Saturday, October 30, 2021

TANZANIA UMOJA WA ULAYA ZAKUBALIANA KUIMARISHA UHUSIANO


 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula  na Mkurugenzi mwendeshaji wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia masuala ya Afrika Mhe. Balozi Rita Laranjinha wakibadilishana hati ya pamoja waliyosaini kufuaatia kumalizika kwa majadiliano ya pamoja kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya yaliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 29 Oktoba 2021


    

Wenyeviti wenza wa majadiliano ya pamoja kati ya  Tanzania na Umoja wa Ulaya ambao ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Mhe. Balozi Liberata Mulamula  na Mkurugenzi mwendeshaji wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia masuala ya Afrika Mhe. Balozi Rita Laranjinha wakizungumza kitu baada ya kubadilishana hati ya pamoja waliyosaini kufuaatia kumalizika kwa majadiliano yao  yaliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 29 Oktoba 2021


           
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula  akionesha hati ya makubalino ya pamoja  aliyokabidhiwa na Mkurugenzi mwendeshaji wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia masuala ya Afrika Mhe. Balozi Rita Laranjinha huku Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stagomena Tax (kulia) akishuhudia baada ya kumalizika kwa majadiliano ya pamoja kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya yaliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 29 Oktoba 2021


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula  na Mkurugenzi mwendeshaji wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia masuala ya Afrika Mhe. Balozi Rita Laranjinha wakionesha hati ya makubalino ya pamoja baada ya kumalizika kwa majadiliano ya pamoja kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya yaliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 29 Oktoba 2021

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula  akimkabidhi zawadi  Mkurugenzi mwendeshaji wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia masuala ya Afrika Mhe. Balozi Rita Laranjinha  baada ya kumalizika kwa majadiliano ya pamoja kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya yaliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 29 Oktoba 2021

                        

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula  na Mkurugenzi mwendeshaji wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia masuala ya Afrika Mhe. Balozi Rita Laranjinha  wakionesha zawadi ya picha baada ya kumalizika kwa majadiliano ya pamoja kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya yaliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 29 Oktoba 2021


Na mwandishi wetu, DSM

Tanzania, Umoja wa Ulaya na nchi wanachama wa Jumuiya hiyo zimekubaliana kuendeleza uhusiano baina yao ambao umekuwepo kwa miongo kadhaa ya urafiki, ushirikiano na kwa maslahi ya pande zote.

Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya kukamilika kwa majadiliano ya pamoja kati ya Tanzania , Umoja wa Ulaya na Nchi wanachama wa Umoja huo yaliyofanyika jijini Dar es salaam tarehe  29 Oktoba 2021.

Katika majadiliano hayo Tanzania na nchi wanachaama wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana kuendelea kufanya kazi kwa pamoja katika kukuza demokrasia, haki za msingi na utawala wa sheria na kuunga mkono sera zinazolenga kuleta maendeleo endelevu.

Pande hizo pia zimeelezea umuhimu wa nafasi ya wanawake na vijana katika maendeleo endelevu pamoja na kuwawezesha na kujadiliania juu ya taarifa ya Tanzania ya mwaka ya haki za binadamu itakayowasilishwa katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa hivi karibuni.

Aidha Umoja wa Ulaya na Tanzania umekubaliana juu ya umuhimu wa maendeleo ya sekta binafsi na uwekezaji kama chachu ya ukuzaji wa uchumi na kutoa ajira kwa watu wengi na wamekubaliana kufanya kazi kwa pamoja ili kufanya mazingira ya biashara nchini yaweze kuvutia zaidi wawekezaji na kukuza biashara za nje kwa pande zote mbili. Pande hizo pia zimeelezea utayari wao wa kujadili masuala yanayoihusu Tanzania katika Mkataba wa ubia wa kibiashara kati ya Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kuhusu kuimarisha uhusiano zaidi katika siku za usoni pande hizo zimekubaliana juu ya umuhimu wa mpango wa ujirani, maendeleo na nyenzo ya ushirikiano wa kimataifa kama nyenzo mpya za kupata ufadhili wa Jumuiya ya Ulaya na kusisitizia umuhimu wa Serikali ya Tanzania kusimamia na kutekeleza kikaamilifu miradi yote iliyo chini ya mpango huo

