Thursday, January 21, 2021
KAIMU KATIBU MKUU AKUTANA NA BALOZI WA VITNAM
Wednesday, January 20, 2021
Friday, January 15, 2021
BALOZI MBUNDI AONGOZA MAJADILIANO BAINA YA TANZANIA NA POLAND
Sehemu ya wajumbe wakifuatilia mazungumo |
Monday, January 11, 2021
RAIS NYUSI AWEKA JIWE LA MSINGI HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA - CHATO
Na Nelson Kessy, Chato
Rais
wa Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi amewasili nchini leo kwa ziara ya kikazi na
kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John
Pombe Magufuli katika uwanja wa ndege wa Geita - Chato na kisha kuweka jiwe la
msingi la ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya Kanda- Chato.
Akizungunza
katika hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali ya Rufaa
ya Kanda-Chato, Rais Magufuli alimshukuru Rais Mhe. Filipe Nyusi kwa
kumtembelea Chato na kuongeza kuwa
Msumbiji ni rafiki wa muda mrefu wa Tanzania na nchi hizo zina makubaliano ya kushirikiana katika mambo
mbalimbali ikiwemo biashara na uwekezaji.
"Biashara
kati ya Tanzania na Msumbiji imeongezeka, hadi kufikia mwaka 2020 ilifikia
shilingi bilioni 93.6, kuna makampuni ya Msumbiji yanafanya kazi hapa na baadhi
ya makampuni ya Tanzania yanafanya kazi kule." Amesema Rais Magufuli.
Rais
Magufuli ameongeza kuwa Januari 9, 1967 Hayati Mwalimu Julius Nyerere
alitembelea Wilaya ya Chato na kufungua kiwanda cha pamba kilichojengwa kwa
shilingi milioni 2 ambacho kilikuwa na uwezo wa kuchakata marobota 20,000.
Aidha,
Rais Magufuli amesema kuwa Mwalimu Nyerere alichangisha fedha na yeye binafsi
kuchangia shilingi 2,000 kwa ajili ya kujenga bandari ya Nyamirembe ili iweze
kusafirisha pamba kwenda Mwanza na Dar es Salaam kwa hiyo wa Rais Nyusi amefika
eneo ambalo alifika Mwalimu Nyerere.
"Kwetu
sisi tunaona hii ni zawadi kubwa kwa wewe kuja kuzindua hospitali hii ambayo ni
kubwa na itahudumia pia nchi za jirani.Nawashukuru Wizara ya Afya na
Wakandarasi, nitawabana Wizara ya Afya
ili hospitali hii ikamilike mara moja." Alisema Rais Magufuli
Kwa
upande wake Rais Nyusi amempongeza Rais Magufuli kwa juhudim kubwa za
kushughulikia maisha ya wananchi wa Tanzania kwa kuendelea kuboresha sekta pamoja
na huduma za afya nchini.
"Nashukuru
kwa Rais Magufuli kunipa nafasi ya kuweka jiwe la msingi kwa sababu Serikali
inayoaangalia afya za wananchi hiyo ni Serikali inayopenda wananchi wake. Rais
Magufuli anashughulikia sana maisha ya wananchi wa watanzania kwa kuangalia
nyumba bora za kuishi, huduma za maji, chakula
na afya bora" amesema Rais Nyusi.
"Kwa
hiyo hii ni zawadi kwetu kwa kutupa
nafasi ya kuweka jiwe la msingi katika hospitali hii kubwa, kule Msumbiji
tumeanza (Program ya presidential
initiatives) ya kujenga hospitali kila wilaya hii ni zawadi kubwa kwetu ya kutupa nafasi ya kuweka jiwe la msingi katika afya ya wananchi," Ameongeza Rais
Nyusi
Aidha,
Rais Nyusi amesema kuwa mkoa wa Geita ni
tajiri kwa kuwa kuna kilimo cha mpunga,
madini ya dhahabu na uvuvi wa
samaki, hivyo kuwataka wananchi wa mkoa huo kufanyakazi kwa bidii.
Naye,
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy
Gwajima amesema kuwa awamu ya kwanza ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda -
Chato ilikadiriwa kutumia sh. bil.16, Serikali imeshatoa sh. bil.14 ambapo
ujenzi umekamilika kwa asilimia 90 na makabidhiano yanatarajiwa kufanyika mwezi
Machi, 2021.
