|
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata
Mulamula na Mkurugenzi mwendeshaji wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia
masuala ya Afrika Mhe. Balozi Rita Laranjinha wakibadilishana hati ya pamoja
waliyosaini kufuaatia kumalizika kwa majadiliano ya pamoja kati ya Tanzania
na Umoja wa Ulaya yaliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 29 Oktoba 2021
|
|
Wenyeviti wenza wa majadiliano ya pamoja kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya ambao ni Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Mhe. Balozi Liberata
Mulamula na Mkurugenzi mwendeshaji wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia
masuala ya Afrika Mhe. Balozi Rita Laranjinha wakizungumza kitu baada ya kubadilishana hati ya pamoja
waliyosaini kufuaatia kumalizika kwa majadiliano yao yaliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 29 Oktoba 2021 |
|
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata
Mulamula akionesha hati ya makubalino ya pamoja aliyokabidhiwa na Mkurugenzi mwendeshaji wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia
masuala ya Afrika Mhe. Balozi Rita Laranjinha huku Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stagomena Tax (kulia) akishuhudia baada ya kumalizika kwa majadiliano ya pamoja kati ya Tanzania
na Umoja wa Ulaya yaliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 29 Oktoba 2021 |
|
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata
Mulamula na
Mkurugenzi mwendeshaji wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia
masuala ya Afrika Mhe. Balozi Rita Laranjinha wakionesha hati ya makubalino ya pamoja baada
ya kumalizika kwa majadiliano ya pamoja kati ya Tanzania
na Umoja wa Ulaya yaliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 29 Oktoba
2021 |
|
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata
Mulamula akimkabidhi zawadi
Mkurugenzi mwendeshaji wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia
masuala ya Afrika Mhe. Balozi Rita Laranjinha baada
ya kumalizika kwa majadiliano ya pamoja kati ya Tanzania
na Umoja wa Ulaya yaliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 29 Oktoba
2021 |
|
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata
Mulamula na
Mkurugenzi mwendeshaji wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia
masuala ya Afrika Mhe. Balozi Rita Laranjinha wakionesha zawadi ya picha baada
ya kumalizika kwa majadiliano ya pamoja kati ya Tanzania
na Umoja wa Ulaya yaliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 29 Oktoba
2021 |
Na mwandishi wetu, DSM
Tanzania,
Umoja wa Ulaya na nchi wanachama wa Jumuiya hiyo zimekubaliana kuendeleza uhusiano
baina yao ambao umekuwepo kwa miongo kadhaa ya urafiki, ushirikiano na kwa maslahi
ya pande zote.
Makubaliano
hayo yamefikiwa baada ya kukamilika kwa majadiliano ya pamoja kati ya Tanzania
, Umoja wa Ulaya na Nchi wanachama wa Umoja huo yaliyofanyika jijini Dar es
salaam tarehe 29 Oktoba 2021.
Katika majadiliano hayo Tanzania na nchi
wanachaama wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana kuendelea kufanya kazi kwa pamoja
katika kukuza demokrasia, haki za msingi na utawala wa sheria na kuunga mkono
sera zinazolenga kuleta maendeleo endelevu.
Pande
hizo pia zimeelezea umuhimu wa nafasi ya wanawake na vijana katika maendeleo
endelevu pamoja na kuwawezesha na kujadiliania juu ya taarifa ya Tanzania ya
mwaka ya haki za binadamu itakayowasilishwa katika Baraza la Haki za Binadamu
la Umoja wa Mataifa hivi karibuni.
Aidha
Umoja wa Ulaya na Tanzania umekubaliana juu ya umuhimu wa maendeleo ya sekta
binafsi na uwekezaji kama chachu ya ukuzaji wa uchumi na kutoa ajira kwa watu
wengi na wamekubaliana kufanya kazi kwa pamoja ili kufanya mazingira ya biashara
nchini yaweze kuvutia zaidi wawekezaji na kukuza biashara za nje kwa pande zote
mbili. Pande hizo pia zimeelezea utayari wao wa kujadili masuala yanayoihusu
Tanzania katika Mkataba wa ubia wa kibiashara kati ya Umoja wa Ulaya na Jumuiya
ya Afrika Mashariki.
Kuhusu
kuimarisha uhusiano zaidi katika siku za usoni pande hizo zimekubaliana juu ya
umuhimu wa mpango wa ujirani, maendeleo na nyenzo ya ushirikiano wa kimataifa kama
nyenzo mpya za kupata ufadhili wa Jumuiya ya Ulaya na kusisitizia umuhimu wa Serikali
ya Tanzania kusimamia na kutekeleza kikaamilifu miradi yote iliyo chini ya
mpango huo
Pande
hizo pia zimekubaliana kubadilishana taarifa juu ya mipango yao ya kisiasa na
kijeshi katika jimbo la Cabo Delgado na
kujadili juu ya madhara ya kibinadamu na kujadili mipango ya maendeleo katika
nchi za Maziwa Makuu na zile za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika
(SADC).
Pia wamejadiliana kuhusu janga la
ugonjwa wa Covid 19 katika maeneo yao na Umoja wa Ulaya umepongeza mwelekeo
mpya wa sera ya afya ya Serikali ya Tanzania hasa katika hatua inazochukua za
kutoa taarifa na kuchanja raia wake. Kikao hicho pia kimeeleza kutambua mpango
wa Serikali ya Tanzania kutengeneza dawa zake yenyewe ikiwa ni pamoja na chanjo
yake.
Kuhusu suala la ulinzi katika ukana wa bahari
pande hizo zimejadiliana aina mbalimbali za uhalifu wa majini ambazo zikiwemo
uvuvi haramu na kuelezea utayari wao juu ya kuchukua hatua za pamoja katika
kutatua tatizo hilo.
Wamekubaliana
kukutana na kufanya majadiliano ya pamoja angalau mara moja kwa mwaka ili kujadili
masuala yanayowakabili wote kwa pamoja.
Majadiliano
hayo ya Pamoja yamefanyika chini ya uenyekiti wenza wa Mkurugenzi mwendeshaji wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia masuala ya
Afrika Balozi Rita Laranjinha na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula na kuhudhuriwa Mawaziri na Makatibu Wakuu kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar.
Majadiliano
hayo pia yamehudhuriwa na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Alfredo Fanti na
mabalozi kutoka nchi za Ubelgiji, Jamhuri ya Czech, Denmark, Finland, Ufaransa,
Ujerumani, Ireland, Italia, Uholanzi, Poland, Hispania na Sweden.