Friday, October 29, 2021

TANZANIA NA UMOJA WA ULAYA WAKUTANA KWA MAJADILIANOO DAR ES SALAAM

Waziri  wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akizungumza kufungua mkutano wa majadiliano kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya uliofanyika jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Joseph Sokoine akizungumza kumkaribisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kufungua mkutano wa majadiliano kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya uliofanyika jijini Dar es Salaam

Balozi wa Umoja wa Ulaya Mhe. Manfredo Fanti akizungumza wakati wa Mkutano wa majadiliano kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya uliofanyika jijini Dar es Salaam

Mwenyekiti mwenza wa Kikao cha Majadiliano ya pamoja kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya ambaye pia ni Mkurugenzi Mwendeshaji anayeshughulikia masuala ya Afrika kutoka  Umoja wa Ulaya Mhe. Balozi Rita Liranjinha akizungumza wakati wa ufunguzi wa  mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam

Mabalozi kutoka nchi za Umoja wanaoziwakilisha nchi zao nchini wakishiriki katika Mkutano wa majadiliano kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya uliofanyika jijini Dar es Salaam

Washiriki wa wa Mkutano wa majadiliano kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya uliofanyika jijini Dar es Salaam wakifuatilia kikao hicho

Washiriki wa wa Mkutano wa majadiliano kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya uliofanyika jijini Dar es Salaam wakifuatilia kikao hicho

 

TANZANIA NA RWANDA ZASAINI HATI YA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA ULINZI

Tanzania na Rwanda zimesaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Sekta ya Ulinzi (Memorandum of Understanding between United Republic of Tanzania and Republic of Rwanda on Defence Cooperation). Hati hiyo imesainiwa tarehe 28 Oktoba, 2021 na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Rwanda Mhe. Dkt. Vincent Biruta kwenye Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano ya Kudumu uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza kwenye Mkutano huo, Waziri Mulamula ameeleza kuwa miongoni mwa faida za mkutano huo ni kusainiwa kwa Hati hiyo ya Makubaliano ambayo itasaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa watu,mali na mipaka baina ya Mataifa haya mawili.

“kusainiwa kwa Hati hii ni hatua muhimu kwenye mahusiano kati ya nchi zetu hizi mbili, vilevile nina imani kubwa yale yote yaliyokubalika yatatekelezwa kwa ufanisi ili kufikia malengo tarajiwa ya nchi hizi mbili na Serikali kwa ujumla” amesema Balozi Mulamula.

Sambamba na kusaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Sekta ya Ulinzi, Tanzania na Rwanda zilijadili na kukubaliana kuhusu maeneo mengine mapya ya ushirikiano ikiwemo Manunuzi ya Umeme kutoka Mradi wa Rusumo, Ushirikiano katika Uchimbaji wa Petroli na Gesi na kubadilishana wanafunzi kati ya Chuo cha Diplomasia cha Tanzania na Chuo cha Diplomasia cha Rwanda kinachorajiwa kuanzishwa mwaka 2022.

Kwa upande wake, Dkt. Birtua aliipongeza na kuishukuru Tanzania kwa kuandaa, kushiriki kikamilifu na kuupa uzito wa hali ya juu Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda ambapo alisema kuwa hiyo ni dalili njema inayoonesha nia iliyopo ya kudumisha na kukuza ushirikiano wa kihistoria na kindugu uliopo kati ya kati Nchi hizi mbili.

Vilevile Balozi Mulamula alitoa wito kwa Sekta zinazohusika na utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa katika Mkutano huo, kuhakikisha zinatekeleza kikamilifu maagizo yaliyotolewa na kuwasilisha ripoti zake katika Mkutano wa Kamati ya Pamoja ya Utekelezaji uliopangwa kufanyika mwezi Machi, 2022 nchini Rwanda. 

Mkutano huu wa Kumi na Tano (15) wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano ya Kudumu ulitanguliwa na Kikao cha Wataalamu wa Tanzania na Rwanda kilichofanyika tarehe 25 na 26 Oktoba, 2021 na kufuatiwa na Kikao cha Makatibu Wakuu wa nchi hizi mbili kilichofanyika tarehe 27 Oktoba, 2021.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiongoza Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda katika ngazi ya Mawaziri uliofanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda katika ngazi ya Mawaziri uliofanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
Meza kuu wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa wa Tanzania na Rwanda unaimbwa kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano katika ngazi ya Mawaziri
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Rwanda Mhe. Dkt. Vincent Biruta akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Rwandakatika ngazi ya Mawaziri uliofanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa Mkutano kutoka Tanzania na Rwanda wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Mataifa hayo mawili unaimbwa kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano katika ngazi ya Mawaziri
Mkutano ukiendelea
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Rwanda Mhe. Dkt. Vincent Biruta wakisaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Sekta ya Ulinzi.
Picha ya pamoja ya Viongozi walioshiriki Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda
Picha ya pamoja ya washiriki wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda

Wednesday, October 27, 2021

BALOZI SOKOINE AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KWENYE MKUTANO WA 15 WA TUME YA PAMOJA YA KUDUMU KATI YA TANZANIA NA RWANDA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine leo tarehe 27 Oktoba 2021 ameongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Rwanda kwa Ngazi ya Makatibu Wakuu uliofanyika katika Ukumbi wa Wakimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam. 

