Tuesday, December 3, 2013

Balozi Chabaka Kilumanga awasilisha Hati za Utambulisho nchini Comoro


Mhe. Dkt. Ikililou Dhoinine, Rais wa Muungano wa Visiwa vya Comoro akisoma Hati za Utambulisho za Mhe. Balozi Chabaka Kilumanga, katika Ikulu ya Beit Salaam, Moroni.



Mhe. Dkt. Ikililou Dhoinine wa Muungano wa Visiwa vya Comoro akiwa katika mazungumzo na Mhe. Balozi Chabaka Kilumanga mara baada ya kupokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi huyo. 















Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Visiwani Comoro, Mhe. Chabaka Kilumanga, leo tarehe 3 Desemba 2013 amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Dkt. Ikililou Dhoinine, Rais wa Muungano wa Visiwa vya Muungano wa Comoro.


Katika hafla hiyo iliyofanyika katika Ikulu ya Beit Salaam, Mhe. Balozi Kilumanga na Mhe. Rais Dhoinine walipata fursa ya kuzungumza machache katika muktadha wa kuimarisha uhusiano wa kihistoria na kindugu uliopo kati ya Tanzania na Comoro kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizo. Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Comoro pamoja na maafisa wa Ubalozi wa Tanzania mjini Moroni.

Kamati ya Bunge ya Biashara na Uchumi yatembelea Ubalozi Mdogo - Dubai


Bw. Omary Mjenga (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Bunge ya Biashara na Uchumi ilipotembelea Ubalozi Mdogo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Dubai hivi karibuni.


Uteuzi wa Dr. Asha-Rose Migiro



Monday, December 2, 2013

A Congratulatory Message to the UAE's 42nd National Day


H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania, has sent a congratulatory message to His Highness Sheikh Khalifa bin Zayed Al Nahyan, President of the United Arab Emirates and Ruler of Abu Dhabi, on the occasion of the 42nd Anniversary of the United Arab Emirates National Day.

The message reads as follows:

“His Highness, Sheikh Khalifa bin Zayed Al Nahyan,
President of the United Arab Emirates and Ruler of Abu Dhabi,
UNITED ARAB EMIRATES.

Your Highness,

On behalf of the Government and the People of the United Republic of Tanzania, and indeed on my own behalf, I would like to sincerely convey my warm congratulations to you, Your Highness and through you, to the Government and the People of the United Arab Emirates on this significant celebrations of the 42nd Anniversary of the United Arab Emirates National Day.

The United Arab Emirates and the United Republic of Tanzania have enjoyed cordial bilateral relations over the years. As you commemorate this joyous occasion of your country’s independence, I wish to take this opportunity to reiterate my Government’s desire and commitment to continue to further enhance the traditional bond of friendship and cooperation existing between our two countries for our mutual benefit.

Please accept, Your Highness, my most sincere congratulations and best wishes for the continued good health and happiness, and to the friendly People of the United Arab Emirates, further progress and prosperity.

Jakaya Mrisho Kikwete
PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA.”


Issued by:

The Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation,

Dar es Salaam,

2 December, 2013.




Saturday, November 30, 2013

Balozi Mero awasilisha hati za utambulisho kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara ya Kimataifa Duniani (WTO)


 Balozi Modest Mero, Balozi wa Tanzania  katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Geneva akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Bw. Roberto Azevedo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara ya Kimataifa  Duniani yaani World Trade Organisation(WTO) mjini Geneva, Uswisi.

  Balozi Modest Mero, Balozi wa Tanzania  katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Geneva katika mazungumzo.

Picha ya pamoja Balozi Mero, Mama Mero na Bw. Azevedo.


Mheshimiwa Balozi Modest Mero, Balozi wa Tanzania  katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Geneva amewasilisha hati za utambulisho kwa Bw. Roberto Azevedo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara ya Kimataifa  Duniani yaani World Trade Organisation(WTO) mjini Geneva, Uswisi.
 Katika mazungumzo,  Mkurugenzi Mkuu amemfahamisha Mh. Balozi  kuwa Shirika la Biashara Duniani liko katika hatua za mwisho kukamilisha  majadiliano ya mikataba ya  Biashara ya Kimataifa katika maeneo matatu kwa pamoja  ikiwa ni masuala ya  Kilimo,  Maendeleo na  Uwezeshaji Biashara.
  Aidha,  Mkurungenzi Mkuu alielezea  mahusiano mazuri aliyonayo na nchi yetu kwa kipindi  kifupi akiwa kama Mkurugenzi Mkuu,  na  kuwa aliliona hilo wakati wa kampeini yake alipokuja nchini kuomba kura yetu. Ni kwa mantiki hiyo na imani aliyo nayo kwa Tanzania, Mkurugenzi huyo ameomba Tanzania itumie ushawishi wake ili kufanikisha mkutano wa Mawaziri wa Biashara utakaofanyika mjini Bali Indonesia kuanzia tarehe 3-6 December 2013, ili kupitisha mikataba ya Biashara katika maeneo  matatu yaliyotajwa hapa juu.



Friday, November 29, 2013

A Condolence message to Islamic Republic of Iran


H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania  has sent a condolence message and sympathy to H.E. Hassan Rohani, President of the Islamic Republic of Iran.

The message reads as follows:

“H.E Hassan Rohani,
President of the Islamic Republic of Iran,
TEHRAN,
IRAN.

Your Excellency,

I learnt with immense shock on the terrorist act of explosions which took place near to the Embassy of the Islamic Republic of Iran in Beirut, Lebanon on 19th November, 2013 and caused martyrdom of the Iranian Cultural Counsellor, Spouse of the one Iranian Diplomat and a number of innocent people.

On behalf of the Government, the people of the United Republic of Tanzania and indeed on my own behalf, I would like to convey to you and through you to the Government and the people of the Islamic Republic of Iran our heartfelt condolence and profound sympathy to the occasion of explosion in Beirut.

In this time of grief, we pray to the Almighty Allah to give the family of the bereaved strength and courage during this difficult period and we also wish the survivors quick recovery.

Please accept, Your Excellency and dear Colleague, the assurance of my highest consideration.

Jakaya Mrisho Kikwete
PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA.”


Issued by:

The Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation,

Dar es Salaam,

29 November, 2013.




Wakurugenzi wa Sera na Mipango wapigwa msasa kuhusu maandalizi ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia



Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais-Tume ya Mipango, Bw. Philp Mpango akiwakarabisha Wakurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara na Taasisi nyingine za Serikali pamoja na wageni waalikwa katika kongamano ambalo mzungumzaji alikuwa Balozi Celestine Mushy, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kongamano hilo lilifanyika jengo la Golden Jubilee jijini Dar es Salaam. 


Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akiwasilisha mada yake kwa wajumbe. Mada hiyo ilihusu mchakato wa kuandaa Malengo ya Maendeleo Endelevu na Agenda ya Maendeleo baada ya mwaka 2015 ambao ni mwaka wa mwisho wa kutekeleza Malengo ya Milenia (Sustainable Development Goals and Post 2015 Development Agenda). Balozi Mushy alisisitiza umuhimu wa taasisi zote husika kushiriki katika vikao vya maandalizi vya mchakato huo au wakishindwa kushiriki waandae taarifa za maandishi ili watakaoshiriki waziwasilishe.


Balozi Mushy akiendelea na mada yake.


Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nao wakisikiliza mada.


Balozi Mushy akibadilishana mawazo na mmoja wa wajumbe wa kongamano hilo baada ya kumaliza kazi ya kuwasilisha mada.