Pande hizo pia zimekubaliana kubadilishana taarifa juu ya mipango yao ya kisiasa na kijeshi  katika jimbo la Cabo Delgado na kujadili juu ya madhara ya kibinadamu na kujadili mipango ya maendeleo katika nchi za Maziwa Makuu na zile za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

Pia wamejadiliana kuhusu janga la ugonjwa wa Covid 19 katika maeneo yao na Umoja wa Ulaya umepongeza mwelekeo mpya wa sera ya afya ya Serikali ya Tanzania hasa katika hatua inazochukua za kutoa taarifa na kuchanja raia wake. Kikao hicho pia kimeeleza kutambua mpango wa Serikali ya Tanzania kutengeneza dawa zake yenyewe ikiwa ni pamoja na chanjo yake.

Kuhusu suala la ulinzi katika ukana wa bahari pande hizo zimejadiliana aina mbalimbali za uhalifu wa majini ambazo zikiwemo uvuvi haramu na kuelezea utayari wao juu ya kuchukua hatua za pamoja katika kutatua tatizo hilo.

Wamekubaliana kukutana na kufanya majadiliano ya pamoja angalau mara moja kwa mwaka ili kujadili masuala yanayowakabili wote kwa pamoja.

Majadiliano hayo ya Pamoja yamefanyika chini ya uenyekiti wenza wa Mkurugenzi mwendeshaji  wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia masuala ya Afrika Balozi Rita Laranjinha na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula na kuhudhuriwa Mawaziri na Makatibu Wakuu kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Majadiliano hayo pia yamehudhuriwa na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Alfredo Fanti na mabalozi kutoka nchi za Ubelgiji, Jamhuri ya Czech, Denmark, Finland, Ufaransa, Ujerumani, Ireland, Italia, Uholanzi, Poland, Hispania na Sweden.

 

Friday, October 29, 2021

UMOJA WA ULAYA WARIDHISHWA NA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI TANZANIA


Mwenyekiti mwenza wa Kikao hicho ambaye pia ni Mkurugenzi Mwendeshaji anayeshughulikia masuala ya Afrika kutoka  Umoja wa Ulaya Balozi Rita Liranjinha akizungumza na waandishi wa habari kuelezea majadiliano ya ushirikiano kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika mashariki na Mwenyekiti mwenza wa Kikao cha  majadiliano ya ushirikiano kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya Mhe. Balozi Liberata Mulamula akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuelezea umuhimu wa kikao hicho

Mkurugenzi Mwendeshaji anayeshughulikia masuala ya Afrika wa  Umoja wa Ulaya Balozi Rita Liranjinha (kushoto) akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kulia) katika picha ya pamoja baada ya kuzungumza na waandishi wa habari kuelezea majadiliano ya ushirikiano kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya yaliyofanyika jijini Dar es Salaam


Mkurugenzi Mwendeshaji anayeshughulikia masuala ya Afrika wa  Umoja wa Ulaya Mhe. Balozi Rita Liranjinha (kushoto) akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Wizara na mabalozi  walioshiriki majadiliano ya pamoja kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya baada ya kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.


Washiriki wa majadiliano ya pamoja kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya yaliyofanyika jijini Dar es Salaam katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mwendeshaji anayeshughulikia masuala ya Afrika wa  Umoja wa Ulaya Balozi Rita Liranjinha na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula


Viongozi walioshiriki majadiliano ya pamoja kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya yaliyofanyika jijini Dar es Salaam katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mwendeshaji anayeshughulikia masuala ya Afrika wa  Umoja wa Ulaya Balozi Rita Liranjinha na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula



 


Na Waandishi wetu, Dar


Umoja wa Ulaya umeoneshwa kuridhishwa na mazingira ya uwekezaji na ufanyaji wa biashara nchini Tanzania na kuahidi kuhamasisha wawekezaji kutoka katika umoja huo kuja kuwekeza na kufanya biashara zaidi.


