Sunday, January 14, 2018

Mawaziri wa Tanzania na Rwanda kujadili Ujenzi wa Reli

Mawaziri wa Tanzania na Rwanda wanaoshughulikia masuala ya miundombinu wameagizwa kukutana mara moja kujadili ujenzi wa Reli ya kiwango cha Kimataifa kutoka Isaka hadi Rwanda. 

Kauli hiyo imetolewa leo Ikulu jijini Dar Es Salaam na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli mbele ya waandishi wa habari akiwa na mgeni wake, Rais wa Rwanda, Mhe. Paul Kagame ambaye amefanya ziara ya kikazi ya siku moja hapa nchini. 

“Kipande cha kutoka Isaka hadi Rwanda ni kilomita 400 tu, hatuwezi kushindwa kukijenga, tumewaagiza Mawaziri wa miundombinu wakutane ili wajadili namna ya kupata fedha na kabla mwaka huu haujaisha tunataka kuweka jiwe la msingi la ujenzi huo”, Rais Magufuli alisema.

Rais Magufuli alieleza kuwa ujenzi wa reli hiyo utasaidia kukuza biashara kati ya Tanzania na Rwanda ambayo kwa sasa, licha ya kuongezeka kidogo lakini kiwango cha biashara kati ya nchi hizo bado kipo chini, akitolea mfano wa kuongezeka kwa mizigo ya Rwanda inayopitia Bandari ya Dar Es Salaam ambayo kwa mwaka jana imefikia idadi ya tani laki tisa na nusu.

Rais Magufuli ambaye alimtaja Rais Kagame kuwa ni mwanamapinduzi wa Afrika, licha ya kumpongeza kwa kushinda kiti cha Rais kwa ushindi wa kishindo mwaka 2017 alimsifu pia kutokana na mipango yake ya kuibadilisha Rwanda na dhamira ya dhati ya kuwaletea maendeleo wananchi wa nchi hiyo. “Watanzania na watu wengine wanajua Rwanda ilipotoka na hatua ulioifikisha hivi sasa”, Rais Magufuli alisema.

Katika ziara hiyo, Rais Magufuli alimuhakikishia Rais Kagame anayewania nafasi ya Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) kwa kipindi cha Mwaka 2018 kuwa Tanzania pamoja na marafiki zake itamuunga mkono kwenye nafasi hiyo. Mhe. Rais alielezea matumaini yake kuwa Rais Kagame atatumia nafasi yake hiyo kwa kushirikiana na viongozi wenzake kuweka mikakati ya kutatua changamoto zinazolikabili Bara la Afrika ikwemo ukosefu wa ajira unaosabisha vijana wengi kukimbia nchi zao. 

Kwa upande wake, Rais Kagame alielezea matumaini yake kuwa Tanznaia itaendelea kushirikiana na Rwanda katika masuala mbalimbali yakiwemo ya kiuchumi kwa faida ya pande zote mbili. 

Akijibu swali kuhusu hatua gani atazichukuwa atakapokuwa Mwenyekiti wa AU kukabiliana na wimbi la vijana wengi wa Afrika kukimbilia ughaibuni kutafuta maisha.

Rais Kagame alijibu kuwa nchi moja moja na kwa ujumla wao barani Afrika ziongeze biashara na uwekezaji baina yao ili kuongeza ajira kwa vijana. Aidha, aliwaasa vijana kuwa jukumu la Serikali zote duniani ni kujenga mazingira mazuri ya uwekezaji na biashara, hivyo vijana hawanabudi kutumia fursa zinazopatikana katika nchi zao badala ya kukimbilia ughaibuni na kutangatanga. 

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dar es Salaam
14 Janauri 2018




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Baadhi ya viongozi wa Serikali mara baada ya kuwasilia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa ajili ya mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mhe.Paul Kagame aliyefanya ziara ya kikazi ya siku moja leo Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mhe. Paul Kagame akishuka kutoka katika ndege kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Terminal I leo Jijini Dar es Salaam. Rais Kagame amefanya ziara ya kikazi ya siku moja. Baadhi ya wananchi wakimlaki Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mhe. Paul Kagame mara baada ya kupokelewa na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.  Dkt. John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) leo Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (kulia) akimkaribisha mgeni wake, Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mhe. Paul Kagame Ikulu Jijini Dar es Dar es Salaam leo. Rais Kagame amekuja nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es Salaam kuelezea masuala waliojadili na mgeni wake Rais Kagame. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu mazungumzo baina yake na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mhe. Paul Kagame (kushoto) leo Ikulu Jijini Dar es Dar es Salaam. Rais Kagame amekuja nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja. Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mhe. Paul Kagame akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu mazungumzo baina yake na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (kulia) leo Ikulu Jijini Dar es Dar es Salaam. Rais Kagame amekuja nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja. Baadhi ya Viongozi wa Serikali waliokuwa Ikulu kushiriki katika ziara ya Rais wa Rwanda, Mhe. Paul Kagame. Baadhi ya viongozi wakifuatilia mkutano wa Marais Dkt. John Pombe Magufuli wa Tanzania na Mhe. Paul Kagame wa Rwanda mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mhe. Paul Kagame leo Ikulu Jijini Dar es Dar es Salaam. Rais Kagame amekuja nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja.

