Tuesday, December 19, 2017

Matukio yanayojiri katika ziara ya kikazi ya Balozi Mahiga nchini China

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiongea jambo wakati alipokuwa katika mazungumzo rasmi na Naibu Waziri wa Biashara wa China, Mhe. Qian Keming jijini Beijing.
Naibu Waziri wa Biashara wa China, Mhe. Qian Keming akisisitiza jambo alipokuwa kwenye mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt.Augustine Mahiga leo jijini Beijing.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akiwa na ujumbe wake aliongozana nao katika ziara ya kikazi nchini China. Kutoka kushoto ni Mwambata Jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini China, Kanali Remigius Ng'umbi anayefuata ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Dkt. Thomas Kashililah na Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki.

Wajumbe wa pande mbili za China na Tanzania wakiwa katika mazungumzo.

Wajumbe wengine wa Tanzania wakifuatilia mazungumzo. Kutoka kulia ni Kamishna Msaidizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Malmeltha Mutagwaba, Naibu Katibu Mkuu wa Biashara na Uwekezaji kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchweishaija na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango kutoka Serikali ya Zanzibar, Bw. Khamis Omar 

Balozi Mahiga akitoa zawadi ya picha kwa Naibu Waziri wa Biashara wa China, Mhe. Qian Keming.

Mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Mipango ya China
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Mipngo ya China, Bw. Ning Jizhe alipowasili ofisini kwake kwa ajili ya kufanya mazungumzo.

Ujumbe wa Tanzania na China wakijadiliana namna nchi zao zitakavyoweza kushirikiano katika masuala ya uchumi, uwekezaji n biashara.

Bw. Jing Jizhe akionesha utayari wa nchi yake wa kushirikiana na Tanzania katika masuala ya maendeleo ya kiuchumi.
 Mazungumzo na wafanyakazi wa Ubalozi
Balozi Mahiga na ujumbe wake wakiwa katika mazungumzo na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini China.

Balozi Mahiga akiwa na katika mazungumzo na mmoja wa wawekezaji aliyedhmiria kuwekeza Tanzania.

Mwekezaji mwingine akisalimiana na Balozi Mahiga kabla ya kuanza kwa mazungumzo yao.

Waziri Mahiga akiwa katika mazungumzo na aliyekuwa Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt, Lu Youqing

Mhe. Balozi, Dkt. Ramadhani Dau awasilisha Hati za Utambulisho kwa Mtukufu Mfalme wa Cambodia

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malaysia anayewakilisha pia nchini Cambodia, Mhe. Dkt. Ramadhani Kitwana Dau (kushoto) akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mfalme wa Cambodia, Mtukufu Preah Bat Samdech Preah Boromneath NORDOM SIHAMON. Makabidhiano hayo yalifanyika tarehe 28 Novemba 2017 Jijini Phnom Pen, Cambodia.
Mhe. Balozi Dkt. Dau (wa pili kushoto) akiwa katika mazungumzo na Mtukufu Mfalme mara baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho. Wanaoshuhudia kulia ni maafisa wa Serikali ya Cambodia na kushoto ni Afisa wa Ubalozi wa Tanzania.

Mazungumzo yao yalijikita katika kuendeleza na kuimarisha uhusiano wa Kidiplomasia uliopo baina ya mataifa hayo ambao ulianzishwa rasmi mwaka 1995. Pia kuimarisha ushirikiano katika masuala ya biashara na uwekezaji. Vilevile Mtukufu Mfalme aliahidi kumpa ushirikiano Mhe. Balozi Dkt. Dau katika utekelezaji wa majukumu yake.



Mhe. Balozi Dkt. Dau akimtambulisha Afisa wa Ubalozi wa Tanzania, Bw. Khatib Makenga aliyeambatana naye katika hafla ya  makabidhiano ya Hati za Utambulisho

Mhe. Balozi Dkt. Dau akipokelewa mara baada ya kuwasili jijini Phnom Penh, Cambodia. 

