Sunday, September 22, 2013

Mhe. Rais Kikwete awasili New York kuhudhuria Kikao cha 68 cha Umoja wa Mataifa



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi mara baada ya kuwasili katika Hoteli ya JW Marriot ya Jijini New York, Marekani. Mhe. Rais Kikwete na Ujumbe wake yupo nchini Marekani kwa ajili ya kuhudhuria Kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) kinachofanyika kuanzia tarehe 17 Septemba hadi 20 Desemba, 2013.


Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Waziri wa kazi na Utumishi wa Umma wa Zanzibar, Mhe. Haroun A. Suleiman

 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) naye akiwasili katika Hoteli ya JW Marriot akiwa amefuatana na Balozi Mushy (kulia) pamoja na Msaidizi wake Bw. Togolani Mavura.





 
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Naibu Mwakilishi wa Kudumu katika Ubalozi wa Tanzania, New York, Mhe. Balozi Ramadhan Mwinyi.
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi wa Iadara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy.






Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Robert Kahendaguza.

Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na  , Bw. Yusuph Tugutu mmoja wa Maafisa katika Ubalozi wa Tanzania, New York waliofika kumpokea Hotelini hapo.
 

Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na  m Bw. Noel Kaganda, Afisa katika Ubalozi wa Tanzania, New York.
 

Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na  Bi. Ramla Khamis mmoja wa Maafisa utoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
 
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na  Bi. Tully Mwaipopo mmoja wa Maafisa katika Ubalozi wa Tanzania, New York.

Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Bibi. Ellen Maduhu mmoja wa Maafisa katika Ubalozi wa Tanzania, New York.
 
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na  Bibi Maura Mwingira mmoja wa Maafisa katika Ubalozi wa Tanzania, New York.
 
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Bw. Grayson Ishengoma, Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
 
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Bi. Tuma Abdallah, Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti la Daily News

Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Bi. Anna Nkinda, Afisa Kutoka Idara ya Habari (MAELEZO).
 

Na Rosemary Malale, New York
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini New York, Marekani tarehe 21 Septemba, 2013 kwa ajili ya kuhudhuria kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (The 68th Session of the United Nations General Assembly (UNGA 68TH) kinachoendela mjini hapa kuanzia tarehe 17 Septemba hadi 20 Desemba, 2013.
 
Kikao hicho kimeazimia kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili dunia kiusalama, kiuchumi, kisiasa na kijamii. Kaulimbiu ya Mjadala Mkuu (General Debate) ni “Post-2015 Development Agenda: Setting the Stage”. Aidha, Mhe. Rais Kikwete, anatarajiwa kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 26 Septemba, 2013.
 
Pamoja na Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kulihutubia Baraza hilo, Mhe. Rais atashiriki mikutano mingine yenye manufaa kwa maendeleo ya Taifa ikiwemo:-  Mkutano wa Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC) kwa ajili ya ufadhili wa miradi ya Awamu ya Pili baada ya Awamu ya Kwanza kumalizika; Mkutano kuhusu Usalama wa Chakula na Lishe; Mkutano wa Kamati ya Marais wa Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi.
 
Mingine ni Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali kuhusu biashara haramu ya Wanyamapori na uvunaji haramu wa Magogo; Mkutano kuhusu maendeleo ya Wanawake na Watoto; Mkutano wa Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) kuhusu hali nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC); na Mkutano kuhusu kuongeza kasi ya utekelezaji wa Malengo ya Milenia.
 
Katika hatua nyingine, Mhe. Rais atapata nafasi ya kukutana na Viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Rais wa Marekani, Mhe. Barack Obama; Waziri Mkuu wa Norway, Mhe. Jes Stoltenberg; Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Ban Ki-moon; Mkurugenzi Mtendaji wa MCC, Bw. Daniel Yohannes na Viongozi wa Makampuni mbalimbali.
 
Aidha, pamoja na mikutano ya ngazi ya juu, Kikao cha Baraza Kuu pia hujumuisha mikutano ya Wataalam kupitia Kamati Sita za Umoja wa Mataifa ambazo ni Kamati inayoshughulikia masuala ya Upokonyaji na Upunguzaji Silaha Duniani; Kamati ya Uchumi na Fedha; Kamati ya Kijamii na Haki za Binadamu; Kamati inayoshughulikia masuala ya Ukombozi Duniani; Kamati ya Bajeti na Utawala; na Kamati ya masuala ya Sheria.
 
