Sunday, March 15, 2020

KAMATI YA BUNGE YA NJE, ULINZI NA USALAMA YATEMBELEA OFISI ZA WIZARA YA MAMBO YA NJE ZILIZOPO MTUMBA JIJINI DODOMA

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), Mhe. Victor Mwambalaswa (Mb.) akizungumza wakati wa ziara ya Wajumbe wa Kamati hiyo walipotembelea Jengo la Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki lililopo Mtumba jijini Dodoma tarehe 15 Machi 2020. Lengo la ziara hiyo lilikuwa ni kukagua miradi inayosimamiwa na Kamati hiyo
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nje, Ulinzi na Usalama walipofanya ziara ya kikazi kwenye Jengo la Wizara lililopo Mtumba jijini Dodoma tarehe 15 Machi 2020
Mhe. Prof. Kabudi akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya NUU
Wajumbe wa Kamati ya NUU akiwemo Mhe. Vuai Nahodha (kulia) wakimsikiliza Prof. Kabudi (hayupo pichani). Kushoto ni Mhe. Augustino Masele.
Wajumbe wengine wa Kamati ya Bunge ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Bonnah Kaluwa na Sophia Mwakagenda nao wakimsikiliza Mhe. Prof. Kabudi ambaye hayupo pichani
Mhe. Masoud Abdalla Salim, Mjumbe wa Kamati akichangia hoja wakati wa ziara yao kwenye Ofisi za Wizara zilizopo Mtumba, Dodoma
Mhe. Prof. Kabudi akimsikiliza Mjumbe wa Kamati, Mhe. Silafu Maufi alipotoa ushauri kwa Wizara kuhusu kuboresha maeneo kadhaa ya Jengo walilotembelea
Mhe. Almas Maige, Mjumbe wa Kamati naye akizungumza. Kulia ni Mhe. Ruth Mollel na Mhe. Mhandisi Gerson Lwenge (kushoto)
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Issa Ng'imba akitoa taarifa kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (hawapo pichani) kuhusu ujenzi wa Jengo la Wizara lililopo Mtumba
Sehemu ya Wakuuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakimsikiliza Bw. Ng'imba ambaye hayupo pichani
Msimamizi wa Miradi ya Majengo ya Wizara, Mhandisi John Kiswaga  akijibu hoja kadhaa zilizowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati wa ziara yao Wizarani
Mhe. Mwakagenda akizungumza wakati wa ziara yao 
Mhe. Prof. Kabudi akiwaeleza jambo Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nje, Ulinzi na Usalama walipotembelea chumba cha ofisi yake wakati wa ziara yao kwenye jengo la Wizara lililopo Mtumba jijini Dodoma


Mhe. Prof. Kabudi akimwonesha Mhe. Mwambalaswa mandhari ya nje ya jengo akiwa ndani ya ofisi yake
Mhe. Prof. Kabudi akiwaonesha Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nje, Ulinzi na Usalama chumba cha wageni mashuhuri kilichopo kwenye Jengo la Wizara lililopo Mtumba

Wajumbe wa Kamati wakipita pembeni mwa eneo la kiwanja cha Wizara kama inavyoonekana
Mhe. Prof. Kabudi akiwaonesha eneo la nje la Jengo la Wizara
Mhe. Mwambalaswa akimweleza jambo Mhe. Prof. Kabudi
Jengo la Wizara kama linavyoonekana
Mhe. Prof. Kabudi akiwaongoza Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nje, Ulinzi na Usalama kurejea ndani mara baada ya kutembelea eneo la nje la Jengo la Wizara lililopo Mtumba jijini Dodoma
Mhe. Prof. Kabudi akijadiliana jambo na  Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nje, Ulinzi na Usalama mara baada ya kukamilisha ziara yao.
Mhe. Prof. Kabudi akiagana na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nje, Ulinzi na Usalama mara baada ya kukamilisha ziara yao kwenye Jengo la Wizara lililopo Mtumba jijini Dodoma
====================================================


WAJUMBE WA KAMATI YA BUNGE YA  NJE, ULINZI NA USALAMA WATEMBELEA JENGO LA WIZARA LILILOPO MTUMBA

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) wakiongozwa na Mhe. Victor Mwambalaswa (Mb.), Mwenyekiti wa Kamati hiyo wamefanya ziara ya kikazi kwenye Jengo la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki lililopo kwenye Mji wa Serikali wa Mtumba jijini Dodoma leo tarehe 15 Machi 2020.

