara. |
Mhe. Nak-Yon akisalimiana na wagonjwa waliokuwepo hospitalini hapo |
Mhe. Nak-Yon akimkabidhi zawadi mmoja wa wamama aliyejifungua Mtoto wa kike ambaye mtoto wake alipewa jina Laura na Mwaziri Mkuu huyo. |
Mhe. Nak-Yon akikabidhi msaada wa magari mawili ya kubebea wagonjwa kwa Mhe. Jafo mara baada ya kumaliza kuitembelea Hospitali hiyo. |
Mhe. Nak-Yon akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali waliohudhuria tukio la kukabidhiwa kwa magari hayo. |
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea Mhe. LEE NAK-YON awasili nchini
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Mkuu wa Korea Mhe. Nak-Yon mara baada ya kuwasili nchini. |
Mhe. Nak - Yon akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Korea Mhe. Matilda Masuka |
Mhe. Majaliwa pamoja na mgeni wake Mhe. Nak - Yon pamoja na Dkt. Mahiga wakitizama kikundi cha ngoma kilichoandaliwa kusherehesha kwenye mapokezi hayo |
Friday, July 20, 2018
Makatibu Wakuu Wizara ya Mambo ya Nje na Wizara ya Habari wakutana kwa kikao kazi
Thursday, July 19, 2018
Ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea nchini Tanzania
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
ZIARA YA WAZIRI MKUU WA
JAMHURI YA KOREA
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea, Mhe. Lee Nak-yon atafanya ziara ya
kikazi nchini kwa mwaliko wa mwenyeji wake, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), kuanzia tarehe 21 hadi 23
Julai 2018. Ziara hiyo itakuwa ya kwanza kufanywa na kiongozi wa ngazi ya juu
kutoka Jamhuri ya Korea tangu nchi zetu mbili zianzishe mahusiano ya
kidiplomasia mwaka 1992.
Madhumuni ya ziara hiyo ni kuimarisha ushirikiano na uhusiano wa
kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili na kufungua zaidi fursa za ushirikiano wa
kibiashara na kiuchumi katika ngazi na sekta mbalimbali. Mhe. Waziri Mkuu Lee atafuatana
na ujumbe mzito wa maafisa wa Serikali, wabunge na wafanyabiashara wakubwa. Ujumbe
wa wafanyabiashara utakaoongozana na Mhe. Lee unatarajiwa kukutana na wenzao wa
Tanzania katika Mkutano wa Pili wa Jukwaa la Wafanyabiashara uliopangwa
kufanyika jijini Dar es Salaam tarehe 23 Julai 2018. Mkutano wa kwanza ambao
ulikuwa na mafanikio makubwa ulifanyika Seoul mwezi Februari 2018.
Mhe. Lee Nak-yon atawasili nchini saa kumi na mbili na nusu jioni (12:30)
ya tarehe 21 Julai 2018 na atapokelewa na mwenyeji wake Mhe. Kassim Majaliwa
Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Siku
inayofuata, Waziri Mkuu Lee na mwenyeji wake Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa
(Mb.), watafanya mazungumzo rasmi jijini Dar es Salaam na baadaye watashuhudia
uwekaji saini wa mkataba wa kuondoa hitaji la visa kwa wenye hati za kusafiria
za kidiplomasia na za utumishi (diplomatic and official/service passport).
Aidha, Mhe. Lee atakutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli kwa ajili ya kusalimiana.
Jamhuri ya Korea ni mshirika mkubwa wa maendeleo wa Tanzania
ambapo kupitia Shirika la Kimataifa la
Maendeleo (KOICA) na Mfuko wa Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo (EDCF)
yamekuwa yakitoa misaada na mikopo mingi ya masharti nafuu kwa Tanzania ikiwemo
misaada ya fedha katika bajeti, ujenzi wa miundombinu ya jamii, mafunzo ya muda
mfupi na mrefu, wataalamu mbalimbali wa kujitolea, vifaa na mashine kwa ajili
ya sekta mbalimbali ikiwemo ya afya.
Baadhi ya miradi ambayo imegharamiwa na Serikali ya Korea ni
pamoja na Mradi wa kuboresha Huduma ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya
Chanika, Mradi wa Mfumo wa Usajili wa Meli na Mabaharia kwa Njia ya Mtandao
Zanzibar, Mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya Taifa ya Taaluma na Tiba (MUHAS)
kampasi ya Mloganzila na ujenzi wa daraja katika mto Malagarasi.