Pamoja na mambo mengine Mkutano wa Makatibu Wakuu umepitia na kuthibitisha agenda mbalimbali zilizowasilishwa kwao na Wataalam kabla ya agenda hizo kuwasilishwa na kupitishwa kwenye Mkutano wa Mawaziri unaotarajiwa kufanyika jijini hapa tarehe 28 Oktoba 2021.

Akizungumza wakati wa hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano huo, Balozi Sokoine amewapongeza Wataalam kutoka Tanzania na Rwanda kwa kukamilisha taarifa kwa wakati na ufanisi na kuwezesha mkutano wa makatibu wakuu kufanyika.

“Mkutano huu wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ni jukwaa muhimu katika kukuza ushirikiano baina ya Nchi zetu hizi mbili jirani na rafiki, kwani hutoa fursa ya kuangalia maeneo ya ushirikiano kwa upana wake pamoja na kutoa nafasi ya kubainisha maeneo ya kipaumbele na kuainisha mpango wa utekelezaji ili kuharakisha maendeleo ya wanachini kupitia programu na miradi tunayokubaliana kuitekeleza” ameeleza Balozi Sokoine

Aliongeza kusema, Mkutano huo wa 15 utatoa nafasi kwa nchi hizi kutathmini namna makubaliano ya awali yalivyotekelezwa, kuainisha changamoto zilizojitokeza kwenye utekelezaji na kutoa suluhu ya namna ya kuzitatua ili kuimarisha ushirikiano uliopo kwa manufaa ya nchi hizi mbili. 

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Rwanda Bi. Shakilla K. Mutoni, ameeleza kuwa pamoja na kupiga hatua kwenye utekelezaji wa maazimio mengi yaliyofikiwa kwenye Mkutano wa mwisho wa Tume hiyo uliofanyika mwezi Julai, 2016 nchini Rwanda, mkutano huu wa 15 umeongeza chachu katika utekelezaji wa makubaliano, programu na miradi ambayo bado iponyuma katika utelezaji. Aidha, ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kutekeleza ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) ambayo baada ya kukamilika kwa ujenzi itarahisisha usafirishaji wa bidhaa kuelekea nchini Rwanda.

Mkutano huu wa Makatibu Wakuu ni mwendelezo wa maandalizi ya Mkutano wa 15 wa Tume ya Kudumu ya Ushirikiano unaotarajiwa kuhitimishwa na Mkutano wa Mawaziri hapo tarehe 28 Agosti 2021.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu (JPC) kati ya Tanzania na Rwanda kwa Ngazi ya Makatibu Wakuu uliofanyika katika Ukumbi wa Wakimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Rwanda, Bi. Shakilla K. Mutoni, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine, na Balozi Naimi Azizi Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mkutano uliokuwa ukiendelea. 
Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu kati ya Tanzania na Rwanda kwa Ngazi ya Makatibu Wakuu uliokuwa ukiendelea JNICC jijini Dar es Salaam
Picha pamoja ya washiriki wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu kati ya Tanzania na Rwanda kwa Ngazi ya Makatibu ulifanyika JNICC jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Dotto James akichangia jambo kwenye Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu kati ya Tanzania na Rwanda kwa Ngazi ya Makatibu Wakuu uliofanyika JNICC jijini Dar es Salaam
Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Kudumu kati ya Tanzania na Rwanda kwa Ngazi ya Makatibu ukiendelea JNICC jijini Dar es Salaam

Monday, October 25, 2021

MKUTANO WA 15 WA TUME YA PAMOJA YA USHIRIKIANO KATI YA TANZANIA NA RWANDA KUFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA.


Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Rwanda umeanza kufanyika leo tarehe 25 Oktoba 2021 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Tanzania. Mkutano huu utakaofanyika kwa kipindi cha siku nne kuanzia tarehe 25 hadi 28 Oktoba, 2021 unalenga kujadili mambo mbalimbali muhimu ya ushirikiano ikiwemo Mahusiano ya Kidiplomasia, miundombinu na usafirishaji, Sekta ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo, nishati, utalii na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano sambamba na kuibua maeneo mapya ya ushikiano kwa lengo la kuchagiza maendeleo baina ya Mataifa haya mawali (Tanzania na Rwanda). 