Ameongeza
kuwa awamu ya pili ya ujenzi imeshaanza
kwa jumla ya gharama ya shilingi bilioni 14 ambapo mpaka sasa Serikali imetoa
shilingi bilioni 4.1 na utekelezaji wake umefikia asilimia 37.
"Hospitali
ya Rufaa ya Kanda - Chato itakapokamilika itakuwa na uwezo wa kuhudumia
wananchi zaidi ya milioni 14 ambapo kwa siku itakuwa na uwezo wa kuhudumia
wagonjwa kati ya 700 - 1000." Amesema Dkt. Gwajima
Rais
wa Msumbiji, Filipe Jacinto Nyusi yupo nchini kwa ziara ya siku moja ambapo
atafanya mazungumzo na Rais Magufuli kuhusu namna ya kuboresha maisha wananchi wetu
pamoja na usalama.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Pombe Joseph
Magufuli akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) muda mfupi kabla ya Rais wa
Msumbiji, Mhe. Filipe Nyusi kuwasili katika uwanja wa ndege wa Geita - Chato
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Pombe Joseph
Magufuli na mgeni wake Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi wakipita katikati ya
gadi ya heshima mara baada ya Rais Nyusi kuwasili nchini
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Pombe Joseph
Magufuli na mgeni wake, Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi wakipata maelezo
kuhusu ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya Kanda - Chato kutoka kwa Katibu Mkuu,
Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Prof. Mabula Mchembe
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Pombe Joseph
Magufuli na mgeni wake, Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi wakimsikiliza maelezo
ya Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy
Gwajima wakati walipofanya ziara katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda - Chato
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Pombe Joseph
Magufuli na mgeni wake Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi wakiweka rasmi jiwe
la msingi katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda - Chato
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Pombe Joseph
Magufuli akihutubia hadhara ya wananchi (hawapo pichani) mara baada ya kuweka
jiwe la msingi katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda - Chato
Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi akihutubia hadhara ya wananchi (hawapo pichani) mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda - Chato |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Pombe Joseph
Magufuli pamoja na Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi wakiwaaga wananchi (hawapo
pichani) mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda
- Chato
Sunday, January 10, 2021
RAIS WA MSUMBIJI FILIPE NYUSI KUFANYA ZIARA YA KIKAZI NCHINI TANZANIA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiongea na waandishi wa Habari Chato mkoani
Geita (Hawapo pichani) kuhusu ziara ya siku mbili ya Rais wa Jamhuri ya
Msumbiji hapa nchini, Mhe. Filipe
Jacinto Nyusi. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali, Wilbert Ibuge, na kushoto ni Mkuu
wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Luhumbi. Picha na Nelson Kessy
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiongea na waandishi wa Habari Chato mkoani
Geita kuhusu ziara ya siku mbili ya Rais wa Jamhuri ya Msumbiji hapa nchini, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi. Kulia ni Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia
Jenerali, Wilbert Ibuge, na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert
Luhumbi. Picha na Nelson Kessy
Na Nelson Kessy, Chato
Rais
wa Jamhuri
ya Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi anatarajia
kufanya ziara ya kikazi ya siku mbili hapa nchini Tanzania kuanzia tarehe 11 -
12 Januari 2021 kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli.
Akithibitisha
juu ya ziara hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof.
Palamagamba John Kabudi (Mb) amesema kuwa Mhe. Nyusi atawasili nchini kwa ziara
ya kikazi ya siku mbili na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika uwanja wa ndege wa Geita -
Chato.
"Ziara hii ya Rais Nyusi ni ziara ya kindugu ambayo ilipangwa
kufanyika muda mrefu lakini haikuweza kufanyika mapema, kutokana na kutokana na
sababu mbalimbali, hususan Uchaguzi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
uliofanyika Oktoba 28, 2020," Amesema Prof. Kabudi.
Aidha,
Prof. Kabudi ameongeza kuwa, ziara ya Mhe Nyusi, ni kwa ajili ya kuendeleza na kuimarisha
mahusiano ya nchi zetu mbili katika maeneo anuwai, yakiwemo yale ya kidiplomasia,
kiuchumi, kisiasa na kijamii; kama yalivyoasisiwa na vyama vya ukombozi vya
nchi zetu, yaani, chama cha TANU na Chama cha Afro-Shirazi na baadaye Chama cha
Mapinduzi (CCM) kwa upande wa Tanzania na kile cha FRELIMO kwa upande wa
Msumbiji. Mtakumbuka, mahusiano haya yaliyotukuka, yaliasisiwa na viongozi
waanzilishi wa nchi zetu huru, yaani Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere kwa upande wa Tanzania na Hayati Dkt. Eduardo Tshivambo
Mondlane kwa upande wa Msumbiji.
