Friday, January 8, 2021

HABARI KTK PICHA WANG Yi AKUTANA, KUFANYA MAZUNGUMZO NA JPM

Mjumbe wa Baraza la Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamuhuri ya Watu wa China, mhe. Wangi Yi ameendelea na ziara yake leo kwa kutembelea eneo la Mwalo wa Chato na kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na kuongea na vyombo vya Habari vya nchini akiwa yeye na mwenyeji wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi, (Mb).

Awali, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa wito kwa Watanzania kutumia uwepo wa soko la China katika kupeleka mazao ya kilimo yaliyoongezwa thamani.

Ametoa wito huo wilayani Chato wakati akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi aliyepo nchini kwa ziara ya kikazi ambapo Rais Magufuli ameiomba serikali ya China kutumia ushirikiano na Tanzania kununua mazao ya kilimo hapa nchini.


Mjumbe wa Baraza la Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamuhuri ya Watu wa China, mhe. Wangi Yi akiangalia jinsi bondo la samaki linavyotolewa na mmoja kati ya wavuvi wanaojishughulisha na shughuli za uvuvi katika Mwalo wa Chato mkoani Geita

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mjumbe wa Baraza la Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamuhuri ya Watu wa China, mhe. Wangi Yi  wakati alipokuwa anaongea na waandishi wa Habari - Chato mkoani Geita

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi moja kati ya zawadi Mjumbe wa Baraza la Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamuhuri ya Watu wa China, mhe. Wangi Yi 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mjumbe wa Baraza la Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamuhuri ya Watu wa China, mhe. Wangi Yi, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi pamoja na baadhi ya Mawaziri wakiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mjumbe wa Baraza la Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamuhuri ya Watu wa China, mhe. Wangi Yi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Kabudi, Balozi wa China Nchini Tanzania, Mhe. Wang Ke pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Kabudi, (Mb) akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani)- Chato mkoani Geita 

Mjumbe wa Baraza la Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamuhuri ya Watu wa China, mhe. Wangi Yi akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) - Chato mkoani Geita 

 

Mjumbe wa Baraza la Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamuhuri ya Watu wa China, mhe. Wangi Yi akiwaaga viongozi mbalimbali katika uwanja wa ndege wa Geita - Chato muda mfupi kabla ya kuondoka kwake



Mawaziri wakiongozwa na Prof. Kabudi wakimuaga Mjumbe wa Baraza la Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamuhuri ya Watu wa China, mhe. Wangi Yi katika uwanja wa ndege wa Geita - Chato   


Ndege aliyokuja nayo Mjumbe wa Baraza la Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamuhuri ya Watu wa China, mhe. Wangi Yi ikiondoka 



















Thursday, January 7, 2021

WANGI YI AWASILI NCHINI, KUZINDUA VETA

Mjumbe wa Baraza la Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamuhuri ya Watu wa China, mhe. Wangi Yi ameanza ziara yake ya kikazi ya kikazi nchini Tanzania.

Mhe. Wangi Yi amewasili majira ya saa 11 jioni katika uwanja wa ndege wa Geita - Chato na kupokelewa na mwenyeji wake Mhe. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi, (Mb).

Mara baada ya kuwasili, Mhe. Wang Yi ameshiriki katika uzinduzi wa chuo cha Veta kilichopo Chato mkoani Geita, ambapo ujenzi wa chuo hicho umegharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumza wakati akimkaribisha Mhe. Wang Yi katika uzinduzi wa chuo hicho, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka umuhimu mkubwa katika Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi, ili kufanikisha kujenga uchumi wa viwanda, na kufikia Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025.