Mkutano huu muhimu kwa ustawi wa ushirikiano na maendeleo baina ya mataifa haya mawili, unafanyika kwa lengo la kufanya ufuatiliaji na tathimini ya utelezaji wa maelekezo yaliyotolewa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mheshimiwa Paul Kagame Rais wa Jamhuri ya Rwanda, wakati wa ziara yake aliyoifanya Nchini Rwanda Agosti 2, 2021. 

Akizungumza kwenye ufunguzi wa Mkutano huo katika ngazi ya Wataalamu, Balozi Naimi S.H. Azizi, Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amebainisha kuwa mkutano huo umetoa fursa hadhimu kwa pande zote mbili kukutana ili kutathmini utekelezaji pia kuweka mipango na mikakati ya pamoja itakayoimarisha ushirikiano kwenye utekelezaji wa vipaumbele vya shughuli za maendeleo katika sekta mbalimbali kwa manufaa ya pande zote mbili. “Natambua dhahiri kuwa Mkutano huu wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano utatuwezesha kufanya tathimini na kubaini hatua tuliyoifikia katika utekezaji wa maagizo yaliyotolewa na Wakuu wetu wa Nchi hizi mbili (Tanzania na Rwanda). Nimatumaini yangu pia, kuwa Mkutano huu utatuwezesha kuweka mikakati na mipango ya pamoja itakayotuwezesha kuongeza kasi ya kutekelezaji katika maeneo ambayo bado hatujafanya vizuri.”Alisema Balozi Naimi S.H. Azizi. 

Balozi Naimi S.H. Azizi aliongeza kusema kuwa ni muhimu wajumbe wa mkutano wajikite katika kujadili masuala muhimu yenye maslahi kwa pande zote mbili ili kukidhi matarajio ya Wakuu wa Nchi hizi mbili, ya kuona Wataalamu katika Serikali wanazoziongoza wanaendelea kuwajibika ipasavyo katika kuwaletea maendeleo wananchi. 

Mkutano huu umejumuisha Viongozi, Watendaji na Maafisa mbalimbali wa Serikali kutoka Tanzania na Rwanda. 
Balozi Naimi S.H. Azizi Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akichangia jambo kwenye Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano katika ngazi ya Wataalam kati ya Tanzania na Rwanda uliokuwa ukiendela katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Balozi Naimi S.H. Azizi Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akizungumza kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda unaofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Bi. Shekila Mutori Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Rwanda akizungumza kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda unaofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Picha ya pamoja ya washiriki wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda unaoendelea jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Mkutano ukiendelea
Kutoka kushoto Balozi wa Rwanda nchini Tanzania Mhe.Maj.Gen.Charles Karamba, Balozi Naimi S.H. Azizi Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Bi. Shekila Mutori Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Rwanda.
Balozi wa Rwanda nchini Tanzania Mhe.Maj.Gen.Charles Karamba, akifuatilia Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda unaofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.

TANZANIA YAUNGA MKONO UN KUMTUMA MJUMBE WAKE ZIMBABWE .. YATOA TAMKO KUUNGA AZIMIO LA SADC KUSITISHA VIKWAZO DHIDI YA ZIMBABWE


 

MAKAMBA AWASILISHA UJUMBE MAALUM WA RAIS SAMIA KWA RAIS WA UMOJA WA FALME ZA KIARABU

Na Mwandishi Wetu,

Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba (Mb), amewasilisha Ujumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Mhe. Khalifa Bin Zayed Al Nahyan.

Mhe. Makamba amewasilisha ujumbe huo Maalum kupitia kwa Waziri wa Nchi anayeshughulikia Mambo ya Nje, Mhe. Sheikh Shakhbout bin Nahyan Al Nahyan, tarehe 24 Oktoba 2021 katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya UAE.

Waziri Makamba yupo nchini Umoja wa Falme za Kiarabu kwa ziara ya kikazi kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika masuala Mafuta na Gesi.

Waziri Makamba ameambatana na Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu, Mhe. Mohamed Mtonga, Kamishina wa Nishati na Gesi kutoka Wizara ya Nishati pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Petroli Nchini (TPDC). 

Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba akiwasilisha Ujumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Mhe. Khalifa Bin Zayed Al Nahyan. Ujumbe huo umepokelewa na Waziri wa Nchi anayeshughulikia Mambo ya Nje, Mhe. Sheikh Shakhbout bin Nahyan Al Nahyan. 


Waziri wa Nchi anayeshughulikia Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa UAE Mhe. Sheikh Shakhbout bin Nahyan Al Nahyan akiuangalia ujumbe wa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Mhe. Khalifa Bin Zayed Al Nahyan aliokabidhiwa na Waziri Makamba kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan


Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba akizungumza na Waziri wa Nchi anayeshughulikia Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa UAE Mhe. Sheikh Shakhbout bin Nahyan Al Nahyan  


Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba katika picha ya pamoja na Waziri wa Nchi anayeshughulikia Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa UAE Mhe. Sheikh Shakhbout bin Nahyan Al Nahyan na Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu, Mhe. Mohamed Mtonga