"Uhusiano
huo pia umeendelea baada ya Msumbiji kupata uhuru wake kupitia mapambano ya
silaha mwaka 1975, ambapo, kama nyote mnavyofahamu, kuanzia Rais wa Kwanza wa
Msumbiji Huru, Hayati Samora Moises Machel, na wengine wote waliomfuatia hadi
leo, na Marais wa Tanzania baada ya Hayati Baba wa Taifa hadi leo, wote
wameendelea kuimarisha mahusiano hayo na undugu wa Watanzania na Watu wa
Msumbiji ambao kwa hakika ni ndugu wa damu," Ameongeza Prof. Kabudi
Prof. Kabudi ameeleza kuwa,
licha ya uhusiano wa Kihistoria na Kidiplomasia kati ya nchi zetu mbili, uhusiano
wa Kiuchumi nao umeendelea kuimarika. Tanzania inafanya biashara na Msumbiji
kupitia mazao ya chakula na biashara pamoja na bidhaa za viwandani. Kwa mfano,
takwimu kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zinaonesha kuwa jumla ya mauzo
ya Nje (Export) kati ya nchi hizi mbili zilifikia Shilingi za Kitanzania
Bilioni 76.4 kwa mwaka 2018 na Shilingi za Tanzania Bilioni 93.5 kwa mwaka
2019.
Kuhusu uwekezaji, hadi sasa
makampuni makubwa ya Kitanzania yaliyowekeza mitaji mikubwa nchini Msumbiji ni
pamoja Bakheresa (Azam), Mohammed Enterprises, Quality Foam (Magodoro Dodoma),
n.k. Vilevile kuna Watanzania wanaomiliki kampuni za usafirishaji wa abiria na
mizigo pamoja na biashara za kati na ndogondogo nchini Msumbiji.
"Licha ya changamoto ya
Ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu (COVID 19) SADC imeendelea kuwezesha na
kusimamia biashara miongoni mwa nchi wanachama. Wakati wa ziara hii viongozi
wetu watabadilishana mawazo ya namna ya kuendelea kuwezesha ufanyaji wa biashara,"
Ameongeza Prof. Kabudi
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa
wa Geita, Mhandisi Robert Luhumbi amewataka wananchi wa Geita kujitokeza kwa
wingi na kumpokea mgeni wakati atakapokuwa amewasili katika uwanja wa ndege wa
Geita - Chato.
"Nawasihi wananchi wa
Geita kujitokeza na kumpokea mgeni wetu, kwani hii ni fursa kwa mkoa wetu,
tunapaswa kuitumia fursa hii vizuri" Amesema Mhandisi Luhumbi.
Friday, January 8, 2021
HABARI KTK PICHA WANG Yi AKUTANA, KUFANYA MAZUNGUMZO NA JPM
Mjumbe wa Baraza la Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamuhuri ya Watu wa China, mhe. Wangi Yi ameendelea na ziara yake leo kwa kutembelea eneo la Mwalo wa Chato na kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na kuongea na vyombo vya Habari vya nchini akiwa yeye na mwenyeji wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi, (Mb).
Awali,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa wito
kwa Watanzania kutumia uwepo wa soko la China katika kupeleka mazao ya kilimo
yaliyoongezwa thamani.
Ametoa
wito huo wilayani Chato wakati akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa China
Wang Yi aliyepo nchini kwa ziara ya kikazi ambapo Rais Magufuli ameiomba
serikali ya China kutumia ushirikiano na Tanzania kununua mazao ya kilimo hapa
nchini.
Mjumbe wa Baraza la Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamuhuri ya Watu wa China, mhe. Wangi Yi akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) - Chato mkoani Geita |
Mjumbe wa Baraza la Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamuhuri ya Watu wa China, mhe. Wangi Yi akiwaaga viongozi mbalimbali katika uwanja wa ndege wa Geita - Chato muda mfupi kabla ya kuondoka kwake |
Mawaziri wakiongozwa na Prof. Kabudi wakimuaga Mjumbe
wa Baraza la Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamuhuri ya Watu wa China, mhe.
Wangi Yi katika uwanja wa ndege wa Geita - Chato |
Ndege aliyokuja nayo Mjumbe wa Baraza la Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamuhuri ya Watu wa China, mhe. Wangi Yi ikiondoka |
Thursday, January 7, 2021
WANGI YI AWASILI NCHINI, KUZINDUA VETA
Mjumbe wa Baraza la Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamuhuri ya Watu wa China, mhe. Wangi Yi ameanza ziara yake ya kikazi ya kikazi nchini Tanzania.
Mhe. Wangi Yi amewasili majira ya saa 11 jioni katika uwanja wa ndege wa Geita - Chato na kupokelewa na mwenyeji wake Mhe. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi, (Mb).
Mara baada ya kuwasili, Mhe. Wang Yi ameshiriki katika uzinduzi wa chuo cha Veta kilichopo Chato mkoani Geita, ambapo ujenzi wa chuo hicho umegharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza wakati akimkaribisha Mhe. Wang Yi katika uzinduzi wa chuo hicho, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka umuhimu mkubwa katika Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi, ili kufanikisha kujenga uchumi wa viwanda, na kufikia Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025.
"Lengo letu ni kujenga angalau kituo kimoja cha umma cha mafunzo ya ufundi stadi katika kila wilaya," amesema Prof. Ndalichako
Aidha, Prof. Ndalichako ameongeza kuwa lengo kubwa la Serikali ni kujenga vyuo vingi vya Veta kwa kutumia vyanzo vya mapato vya ndani na kwa ushirikiano na mataifa rafiki ambapo mpaka sasa Serikali ina vituo 41 vya umma vya mafunzo ya ufundi stadi nchini na vingine 29 vinaendelea kujengwa.
Pia Prof. Ndalichako amesema Serikali ya Tanzania iko tayari kupokea moja ya kati ya karakana 10 za mafunzo za Luban (Luban Workshops), ambazo China imedhamiria kuzijenga barani Afrika, ili kutoa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana wa ki-afrika. Karakana hiyo inaweza kuwa sehemu ya Kituo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Wilaya ya Chato ambacho tumekizindua leo.
Kwa upande wake Mjumbe wa Baraza la
Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Wang Yi,
amesema ili Taifa lolote liweze kupiga hatua za na kiteknolojia na kufikia
malengo ya mapinduzi ya viwanda ni lazima taifa hilo liwe na vijana wenye ujuzi
wa kitaaluma hivyo chuo cha Veta ni mojawapo ya maeneo ya kuwajengea vijana uwezo
wa kitaaluma.
Mhe. Wang Yi ameongeza kuwa Serikali ya China ipo pamoja na Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha vijana wanapata mafunzo ya kitaaluma katika vyuo vya Veta na kwa kudhihirisha hilo, China inachangia kiasi cha RB 1,000,000 za China sawa na fedha za kitanzania Shilingi 350 milioni kwa ajili ya kuendeleza chuo cha Veta - Chato.
"Binafsi naomba kumpongeza Rais
wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwa mwanamapinduzi
wa kweli kiuchumi na kitaaluma ambapo amefanikiwa kujenga idadi kubwa ya vyuo
vya ufundi ili kuwajengea vijana uwezo wa kitaaluma jambo ambalo litachangia
mapinduzi ya kiuchumi," Amesema Wang Yi.
China inasaidia Tanzania chuo cha VETA mkoani Kagera ambacho kina uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,000 ambapo ujenzi wake unaendelea.
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi, (Mb) pamoja na
mgeni wake Mjumbe wa Baraza la Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamuhuri ya
Watu wa China, mhe. Wangi Yi wakiangalia vikundi vya ngoma katika uwanja wa
ndege wa Geita-Chato |
Waziri wa Elimu Sayansi na
Teknolojia, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako, (Mb) pamoja na Mjumbe wa Baraza la
Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamuhuri ya Watu wa China, mhe. Wangi Yi wakizindua
rasmi chuo cha VETA |
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi na Waziri wa
Elimu Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako pamoja na Mjumbe wa
Baraza la Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamuhuri ya Watu wa China, mhe.
Wangi Yi wakizindua chuo cha VETA |
Makatibu Wakuu, Mabalozi na viongozi
waandamizi wa Serikali wakishuhudia uzinduzi wa chuo cha VETA Chato leo Mkoani Geita |
Mjumbe wa Baraza la Taifa na Waziri wa
Mambo ya Nje wa Jamuhuri ya Watu wa China, mhe. Wangi Yi akimkabidhi Waziri wa
Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako kiasi cha Shilingi milioni
350 kwa ajili ya kuendeleza chuo cha VETA. Chuo hicho kimejengwa kwa fedha za
Serikali ya Tanzania. |