"Lengo letu ni kujenga angalau kituo kimoja cha umma cha mafunzo ya ufundi stadi katika kila wilaya," amesema Prof. Ndalichako  

Aidha, Prof. Ndalichako ameongeza kuwa lengo kubwa la Serikali ni kujenga vyuo vingi vya Veta kwa kutumia vyanzo vya mapato vya ndani na kwa ushirikiano na mataifa rafiki ambapo mpaka sasa Serikali ina vituo 41 vya umma vya mafunzo ya ufundi stadi nchini na vingine 29 vinaendelea kujengwa.

Pia Prof. Ndalichako amesema Serikali ya Tanzania iko tayari kupokea moja ya kati ya karakana 10 za mafunzo za Luban (Luban Workshops), ambazo China imedhamiria kuzijenga barani Afrika, ili kutoa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana wa ki-afrika. Karakana hiyo inaweza kuwa sehemu ya Kituo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Wilaya ya Chato ambacho tumekizindua leo.

Kwa upande wake Mjumbe wa Baraza la Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Wang Yi, amesema ili Taifa lolote liweze kupiga hatua za na kiteknolojia na kufikia malengo ya mapinduzi ya viwanda ni lazima taifa hilo liwe na vijana wenye ujuzi wa kitaaluma hivyo chuo cha Veta ni mojawapo ya maeneo ya kuwajengea vijana uwezo wa kitaaluma.

Mhe. Wang Yi ameongeza kuwa Serikali ya China ipo pamoja na Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha vijana wanapata mafunzo ya kitaaluma katika vyuo vya Veta na kwa kudhihirisha hilo, China inachangia kiasi cha RB 1,000,000 za China sawa na fedha za kitanzania Shilingi 350 milioni kwa ajili ya kuendeleza chuo cha Veta - Chato.     

"Binafsi naomba kumpongeza Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwa mwanamapinduzi wa kweli kiuchumi na kitaaluma ambapo amefanikiwa kujenga idadi kubwa ya vyuo vya ufundi ili kuwajengea vijana uwezo wa kitaaluma jambo ambalo litachangia mapinduzi ya kiuchumi," Amesema Wang Yi.

China inasaidia Tanzania chuo cha VETA mkoani Kagera ambacho kina uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,000 ambapo ujenzi wake unaendelea.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi, (Mb) pamoja na mgeni wake Mjumbe wa Baraza la Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamuhuri ya Watu wa China, mhe. Wangi Yi wakiangalia vikundi vya ngoma katika uwanja wa ndege wa Geita-Chato


Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako, (Mb) pamoja na Mjumbe wa Baraza la Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamuhuri ya Watu wa China, mhe. Wangi Yi wakizindua rasmi chuo cha VETA


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako pamoja na Mjumbe wa Baraza la Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamuhuri ya Watu wa China, mhe. Wangi Yi wakizindua chuo cha VETA


Makatibu Wakuu, Mabalozi na viongozi waandamizi wa Serikali wakishuhudia uzinduzi wa chuo cha VETA Chato leo Mkoani Geita


Mjumbe wa Baraza la Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamuhuri ya Watu wa China, mhe. Wangi Yi akimkabidhi Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako kiasi cha Shilingi milioni 350 kwa ajili ya kuendeleza chuo cha VETA. Chuo hicho kimejengwa kwa fedha za Serikali ya Tanzania. 



Wednesday, January 6, 2021

PROF. KABUDI: WANGI YI KUWASILI TANZANIA KESHO

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amesema kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa China mhe. Wangi Yi atawasili nchini Tanzania kesho kwa ziara ya kikazi ya siku mbili tarehe 7 na 8 Januari 2021.

Prof. Kabudi ametoa kauli hiyo wakati anaongea na waandishi wa Habari leo Wilayani Chato mkoani Geita, ambapo amesema kuwa Waziri Yi atakapokuwa nchini atafanya shughuli mbalimbali ikiwemo kuzindua Chuo cha Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA) katika wilaya ya Chato mkoani Geita.

“Hapo kesho mara baada ya Mhe. Yi kuwasili hapa Chato, atazindua Chuo cha VETA cha wilaya ya Chato ambacho kimejengwa kwa fedha za watanzania,” alisema Prof. Kabudi.

