Monday, November 1, 2021

MKUTANO WA KIMATAAIFA WA MAHAKAMA YA AFRIKA YA WATU NA HAKI ZA BINADAMU WAANZA DSM


 

 Waziri wa Nchi , Katiba, Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman akifungua Mkutano wa Kimataaifa wa Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi  jijini Dar es Salaam


Washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu wakifuatilia ufunguzi wa mkutano huo

Washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu wakifuatilia ufunguzi wa mkutano huo

Washiriki wa Mkutano wa Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Mhe. Haroun Ali Suleiman na Rais wa Mahaka ya Afrika baada ya ufunguzi wa Mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salaam


Mmoja wa viongozi wanaoshiriki katika mkutano huo akizungumza kitu na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu Mhe. Jaji Iman Abood baada y aufunguzi wa mkutano huo jijini Dar es Salaam

Waziri wa Nchi , Katiba, Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman akizungumza na mmoja wa viongozi wanaoshiriki mkutano huo baada ya ufunguzi rasmi.


Na mwandishi wetu, Dsm


Mkutano wa Kimataaifa kujadili utekelezaji wa maamuzi ya Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu, changamoto na matarajio yake umeanza jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo wa siku tatu umefunguliwa na Waziri wa Nchi Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora  wa Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussien Ali Mwinyi.

Akifungua mkutano huo Mhe. Suleiman amezitaka nchi za Afrika kuhakikisha Mahakama hiyo inakamilisha malengo ya kuanzishwa kwake.

"Mahakama ya Afrika ni taasisi yetu sote, tumeiunda sisi wenyewe na kwa maana hiyo naamini kuwa ni kwa maslahi yetu sote Waafrika tunajukumu la kuhakikisha taasisi hii haishindwi kufikia malengo yake" alisema Mhe. Suleiman na kuongeza kuwa   hakuna mtu atakayenufaika iwapo Mahakama hiyo itafeli au kuwa taasisi isiyotekeleza kazi ya kulinda na kukuza haki za binadamu barani Afrika.

Amesema malengo ya Mahakama hiyo yataweza kufikiwa iwapo tu Serikali zote za bara la Afrika zitatelekeza kikamilifu maamuzi ya Mahakama hiyo.

" Niwaambie  kuwa namna moja kuu ambayo Serikali zitawezesha Mahakama hii kufikia malengo yake ni kwa kutekeleza kikamilifu maamuzi yanayotolewa" alisema na kuongeza kuwa kufanya hivyo kutaionesha dunia kuwa nchi za Afrika zinachukua hatua kulinda na kukuza haki za binadamu kwa nguvu zote.

Awali akizungumza katika mkutano huo,  Rais wa Mahakama ya Afrika Mhe. Jaji Iman Abood alisema mkutano huo umelenga kuangalia namna bora ya kuboresha utendaji kazi wa mahakama hiyo na changamoto zinazopitia nchi katika kutekeleza maamuzi yanayotolewa na Mahakama hiyo na hivyo kuja na suluhisho la pamoja ili kuziwezesha nchi zote kutekeleza maamuzi hayo.

Mkutano huo unashirikisha  nchi wanachama wa Umoja wa Afrika na unahudhuriwa  wanasheria waandamizi kutoka katika Serikali za nchi za Afrika kwa lengo la kuangalia utekelezaji wa maamuzi yanayotolewa na Mahakama hiyo kwa nchi wanachama pamoja na changamoto zinazopitia nchi hizo na kutafuta namna ya kukabiliana nazo na matarajio yaliyopo kutokana na kuwepo kwa mahakama Mahakama hiyo.


Saturday, October 30, 2021

WAZIRI MULAMULA ASHIRIKI MAADHIMISHO UHURU WA TAIFA LA UTURUKI NA INDIA.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) ameshiriki hafla ya maadhimisho ya miaka 70 ya Uhuru wa India na miaka 98 ya Uhuru wa Uturuki. Hafla hizo zilizoandaliwa na Ofisi za Ubalozi wa Mataifa hayo hapa nchini zimefanyika kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam.   

Waziri Mulamula kwa nyakati tofauti akizungumza katika maadhimisho hayo amesifu mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Mataifa hayo na Tanzania na ushirikiano katika maeneo mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu, Afya, Kilimo, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, utalii, biashara na uwekezaji. Vilevile alielezea dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi mahiri wa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania wa kuendelea kuimarisha mahusiano mazuri yaliyopo na Mataifa hayo (India na Uturuki). 

