Saturday, January 13, 2018

Dkt. Mahiga akutana na Timu ya kuchunguza mauaji ya askari nchini DRC

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akisalimiana na Bw. Domitry Titov, Kiongozi wa Timu ya Umoja wa Mataifa inayochunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Wawili hao walifanya mazungumzo jijini Dar Es Salaam leo ambapo Bw. Titov aliahidi kuwa Timu yake itaifanya kazi hiyo kwa uadilifu mkubwa ili kubaini chanzo cha mauaji na kutoa mapendekezo ya kuhakikisha kuwa matukio kama hayo hayatokei tena katika siku zijazo.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akisalimiana na mjumbe wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini DRC.

Mjumbe kutoka Tanzania wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini DRC akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga

Mjumbe pekee wa kike wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini DRC akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga.

Mjumbe mwingine wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini DRC akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga.

Mjumbe kutoka Nigeria wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini DRC akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga.

Wajumbe wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini DRC wakiendelea kusalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akiwa katika mazungumzo na Bw. Domitry Titov, Kiongozi wa Timu ya Umoja wa Mataifa inayochunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini DRC wakifuatilia mazungumzo.
Ujumbe wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ukifuatilia mazungumzo hayo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy na Msemaji wa Wizara na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Bi. Mindi Kasiga.

Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakinukuu mambo muhimu ya mazungumzo.

Wajumbe wa pande mbili wakiwa katika mazungumzo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga mstari wa mbele katikati akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini DRC na maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Tuesday, January 9, 2018

Balozi Possi Akabidhi Hati za Utambulisho Nchini Austria

Mheshimiwa Dkt. Abdallah Possi, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani ambaye pia anaiwakilisha nchi huko Austria akiwasili katika Ikulu ya Vienna tayari kwa kujitambulisha rasmi nchini humo kwa kukabidhi hati za utambulisho. 

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani na Austria Mheshimiwa Dkt. Abdallah Possi akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Austria Mheshimiwa Dkt. Alexander Van der Bellen kwenye hafla fupi ya kujitambulisha iliyofanyika kwenye Ikulu ya Vienna, Austria.

 

Rais wa Jamhuri ya Austria Mhe. Dkt. Alexander Van der Bellen akizungumza na hatimaye kupiga picha ya pamoja na Mhe. Dkt. Abdallah Possi, Balozi wa Tanzania nchini Austria mwenye makazi yake nchini Ujerumani. 

Friday, January 5, 2018

Balozi Mteule wa Ufaransa awasilisha Nakala za Hati za Utambulisho

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akisalimiana na Balozi Mteule wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frédéric Clavier ambaye alifika ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje leo kwa ajili ya kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Ufaransa hapa nchini, Mhe. Frédéric Clavier.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Ufaransa hapa nchini, Mhe. Frédéric Clavier baada ya Mhe. Balozi kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho. Wawili hao pamoja na mambo mengine walizungumzia masuala ya uwekezaji ambapo Ufaransa inahitaji kuongeza uwekezaji wa makampuni yake hapa nchini ili kuunga juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

Ujumbe wa Wizara ulioshiriki mazungumzo hayo. Kutoka kulia ni Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Bi. Mindi Kasiga; Kaimu Mkuu wa Itifaki, Bw. Jacob Msekwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bw. Salvator Mbilinyi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Balozi Mteule wa Ufaransa wakiendelea na mazungumzo yao.



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akiteta jambo na Balozi Mteule wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frédéric Clavier mara baada ya wawili hao kubadilishana mawazo kuhusu namna ya kuimarisha uhusiano baina ya nchi zao.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga wa pili kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mteule wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frédéric Clavier wa pili kutoka kushoto. Wengine katika picha ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bw. Salvator Mbilinyi (kulia) na Naibu Balozi wa Ufaransa, Bw. Alexandre Peaudeau.

Friday, December 29, 2017

Waziri Mahiga apokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Uturuki nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Jamhuri ya Uturuki nchini, Mhe.Ali Dovutoglu. Makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Desemba 2017.
Mhe. Waziri Mahiga akizungumza na Mhe. Dovitoglu ambapo alimuhakikishia kumpa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake pamoja na kumpongeza kwa kuteuliwa kwake kwa awamu nyingine kuiwakilisha Jamhuri ya Uturuki nchini.

Waziri Mahiga akutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb) akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini, Mhe. Song Geum - Young alipomtembelea katika ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Desemba 2017.
Mazungumzo yao yalijikita katika kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia uliopo baina ya mataifa hayo, kuanzisha maeneo mapya ya ushirikiano sambamba na hali halisi ya utekelezaji wa  miradi ya maendeleo inayotekeleza kwa ushirikiano baina ya Tanzania na Korea.