Prof. Kabudi ameongeza kuwa “sababu ya kumuomba afungue chuo hicho ni utamaduni wetu wa kumpa heshima mgeni anapokuja hapa nchini kwetu, sambamba na kutambua elimu ya mafunzo na ufundi stadi ilivyopiga hatua huko nchini China.”

Pamoja na mambo mengine, Prof. Kabudi amesema kuwa  Serikali ya China itajenga Chuo cha Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA) mkoani Kagera ikiwa ni namna ya kufikia lengo la  Serikali  ya Awamu ya Tano ya kujenga VETA kila Wilaya hapa nchini.

Waziri Kabudi ameongeza kuwa shughuli nyingine zitakazofanywa na Waziri wa Mambo ya Nje wa China, kuwa ni  mazungumzo na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, pamoja na kufanya  mazungumzo rasmi kati yake na ujumbe wake kutoka nchini China.

Aidha, shughuli nyingine atakazofanya Waziri Yi ni pamoja na kutembelea mwalo wa Chato ili kuona shughuli za uvuvi, ikizingatiwa kuwa ziwa Viktoria ni ziwa la pili kwa ukubwa dunia Pamoja na kusaini mkataba wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha tano kutoka Mwanza hadi Isaka chenye urefu wa km 341 ambapo kitagharimu kiasi cha Shilingi trilioni 3.0617

Waziri Kabudi ameogeza kuwa, Februari mwaka huu Serikali ya Tanzania inatarajia kuanzisha  safari za ndege za moja kwa moja kutoka Dar es Salaam hadi Guanzhou  nchini China ili kukuza sekta ya utalii. 

Historia ya mahusiano ya kidiplomasia kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya watu wa China ulianza mwaka 1965.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwaelezea waandishi wa Habari Chato mkoani Geita (Hawapo pichani) juu ya ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China Mhe. Wang Yi ambaye anatarajiwa kuwasili nchini Tarehe 7 Januari, 2021. 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiongea na waandishi wa Habari Chato mkoani Geita (Hawapo pichani) juu ya ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China Mhe. Wang Yi. Kulia mwa Prof. Kabudi ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali, Wilbert Ibuge, na kushoto mwa Waziri ni Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki.


Mkutano ukiendelea



Sunday, December 20, 2020

JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YAJIVUNIA MRADI WA UJENZI WA BWAWA LA KUZALISHA UMEME LA JULIUS NYERERE.


Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki imeeleza jinsi inavyojivunia na mradi wa ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere ambalo baada ya kukamilika kwake hapo Juni 2022 linatarajiwa kuzalisha Migawati 2115 za umeme. 

Haya yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala Mhandisi Steven Mlote alipotembelea mradi huo ambao kwa ndio mradi pekee mkubwa wa umeme kwa sasa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Ameongeza kuwa mradi huu sio tu ni muhimu kwa Tanzania bali utazinufaisha pia nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki na nchi zingine jirani. Mhandisi Mlote pia ameeleza kuridhishwa kwake na ushiriki wa Watanzania katika katika ujenzi wa mradi huo, ambapo kati ya Wafanyakazi zaidi ya 5000, asilimia 90 ni Watanzania. 

Eng. Mlote ameonesha furaha yake baada ya kuelezwa kuwa mradi huo mkubwa Afrika Mashariki kwa sasa unafadhiliwa na Serikali ya Jumhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimi 100, chini ya Uongozi wa Rais Dkt John Pombe Magufuli. Mhandisi Mlote ametoa wito kwa Watanzania hasa ambao wanazunguka eneo mradi wa kutunza mazingira ili kuufanya mradi huo kuendelea kuwa katika mazingira mazuri na salama wakati wote.

