Sunday, December 10, 2017

Sherehe za Maadhimisho ya siku ya Uhuru

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akikagua gwaride wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Tanganyika tarehe 9/12/2017. Maadhimisho hayo yalifanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akimtambulisha Spika wa Bunge la Morocco Mhe. Habib El Malki katika maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Tanganyika tarehe 9/12/2017. Kulia kwake ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa. Mhe. Rais alisema Spika ametumwa na Mfalme Mohamed VI wa Morocco kuja kuangalia sehemu ambayo utajengwa Uwanja Mkubwa na wa Kisasa wa mpira Dodoma, hii ikiwa ni kati ya ahadi zilizotolewa na Mfalme MohamedVI alipotembelea Tanzania Oktoba,2016. 



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt Augustine Mahiga(wa tatu mbele), anayefuata ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dkt Suzan Kolimba pamoja na Mawaziri na Viongozi mbalimbali wa Serikali wakifuatilia sherehe za maadhimisho ya Uhuru wa Tanganyika  zilizofanyika Uwanja wa Jamhuri Dodoma, tarehe 9/11/2017




Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof.Aldof Mkenda(wa mwisho mstari wa kwanza, mwenye miwani) pamoja na sehemu ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wakifuatilia Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Tanganyika zilizofanyika Uwanja wa Jamhuri, Dododoma, tarehe 9/12/2017.

Sehemu ya Mabalozi (walio mstari wa mbele) pamoja na wageni wengine waalikwa wakifuatilia Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Tanganyika, tarehe 9/12/2017

Sehemu ya Wakurugenzi na watumishi wa Wizara(walioshikilia bendera mstari wa mbele) wakifuatilia Sherehe za Maadhimsho.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.