Mhe. Waziri Mahiga akielekezana jambo na Mhe. Song Geum-Young.
Mhe.Waziri Mahiga akiagana na Mhe Song Geum-Young.



Thursday, December 21, 2017

Dkt. Mahiga ahutubia Chuo Kikuu cha Mambo ya Nje cha China

Wziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa Chuo cha Mambo ya Nje cha China kabla ya wawili hao hawajaelekea kwenye ukumbi kuhutubia wanafunzi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augastine Mahiga akihutubia wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mambo ya Nje cha China. Dkt. Mahiga alieleza ushirikiano wa Tanzania na China ulipoanza hadi leo na kuwasihi wanafunzi hao waangalie namna y kuuimarisha kutokana na nafasi zao.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mambo ya Nje cha China wakisikiliza Hotuba ya Dkt. Mahiga. Wanafunzi hao ambao walikuwa wadadisi sana walifurahi sana kutokana na elimu ya siku moja waliopata kutoka kwa Mbobezi wa masuala ya Diplomasia.

Dkt. Mahiga akiendelea na hotuba yake huku Mkuu wa Chuo akisikiliza kwa makini. Mkuu huyo alikiri kuwa kutokana na hotuba hiyo amejifunza vitu vingi sana.

Ujumbe uliomsindikiza Waziri Mahiga, kutoka kulia ni Bw. Benedict Msuya, Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Gerald Mbwafu, Katibu wa Waziri na Kanali Remigius Ng'umbi, Mwambata Jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini China.

Mstari wa Mbele kutoka kushoto ni Kamishna msaidizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Malmeltha Mtagwaba, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Dkt. Thomas Kashililah, Naibu Katibu Mkuu wa Biashara na Uwekezaji kutoka Wizara ya Vwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchweishaija, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha wa Zanzibar, Bw. Khams Omar na Balozi wa Tnzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki wakifuatilia hotuba hiyo.

Mmoja wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mambo ya Nje cha China akiuliza sawali kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga.

Picha ya Pamoja.


 Ziara katika kampuni ya magari ya Foton Motors Group


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa viongozi wa kampuni ya Foton Motors Group kabla ya kuanza kutembelea kampuni hiyo kujionea shughuli zake.

Baadhi ya aina ya magari yanayotengenezwa na kampuni ya Foton Motors Group.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa ndani ya moja ya magari yanayotengenezwa na kampuni ya Foton Motors Group.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa ndani ya karakana ya Foton Motors Group kuangalia shughuli za uzalishaji wa magari zinavyofanyika.

Baada ya kuona shughuli za kampuni hiyo, Waziri Mahiga alifanya mazungumzo rasmi na viongozi wa kampuni hiyo ambapo walimuomba awasaidie ili waweze kuwekeza nchini Tanzania. Kampuni hiyo inataka kufungua kiwanda cha kuunganisha magari yao kwa lengo la kuuza Tnzania na soko la Afrika. Walisema kampuni yao inatengeneza magari ya aina yote makubwa, madogo, mabasi na malori ndio inayoongoza kwa mauzo nchini China kwa kipindi cha miaka 13 sasa.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akipokea zawadi ya mfano wa moja ya magari yanayotengenezwa na kampuni ya Foton Motors Group.

Mazungumzo na Makamu wa Rais wa Kampuni ya China Merchant

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Kampuni ya China Merchant inayowekeza kwenye mradi wa Bandari ya Bagamoyo. Makamu wa Rais huyo pamoja na mambo mengine alielezea kufurahishwa kwake na uamuzi wa Serikali kuidhinisha rasmi utekelezaji wa mradi huo.

Tuesday, December 19, 2017

China yaunga mkono juhudi za Rais Magufuli.



 Na Mwandishi Maalum, Beijing

China imeahidi kushirikiana na Tanzania kikamilifu katika miradi ya kipaumbele ambayo Serikali ya AwamuyaTano imepanga kuitekeleza ili kufikia azma yake ya uchumi wa viwanda ifikapo 2020 na baadaye uchumi wa Kati ifikapo 2025.

Hayo yalibainishwa leo jijini Beijing  na Naibu Waziri wa Biashara wa China, Mhe. Qian Keming na baadaye kukaririwa tena na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Mipango (NDRC), Bw. Ning Jizhe walipofanya mazungumzo kwa nyakati tofauti na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga.

Katika mazungumzo hayo, Balozi Mahiga aliainisha na kufafanua namna Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Maguful iilivyokusudia kuwashirikisha wadau mbalimbali kwenye utekelezaji wa miradi ya kipaumbele ambayo inalenga kuchochea agenda ya uchumi wa viwanda. 