Saturday, January 13, 2018

Balozi Mteule wa Australia awasilisha Nakala za Hati za Utambulisho

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi Mteule wa Australia nchiniTanzania mwenye makazi yake Nairobi, Kenya, Mhe. Alison Chartres kabla ya kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho.

Balozi Mteule wa Australia nchiniTanzania mwenye makazi yake Nairobi, Kenya, Mhe. Alison Chartres akiwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga jijini Dar Es Salaam leo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Australia nchiniTanzania mwenye makazi yake Nairobi, Kenya, Mhe. Alison Chartres mara baada ya zoezi la kwasilisha Nakala za Hati za Utambulishokukamilika.

Mazungumzo yanaendelea.

Dkt. Mahiga akutana na Timu ya kuchunguza mauaji ya askari nchini DRC

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akisalimiana na Bw. Domitry Titov, Kiongozi wa Timu ya Umoja wa Mataifa inayochunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Wawili hao walifanya mazungumzo jijini Dar Es Salaam leo ambapo Bw. Titov aliahidi kuwa Timu yake itaifanya kazi hiyo kwa uadilifu mkubwa ili kubaini chanzo cha mauaji na kutoa mapendekezo ya kuhakikisha kuwa matukio kama hayo hayatokei tena katika siku zijazo.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akisalimiana na mjumbe wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini DRC.

Mjumbe kutoka Tanzania wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini DRC akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga

Mjumbe pekee wa kike wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini DRC akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga.

Mjumbe mwingine wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini DRC akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga.

Mjumbe kutoka Nigeria wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini DRC akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga.

Wajumbe wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini DRC wakiendelea kusalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akiwa katika mazungumzo na Bw. Domitry Titov, Kiongozi wa Timu ya Umoja wa Mataifa inayochunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini DRC wakifuatilia mazungumzo.
Ujumbe wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ukifuatilia mazungumzo hayo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy na Msemaji wa Wizara na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Bi. Mindi Kasiga.

Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakinukuu mambo muhimu ya mazungumzo.

Wajumbe wa pande mbili wakiwa katika mazungumzo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga mstari wa mbele katikati akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini DRC na maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Tuesday, January 9, 2018

Balozi Possi Akabidhi Hati za Utambulisho Nchini Austria

Mheshimiwa Dkt. Abdallah Possi, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani ambaye pia anaiwakilisha nchi huko Austria akiwasili katika Ikulu ya Vienna tayari kwa kujitambulisha rasmi nchini humo kwa kukabidhi hati za utambulisho. 

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani na Austria Mheshimiwa Dkt. Abdallah Possi akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Austria Mheshimiwa Dkt. Alexander Van der Bellen kwenye hafla fupi ya kujitambulisha iliyofanyika kwenye Ikulu ya Vienna, Austria.

 

Rais wa Jamhuri ya Austria Mhe. Dkt. Alexander Van der Bellen akizungumza na hatimaye kupiga picha ya pamoja na Mhe. Dkt. Abdallah Possi, Balozi wa Tanzania nchini Austria mwenye makazi yake nchini Ujerumani. 

Friday, January 5, 2018

Balozi Mteule wa Ufaransa awasilisha Nakala za Hati za Utambulisho

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akisalimiana na Balozi Mteule wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frédéric Clavier ambaye alifika ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje leo kwa ajili ya kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Ufaransa hapa nchini, Mhe. Frédéric Clavier.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Ufaransa hapa nchini, Mhe. Frédéric Clavier baada ya Mhe. Balozi kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho. Wawili hao pamoja na mambo mengine walizungumzia masuala ya uwekezaji ambapo Ufaransa inahitaji kuongeza uwekezaji wa makampuni yake hapa nchini ili kuunga juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

Ujumbe wa Wizara ulioshiriki mazungumzo hayo. Kutoka kulia ni Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, Bi. Mindi Kasiga; Kaimu Mkuu wa Itifaki, Bw. Jacob Msekwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bw. Salvator Mbilinyi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Balozi Mteule wa Ufaransa wakiendelea na mazungumzo yao.



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akiteta jambo na Balozi Mteule wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frédéric Clavier mara baada ya wawili hao kubadilishana mawazo kuhusu namna ya kuimarisha uhusiano baina ya nchi zao.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga wa pili kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mteule wa Ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frédéric Clavier wa pili kutoka kushoto. Wengine katika picha ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bw. Salvator Mbilinyi (kulia) na Naibu Balozi wa Ufaransa, Bw. Alexandre Peaudeau.