Vile vile, Korea ni mshirika mkubwa katika kusaidia maendeleo ya
Bara la Afrika ambapo hivi karibuni katika mkutano wa Sita wa Jukwaa la
Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea na Africa (KOAFEC VI) uliofanyika mwezi
Mei 2018, Busan, Korea ambapo Serikali ya Korea ilitangaza msaada wa Dola za Marekani bilioni 5 kwa ajili ya
Bara la Afrika kwa kipindi cha mwaka 2018/2020. Tanzania ni miongoni mwa nchi zitakazonufaika
na msaada huo.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam
19 Julai 2018
Wednesday, July 18, 2018
Mabalozi wanne waagwa jijini Dar Es Salaam
Dkt. Mahiga akizungumza kwenye hafla ya kuwaaga Waheshimiwa Mabalozi walio maliza muda wao wa uwawakilishi nchini. |
Sehemu ya Mabalozi walio hudhuria hafla hiyo wakisimsikiliza kwa makini Mhe. Dkt. Mahiga (hayupo pichani). |
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya naAmerika, Bw. Jestas Nyamanga (kulia) pamoja na Balozi Rangnitt nao wakimsikiliza kwa makini Dkt. Mahiga. |
Sehemu nyingine ya Mabalozi waliohudhuria hafla hiyo |
Mabalozi walio maliza muda wa uwakilishi nchini wakigonga glasi na Waziri Mahiga ikiwa ni ishara ya kuwatakia Viongozi wa Nchi zao Afya njema na Baraka tele kwenye kufanikisha gurudumu la maendeleo. |
Balozi wa Malawi naye alipewa Picha yenye tembo wa Tatu na mlima Kilimanjaro |
Dkt. Mahiga akimkabidhi Balozi wa Norway picha inayofanana na wenzake isipokuwa yake ilikuwa na Michoro ya Wanyama aina ya Twiga, Tembo pamoja na Mlima Kilimanjaro. |
Balozi wa Canada naye alipata zawadi ya picha yenye mchoro wa Tembo pamoja na Mlima Kilimanjaro, kwa pamoja Mabalozi hao walionyesha kuzifurahia zawadi hizo. |
Dkt. Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi waliomaliza muda wa uwakilishi nchini pamoja na Mabalozi ambao bado wanaendelea kuziwakilisha nchi zao. |
Tuesday, July 17, 2018
Waziri Mahiga apokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Kenya nchini
Dkt. Mahiga akiendelea na mazungumzo na Balozi Mteule wa Kenya hapa nchini |
Balozi Kazungu akimweleza jambo Dkt. Mahiga |
Mazungumzo yakiendelea kati ya Dkt. Mahiga na Balozi Kazungu |
Picha ya pamoja. |
Dkt. Mahiga akiagana na Balozi Mteule wa Kenya nchini Tanzania. |
Thursday, July 12, 2018
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU FURSA ZA MASOMO
TAARIFA
KWA VYOMBO VY HABARI
FURSA
ZA UFADHILI WA MASOMO
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imepokea fursa za ufadhili
wa masomo katika kozi mbalimbali kutoka Serikali ya Saudi Arabia.
Mafunzo
hayo yatatolewa katika Chuo Kikuu cha Imam Abdulrahman bin Faisal kilichopo
Saudi Arabia. Taarifa kamili kuhusu ufadhili, kozi na taratibu zote za namna ya
kuomba zinapatikana kupitia tovuti ya Chuo hicho www.iau.edu.sa
Imetolewa na:
Kitengo cha
Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya
Nje Na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam
12 Julai, 2018
Tuesday, July 10, 2018
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki yaendelea kutoa huduma kwenye maonesho ya sabasaba
![]() |
Mhe. Balozi Rajab Luhwavi Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji (wa kwanza kulia) akizungumza na baadhi ya watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alipotembelea banda la Wizara hiyo kwenye maonesho ya sabasaba. |
![]() |
Bw. Teodos Komba akifanunua jambo kwa mteja aliyembelea banda la Wizara kwenye maonesho ya sabasaba |
![]() |
Wanafunzi kutoka Dar es Salaam Islamic Secondary School wakipewa maelezo walipotembelea banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye maonesho ya sabasaba |
![]() |
Balozi Ramadhani Mwinyi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiangalia bidhaa kwenye maonesho ya sabasaba |
![]() |
Balozi Ramadhani Mwinyi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiangalia bidhaa kwenye maonesho ya sabasaba |
![]() |
Balozi Ramadhani Mwinyi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akitoka kuangalia bidhaa kwenye jengo la Zanzibar katika maonesho ya sabasaba |
Subscribe to:
Posts (Atom)