Miradi hiyo ni pamoja na kuendeleza nishati ya umeme ambapo Serikali imedhamiria kuzalisha umeme wa megawatts 5000 ifikapo mwaka 2020 ili kuharakisha utekelezaji wa agenda ya uchumi wa viwanda ambayo haitaweza kufanikiwa kama hakutakuwa na umeme wa kutosha na wauhakika.
Kutokana na uhalisia huo, Serikali imepanga kujenga kituo cha kuzalisha umeme wa megawatts 2100 kwenye mto Rufiji na kujenga njia za kusambaza umeme huo kutoka Rufiji, Chalinze hadi Dodoma na nyingine kutokaChalinze, Kilimanjaro hadi Arusha. 

Miradi mingine ni ujenzi wa mtandao wa usafiri wa reli na uboreshaji wa reli ya TAZARA, ujenzi wa bandari ya Bagamoyo na viwanja vya ndege ikiwa ni pamoja na kujenga jengo  la abiria katika Kiwanja cha ndege cha Mwanza.
Waziri Mahiga alisisitiza umuhimu wa miundombinu hiyo kuunganishwa ili iweze kuleta tija iliyokusudiwa katika uchumi. Aliongeza kuwa uchumi wa Tanzania unakua kwa wastani wa asilimia 7 kwa mwaka na uchumi wa nchi za jirani ambazo zinategemea bandari za Tanzania pia unakua, hivyo kuendeleza na kuunganisha miundombinu ya usafiri ni muhimu kwa ustawi wa uchumi wa nchi hizo na uchumi wa Tanzania.

Aidha, Waziri Mahiga alieleza namna Serikali inavyoendelea na zoezi la kuhamisha makao makuu ya Serikali kwenda Dodoma na kukaribisha makampuni ya China kushiriki kwenye uwekezaji wa miundombinu mbalimbali kwenye mji huo mpya wa makao makuu.

Baadhi ya miundombinu muhimu inayohitajika Mjini Dodoma ni upatikanaji wa maji safi ya na ya uhakika na kuiomba China ishiriki katika ujenzi wa Bwawa la Kidunda mkoani Morogoro. Bwawa hilo likijengwa na kukamilika litasaidia sio tu kusambaza maji ya uhakika mkoani Dodoma bali hata mkoa wa Dar Es Salaam ambao matumizi ya maji yanaongezeka kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu kila siku.

Waziri Mahiga aliahidi kuwa Serikali yake itakamilisha taratibu zilizosalia ili mradi wa Mchuchuma na Liganga uweze kuanza kwa kuwa mradi huo ni muhimu sana katika sera ya uchumi wa viwanda.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Biashara aliahidi kuwa Serikali ya China itafanyia kazi kwa haraka miradi yote iliyowasilishwa ili Tanzania iweze kutimiza malengo yake ya kuwaletea maendeleo wanachi. 

Aliongeza kuwa Serikali yake itaharakisha kufanya upembuzi yakinifu wa miradi hiyo kwa madhumuni ya kutimiza masharti ya kampuni za uwekezaji na taasisi zinazotoa fedha nchini China.

Aidha, alipongeza hatua ya Serikali ya Tanzania ya kuweka mikakati ya kuzalisha umeme wa megawatts 5000 ifikapo mwaka 2020. Hivyo, aliahidi kuwa atazishawishi kampuni za China zinazozalisha umeme wa jua, upepo na joto ardhi zijek uwekeza nchini ili lengo hilo litimie kwa haraka.

Wakati huo huo, Waziri Mahiga alikutana na watendaji wa makampuni mbalimbali ya uwekezaji yaliyodhamiria kuwekeza nchini kwenye sekta mbalimbali. Makampuni hayo yanataka kuwekeza kwenye uzalishaji wa Sukari, ujenzi wa kiwanda cha kusindika mihogo, uagizaji wa mihogo mikavu toka Tanzania kwa wastani wa tani laki 3 hadi 5 kwa mwaka na huduma za kitalii kama ujenzi wa mahoteli yenye hadhi ya nyota tano. 

Kampuni hizo zote zimeomba kukutanishwa na wadau husika ili wkamilishe taratibu zinazotakiwa waanze uwekezaji haraka iwezekanavyo.

Waziri Mahiga aliwahakikishia wawekezaji hao kuwa uamuzi wao wa kuwekeza Tanzania hawataujutia kwa kuwa Tanzania ni nchi tulivu na yenye amani, ina rasilimali nyingi na soko kubwa kutokana na kuwa mwanachama wa SADC na EAC.