Viongozi wengine watakaoambatana na Mhe. Rais Kikwete ni pamoja na Mke wa Rais, Mhe. Mama Salma Kikwete; Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.); Waziri wa Kazi Zanzibar, Mhe. Haroun Ali Suleiman; Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Khamis Kagasheki (Mb.); Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Hussein Mwinyi (Mb); na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Mhe. Terezya Huvisa (Mb.).
 
Wengine ni Mhe. Khalifa Suleiman Khalifa (Mb.), Mhe. Anastazia Wambura (Mb); Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango; na Maafisa Waandamizi kutoka Serikalini.
 
-Mwisho-




Saturday, September 21, 2013

RAIS KIKWETE ATUNUKIWA SHAHADA YA UZAMIVU YA CHUO KIKUU CHA GUELPH JIMBONI ONTARIO, CANADA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitunukiwa Shahada ya Uzamivu na Provost na Makamu wa Rais wa Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario, Dkt Maureen Mancuso , Ijumaa Septemba 20, 2013.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Wakuu wa Chuo Kikuu Guelph pamoja na na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario Ijumaa Septemba 20, 2013 Ijumaa Septemba 20, 2013.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa (kulia) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario Ijumaa Septemba 20, 2013.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Ijumaa, Septemba 20, 2013, ametunukiwa Shahada ya Uzamivu (PHD) na Chuo Kikuu cha Guelph katika jimbo la Ontario nchini Canada kwa kutambua mchango na uongozi wake katika kuleta mageuzi ya kilimo katika Afrika.
Viongozi wa Chuo hicho wanasema kuwa wamefanya uamuzi wa kumtunuku Rais Kikwete kutokana na jitihada zake za kukabiliana na changamoto zinazokabili kilimo, jitihada zake za kuleta usalama wa chakula na pia majaribio makubwa ya kuongeza matumizi ya technolojia katika kilimo cha Tanzania na Afrika.
Rais Kikwete ambaye amewasili Canada usiku wa Alhamisi, Septemba 19, 2013 akitokea Washington, D.C., Marekani ambako alikuwa kwa siku mbili akitokea Jimbo la California amekuwa Mtanzania wa kwanza kutunukiwa shahada ya juu kabisa katika historia ya Chuo hicho.
Chuo cha Guelph ni moja ya vyuo vikuu vinavyoheshimiwa zaidi katika Canada na duniani katika Nyanja za kilimo na kilianzishwa rasmi kama Chuo cha Kilimo cha Jimbo la Ontario Mei Mosi, mwaka 1874.
Chuo hicho ambacho kimejipatia umaarufu kutokana na ubora wa shughuli zake za utafiti kimekuwa katika mstari wa mbele kutafuta majawabu ya changamoto zinazoikabili dunia katika masuala ya kilimo, raslimali za maji, matatizo makubwa ya magonjwa ya mimea, matatizo ya ukuaji haraka wa miji duniani na changamoto za biashara za kimataifa.
Katika miaka ya karibuni kufuatia tishio kubwa kimataifa la ongezeko la bei za vyakula duniani na hasa katika nchi masikini, mabadiliko ya tabianchi, ongezeko la uchafuzi wa hali ya hewa, uharibifu wa mazingira, changamoto za upatikanaji wa maji safi na salama duniani, kazi ya Chuo hicho imeongezeka sana.
Chuo hicho kimeichagua Tanzania kama nchi ya kufanya nayo kazi katika Afrika kukabiliana na changamoto hizo na kimemtambua Rais Kikwete kutokana na mchango wake mkubwa katika sekta ya kilimo katika miaka yote ya uongozi wake na mipango yake ya kuboresha kilimo katika Tanzania kama ASDP, Kilimo Kwanza na SAGCOT ambayo yote inasifiwa sana kimataifa.
Chuo hicho kina mahusiano ya karibu na Vyuo Vikuu vya Dar es Salaam, Sokoine cha Mzumbe – Morogoro na UDOM – Dodoma. Kati ya mwaka jana na mwaka huu, Chuo hicho kimetiliana saini Makubaliano ya Ushirikiano (MOU) na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine cha Mzumbe – Morogoro na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Mara nne kati ya Januari, mwaka jana, 2012 na Juni, mwaka huu, 2013, uongozi wa Chuo hicho ukiongozwa na Rais na Makamu Mkuu wa Chuo, Dkt. Alastair Summerlee na Makamu wa Rais wa Utafiti Dkt. Kevin Hall umetembelea Tanzania na kukutana na viongozi wa Serikali pamoja na wale wa Vyuo Vikuu vya Dar Es Salaam na Sokoine cha Mzumbe, Morogoro.
Mbali na ujumbe ambao unaongozana na Rais Kikwete, sherehe za kutunukiwa kwa Kiongozi Mkuu huyo wa Tanzania pia zimehudhuriwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe, Jumuia ya Watanzania wanaoishi Canada pamoja na maofisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini humo.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu,

DAR ES SALAAM.