Thursday, December 14, 2017

Rais Dkt. John Pombe Magufuli ampokea Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mgeni wake Rais wa Msumbiji Mhe.Filipe Nyusi wakipita kwenye gadi ya heshima iliyoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakati Rais huyo akiwasili katika uwanja wa ndege wa mjini Dodoma

Vikundi vya ngoma za jadi vikisherehesha katika shughuli za mapokezi ya Rais wa Msumbiji Mhe.Filipe Nyusi katika uwanja wa ndege wa mjini Dodoma


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mgeni wake Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi wakati akimpokea mjini Dodoma. Rais Nyusi amewasili leo mjini Dodoma kwa ziara ya kikazi ya siku moja na kupokelewa na mwenyeji wake Rais Magufuli, kabla ya kuelekea Ofisini kwa mazungumzo. Katika mazungumzo yao wamejadili na kukubaliana masuala mbalimbali ya kukuza na kuendeleza ushirikiano uliodumu kwa muda mrefu baina ya Mataifa haya mawili (Tanzani na Msumbiji). Aidha Rais Magufuli na Rais Nyusi wamekubaliana kuanzisha ushirikiano katika masuala mbalimbali ya kiuchumi ikiwemo katika sekta ya gesi usafiri wa anga na miundombinu.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Rais wa Msumbiji Mhe.Filipe Nyusi alipowasili uwanja wa ndege wa mjini Dodoma kwa ziara ya kikazi ya siku moja


        Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.               Dkt.  John Pombe Magufuli  akiwa na Mgeni wake Rais wa Msumbiji Mhe.Filipe Nyusi katika Ikulu ndogo ya Mjini Dodoma kabla ya kuanza mazungumzo yao

Wednesday, December 13, 2017

TANZANIA'S POSITION ON THE STATUS OF JERUSALEM



TANZIA


TANZIA

Marehemu Mama Badriya Kiondo
Familia za Bw. Kiondo wa Kwaminchi Tanga na Bw. Ramadhan Haji wa Betras, Zanzibar wanasikitika kutangaza kifo cha Mtoto wao mpendwa, Bi. Badriya Ramadhan Kiondo aliyekuwa Mkuu wa Utawala na Fedha katika Ubalozi wa Tanzania nchini India kilichotokea tarehe 11 Desemba, 2017 katika Hospitali ya Apollo mjini New Delhi, India. 

Mwili wa Marehemu Mama Kiondo unatarajiwa kuwasili nchini Alhamisi tarehe 14 Desemba, 2017 saa 8.45 mchana kwa Ndege ya Shirika la Emirates. Aidha, mazishi yatafanyika katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam Ijumaa tarehe 15 Desemba, 2017 saa 10.00 jioni.

Msiba wa Marehemu Mama Kiondo upo nyumbani kwa mumewe Bw. Frank Mwamkai Kiondo maeneo ya Ada Estate, Na. 73, Kinondoni, Barabara ya Ali Hassan Mwinyi karibu na Ubalozi wa Ufaransa.

Habari ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki wote wa familia hizi popote pale walipo.


Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina



RATIBA YA MAZISHI YA MAREHEMU BI. BADRIYA RAMADHAN KIONDO




Tuesday, December 12, 2017

Waziri Mahiga awaasa Wabunge Wateule wa Tanzania kwenye Bunge la nne (4) la Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa Wazalendo na kusimamia maslahi ya Jumuiya.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga(katikati) akiongea katika kikao cha uongozi wa Wizara hiyo na Wabunge Wateule wa Tanzania kwenye Bunge la nne (4) la Jumuiya ya Afrika Mashariki, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, tarehe 12 Disemba 2017. Pembeni yake kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba na kulia ni Mwenyekiti wa Wabunge wateule wa Bunge la Afika Mashariki, Mhe. Abdullah Makame.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda (kulia) akiongea katika kikao hicho ambapo aliwakaribisha Waheshimiwa Wabunge wateule pamoja na kuwaeleza kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ipo tayari kuwapa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao. Pembeni yake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi.

Mwenyekiti wa Wabunge Wateule wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe.Dkt. Abdullah Makame akiushukuru uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kikao kizuri cha utangulizi kabla ya kuanza kwa Bunge hilo na pia akaahidi kuwa wataenda kuliwakilisha Taifa vizuri sambamba na kusimamia maslahi ya Jumuiya kwa maendeleo na ustawi wa wananchi wake.

Sehemu ya Waheshimiwa Wabunge Wateule wa Bunge la Afrika Mashariki wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yakitolewa na Mhe. Waziri Mahiga (hayupo pichani)

Sehemu nyingine ya Waheshimiwa Wabunge wakifuatilia kikao hicho.
Wakurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia kikao hicho. Kutoka kulia  Bw. Eliabi Chodota, Bw. Bernard Haule na Bw.Joachim Otaru.



Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Stephen Mbundi akitoa ufafanuzi kuhusiana na taratibu na miongozo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Waheshima Wabunge Wateule. 