Wajumbe hao ambao wapo kwenye program ya kukagua miradi iliyopo kwenye Wizara zinazosimamiwa na Kamati hiyo, wamepokelewa na mwenyeji wao Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki mara baada ya kuwasili.

Wakizungumza wakati wa ziara hiyo, baadhi ya Wajumbe hao, wameipongeza Wizara kwa kukamilisha ujenzi wa jengo hilo kwa wakati ikiwa ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuhamia Dodoma. Pia wameishauri Wizara kuendelea kuboresha maeneo kadhaa katika jengo hilo ikiwa ni pamoja na kuweka uzio kuzunguka jengo hilo na kukamilisha mfumo wa TEHAMA kwa ajili ya kuboresha mawasiliano. Vilevile, Wajumbe wa Kamati hiyo wameitaka Wizara kuzingatia kanuni za ujenzi wa majengo ya Ofisi za Mambo ya Nje pale Wizara itakapoanza ujenzi wa jengo lake la kudumu katika siku zijazo.

Kwa upande wake, Mhe. Prof. Kabudi aliahidi kutekeleza ushauri uliotolewa na Wajumbe wa Kamati hiyo na kuwahakikishia kuwa, mapungufu kadhaa yaliyopo yatafanyiwa kazi haraka iwezekanavyo.

Aidha, akitoa taarifa fupi kuhusu ugonjwa wa Corona kwa Wajumbe wa Kamati hiyo, Mhe. Prof. Kabudi alisema kuwa, Serikali ya Tanzania imechukua hatua madhubuti kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa huo endapo utaingia nchini. Hatua hizo ni pamoja na mikutano ya kikanda kuanza kufanyika kwa njia ya video ukiwemo Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika nchini kuanzia tarehe 16 hadi 18 Machi 2020.

Pia Kamati ya Kitaifa inayojumuisha Sekta mbalimbali imeundwa kwa ajili ya kuandaa mikakati mbalimbali ya kukabiliana na ugonjwa huo. Kadhalika vifaa, wataalam na maeneo ya karantini tayari yametengwa kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa huo.

“Tanzania inaendelea kuchukua tahadhari mbalimbali kuhusu ugonjwa wa Corona ambao hadi sasa haujaingia nchini. Hatua hizo ni pamoja na kuandaa mikutano ya kikanda ambayo itafanyika kwa njia ya video. Katika kutekeleza hilo, Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC unaoanza tarehe 16 Machi mwaka huu utafanyika kwa njia ya video na utafuata taratibu zote za mikutano ya kikanda wakati wa ufunguzi” alisisitiza Prof. Kabudi.

Jengo la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambalo lipo Mtumba jijini Dodoma lina ukubwa wa Mita za Mraba 1,002 na vyumba 17 vyenye matumizi mbalimbali zikiwemo Ofisi. Jengo hilo lilianza kujengwa mwezi Desemba 2018 na kukamilika mwezi Machi 2019.