Awali ujumbe huo wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki umetembelea mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kwa lengo la kijionea maendeleo ya ujenzi wa maradi huo na kueleza kufurahishwa na kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, vilevile ametumia fursa hiyo kuwasihi vijana wa Kitanzania waliopata fursa ya ujenzi wa reli kuendelea kujifunza kwa moyo na kwa kujituma ili kupata maarifa na ujuzi wa kuendelea kutunza, kuendesha na kuendeleza miradi hata baada ya wataalmu kutoka makampuni yanayohusika na ujenzi kuondoka nchini. 

Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala Mhandisi Steven Mlote (Wapili kusho) akimsikiliza mtaalamu (hayupo pichani) aliyekuwa akielezea masuala mbalimbali kuhusu ujenzi wa mradi wa bwawa la umeme la Julius Nyerere alipotembelea mradi huo.

Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala Mhandisi Steven Mlote akifurahia jambo na wadau wengine walioenda kutembelea na kujifunza katika mradi huo.
Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala Mhandisi Steven Mlote kiwa katika picha ya pamoja na wadau wa sekta ya elimu walioenda kutembelea mradi huo

Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala Mhandisi Steven Mlote akifuatilia wasilisho (presentation) kuhusu mradi wa bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere kutoka kwa mtaalamu muda mfupi kabla ya kwenda kutembelea eno la mradi.




Saturday, December 19, 2020

Ujumbe wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki watembelea Mradi wa Ujenzi wa SGR


Ujumbe wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki umetembelea mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kwa lengo la kijionea maendeleo ya ujenzi wa maradi huo unaotekelezwa hapa nchi. Ujumbe huo ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya anayeshughulikia masuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala Eng. Steven Mlote ulianza safari ya kutembelea mradi huo kuanzi Makutopola hadi Dar es Salaam. Ujumbe ulipate fursa ya kujionea hatau ya maendeleo iliyofikiwa sambamba na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na katika utelezaji wa mradi, ikiwemo viwanda vya kuzalishia baadhi vifaa vinavyotumika katika ujenzi wa mradi.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Eng. Mlote amesema amefurahishwa na kazi kubwa inayofanywa na Serikali katika kutekeleza mradi huo ambao unamanufaa makubwa kwa Taifa na kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki. “tuemona kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuteleza mradi huu mkubwa, tunampongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kwa kubuni mradi huu.” Eng.Mlote. Aidha, aliongezea kusema amefurahishwa na ushiriki wa idadi kubwa ya vijana wa Kitanzania katika sekta mbalimbali za ujenzi wa mradi huo ulioajiri takribani watu 13,796. Amewasihi vijana wa Kitanzania waliopata fursa ya ujenzi wa reli kuendelea kujifunza kwa moyo na kwa kujituma ili kupata maarifa na ujunzi wa kuendelea kutunza, kuendesha na kuendeleza mradi huo hata baada ya wataalmu kutoka kampuni inayohusika na ujenzi kuondoka nchi. 

Kwa upande mwingine Eng. Mlote ametoa wito kwa Watanzania hasa ambao wanazunguka eneo la mrafi, wikuanza kujiandaa kikamilifu katika kunufaika na fursa zitakazotokana na mradi wa reli ya kisasa kwa kuanza kuongeza uzalisha wa mazao shambani na bidhaa za viwandani kwa kuwa mradi huo utarahisisha usafirishaji wa bidhaa na watu kwenda nchi jirani za Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Nchi za Afrika ya Kati. 

Ujumbe wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki pia unatarajia kutembelea mradi wa ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere, lililopo Wilayani Rufiji kwa lengo la kujionea hatua iliyofikiwa katika ujenzi.

Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala Eng. Steven Mlote akifualia mada iliyokuwa ikiwalishwa na mtalaamu wa ujenzi kuhusu hatua mbalimbali zilizofikiwa katika ujenzi wa mradi wa treni ya kisasa (SGR) mara baada ya kuwasili katika eneo la makutupola jijini Dodoma.

