 |
Katibu
Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph
Sokoine akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha wadau wa ndani wa Jumuiya ya Nchi zilizopo
kwenye mwambao wa Bahari ya Hindi (IORA) kinachofanyika mjini Zanzibar
|
 |
Katibu
Mkuu Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Aboud S. Jumbe (kushoto) akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph
Sokoine katika kikao kazi cha wadau wa ndani wa Jumuiya ya Nchi zilizopo
kwenye mwambao wa Bahari ya Hindi (IORA) |
 |
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa
Kikanda kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Agness Kayola akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha wadau wa ndani wa Jumuiya ya Nchi zilizopo
kwenye mwambao wa Bahari ya Hindi (IORA)kinachofanyika mjini Zanzibar
|
 |
Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar Balozi Masoud A Balozi (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Ushirikiano wa
Kikanda Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Agness Kayola wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha wadau wa ndani wa Jumuiya ya Nchi zilizopo
kwenye mwambao wa Bahari ya Hindi (IORA) kinachofanyika mjini Zanzibar |
Wadau wa ndani wa Jumuiya ya Nchi zilizopo
kwenye mwambao wa Bahari ya Hindi (IORA) kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakimsikiliza Mratibu wa masuala ya IORA Tanzania Balozi Agness Kayola kinachofanyika mjini Zanzibar |
Wadau wa ndani wa Jumuiya ya Nchi zilizopo
kwenye mwambao wa Bahari ya Hindi (IORA) kutoka Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania katika picha ya Pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine baada ya ufunguzi wa kikao kazi chao kinachofanyika mjini Zanzibar |
Na mwandishi wetu, Zanzibar
Katibu
Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph
Sokoine amefungua kikao kazi cha wadau wa ndani wa Jumuiya ya Nchi zilizopo
kwenye mwambao wa Bahari ya Hindi (IORA) na kuwataka washiriki wa kikao hicho kutoa
msukumo na kipaumbele kwa shughuli zinazoratibiwa na Jumuiya hiyo.
Balozi
Sokoine amesema hayo mjini Zanzibar alipokuwa akifungua kikao kazi hicho na kuongeza
kuwa kufanya hivyo watakuwa wanalinda kwa vitendo maslahi ya Taifa na
kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya Tanzania, Nchi Wanachama na Washirika wa
Mazungumzo na hivyo kuleta tija kwa Tanzania.
Amesema
uanachama wa Tanzania kwenye Jumuiya hiyo ni muhimu kwa maendeleo ya
diplomasia, ushirikiano wa kikanda na kimataifa hasa ikizingatiwa kuwa inakutanisha
nchi mbalimbali kubwa zilizoendeleana kwamba Tanzania inaweza kutumia fursa ya Jukwaa la
IORA kuimarisha ushirikiano wa nchi na nchi na Washirika wa Mazungumzo ambao
wana nguvu kiuchumi na wameendelea kisayani na kiteknolojia.
Amewataka
wadau hao kuandaa Mapendekezo ya Miradi yenye sifa na vigezo vya kupatiwa ufadhili
kwenye Mfuko Maalum wa Jumuiya ya IORA ili kusaidia kuwezesha, kuhudumia
wananchi na kuwezesha jamii inayozunguka
maeneo ya ukanda wa bahari, uhifadhi wa
mazingira ya bahari, uvunaji endelevu wa rasilimali za bahari, uwezeshaji
wananchi kiuchumi na maeneo mengine mtambuka yenye tija na maslahi kwa
wananchi.
Awali
akizungumza katika kikao kazi hicho Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa
Kikanda Balozi Agness Kayola alisema Kikao Kazi hiko kina lengo la kuimarisha
ushiriki wa Nchi kwenye Jumuiya ya IORA; kuimarisha ushirikiano wa kisekta kati
ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar na kuimarisha vikundi kazi ili kuweza kunufaika na uanachama wa Tanzania
katika IORA.
Alisema
kwa sasa, IORA ina vikundi kazi vinane (8) ambavyo vinafanya kazi chini ya
Uratibu wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda - Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Amevitaja vikundi hivyo kuwa ni Ulinzi na
Usalama; Biashara na Uwekezaji; Kazi cha Utalii na Utamaduni; Uwezeshaji
Wanawake Kiuchumi; Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ubunifu; Uvuvi; Maafa na Uchumi
wa Bluu
Kikao
kazi hicho kinajadili mada zinazohusiana na
upatikanaji wa fursa za uwekezaji zilizopo kwenye uchumi wa bluu; sheria,
kanuni na taratibu za kuvuna na kuhifadhi rasilimali zilizopo kwenye bahari
hususan kwenye ukanda wa bahari kuu; sera na mwongozo wa kufanikisha
utekelezaji wa masuala ya uchumi wa bluu pamoja na umuhimu wa kuhifadhi mazingira
ya bahari kwa maendeleo endelevu na usalama wa eneo la bahari.
Jumuiya
ya Nchi zilizopo kwenye Mwambao wa Bahari ya Hindi inaundwa na nchi 23 ambazo
ni Australia, Afrika Kusini, Bangladesh,
Comoro, India, Indonesia, Iran, Kenya, Madagascar, Malaysia, Maldieves, Msumbiji,
Mauritius, Oman, Seychelles, Singapore, Somalia, Sri Lanka, Tanzania na
Thailand, Umoja wa Falme za Kiarabu, Yemen na Ufaransa kupitia Visiwa vya
Reunion ambavyo inavimiliki.