Tuesday, December 15, 2015

Balozi Dkt. Mahiga akutana na Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na iliyokuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula aliyesimama akitoa neno kabla ya kumkaribisha, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga   (katikati) kuongea na Wakuu wa Idara/Vitengo wa Wizara hiyo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Suzan Kolimba     
Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Balozi Mbelwa Kairuki (wa kwanza kushoto), Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi, Bw. Wilfred Masanja (wa kwanza kulia), na Kaimu Mkuu wa Idara ya Sera na Mipango, Bw. John Ngowo wakisikiliza kwa makini neno la ukaribisho kutoka kwa  Balozi Mulamula akimkaribisha Mhe. Waziri kuzungumza na Wakuu wa Idara/Vitengo.
Sehemu nyingine ya Wakurugenzi walioudhuria kikao hicho, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bw. Negel Msangi, Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora, Balozi Anisa Mbega (katikati) na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Balozi Innocent Shiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga (wa kwanza kulia), Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Itifaki Bi. Grace Martine (wa kwanza kushoto), Kaimu Mkurugenzi Idara ya Amerika na Ulaya, Bi. Tunsume Mwangolombe (wa pili kutoka kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Eva Ng'itu nao wakiwa kwenye mkutano wa Mhe. Waziri Mahiga na Mhe. Naibu Waziri Dkt. Kolimba (hwapo pichani).
Sehemu nyingine ya Viongozi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, Balozi Samuel Shelukindo, Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani Bw. Marthias Abisai (wa kwanza kushoto), na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Bw. Nassoro Msumi (katikati).  
Kikao kikiendele


========Kikao na Uongozi wa iliyokuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki========
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (wa pili kutoka kushoto), na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Suzani Kolimba (wa kwanza kushoto) wakimsiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Iliyokuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Joyce Mapunjo (wa pili kutoka kulia) katika kikao baina ya Mhe. Waziri na Wakuu wa Idara na Vitengo, wa iliyokuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Mwingine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu, Bw. Amantius Msole.
Mhe. Joyce Mapunjo akiwatambulisha Wakurugenzi wake (hawapo pichani) kwa Mhe. Waziri Mahiga na Naibu Waziri Kolimba
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Ulinzi na Siasa Bw. Amani Mwatonoka akijitambulisha kwa Mhe. Waziri Mahiga na Naibu Waziri Dkt. Kolimba (hawapo pichani).
Wakurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi wakifuatilia kwa makini kikao kilichokuwa kinaendelea.
Makatibu wa Mawaziri nao wakifuatilia kwa makini mkutano huo, wa kwanza kushoto ni Bw. Thobias Makoba, na Adam Isara (wa kwanza kulia).
Kikao kikiendelea
Picha na Reginald Philip


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Naibu Waziri wake, Mhe. Dkt. Suzan Kolimba waliwasili Wizarani kuanza kazi rasmi siku ya Jumamosi tarehe 12 Desemba 2015. Viongozi hao wapya wa Wizara walipokelewa na watumishi kwa shangwe walipowasili wizarani, muda mfupi baada ya kula kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika Ikulu ya Dar es Salaam.  

Siku ya kwanza Wizarani, Waheshimiwa Mawaziri walipata fursa ya kukutana na uongozi wa Wizara ukiongozwa na Katibu Mkuu, Balozi Liberata Mulamula na Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Joyce Mapunjo. Makatibu Wakuu hao pamoja na mambo mengine, walikabidhi kwa Waheshimiwa Mawaziri nyaraka muhimu za Wizara zitakazowaongoza katika utekelezaji wa majukumu yao.


Aidha, walitumia fursa hiyo kueleza utekelezaji wa majukumu ya Wizara na masuala ambayo yanahitaji miongozo yao ili yaweze kufanyiwa kazi na kukamilishwa.

Balozi Mahiga na Dkt. Kolimba walipata fursa pia ya kutembelea watumishi wa iliyokuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki siku ya tarehe 14 Desemba 2015 kwenye Jengo la Waterfront. Watumishi hao kama walivyofanya wenzao waliwapokea viongozi wapya kwa shangwe na baadaye kufanya kikao na Wakuu wa Idara na Vitengo.