Mhe. Waziri na  Naibu Waziri  wakiwa katika picha ya pamoja na Wabunge Wateule wa Tanzania kwenye Bunge la nne la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Picha ya pamoja uongozi wa Wizara  na Wabunge Wateule wa Tanzania kwenye Bunge la nne la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Sunday, December 10, 2017

Spika wa Bunge la Morocco atembelea Tanzania

 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Job Ndugai akimkaribisha Spika wa Bunge la Morocco Mhe. Habib El Malki nyumbani kwake Mjini Dodoma, tarehe 9/12/2017

Mhe.Habib El Malki (wa kwanza kulia)-Spika wa Bunge la Morocco, Mhe. Job Ndugai- Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Zubeir Ali Maulid - Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Dkt. Suzan Kolimba Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Pamoja na wajumbe wengine kutoka Ofisi ya Bunge na Ujumbe wa Morocco ulioambatana na Spika wa Morocco wakiwa katika mazungumzo Bungeni Dodoma, tarehe 9/12/2017.

Katika mazungumzo hayo Mhe.El Malk alitoa mwaliko kwa Mhe. Ndugai na Mhe. Ali Maulid, Mhe. El Malki alisema amefurahishwa sana na jinsi alivyopokelewa na kwa umaalum zaidi alimshukuru Mhe. Rais kwa kumpa heshima ya kipekee kwa kumtambulisha kwa Umma wa Watanzania wakati wa sherehe za maadhimisho ya Uhuru. Mhe. El Malki alisema Morocco ina mengi ya kujifunza kwa Tanzania hasa katika eneo la Demokrasia "nimeshangazwa sana kuona Marais Waastafu wanakaa pamoja na kuunga mkono Rais aliye madarakani, hili ni jambo tunalopaswa kuiga hasa kwa nchi za Afrika, tumezoea kuiga mambo mengi kutoka nchi za Magharibi na kudharau mambo mazuri ambayo yako kati yetu" alisema Mhe. El Malki.

Mhe. Ndugai akimweleza jambo Mhe. El Malki alipomtembeza kwenye ukumbi wa Bunge, wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Suzan Kolimba na anayefuatia ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar 


Wakiwa katika picha ya Pamoja baada ya Mazungumzo, tarehe 9/12/2017
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Balozi Dkt Augustine Mahiga akiwa katika mazungumzo na Spika wa Bunge la Morocco Mhe. Habib El Malki, anayefuatilia mazungumzo hayo ni Balozi wa Morocco nchini Mhe. Mhe. Abdelilah Benryane katika ukumbi wa VIP wa Uwanja wa ndege Dodoma, tarehe 9/12/2017. 

Katika mazungumzo yao Mhe.  El Malki na Mhe. Waziri walizungumzia masuala mbalimbali ya kudumisha na kukuza ushirikiano wa kidiplomasia,uchumi na utalii.
                                         
Mhe. Waziri Balozi Dkt. Augustine Mahiga, akimuaga  Mhe. Spika wa Morocco katika uwanja wa ndege wa Dodoma, tarehe 9/12/2017. Kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika NMashariki, Mhe. Dkt Suzan Kolimba na anayefuata ni Katibu Mkuu Prof. Aldof Mkenda

Sherehe za Maadhimisho ya siku ya Uhuru

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akikagua gwaride wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Tanganyika tarehe 9/12/2017. Maadhimisho hayo yalifanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akimtambulisha Spika wa Bunge la Morocco Mhe. Habib El Malki katika maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Tanganyika tarehe 9/12/2017. Kulia kwake ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa. Mhe. Rais alisema Spika ametumwa na Mfalme Mohamed VI wa Morocco kuja kuangalia sehemu ambayo utajengwa Uwanja Mkubwa na wa Kisasa wa mpira Dodoma, hii ikiwa ni kati ya ahadi zilizotolewa na Mfalme MohamedVI alipotembelea Tanzania Oktoba,2016. 



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt Augustine Mahiga(wa tatu mbele), anayefuata ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dkt Suzan Kolimba pamoja na Mawaziri na Viongozi mbalimbali wa Serikali wakifuatilia sherehe za maadhimisho ya Uhuru wa Tanganyika  zilizofanyika Uwanja wa Jamhuri Dodoma, tarehe 9/11/2017



Thursday, December 7, 2017

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa afanya uzinduzi wa ofisi za Umoja wa Mataifa mkoani Dodoma

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa  akihutubia katika sherehe za uzinduzi wa majengo ya ofisi za mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini zilizofanyika mkoani Dodoma tarehe 7 Disemba 2017.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akihutubia katika sherehe za uzinduzi wa ofisi za mashirika ya Umoja wa Mataifa zilizofanyika mkoani Dodoma tarehe 7 Disemba 2018.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez akihutubia kwa lugha ya kiswahili katika sherehe za uzinduzi wa Ofisi za mashirika ya Umoja wa Mataifa mkoani Dodoma tarehe 7 Disemba 2017.


