|
Jaji Imani Aboud wa Tanzania |
JAJI IMANI ABOUD WA TANZANIA ASHINDA UCHAGUZI WA
MAJAJI WA MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU NA WATU
Mkutano
wa 33 wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Afrika unaoendelea
Jijini Nouakchott, Mauritania kwa siku mbili, leo tarehe 29 Juni, 2018 umefanya
uchaguzi wa Majaji wanne wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu.
Mgombea
wa Tanzania Mhe. Jaji Imani D. Aboud ameshinda uchaguzi huo kwa kura 47 kati ya
kura 50 zilizopigwa na kufanikiwa kuchukua nafasi ya Jaji Solomy Balungi Bossa
wa Uganda aliyejiuzulu nafasi hiyo kabla ya kumaliza kipindi chake.
Kwa
ushindi huo, Mhe. Jaji Aboud atakuwa Jaji wa Mahakama hiyo akiwakilisha Kanda
ya Afrika Mashariki kwa kipindi cha miaka miwili.
Majaji
wengine walioshinda kwenye uchaguzi huo ni pamoja na Jaji Kioko Ben (Kenya),
Jaji Tchikaye Balise (Jamhuri ya Congo), na Jaji Anukam Stella Isibhkhomen
(Nigeria).
Ushindi
huu unadhihirisha uwezo mkubwa alionao Mhe. Jaji Aboud na heshima kubwa iliyonayo
nchi yetu katika Bara la Afrika.
-Mwisho-
Imetolewa na:
Kitengo cha
Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam, 29 Juni, 2018