Mama Anna Mkapa Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa, akiangalia moja ya machapisho yanayopatikana katika banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye maonesho ya biashara ya sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Wananchi wengi wameendelea kujitokeza kwenye banda la Wizara ili kuongeza uelewa juu ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wizara, ikiwemo namna Wizara inavyosimamia na kuteleza sera ya mambo ya nje ya nchi, faida na hatua mbalimbali za mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki lipo katika jengo la sabasaba hall.Wananchi wote wanakaribishwa
Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kushoto) wakizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye banda la Wizara (kulia)
Sehemu nyingine ya watumishi wa Wizara wakihudumia wananchi
Sehemu nyingine ya wananchi wakiuliza masuala mbalimbali kwa watumishi wa Wizara
Sehemu nyingine ya wananchi wakipata maelezo kutoka kwa watumishi wa Wizara
Sehemu nyingine ya wananchi wakipewa maelezo na mtumishi wa Wizara
Mhe. Prof. Makame Mbarawa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, akizungumza kwenye Mkutano wa 15 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano na Hali ya Hewa la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha katika ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mhe. Prof.Mbarawa akizungumza katika mkutano huo amezisihi nchi wananchama za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuongeza kasi ya kutekeleza miradi inayopangwa katika ngazi ya Jumuiya kwa kuzingatia ukomo wa tarehe.
Mhe. Prof. Makame Mbarawa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano akisaini taarifa ya mkutano mara baada ya majadiliano
Kutoka kushoto Bibi. Zaina Ibrahim Mwalukuta Mkurugenzi wa Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA), Dkt. Leonard Chamuriho Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Maria Sassabo Katibu Mkuu Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Mhandisi Happiness Mgalula Mkurugenzi wa barabara, Wizara ya Ujuenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya Ujenzi wakifuatilia mkutano
Meza kuu ikiongoza mjadala wakati wa mkutano
Sehemu ya wajumbe wakifuatilia mkutano
Mhe. Prof. Mbarawa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano akizungumza wakati wa mkutano
JAJI IMANI ABOUD WA TANZANIA ASHINDA UCHAGUZI WA
MAJAJI WA MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU NA WATU
Mkutano
wa 33 wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Afrika unaoendelea
Jijini Nouakchott, Mauritania kwa siku mbili, leo tarehe 29 Juni, 2018 umefanya
uchaguzi wa Majaji wanne wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu.
Mgombea
wa Tanzania Mhe. Jaji Imani D. Aboud ameshinda uchaguzi huo kwa kura 47 kati ya
kura 50 zilizopigwa na kufanikiwa kuchukua nafasi ya Jaji Solomy Balungi Bossa
wa Uganda aliyejiuzulu nafasi hiyo kabla ya kumaliza kipindi chake.
Kwa
ushindi huo, Mhe. Jaji Aboud atakuwa Jaji wa Mahakama hiyo akiwakilisha Kanda
ya Afrika Mashariki kwa kipindi cha miaka miwili.
Majaji
wengine walioshinda kwenye uchaguzi huo ni pamoja na Jaji Kioko Ben (Kenya),
Jaji Tchikaye Balise (Jamhuri ya Congo), na Jaji Anukam Stella Isibhkhomen
(Nigeria).
Ushindi
huu unadhihirisha uwezo mkubwa alionao Mhe. Jaji Aboud na heshima kubwa iliyonayo
nchi yetu katika Bara la Afrika.
-Mwisho-
Imetolewa na:
Kitengo cha
Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akizungumza jambo na
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Edmund
Mndolwa mara baada ya kuwasili katika Chuo cha Kilimo na Mifugo cha
Kaole Bagamoyo mkoani Pwani. Rais huyo wa Zimbabwe alisoma Shuleni hapo
mwaka 1963 pamoja na wapigania Uhuru wa Chama cha FRELIMO na ilijulikana
kama Shule ya Mafunzo ya Ufundi ya Wapigania Uhuru wa Chama cha
FRELIMO.
Rais wa Zimbabwe Mhe. Emmerson Mnangagwa akizungumza na wafanyakazi
pamoja na wanafunzi wanaosoma katika Chuo cha Kilimo na Mifugo cha Kaole (hawapo pichani).
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akiangalia moja ya
sufuria waliokuwa wakiitumia kila siku miaka ya sitini, wakati
wakisoma katika Shule ya Mafunzo ya Ufundi ya wapigani Uhuru ya Chama
cha FRELIMO.
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akitoka katika moja ya mabweni
yaliyotumika katika mwaka 1963 wakati wakiwa katika Shule ya Mafunzo
ya Ufundi ya wapigani Uhuru ya Chama cha FRELIMO ambacho sasa kinajulikana kama Chuo cha Kilimo na Mifugo cha Kaole Bagamoyo mkoani Pwani.