Katika vikao vyote,  Mhe. Waziri aliomba ushirikiano kutoka kwa Wakuu wa Idara/Vitengo na watumishi wote kwa jumla ili kwa pamoja waweze kuendana na kasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye kaulimbiu ya “Hapa kazi tu”




Saturday, December 12, 2015

Waziri na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wakaribishwa rasmi katika Ofisi zao tayari kuanza kazi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Augustine Mahiga akisaini Kitabu cha Wageni alipowasili Ofisini kwake kwa mara ya kwanza baada ya kuapishwa. 
Mhe. Balozi Mahiga akifurahia jambo Ofisini kwake na Makatibu Wakuu wa Wizara ya  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,  Balozi Liberata Mulamula (kushoto) na Bibi Joyce Mapunjo (kulia).
Balozi Mulamula akimkabidhi Mhe. Waziri machapisho mbalimbali ya Wizara ikiwemo Sera ya Mambo ya Nje
Bibi Mapunjo akimkabidhi Mhe. waziri makabrasha mbalimbali ya iliyokuwa Wizara ya Afrika Mashariki
Mhe. Balozi Mahiga akipata picha ya pamoja na Watumishi walio katika Ofisi yake. Kutoka kulia ni Bi. Catherine Kijuu, Katibu Mahsusi wa Waziri, Bw. Thobias Makoba, Katibu wa Waziri na Bi. Nsia Paul, Katibu Mahsusi wa Waziri.
Balozi Mulamula wakati akimwongoza Mhe. Balozi Mahiga kuingia Ofisini kwake kwa mara ya kwanza

.....Naibu Waziri akiwa Ofisini

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Suzan Kolimba akisaini Kitabu cha Wageni alipowasili Ofisini kwake kwa mara ya kwanza baada ya kuapishwa. 
Balozi Mulamula akimkabidhi Mhe. Naibu Waziri machapisho mbalimbali ya Wizara ikiwemo Sera ya Mambo ya Nje
Mhe. Dkt. Kolimba akisaini Kitabu cha Wageni alipowasili Ofisini kwake kwa mara ya kwanza
Mhe. Dkt. Kolimba akiwa katika picha ya pamoja na Katibu wake, Bw. Adam Isara
Mhe. Dkt. Kolimba akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Wizara katika Ofisi yake. Kushoto ni Bi. Eva Mnembuka na Bi. Moshi Ibrahim (kulia)

Picha na Reginald Philip




Waziri na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wawasili rasmi Wizarani baada ya kuapishwa


Waziri wa Mambo wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Augustine Mahiga akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
Naibu Waziri wa Mambo wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Suzani Kolimba akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akimkaribisha  Wizarani kwa mara ya kwanza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Augustine Mahiga mara alipowasili Wizarani baada ya kuapishwa Ikulu tarehe 12 Desemba, 2015. Aliyesimama pembeni ni Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bibi Joyce Mapunjo.
Mhe. Balozi Mahiga akikaribishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Simba Yahya.
Mhe. Balozi Mahiga akipokea shada la maua kutoka kwa mmoja wa Watumishi wa Wizara Bi. Nsia Paul wakati wa mapokezi yake Wizarani
Naibu Waziri wa  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Suzan Kolimba akipokea shada la maua kutoka kwa mmoja wa Watumishi wa Wizara Bi. Tagie Mwakawago mara baada ya kuwasili rasmi Wizarani
Wakurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa wakimpokea Mhe. Waziri Wizarani. Pichani Mhe. Waziri akisalimiana na Balozi Anisa Mbega, Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora.
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa wakimkaribisha kwa shangwe na furaha Mhe. Balozi Mahiga Wizarani.
Mhe. Waziri akisalimiana na Watumishi wa Wizara waliojitokeza kumpokea mara baada ya kuwasili Wizarani rasmi baada ya kuapishwa.
Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bibi Mapunjo akijitambulisha rasmi kwa Waziri, Mhe. Balozi Mahiga na Mhe. Naibu Waziri, Mhe. Kolimba (kushoto).
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Simba Yahya akijitambulisha  rasmi kwa Waziri, Mhe. Balozi Mahiga na Mhe. Naibu Waziri, Mhe. Kolimba (kushoto). Mwingine katika picha ni Katibu Mkuu, Balozi Mulamula
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa akiongea jambo wakati wa mapokezi ya Mhe. Waziri na Naibu Waziri.
Waziri, Mhe. Balozi Mahiga kwa pamoja na Naibu Waziri, Mhe. Kolimba wakiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu, Balozi Mulamula na Bibi Mapunjo na Naibu Makatibu Wakuu, Balozi Yahya na Bw. Amantius Msole (wa kwanza kulia)
Picha ya pamoja

Picha na Reginald Philip

Kenya Embassy Celebrates 52 Independece Anniversary

Permanent Secretary at the Minisry of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation, Amb. Liberata Mulamula who was the Guest of Honor delivers a speech at the reception hosted by the Kenya Embassy to mark 52 years of Independence.