 


Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhandisi Steven Mlote akiwa na Mhandisi Ignas Lymo kutoka Shirika la Reli Tanzania wakitokea kwenye moja ya handaki (tunnel) la kupita treni.

Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhandisi Steven Mlote akisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalamu alipotembelea moja ya handaki (tunnel) ya kupita treni ambalo lipo katika hatua za mwisho za ujenzi.

Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhandisi Steven Mlote  (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watalumu wa ujenzi na Watumishi wa Shirika la Reli Tanzania nje ya handaki (tunnel) la kupia treni.


Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhandisi Steven Mlote akifualia mada iliyokuwa ikiwalishwa na mtalaamu wa ujenzi kuhusu hatua mbalimbali zilizofikiwa katika ujenzi wa mradi wa treni ya kisasa (SGR) mara baada ya kuwasili katika eneo la kambi ya Soga, mkoani Pwani.

Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhandisi Steven Mlote akitembea pembezoni mwa reli ambayo ipo katika hatua za mwisho za ujenzi.


Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhandisi Steven Mlote akijadili jambo na watalamu wa ujenzi wa reli ya kisasa alipo tembelea ili kujionea maendeleo ya ujenzi wa mradi huo

Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhandisi Steven Mlote akisikiliza malezo kutoka kwa Mhandisi Ignas Lyimo kutoka Shirika la Reli Tanzania alipotembelea Stesheni ya Treni ya Morogoro mjini.


Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhandisi Steven Mlote akiendelea kusikiliza maelezo kutoka kwa Mhandisi Ignas Lyimo kutoka Shirika la Reli Tanzania alipotembelea Stesheni ya Treni ya Morogoro mjini.

 

Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhandisi Steven Mlote akisikiliza maelezo kutoka kwa mataalamu alipotembelea Stesheni ya Treni ya iliyopo eneo la Tazara jijini Dar es Salaam

Friday, December 18, 2020

TANZANIA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA IORA

 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha akishiriki Mkutano wa 20 wa Baraza la Mawaziri wa Nchi zilizopo kwenye Mwambao wa Bahari ya Hindi (Indian Ocean Rim Association – IORA) uliofanyika tarehe 17 Disemba, 2020 kwa njia ya mtandao.


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha akifuatilia Mkutano wa 20 wa Baraza la Mawaziri wa Nchi zilizopo kwenye Mwambao wa Bahari  ya Hindi (Indian Ocean Rim Association – IORA) uliofanyika     tarehe 17 Disemba, 2020 kwa njia ya mtandao. Kulia akifuatilia mkutano huo ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano     wa Afrika Mashariki Bi. Agness Kayola

      

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha akifuatilia Mkutano wa 20 wa Baraza la Mawaziri wa Nchi zilizopo kwenye Mwambao wa Bahari ya Hindi (Indian Ocean Rim Association – IORA) 


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha akifuatilia Mkutano wa 20 wa Baraza la Mawaziri wa Nchi zilizopo kwenye Mwambao wa Bahari ya Hindi (Indian Ocean Rim Association – IORA) 


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha akiongoza ujumbe wa Tanzania ulioshiriki Mkutano wa 20 wa Baraza la Mawaziri wa Nchi zilizopo kwenye Mwambao wa Bahari ya Hindi (Indian Ocean Rim Association – IORA) uliofanyika tarehe 17 Disemba, 2020 kwa njia ya mtandao. 


TANZANIA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA IORA

Tanzania imedhamiria kuimarisha ushirikiano na Jumuiya ya Nchi zilizo kwenye Mwambao wa Bahari ya Hindi (Indian Ocean Rim Association – IORA) katika kutekeleza mikakati ya uchumi wa bluu ambao unalenga kuimarisha sekta ya uvuvi hususan uvuvi wa bahari kuu.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha amesema hayo aliposhiriki Mkutano wa 20 wa Baraza la Mawaziri wa Nchi zilizopo kwenye Mwambao wa Bahari ya Hindi (Indian Ocean Rim Association – IORA) uliofanyika tarehe 17 Disemba, 2020 kwa njia ya mtandao.