Saturday, March 14, 2020

PROF. KABUDI AWATAKA WATUMISHI WA WIZARA YA MAMBO YA NJE KUJITOA MHANGA


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akifungua rasmi Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara lililofanyika kwenye Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma tarehe 14 Machi, 2020. Pamoja na mambo mengine, Mhe. Prof. Kabudi amewataka Wafanyakazi wa Wizara hiyo kutekeleza majukumu yao kwa kujituma na kutanguliza mbele maslahi ya Taifa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Wizara, Bw. Issa Ng'imba wakati wa ufunguzi wa  Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika jijini Dodoma

Sehemu ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia hotuba ya Mhe. Prof. Kabudi (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanayakazi wa Wizara hiyo uliofanyika jijini Dodoma
Sehemu nyingine ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki nao wakifuatilia hotuba ya Mhe. Prof. Kabudi (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanayakazi wa Wizara hiyo uliofanyika jijini Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Ibuge naye akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika jijini Dodoma
Mhe. Prof. Kabudi na wajumbe wengine wakimsikiliza Katibu Mkuu, Balozi Kanali Ibuge (hayupo pichani)
Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Baraza hilo
Naibu Katibu Mkuu TUGHE-Taifa, Bw. Amani Simon Msuya akiwa na Mwakilishi wa TUGHE-Dodoma wakifuatilia ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Wajumbe wa Baraza la Wafanayakazi wakiwa kwenye ufunguzi wa mkutano
Sehemu nyingine ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa kwenye ufunguzi wa mkutano wa Baraza hilo
Wajumbe wa Baraza wakiwa kwenye ufunguzi wa mkutano
Naibu Katibu Mkuu TUGHE-Taifa, Bw. Msuya nae akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanayakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu TUGHE-Taifa, Bw. Msuya (hayupo pichani)

Sehemu nyingine ya Wajumbe wa Baraza
Mjumbe wa Baraza la Wafanayakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Zanzibar, Balozi Mohammed Hamza akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Wajumbe wa Baraza hilo wakati wa ufunguzi 


Sehemu ya Wajumbe wa Baraza wakimsikiliza Balozi Hamza (hayupo pichani)
Wajumbe wa Baraza
Wajumbe wengine wa Baraza
Mhe. Prof. Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu, Balozi Ibuge na Wajumbe wa TUGHE-Taifa na Wizarani
Mhe. Prof. Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ambao pia ni Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi mara baada ya kufungua rasmi Mkutano wa Baraza hilo
Mhe. Prof. Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wote wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Thursday, March 12, 2020

Balozi Amour katika juhudi za kutafuta fursa nchini Kuwait

Balozi wa Tanzania nchini Kuwait, Mhandisi Aisha S. Amour amekutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Fawaz Al-Khaled Al-Hamad Al-Sabah, Gavana wa Mkoa wa Ahmadi, Kuwait.  Uongozi huo wa Mkoa wa Ahmadi ulionyesha utayari wa kushirikiana na Mkoa mmojawapo wa Tanzania katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo mara baada ya kukubaliana kwa kupitia Wizara ya Mambo Nje ya Kuwait.

Mhe. Mhandisi Aisha S. Amour, Balozi wa Tanzania nchini Kuwait akipokea zawadi ya alama ya Mkoa toka kwa Mhe. Fawaz Al-Khaled Al-Hamad Al-Sabah, Gavana wa Mkoa wa Ahmadi, Kuwait katika ofisi za Mkoa huo, ambapo Mhe. Balozi alifanya ziara.

Balozi wa Tanzania nchini Kuwait, Mhandisi Aisha S. Amour atembelea ofisi za Mamlaka ya Kilimo na Uvuvi ya Kuwait na kufanya mazungumzo na Mhe.Mohamed Al-Yousef Al-Sabah, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo.  Mkurugenzi huyo alieleza utayari wa kushirikiana na Mamlaka za Tanzania katika sekta ya kilimo na uvuvi kwa ajili ya kubadilishana uzoefu katika tafiti na teknolojia mbalimbali hasa katika mbegu, kilimo cha umwagiliaji, pamoja na kilimo cha kitalu nyumba.
 Balozi wa Tanzania nchini Kuwait, Mhandisi Aisha S. Amour atembelea mashamba ya tafiti wa kilimo cha mbogamboga kwa upandaji wa kawaida. Kushoto kwa Mhe. Balozi ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Utafiti wa mazao, Dr. Reem Ahmed Al-Hazeem.
Balozi wa Tanzania nchini Kuwait, Mhandisi Aisha S. Amour akiangalia uzalishaji wa bilinganya kwa ajili ya utafiti kwa kwa njia ya kitalu nyumba, ‘greenhouse.