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akimsikiliza Waziri wa Katiba
na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi mara baada ya kumaliza kukagua
baadhi ya madarasa na mabweni waliyokuwa wakiyatumia katika Shule ya
Mafunzo ya Ufundi ya wapigani Uhuru ya Chama cha FRELIMO ambacho sasa
kinajulikana kama Chuo cha Kilimo na Mifugo cha Kaole Bagamoyo mkoani
Pwani.
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa akiwa katika picha na Waziri
wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Wazazi ya Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Edmund Mndolwa, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Susan Kolimba (Mb.) (wa nne kutoka kushoto mstari wa pili), viongozi wengine
wa Tanzania na Zimbabwe pamoja na wanafunzi wanaosoma katika Chuo cha
Kilimo na Mifugo cha Kaole Bagamoyo mkoani Pwani
Ndege iliyombeba Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe Mhe. Emmerson Dambudzo Mnangagwa ikiwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es salaam, tarehe 28 Juni 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akimkaribisha mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe Mhe. Emmerson Dambudzo Mnangagwa mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Mhe. Rais Mnangagwa akiwapungia mkono wananchi waliofurika kumlaki katika uwanja wa ndege Dar es salaam.
Mhe. Rais Magufuli akiwa na mgeni wake Mhe. Rais Mnangagwa mara baada ya kukagua vikundi vya ngoma vilivyokuwa vikitumbuiza uwanjani hapo.
Mwonekano wa jengo la Tunduma OSBP kwa upande mbele (upande wa kuingilia)
Mwonekano wa jengo la Tunduma OSBP kwa upande wa kuingilia
Mwonekano wa jengo la Tunduma OSBP kwa upande wa kutokea (kuelekea Nakonde, Zambia)
Mwonekano wa jengo la Tunduma OSBP kwa ndani
Baadhi ya vifaa vya ujenzi vikiwa kazini.
Kamati ya ujenzi wa Tunduma OSBP ikiwa kwenye kikao cha kutathimini maendeleo ya ujenzi kilichofanyika katika moja ya ukumbi wa mikutano uliopo kwenye jengo hilo hivi karibuni.
Kamati ya ujenzi ikitembelea sehemu ya eneo la kuegesha magari ambalo ujenzi wake bado unaendelea
Kamati ya ujenzi ikiangalia maendeleo ya ujenzi wa ghala la kuhifadhia bidhaa katika kituo hicho.
Mradi wa ujenzi wa Kituo cha Kutoa Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) cha Tunduma, mpaka kati ya Tanzania na Zambia umekamilika kwa takribani 95%.
Ujenzi wa Kituo hiki unatarajiwa kuboresha mazingira ya biashara baina ya nchi hizi mbili (Tanzania/Zambia).
Ujenzi wa mradi huu ulioanza mwaka 2016 umechukua ukubwa wa eneo linalokadiriwa kuwa na takriban kilomita za mraba 43,000.
Ujenzi wa mradi huu unafadhiliwa na shirika la TradeMark East Afrika.
Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Astralasia Bibi Yusta Nyange (wa pili kutoka kushoto) akifurahia jambo kwenye majadiliano ya 16 ya Kisiasa kati ya Tanzania na Jamhuri ya Korea, yaliyofanyika tarehe 27 Juni 2018 , katika ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere(JNICC), Dar es salaam.
Wengine katika picha ni Maafisa kutoka Wizarani Emmanuel Luangisa(wa mwisho kulia), Ramla Hamisi(wa kwanza kulia) na anayefuata ni Bi Blandina Kasagama wakifuatilia majadiliano hayo.
Pamoja na mambo mengine majadiliano hayo yalijikita katika kuzungumzia namna ya kuimarisha mahusiano yaliyopo kati ya Tanzania na Korea katika maeneo mbalimbali.
Mkutano ukiendelea
Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika na Mashariki ya Kati, Bw. KOH Kyung-sok(wa pili kushoto), akiwa na ujumbe wake kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea na Ubalozi wa Korea nchini wakiwa katika majadiliano hayo.
Bibi Yusta Nyange(kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Bw. KOH Kyung-sok baada ya Mkutano.
Bibi Yusta Nyange(kulia) akimkabidhi zawadi Bw. KOH Kyung-sok baada ya Mkutano.
Mheshimiwa Emmerson Dambudzo Mnangagwa, Rais wa
Jamhuri ya Zimbabwe atafanya ziara ya kitaifa nchini Tanzania tarehe 28 hadi 29
Juni, 2018. Hii itakuwa ziara ya kwanza ya Mheshimiwa Rais Mnangagwa nchini
Tanzania tangu aingie madarakani mwezi Novemba, 2017.
Lengo la ziara hii ya Rais wa Zimbabwe ni
kujitambulisha kwa Rais na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tangu
aingie madarakani, Mheshimiwa Rais Mnangagwa ameshafanya ziara katika nchi za
Namibia, Zambia, Msumbiji, Angola, Afrika Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo na Botswana.
Ziara hii ni muhimu kwa Tanzania kwani itatoa fursa
ya kuimarisha na kukuza zaidi mahusiano mazuri yaliyopo ya kidiplomasia,
kihistoria, kiuchumi na kijamii kati ya nchi hizi mbili. Ziara hii pia itatoa
fursa kwa viongozi wetu kujadili masuala mbalimbali yanayohusu nchi hizi mbili
ya kikanda na kimataifa.
Wakati wa ziara hiyo,Mhe. Rais Mnangagwa atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais Mnangagwa anatarajiwa
pia kutembelea Chuo cha Kilimo cha Wazazi Kaole Bagamoyo ambacho awali kilitumika
kutoa mafunzo kwa wapigania uhuru kutoka nchi za Kusini mwa Bara la Afrika na
Mhe. Rais Mnangagwa ni miongoni mwa waliopata mafunzo katika chuo hicho.
Mhe.
Rais Mnangagwa anatarajiwa kuondoka tarehe 29 Juni 2018 kurejea chini Zimbabwe.
-Mwisho-
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki,
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Dkt. Asha-Rose Migiro akiitazama keki iliyoandaliwa wakati wa uzinduzi rasmi wa Jumuiya ya Watanzania waishio Uingereza (Association of Tanzanians in the UK-ATUK)
Mhe. Balozi Migiro akifurahia jambo na sehemu ya Watanzania walioshiriki uzinduzi huo
Sehemu ya Watanzania na wageni waalikwa waliohudhuria tukio hilo la kihistoria
UZINDUZI WA ASSOCIATION OF TANZANIANS IN
THE UK – ATUK
Mhe. Dkt.
Asha-Rose Migiro, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, alikuwa mgeni rasmi
kwenye sherehe za uzinduzi wa Jumuiya Mwamvuli ya Watanzania waishio nchini
Uingereza na Ireland ya Kaskazini iitwayo ATUK –Association
of Tanzanians in the UK zilizofanyika mjini Reading tarehe 23
Juni, 2018. Jumuiya hii inatokana na muungano wa jumuiya za diaspora kutoka
mikoa mbalimbali ya hapa Uingereza na wanachama wa kujitegemea.
Wajumbe
wa Kamati ya Muda iliyoratibu kuanzishwa kwa ATUK walipongeza
na kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli za
kupambana na ufisadi, kusimamia uwazi na uwajibikaji katika utumishi wa umma na
kuongeza kasi ya kujenga uchumi wa viwanda. Kauli mbiu ya hafla hii ilikuwa
“UMOJA NI NGUVU, TANZANIA YA VIWANDA INAWEZEKANA”. Hivyo mojawapo ya malengo ya
kuanzishwa kwa ATUK ni kujenga umoja na kukusanya nguvu za kuchangia jitihada
za kujenga uchumi wa viwanda nchini mwetu.
Akihutubia
hadhara hiyo Balozi Migiro aliwapongeza ATUK na
alihimiza umoja na kukumbusha kwamba wakati wote Mhe. Rais amekuwa akisisitiza
umoja wa Watanzania bila kujali tofauti zao kwani umoja ni nyenzo muhimu ya
kujiteletea maendeleo. Hivyo Balozi Migiro aliwashukuru kwa Muungano huo na
kueleza kwamba wakiendeleza mshikamano wataweza kuchangia kwa
ufanisi jitihada kubwa za Mhe. Rais Magufuli na Serikali ya Awamu ya
Tano katika kuwaletea maendeleo Watanzania wote.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Aldof Mkenda akisistiza jambo wakati wa ufunguzi wa Mkutano kati ya Serikali na Umoja wa Mataifa na Taasisi zake kujadili utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC), Dar es Salaam, Tarehe 26 Juni2018.
Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia(SDGs) yako 17 yenye shabaha 169 na Viashiria 232, malengo hayo yanatekelezwa kwa pamoja na Jumuiya ya Kimataifa kwa kushirikisha kila sekta na utekelezaji wake unahimiza ushiriki wa kila kundi kwenye jamii.
Katibu Mkuu Prof. Mkenda( wa pili kushoto), Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Prof. Faustine Kamuzora, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (mwisho kulia) na wa mwisho kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Bw. Alvaro Rodriguez, wakifuatilia majadiliano ya Mkutano huo.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akielezea malengo ya Mkutano huo.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Bw. Alvaro Rodriguez, akitoa taarifa ya ufunguzi kwa upande wa Umoja wa Mataifa.
Sehemu ya washiriki wakifuatilia mkutano huo.
Wa pili kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar na washiriki wengine kutoka Serikalini walioshiriki katika mkutano huo.
Sehemu ya Maafisa kutoka Wizarani wakifuatilia mkutano huo.
Katibu Mkuu Prof. Mkenda akiwaelezea wanahabari kuhusu mpira uliondikwa Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia, aliokabidhiwa na Bw. Rodriguez kuashiria utekelezaji wa malengo hayo kwa kasi na kuzingatia Muktadha wa mazingira ya Tanzania.