==============================================

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amezindua rasmi Ofisi za Umoja wa Mataifa, mkoani Dodoma tarehe 7 Disemba 2017. 

Ofisi hiyo ambayo ipo katika Mtaa wa Mlimwa, Area D, nje kidogo ya Mji wa Dodoma, itakuwa na Ofisi za Mashirika saba (7) kati ya 23 ya Umoja wa Mataifa yanayofanya kazi nchini Tanzania hivi sasa. Mashirika hayo ni pamoja na UNICEF, UNDP, UNFPA, UN Women, IOM, FAO na WHO.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bw. Jabir Shekimweri, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Bw. Alvaro Rodriguez, Mwakilishi wa Nchi wa UNICEF, Bi. Maniza Zaman, Maofisa wa Serikali na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa.

Akizindua Ofisi hiyo Mhe. Waziri Mkuu aliwapongeza Umoja wa Mataifa kwa hatua yao ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano(5) ya kuhamishia Makao makuu ya nchi mjini Dodoma “Serikali ya awamu ya tano(5) iliazimia kuunga mkono kwa vitendo tamko la Baba wa Taifa la Mwaka 1973 la kuifanya Dodoma kuwa Makao Makuu ya nchi". alisema.

Aidha, alifafanua kuwa hadi sasa Waziri Mkuu, Mawaziri, watendaji wa Serikali na watumishi wa umma zaidi ya 2000 wamehamia Dodoma na mwisho wa Mwezi huu Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuhamia Dodoma na Mheshimiwa Rais anatarajiwa kuhamia Dodoma mapema mwakani. 

Halikadharika, Waziri Mkuu ameyahakikishia Mashirika ya Kimataifa kuwa Serikali imeandaa utaratibu mzuri wa kuhakikisha mashirika hayo pamoja na ofisi za ubalozi zinazowakilisha nchini zinapata viwanja kwa ajili ya kujenga ofisi na makazi mkoani Dodoma.

Akizungumza katika uzinduzi huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb), alisema "Umoja wa Mataifa umeonesha dira na kuwa nyota kwa Mashirika mengine ya Kimataifa na Balozi mbalimbali zinazowakilisha hapa nchini kwa kufungua ofisi zao hapa Dodoma".

Vilevile Mhe. Waziri Mahiga alielezea mchango wa Tanzania kwa kushiriki katika mchakato wa maboresho ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa ili yaweze kufanya kazi kwa Pamoja, pia  alifafanua kuwa Tanzania na Ireland ndio walipewa jukumu la kukusanya maoni na kuja na andiko la kuboresha utendaji kazi wa Masharika ya Umoja wa Mataifa na andiko hilo ndilo lilozaa “United Nation delivering as One”, na kwa sasa utaratibu huu unatoa fursa ya mashirika ya Umoja wa Mataifa kutoa huduma zao katika jengo moja.

Kwa upande mwingine, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Bw. Rodriguez, alisema, “ Uzinduzi wa Ofisi hii utawezesha kukuza ushirikiano wa Umoja wa Mataifa na Serikali hasa katika kipindi hiki muhimu Serikali inapohamia Dodoma na kwamba mashirika ya Umoja wa Mataifa yamekuwa yakifanya kazi kwa karibu na Serikali"


Malengo ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa tangu miaka 72 iliyopita ni pamoja na kusimamia na kuleta maelewano baina ya nchi na nchi,kuhamasisha na kuleta maendeleo hasa kwa nchi zinazoendelea, kulinda, kuleta heshima kwa watu wote hasa kwa watu wanaonyanyaswa na wale wa makundi maalum na kusimamia na kulinda haki za binadamu ikiwemo haki ya kujitawala. Umoja wa Mataifa  una jumla ya Mashirika 50 Duniani na hapa Tanzania inawakilishwa na jumla ya Mashirika 23.

Mhe.Waziri Mkuu akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa majengo ya ofisi za mashirika ya Umoja wa Mataifa mkoani Dodoma. Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bw.Jabir Shekimweri, Mhe. Waziri Mahiga na wengine ni wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini.
Bw. Alvaro Rodriguez akikabidhi zawadi ya ngao kwa Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.



Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Dodoma wakitumbuiza katika sherehe za uzinduzi wa ofisi za Mashirika ya Umoja wa Mataifa Mkoani Dodoma.

Vikundi vya ngoma vikitumbuiza.

Picha ya pamoja meza kuu pamoja na wawakilishi wa Taasisi za Serikali.
Picha ya pamoja meza kuu pamoja na watumishi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa.