Na Mwandishi wetu, Zanzibar
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema
Zanzibar iko salama na mazingira ya kisiasa yanatoa fursa ya kuwaletea wananchi
wa Zanzibar maendeleo kutokana na uwepo wa Serikali ya umoja wa kitaifa.
Rais
Mwinyi ameyasema hayo Ikulu ya Zanzibar wakati alipokutana na ufanya mazungumzo
na uongozi wa juu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof.
Palamagamba John Kabudi na kuongeza kuwa uongozi wake unajipanga kutimiza ahadi
alizotoa kwa wananchi.
Pia
Rais Mwinyi ameongeza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja
na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetoa kipaumbele katika kuimarisha Uchumi
wa Bahari kuu hasa Uchumi wa bluu kama chanzo mbadala cha mapato kitakachosaidia
kukuza uchumi na kupunguza mzigo wa kodi kwa wananchi.
“Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimetoa
kipaumbele katika kuimarisha Uchumi wa Bahari kuu hasa Uchumi wa bluu kama
chanzo mbadala cha mapato kitakachosaidia kukuza uchumi,” Amesema Dkt.
Mwinyi
Katika
tukio jingine, Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje umekutana na kufanya
mazungumzo na Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,
Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad ambaye amesisitiza kuwa uchumi wa bluu ni muhimu
sana kwa maendeleo ya Zanzibar hivyo ni muhimu kwa Serikali zote mbili
(Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania) kulinda mipaka yake ya bahari ambapo pia ulinzi huo utasaidia kuzuia
na kupambana na uingizwaji wa dawa za kulevya hapa nchini.
“Naamini
kabisa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania tukishirikiana katika kuimarisha ulinzi wa baharini itasaidia
kupunguza uingizwaji wa dawa a kulevya hapa nchini,” Amesema Maalim Seif
Kwa
upande wake Prof. Palamagamba John Kabudi ameupongeza uongozi wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kwa kwa hatua ulizozichukua katika kuhakikisha uwepo wa
amani na utulivu visiwani humo na kwamba uwepo wa amani na utulivu utachangia
kuleta maendeleo haraka kwa wananchi wa Zanzibar.
“Zanzibar
imetulia na uchumi wake umezidi kuimarika sote ni mashahidi wa ongezeko la
watalii hapa Zanzibar hii ni ishara ya kuwa na amani na utulivu, na jambo hili
linachangia kukua kwa uchumi wa Zanzibar,” Amesema Prof. Kabudi
Mbali
na kukutana na Rais wa Zanzibar na Makamu wa Kwanza wa Rais, pia Uongozi huo
umekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ambapo wamejadili masuala
mbalimbali ya maendeleo yanayohusu Tanzania Bara na Zanzibar hususan yanayohusu
Muungano.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John
Kabudi katika ziara yake ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. William Olenasha pamoja na Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiongea
na uongozi wa juu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof.
Palamagamba John Kabudi (Mb) Ikulu Zanzibar wakati wa ziara ya kikazi ya Prof.
Kabudi Zanzibar. Prof. Kabudi ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. William Olenasha pamoja na Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiongea
na viongozi wa juu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, (hawapo pichani) katika Ikulu ya Zanzibar
Kikao
cha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali
Mwinyi na uongozi wa juu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, kikiendelea katika Ikulu ya Zanzibar
Makamu
wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif
Hamad akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Prof. Palamagamba John Kabudi wakati alipokuwa akimuelezea jambo wakati uongozi
wa Wizara ulipomtembelea Mhe. Seif kwa zaiara ya kikazi mjini Zanzibar
Kikao
cha Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Maalim Seif
Sharif Hamad na uongozi wa juu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki kikiendelea katika Ikulu ya Zanzibar