Kenyan Ambassador to Tanzania, H.E Chirau Ali Mwakwere presents a statement at the 52 Independece anniversary reception held at his residence yesterday.

Invited guests who were Diplomatic Community in the country, government officials and Private Sector follow attentively the statements delivered by the Guest of Honor and Kenyan Ambassador to Tanzania.

Permanent Secretary at the Minisry of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation, Amb. Liberata Mulamula (L) and Ambassador of Kenya to Tanzania, H.E Chirau Ali Mwakwere raise their glasses in a toast to the health of the Presidents of Tanzania and Kenya and prosperity of these two nations.

Director of Africa Department at the Minisry of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation, Amb. Samuel Shelukindo (L) exchanges views with Comoros Ambassador to Tanzania, H.E Dr. Ahamada El Badaoui Mohamed during the reception.

Amb. Mulamula (C) chats with the various Diplomats at the Reception.

Invited guests including Medard Ngaiza (R) official from the Ministry of Foreign Affairs enjoy their snacks during the reception.

Executive Director of the Tanzania Investment Centre (TIC), Ms. Juliet R. Kairuki shakes hands with Kenyan Embassy official during her arrival at the reception to mark 52 anniversary of Kenya Independence.

Friday, December 11, 2015

ushiriki wa Tanzania katika Mkutano wa Shirika la Msalaba Mwekundu Duniani jijini Geneva

Pichani ni ushiriki wa Tanzania katika Mkutano wa Shirika la Msalaba Mwekundu Duniani ambao Rais wa Msalaba Mwekundu Tanzania ambapo Dr. Zainab Amir Gama na Mh. Balozi Modest Mero wanashiriki jijini Geneva Uswisi.  Mkutano hio ulioanza tarehe 4 Desemba na utaisha leo tarehe 10 Disemba 2015. Huu ni mkutano mkuu wa Msalaba Mwekundu na Hilari Nyekundu wa dunia ambao maudhui ya mkutano huu ni mjadala na maamuzi ya uongozi, amani, uhamiaji na  unyanyasaji wa wanawake na watoto,  mpango wa kupanua huduma za kibinadamu kufikiakaribu bilioni moja ifikapo mwaka 2030,  umuhimu wa jumuiya za Msalaba Mwekundu na Hilari Nyekundu kuwa mdau mkuu wa serikali bila ya kwenda kinyume na misingi yao saba mwisho,  ushiriki wa vijana na  vile vile kuikaribisha nchi ya Tuvalu kuwa mwanachama wa 190.

Thursday, December 10, 2015

Tawi la TUGHE-Wanawake la Mambo ya Nje wakutana kupanga mikakati ya utendaji kazi

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje n aUshirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akiwa na Bibi Amisa Mwakawago, Mwenyekiti wa Tawi la TUGHE-Wanawale la Wizara katika Mkutano na wanachama wa Tawi hilo uliofanyika Wizarani hivi karibuni kujadili malengo mbalimbali waliyojiwekea katika utekelezaji wa majukumu ya kazi na yale yanayohusu maendeleo yao. Balozi Mulamula  pia ni Mama Mlezi wa Tawi la TUGHE Wanawake la Wizara.
Sehemu ya Wanawake wakimsikiliza Balozi Mulamula
Mmoja wa Wanachama, Bi. Mindi Kasiga akichangia wakati wa mkutano huo. Kulia ni Mjumbe wa Tawi, Bi. Grace Martin
Balozi Mulamula  kwa pamoja na Bi Mwakawago wakimsikiliza Bi. Kasiga (hayupo pichani) alipochangia mada
Katibu wa Tawi, Bi. Annagrace Rwalanda akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya agenda zilizowasilishwa wakati wa mkutano huo.
JUU NA CHINI: Sehemu ya wanachama wakifuatilia mkutano
Wanachama wakisikiliza hoja mbalimbali wakati wa mkutano

Sehemu nyingine ya wanachama

Wanachama wakifuatilia mada na matukio wakati wa mkutano huo