Akizungumza katika ufunguzi wa majadiliano kuhusu masuala mtambuka na kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Umoja wa Ulaya yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti mwenza wa Kikao hicho ambaye pia ni Mkurugenzi Mwendeshaji anayeshughulikia masuala ya Afrika kutoka  Umoja wa Ulaya Balozi Rita Liranjinha amesema Umoja wa Ulaya Umeridhishwa na mazingira ya biashara na uwekezaji hapa Tanzania na kuahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika Sekta ya biashara na uwekezaji.

Balozi Rita pia amepongeza kitendo cha Tanzania kuzifanyia marekebisho sheria mbalimbali katika harakati za kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara nchini na hivyo kuvutia wafanyabiashara na wawekezaji wengi nchini. 

Kadhalika, Balozi Rita ameipongeza Tanzania kwa kufanya kazi na watanzania wote hasa sekta binafsi kwani huchangia kutoa ajira kwa watu wengi na kuichangia kuinua maendeleo.

“Naipongeza Serikali kwa kusikiliza sauti za wananchi na kuchukua hatua kukabiliana na changammoto zinazowakabili wananchi kwa wakati ambacho amekielezea kuwa ni sawa na kupanda mbegu ya matumaini kwa wanachi,” amesema Balozi Rita.

Ameongeza kuwa Umoja wa Ulaya unaiona Tanzania ni mdau mkubwa wa Tanzania na kwamba umoja huo utaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha maendeleo ya kweli yanapatikana kwa maslahi ya pande zote mbili.   

“Umoja wa Ulaya utaendelea kushirikiana na Tanzania kuboresha mazingira bora ya biashara na uwekezaji ikiwa ni pamoja na  kukabiliana na magonjwa ya mlipuko kama Uviko 19, mabadiliko ya tabia nchi na kuondoa umasikini,” amesema Balozi Rita.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti mwenza wa majadiliano hayo, Balozi Liberata Mulamula (Mb) ameupongeza Umoja wa Ulaya kwa  utayari wake wa kuisaida Tanzania kukabiliana na changamoto mbalimbali ambazo zinaikabili dunia kwa sasa.

Balozi Mulamula amesema Uhusiano wa Tanzania na Umoja wa Ulaya umedumu kwa muda mrefu na kwamba Tanzania itaendelea kushirikiana na Umoja wa Ulaya katika kukuza na kuendeleza ushirikiano huo kwa maslahi ya pande zote mbili hasa katika kukuza na kuendeleza  biashara, uwekezaji, haki za binadamu na mapambano dhidi ya ugonjwa wa UVIKO19.  

Balozi Mulamula ameihakikisha Jumuiya hiyo kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Umoja wa Ulaya katika harakati zake za kupambana na umasikini nchini hata kwa nchi nyingine zinazoizunguka.

Ameongeza kuwa pamoja na changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikijitokeza kama vile ugonjwa wa Uviko 19, Tanzania itaendelea kuchukua tahadhari na kuimarisha sekta ya afya ili kuendelea kupambana na janga hilo.

Waziri Mulamula ameuhakikishia Umoja wa Ulaya kuwa Tanzania itaendelea kuimarisha na kuboresha mazingira ya  biashara na uwekezaji nchini ili kukuza uchumi na hivyo kuleta maendeleo.

Majadiliano hayo yamehudhuriwa na mabalozi mbalimbali kutoka Umoja wa Ulaya ambao ni Balozi wa Umoja wa Ulaya, Ubelgiji, Finland, Sweden, Denmark, Italia, Czech, Ufaransa, Ujerumani, Hispania, Canada, Poland, Ireland na Uholanzi.