Balozi wa Tanzania nchini Kuwait Mhandisi Aisha S. Amour akingalia uzalishaji wa matango kwa ajili ya utafiti kwa njia ya kitalu nyumba.
 Balozi wa Tanzania nchini Kuwait. Mhe. Mhandisi Aisha S. Amour alikutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Balozi Abdulhamid Al-Failakawi, Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje ya Kuwait – Idara ya Afrika. Katika mazungumzo hayo, Mhe. Balozi Eng. Aisha aliwasilisha salamu za shukrani kwa Serikali ya Kuwait kwa ushirikiano mkubwa katika ujenzi wa miradi ya maendeleo kwa kupitia Kuwait Fund. Aidha, alieleza fursa mbalimbali za uwekezaji, biashara na Utalii zilizopo Tanzania na kumuomba kuwezesha katika kukutana na Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali ya Kuwait ili kuangalia uwezekano wa ushirikiano kati ya Kuwait na Tanzania katika nyanja mbalimbali.
Balozi wa Tanzania nchini Kuwait, Mhe. Mhandisi Aisha S. Amour afanya mazungumzo na Bw. Emad Abdullah Al-Zaid, Mkurugenzi Msaidizi wa Kuwait Chamber of Commerce & Industry kuhusu kupanga mikakati ya kuwakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na Kuwait pamoja na kutangaza fursa mbalimbali zilizopo Tanzania. 

Balozi wa Tanzania nchini Kuwait, Mhe. Mhandisi Aisha S. Amour atembelea kiwanda cha AlHomaizi Food kiwanda cha kuchakata nafaka.  Al-Homaizi ni Kampuni mama ya Alrifai ambayo imeanza kununua korosho za Tanzania na kuzisafirisha nchi za Mashariki ya kati ikiwa ni pamoja na Kuwait.

Balozi wa Tanzania nchini Kuwait, Mhandisi Aisha S. Amour akiwa katika maabara ya kiwanda hicho, akipewa maelezo namna ya upimaji ubora wa mazao ya nafaka kabla ya kuchakata na baada.

 Balozi wa Tanzania nchini Kuwait, Mhandisi Aisha S. Amour akutana na kufanya mazungumzo na Bw. Ahmad A. Eid, Mkurugenzi Mtendaji wa Ushirika wa Kuwait Shipping Companies & Agent Association kuhusu fursa za uwekezaji na usafirishaji wa baharini. Bw. Ahmad alieleza utayari wa kuleta meli nchini Tanzania kuchukua mizigo ya biashara moja kwa moja kutoka Tanzania mpaka Kuwait.
Balozi wa Tanzania nchini Kuwait. Mhandisi Aisha S. Amour,  akutana na kufanya mazungumzo viongozi wa Umoja wa Watalii Kuwait kuhusu masuala ya utalii Tanzania. Katika mazungumzo na viongozi hao ambao wanawanachama Zaidi ya 150, ilikubalika kuandaa kwa safari ya watalii Zaidi ya 70 kuja Tanzania mwezi Julai 2020. Aidha, viongozi hao walikubali kuwa mabalozi wa utalii wa Tanzania nchini Kuwait.
 Balozi wa Tanzania nchini Kuwait. Mhe. Mhandisi Aisha S. Amour akutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Automobile Agents kuhusu fursa za uwekezaji zinazopatikana Tanzania katika sekta hiyo. Viongozi hao walikubali kufikisha taarifa kwa wajumbe wa umoja wao na kujipanga kufika Tanzania kuangalia utaratibu wa uwekezaji katika sekta yao ya magari.