“Tunashukuru Serikali ya India kwa msaada wa mradi wa usambazaji wa maji safi na salama katika miji 17 ya Tanzania ikiwemo katika maeneo ya jiji la Dar es Salaam na Chalinze. Vilevile kwa mradi wa upanuzi, ukarabati na uboreshaji wa huduma ya maji Zanzibar. Tanzania inaichukulia India kama moja ya washirika muhimu wa kimkakati kati ya Nchi za Asia” Alisema Waziri Mulamula

Kwa miaka mingi Vyuo Vikuu vingi vya nchini Uturuki vimetia saini Mikataba ya Makubaliano na Vyuo Vikuu vya nchini Tanzania ya kushirikiana katika kubadilishana programu, mafunzo na utafiti. Aidha, zaidi ya wanafunzi 400 wa Kitanzania wanaendelea na masomo yao nchini Uturuki katika fani mbalimbali ikiwemo udaktari, uhandisi na Sayansi. Ushirikiano huu umechangia kwa kiasi kikubwa kuendeleza mahusiano ya watu wa Mataifa haya mawili. 

Mwisho Waziri Mulamula alieleza kuwa Serikali ya Tanzania inaendelea na jitihada za kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini kwa kufanya marekebisho mbalimbali ya kisera na kisheria. Ametoa wito kwa Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka India na Uturuki na Mataifa mengine duniani kuja kuwekeza hapa nchini.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) akihutubia kwenye maadhimisho ya 98 ya Uhuru wa Taifa la Uturuki yaliyofanyika kwenye Ubalozi wa Taifa hilo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (wa pili kushoto) akifuatilia onesho ya sanaa (hayapo pichani) yaliyokuwa yakiendelea kwenye maadhimisho ya 98 ya Uhuru wa Taifa la Uturuki yaliyofanyika kwenye Ubalozi wa Taifa hilo jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Uturuki hapa nchini Mhe. Dr. Mehmet Gulluoglu akihutubia kwenye maadhimisho ya 98 ya Uhuru wa Taifa la Uturuki yaliyofanyika kwenye Ubalozi wa Taifa hilo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) na Balozi wa Uturuki hapa nchini Mhe. Dr. Mehmet Gulluoglu wakiwa na mshindi wa tiketi ya ndege ya Turkish Airlines katika bahati nasibu iliyochezeshwa kwenye maadhimisho ya 98 ya Uhuru wa Taifa la Uturuki yaliyofanyika kwenye Ubalozi wa Taifa hilo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) na Balozi wa Uturuki hapa nchini Mhe. Dr. Mehmet Gulluoglu wakiwa na mshindi wa tiketi ya ndege ya Turkish Airlines katika bahati nasibu iliyochezeshwa kwenye maadhimisho ya 98 ya Uhuru wa Taifa la Uturuki yaliyofanyika kwenye Ubalozi wa Taifa hilo jijini Dar es Salaam.
Hafla ya maadhimisho ya 98 ya Uhuru wa Taifa la Uturuki yaliyofanyika kwenye Ubalozi wa Taifa hilo jijini Dar es Salaam ikiendelea.
Balozi wa Comoron na Kiongozi wa Mabalozi hapa nchini Mhe. Ahamada El Badaoui Mohamed Fakih akihutubia kwenye maadhimisho ya 98 ya Uhuru wa Taifa la Uturuki yaliyofanyika kwenye Ubalozi wa Taifa hilo jijini Dar es Salaam.

BALOZI MULAMULA ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO UBALOZI WA JAMHURI YA KOREA JIJINI DAR ES SALAAM

 

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula alipowasili katika Ofisi za Ubalozi wa Jamhuri ya Korea na kulakiwa na Balozi wa Korea nchini  Mhe. Tae-ick Cho kwa ajili ya kusaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi huo jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha Rais wa zamani wa nchi hiyo Tae-woo ROH aliyefariki dunia tarehe 26 Oktoba 2021
                                                                                 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akisaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Jamhuri ya Korea jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha Rais wa zamani wa nchi hiyo Tae-woo ROH aliyefariki dunia tarehe 26 Oktoba 2021

                                                                                

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akisaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Jamhuri ya Korea jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha Rais wa zamani wa nchi hiyo Tae-woo ROH aliyefariki dunia tarehe 26 Oktoba 2021
                                                                                                                                                                     
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini  Mhe. Tae-ick Cho baada ya kusaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi huo jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha Rais wa zamani wa nchi hiyo Tae-woo ROH aliyefariki dunia tarehe 26 Oktoba 2021  
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Korea baada ya kusaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi huo jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha Rais wa zamani wa nchi hiyo Tae-woo ROH aliyefariki dunia tarehe 26 Oktoba 2021

                                                          

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini  Mhe. Tae-ick Cho baada ya mazungumzo na kusaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi huo jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha Rais wa zamani wa nchi hiyo Tae-woo ROH aliyefariki dunia tarehe 26 Oktoba 2021