Amesema Tanzania itaboresha Sekta ya Uvuvi kwa kuimarisha kilimo cha mwani, utalii wa meli (cruise tourism), michezo ya baharini, utafutaji wa rasilimali za mafuta na gesi kwenye eneo la bahari, ujenzi wa bandari maalum za uvuvi, mafuta na gesi na masuala mengine muhimu ya kuimarisha uchumi na ustawi wa wananchi.

Mhe. Ole Nasha ametumia mkutano huo kuwakaribisha wenye nia ya kuwekeza nchini kuja kwa wingi ili kutumia rasilimali zilizopo kwa pamoja na kwa faida ya pande zote mbili.

Amesema Serikali ya Tanzania imejipanga kutumia rasilimali zilizopo katika bahari ya Hindi na kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji ili kuwavutia na kuimarisha Ushirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi.

Mkutano wa 20 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo ya IORA umejadili masuala ya maendeleo katika eneo la Bahari ya Hindi ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa mpango kazi wa Jumuiya ya IORA wa mwaka 2017 – 2021. maandalizi ya mpango kazi mpya wa IORA wa mwaka 2022 – 2026; ushiriki na ushirikishwaji wa washirika wa mazungumzo katika masuala ya miradi na program za Jumuiya; masuala ya ulinzi na usalama wa bahari ya Hindi, mkakati wa kupambana na uhalifu, uharamia na biashara haramu ya binadamu katika eneo hilo la bahari.

Mkutano huo wa Baraza la Mawaziri ulitanguliwa na Mkutano wa 22 wa Kamati ya Makatibu Wakuu/ Maafisa waandamizi wa Jumuiya ya IORA uliofanyika tarehe 15 – 17 Desemba, 2020.

 

 


Thursday, December 17, 2020

HABARI KTK PICHA ZIARA YA WAWEKEZAJI KUTOKA UTURUKI NCHINI TANZANIA


Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo akielezea juu ya ziara ya wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Uturuki katika studio za Radio Uhuru (Uhuru FM) Leo Jijini Dar es Salaam

 

Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo akiwa na wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Uturuki pamoja na wadau kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Shirika la Viwanda Vidogo nchini (SIDO) na Mamlaka ya Kanda za Kusindika Usafirishaji Tanzania (EPZA) wakiwa tayari kwa kikao kazi. Wadau hao wamekutana kwa pamoja katika ofisi za TIC Jijini Dar es Salaam kuwaelezea wawekezaji kuhusu fursa mbalimbali za biashara zilizopo nchini. 


Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo (wa kwanza kushoto) pamoja na wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Uturuki wakifuatilia mada iliyokuwa inawasilishwa katika Ofisi za TIC, leo jijini Dar es Salaam


Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo (wa kwanza kushoto), wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Uturuki pamoja na wadau kutoka TIC, EPZA, TCCIA, TPSF na SIDO wakisikiliza mada iliyokuwa inahusu fursa mbalimbali za uwekezaji hapa nchini leo jijini Dar es Salaam


Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo akiongea na wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya kumalizika kwa kikao baina ya Wawekezaji na Wafanyabiashara kutoka Uturuki pamoja na wadau kutoka TIC, EPZA, SIDO, TCCIA na TPSF Jijini Dar es Salaam 


Mwenyekiti wa Bodi wa Kampuni ya Kardag kutoka Uturuki ambae pia ni mmoja kati ya wawekezaji akiongea na wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya kumalizika kwa kikao baina yao na wadau kutoka TIC, EPZA, SIDO, TCCIA na TPSF Jijini Dar es Salaam 












Tuesday, December 15, 2020

WAWEKEZAJI KUTOKA UTURUKI WAWASILI TANZANIA KUWEKEZA

Wawekezaji kutoka nchini Uturuki wamewasili nchini Tanzania kwa ajili ya kujionea fursa za uwekezaji na biashara zilizopo nchini ili waweze kuwekeza na kukuza Diplomasia ya Uchumi baina ya mataifa hayo.

Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo amethibisha kuwasili kwa wawekezaji hao wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Waturiki "Compass Partners" leo jijini Dar es Salaam, na kuongeza kuwa wawekezaji watano kati ya kumi wamefika nchini na kujumika na waturuki wengine wanaofanya biashara zao hapa nchini.

"Wawekezaji hawa kutoka Uturuki wamekuja na wamefungua taasisi yao inayojulikana kwa jina la "Compass Partners" ili kuendeleza biashara na tunaamini kwa kutekeleza biashara hii tunaenda kuendeleza uchumi wa Tanzania na kutengeneza ajira kwa watanzania," Amesema Prof. Kiondo

Prof. Kiondo ameongeza kuwa, hatua ya kwanza wawekezaji hao wameleta bidhaa mbalimbali ili watanzania wazione, hatua ya pili itakuwa ni uwekezaji wa kiwanda hapa nchini kwa ajili ya kuanza uzalishaji wa bidhaa ambazo zitauzwa hapa nchini.

Aidha, kwa upande wa bidha zinazozalishwa hapa nchini ambazo zina fursa ya kuuzwa Uturuki ni pamoja na chai, pamba, tumbaku na kahawa bidhaa hizi zote zina soko kubwa sana nchini Uturuki.

Tunazalisha tani 350,000 za pamba lakini tunaweza kuchakata asilimia 15 tu, hivyo tumepata tayari mwekezaji ambaye atawekeza katika kiwanda cha nguo mkonani simiyu ili kuongeza thamani ya bidhaa ya pamba hapa nchini.

Balozi, Prof. Kiondo ametoa wito kwa Watanzania kuanza kuchangamkia fursa hizo za biashara ili waweze kuongeza kipato na kuongeza biashara zao.

Kwa upande wake, Kaimu Balozi wa Uturiki hapa Nchini, Mhe. Onur Yah amesema kuwa biashara kati ya Tanzania na Uturiki imekuwa ikiimarika kila wakati kwani Tanzania ni sehemu salama ya kuwekeza na kufanya biashara.

"Kupitia uwekezaji katika sekta mbalimbali ni imani yangu kuwa tutaendelea kukuza na kuimarisha uhusiano wetu wa kidiplomasia," Amesema Mhe. Yah

Aidha, amewataka Waturuki na Watanzania kutumia fursa za biashara zinazopatikana baina ya mataifa hayo ili kufanya biashara na kukuza uchumi wao.

Ushirikiano wa Tanzania na Uturuki ni wa muda mrefu, pamoja na mambo mengine uhusiano huo umekuwa ukijikita zaidi katika kuendeleza uwekezaji wa viwanda, elimu na utalii hasa katika kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania nchini Uturuki.

Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo akiongea na wanahabari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Waturiki "Compass Partners" leo jijini Dar es Salaam


Kaimu Balozi wa Uturiki hapa Nchini, Mhe. Onur Yah akiongea na wanahabari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Waturiki "Compass Partners" leo jijini Dar es Salaam


Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo pamoja na Kaimu Balozi wa Uturiki hapa Nchini, Mhe. Onur Yah wakikata utepe wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Waturiki "Compass Partners" leo jijini Dar es Salaam



 

 

WAZIRI KABUDI AHIMIZA USHIRIKIANO MIONGONI MWA NCHI ZA OACPS


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palagamba John Kabudi (Mb) akiongoza Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (OACPS) uliokuwa ukiendelea kwa njia ya mtandao (Video Conference). Prof. Kabudi ni Rais wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo hadi Januari 31, 2021

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palagamba John Kabudi (Mb) akiwa na ujumbe wa Tanzania alipokuwa akiongoza Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (OACPS). Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mshariki Mhe. William Tate Ole Nasha, Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Mhe. Jestas Abouk Nyamanga, Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mwanaid Ali Hamis

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palagamba John Kabudi (Mb) akiwa na ujumbe wa Tanzania akiongoza Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (OACPS).