20 Septemba, 2013



Picha na habari kwa hisani ya:  www.ikulublog.com



Friday, September 20, 2013

Waziri Membe akiwa na Mabalozi wa Heshima


Mhe. Balozi Liberata Mulamula na Balozi wa Heshima Kjell Bergh kutoka Minnesota wakitia saini mkataba wa Ubalozi wa Heshima huku Afisa Paul Mwafongo (kushoto) na Afisa Suleiman Saleh (watatu toka kushoto) wakiwaelekeza.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard K. Membe (Mb), akimkabidhi mkataba mmoja wa Mabalozi wa Heshima Kjell Bergh kutoka Minnesota.
 

 Mhe. Balozi Liberata Mulamula na Balozi wa Heshima Hon. Charles Gray kutoka Pennsylvania wakitia saiini mkataba wa Ubalozi wa Heshima huku wakisaidiwa na Afisa Paul Mwafongo na Suleiman Saleh.


Mhe. Waziri Membe akiongea machache mara baada ya zoezi zima la utiaji saini wa Mabalozi wa Heshima kukamilika.  Kulia ni Afisa wa Habari wa Ubalozi Mindi Kasiga, ambaye alikuwa mshereheshaji wa hafla hiyo.
Mhe. Waziri Bernard K. Membe (Mb) (watatu kushoto), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wa Heshima nchini Marekani.  Wengine katika picha ni Mhe. Balozi Liberata Mulamula (wa nne kulia), Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico na Balozi Dora Msechu (wa pili kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.



Picha na maelezo kutoka Vijimambo blog


A Congratulatory Message to the Kingdom of Saudi Arabia




H.E. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a Congratulatory Message to His Royal Highness Abdullah bin Abdul Aziz Al Saud, King of the Kingdom of Saudi Arabia and the Custodian of the Two Holly Mosques on the occasion of marking the 83rd anniversary of the National Day.

The message reads as follows:
“His Royal Highness Abdullah bin Abdul Aziz Al Saud,
King of the Kingdom of Saudi Arabia,
Riyadh,
SAUDI ARABIA.

Your Royal Highness,

On behalf of the Government and the People of the United Republic of Tanzania and indeed on my own behalf, I would like to convey my warm congratulations to Your Royal Highness and through you, to the Government and the People of the Kingdom
of Saudi Arabia on the Occasion of the 83rd Anniversary to commemorate the National Day.

Over the years, Saudi Arabia and the United Republic of Tanzania have enjoyed strong ties of friendship and cooperation. It is my sincere hope that the traditional bonds of relationship between our countries will be cemented even further so as to enable us to jointly address matters of common interest.

As you commemorate this joyous occasion of your Country’s National Day, let me once again take this opportunity to reiterate my Government’s desire to further expand and strengthen the friendly relations and cooperation that exist between the two countries and Peoples for our mutual benefit.

Please accept, Your Royal Highness, my best wishes for your continued good health, progress and prosperity of the People of the Kingdom of Saudi Arabia.

Dr.Jakaya Mrisho Kikwete

PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA”




Issued by: 

The Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation, 

Dar es Salaam,


20th September, 2013.



Ziara ya Mhe. Rais Kikwete nchini Marekani







CALIFORNIA:  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya Watanzania waishio katika mji wa Vallejo jimbo la California nchini Marekani leo wakati Rais alipotembelea mji huo wa kibiashara kwa mwaliko wa meya wa mji huo Mstahiki Osby Davis.

WASHINGTON, DC:  Rais Dkt. Jakaya Kikwete akisaini kitabu cha wageni huku Mhe. Waziri Bernard Membe na Mhe. Balozi Liberata Mulamula wakishuhudia.

Rais Dkt. Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula.
 Rais Dkt. Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na Balozi wa Heshima Hon. Robert Samuel Shumake.

 Rais Dkt. Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na Balozi wa Heshima Hon. Kjell Bergh.

 Rais Dkt. Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na Balozi wa Heshima Hon. Cemil Teber.
 Rais Dkt. Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na Balozi wa Heshima Hon. Suzanne Alyce Terrell.
 Rais Dkt. Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na Balozi wa Heshima Hon. Charles Gray.



Rais Dkt. Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na Balozi wa Heshima Hon. Ahmed Issa na mkewe Cherry Julian.

Rais Dkt. Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na Balozi wa Heshima Hon. Dallas Browne. 


All photos courtesy of Vijimambo blog