Sehemu ya Ujumbe wa Tanzania wakifuatilia Makutano wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (OACPS).

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palagamba John Kabudi (Mb)akisisitiza jambo wakati akiongoza Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (OACPS) uliokuwa ukiendelea kwa njia ya mtandao (Video Conference). Prof. Kabudi ni Rais wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo hadi Januari 31, 2021.


Monday, December 14, 2020

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI QATAR WAANZISHA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WATANZANIA WANAOAJIRIWA NCHINI HUMO

Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar umeanzisha rasmi programu ya  mafunzo  kwa waajiriwa wapya kutoka Tanzania wanaokwenda kufanya kazi nchini humo.

Mafunzo hayo yameanzishwa kwa makubaliano kati ya Ubalozi na  Kampuni zote zinazoajiri wafanyakazi kutoka Tanzania ambao  Ubalozi huwapatia barua kwa ajili ya kuthibitisha uhalali wao ili kupata kibali cha kuingia nchini humo. Mafunzo hayo ambayo hutolewa mara tu wanapowasili nchini humo, yanalenga kuwajengea uwezo wa kazi pamoja na kuwaelewesha sheria na taratibu za ajira za Qatar pamoja na haki zao za msingi.

Kadhalika, mafunzo hayo  yameanzishwa ili kuwajulisha maadili, mila na utamaduni za Qatar pamoja na kuwahimiza kujua wajibu wao ili kudumisha heshima ya Tanzania kimataifa na kuitangaza vyema nchi. 

Mafunzo ya awali yametolewa tarehe 12 Desemba, 2020 kwa Mabinti 9 kutoka Tanzania ambao wameajiriwa na Kampuni ya Qatar Manpower Solutions (WISA) inayomilikiwa na Serikali kwa ajili kufanya usafi na huduma za ndani. 

Mafunzo hayo ambayo yamesimamiwa na Bw. Volka Gowele, Afisa wa Ubalozi yameendeshwa na Bw. Sahim Ayoub Khatib, Diaspora wa Tanzania na Mwajiriwa kwenye Kampuni ya HBK ya Qatar kwenye Kitengo cha Utawala na Rasilimali Watu. Bw. Khatib amejitolea kusaidia kuendesha mafunzo hayo kwa Watanzania.

Bw. Sahim Ayoub Khatib (mwenye karatasi), Diaspora wa Tanzania nchini Qatar ambaye pia ni Mwajiriwa wa Kampuni ya HBK ya nchini humo akitoa mafunzo kwa Mabinti 9 kutoka Tanzania ambao wameaajiriwa na Kampuni ya Manpower Solutions (WISA) inayomilikiwa na Serikali kwa ajili ya kufanya kazi za usafi na huduma za ndani. Mafunzo hayo ambayo yanalenga kuwajengea uwezo  pamoja na kuwaelewesha sheria na taratibu za ajira za Qatar, yameandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini humo. Mafunzo hayo yalifanyika kwenye Ofisi za Ubalozi hivi karibuni na kusimamiwa na Bw. Volka Gowele (mwenye barakoa), Afisa wa Ubalozi.


Mafunzo yakiendelea kwa Mabinti hao
Mabinti tisa kutoka Tanzania walioshirki mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar


Picha ya pamoja kati ya Bw. Khatib (kushoto), Bw. Gowele (wa pili kushoto) pamoja na Mabinti tisa kutoka Tanzania walioshiriki mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar.