Kushoto ni afisa kutoka Ubalozi wa Marekani, Bi. Kristin Mencer akifuatilia mazungumzo. |
Kutoka kulia ni Katibu wa Waziri, Bw. Seif Kamtunda na Afisa Mambo ya Nje Bi. Talha Waziri wakifuatilia mazungumzo. |
Mazungumzo yakiendelea. |
Picha ya Pamoja. |
Kushoto ni afisa kutoka Ubalozi wa Marekani, Bi. Kristin Mencer akifuatilia mazungumzo. |
Kutoka kulia ni Katibu wa Waziri, Bw. Seif Kamtunda na Afisa Mambo ya Nje Bi. Talha Waziri wakifuatilia mazungumzo. |
Mazungumzo yakiendelea. |
Picha ya Pamoja. |
Mazungumzo yakiendelea. |
Picha ya pamoja |
Mhe. Balozi Mulamula akimkabidhi Mhe. Gambo Calenda na Shajara za Wizara. |
Mhe. Waziri akimkabidhi pia Bw. Mulla calenda ya Wizara |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akifurahia jambo alipokuwa akizungumza na Watumishi wa Wizara jijini Dodoma |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Nassor Mbarouk (Mb), akizungumza na watumishi wa Wizara kwenye kikao kilichofanyika jijini Dodoma |
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akizungumza na watumishi wa Wizara kwenye kikao kilichofanyika jijini Dodoma |
Kikao kikiendelea |
Kikao kikiendelea |
Picha ya pamoja Meza Kuu na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki |
Picha ya pamoja Meza Kuu na Wakuu wa Taasisi zilipo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki |
Picha ya pamoja Meza Kuu na baadhi ya Watumishi wa Wizara |
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Mauritius zimesaini Mkataba wa Jumla (General Framework Agreement - GFA)
Mkataba huo umesainiwa na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Mauritius mwenye makazi yake Harare Zimbabwe Mhe. Prof. Emmanuel Mbennah pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kikanda na Biashara za Kimataifa ya nchini Mauritius Mhe. Balozi Haymandoyal Dillum na kushuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kikanda na Biashara za Kimataifa Mhe. Alan Ganoo
Mkataba huo pamoja na mambo mengine utaimarisha uhusiano wa kiuchumi, kisayansi na kiutamaduni. Mkataba huo pia utaanzisha Tume ya Pamoja ya Kudumu baina ya Nchi itakayokuwa ikifuatilia utekelezaji wa masuala mbalimbli kuhusu ushirikiano wa Tanzania na Mauritius. Hafla ya Uwekaji saini ilihudhuriwa pia na Viongozi wa Serikali na Taasisi kutoka Sekta Binafsi.
Aidha, kwa nyakati tofauti Balozi Mbennah alikutana kwa mazungumzo na Waziri mwenye dhamana na masuala ya Biashara Mhe. Soodesh Satkam Callichurn na Waziri mwenye dhamana na masuala ya Viwanda Mhe. Soomilduth Bholah.
Mazungumzo na viongozi hao yalijikita katika utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi ili Tanzania na Mauritius ziweze kunufaika na fursa zilizopo katika Nchi hizo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula katika mazungumzo na Balozi wa Finland nchini Mhe. Riitta Swan leo katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiteta jambo na Balozi wa Finland nchini Mhe. Riitta Swan pamoja na Afisa kutoka Ubalozi wa Finland nchini |
Na Mwandishi wetu, Dar
Tanzania na India zimeahidi kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano katika kuhakikisha maendeleo endelevu kwa maslahi mapana ya pande zote mbili.
Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula wakati akihutubia sherehe za maadhimisho ya 73 ya Jamhuri ya India jana jioni Jijini Dar es Salaam.
Tanzania na India zimedhamiria kufanya kazi kwa karibu katika kutafuta njia bora ya kufungua fursa mpya na kuimarisha fursa mpya za biashara na uwekezaji zilizopo kati ya nchi hizo.
“Kuanza kwa safari za ndege za moja kwa moja kutoka Dar es Salaam hadi Mumbai kwa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) na kufunguliwa kwa soko la parachichi nchini India ni miongoni mwa hatua zilizochukuliwa ili kuimarisha na kukuza uhusiano wetu katika sekta za biashara na uwekuzaji pamoja na utalii kati ya India na Tanzania,” Amesema Balozi Mulamula.
Pamoja na mambo mengine, Balozi Mulamula ameongeza kuwa Tanzania na India kwa sasa zimeanzisha ushirikiano katika usambazaji wa nishati, ujenzi wa miundombinu na Kilimo. Matarajio ya kuimarisha ushirikiano unaoendelea kati ya nchi hizi mbili ni mazuri na yanatia matumaini.
“Uwekezaji wa India pamoja na idadi ya Wahindi wanaotembelea Tanzania kwa madhumuni ya kuwekeza katika sekta za madini, utalii, viwanda, kilimo, usindikaji wa mazao ya kilimo, nishati, usafirishaji, ujenzi, huduma za fedha na maendeleo ya rasilimali watu unaendelea kuongezeka kwa kasi,” amesema Balozi Mulamula.
Kwa upande wake, Balozi wa India nchini, Mhe. Binaya Srikanta Pradhan amesema kuwa Tanzania imekuwa na uhusiano mzuri na India ambapo uhusiano huo umekuwa ni chachu ya maendeleo kwa mataifa yote mawili na umepelekea kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano.
“Ushirikiano na mshikamano uliopo baaina ya mataifa yetu mawili umekuwa chachu ya maendeleo na lengo la ushirikiano wetu yetu ni kukuza uchumi wetu,” amesema Balozi Pradhan
Aidha, Balozi Pradhan amebainisha kuwa Tanzania itaendelea kuwa ya kipekee kwa taifa la India kutokana na mshikamano ambao umepelekea mataifa haya kufanya biashara, uwekezaji, kujenga uwezo, ujenzi wa miundiombinu pamoja na maendeleo ya kiuchumi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akihutubia sherehe za maadhimisho ya 73 ya Jamhuri ya India jana jioni Jijini Dar es Salaam |
Sherehe za maadhimisho ya 73 ya Jamhuri ya India zikiendelea jana jioni Jijini Dar es Salaam |
Balozi Mulamula na baadhi ya Mabalozi wakifuatilia sherehe za maadhimisho ya 73 ya Jamhuri ya India jana jioni Jijini Dar es Salaam |
Sehemu ya Mabalozi wakifuatilia sherehe za maadhimisho ya 73 ya Jamhuri ya India jana jioni Jijini Dar es Salaam |
Sherehe za maadhimisho ya 73 ya Jamhuri ya India jana jioni Jijini Dar es Salaam |
Mabalozi na wageni waalikwa wakifuatilia sherehe za maadhimisho ya 73 ya Jamhuri ya India |
Sehemu ya Mabalozi wakifuatilia sherehe za maadhimisho ya 73 ya Jamhuri ya India |
Tanzania na Morocco zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika nyanja za biashara na uwekezaji, elimu, utalii, uwezeshaji wa kiuchumi kwa wanawake na vijana.
Makubaliano hayo yamefikiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco Bw. Nasser Bourita walipofanya mkutano wa kwa njia ya mtandao. Balozi Mulamula ameshiriki katika mkutano huo akiwa katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
“Tumezungumzia masuala ya kuimarisha uhusiano wetu baina ya Tanzania na Morocco na tumepitia makubaliano yaliyofikiwa wakati wa ziara ya Mfalme wa Morocco alipotembelea Tanzania mwaka 2016 pamoja na kuangalia mikataba mbalimbali iliyotiwa saini wakati wa ziara ya Mfalme wa Morocco ……… laikini pia tumejadili umuhimu wa kuwa na tume ya pamoja ya ushirikiano,” Amesema Balozi Mulamula.
Katika mkutano huo, viongozi hao wamejadili na kukubaliana kuimarisha ushirikiano wa karibu katika sekta za biashara na uwekezaji, utalii, elimu hasa katika kuongeza idadi ya ufadhili wa masomo kwa watanzania kutoka wanafunzi 30 hadi 50.
“Morocco ni nchi inayopata watalii wengi, hivyo tumekubaliana kushirikian kwa karibu zaidi ili kuweza kupata uzoefu ni njia gani wanatumia katika kukuza sekta ya utalii,” ameongeza Balozi Mulamula.
Katika tukio jingine, Balozi Mulamula amekutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Oman nchini Dkt. Salim Saif Al Harbi katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo ya viongozi hao yamelenga kujadilia masuala mbalimbali ya kuendeleza na kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya Serikali ya Tanzania na Oman.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akifuatilia mkutano Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco Bw. Nasser Bourita akimsikiliza Balozi Mulamula (hayupo pichani) katika mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao
BOFYA HAPA KUSIKILIZA HOTUBA YA MHE. WAZIRI MULAMULA KWENYE DIPLOMATIC SHERRY PARTY ILIYOFANYIKA TAREHE 24 JANUARI 2022, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana aliwaalika Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa katika Sherehe za Mwaka Mpya 2022 kwa Mabalozi (Diplomatic Sherry Party) Ikulu – Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine, katika sherehe hizo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alisema Sera Mpya ya Mambo ya Nje itaendelea kuzingatia Diplomasia ya Uchumi na kuakisi maendeleo mapya kama vile uchumi wa bluu, mabadiliko ya tabianchi, uchumi wa kidigitali pamoja kukuza lugha ya Kiswahili kama lugha ya kidiplomasiana kibiashara.
Awali, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula aliwahakikishia Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na Waakilishi wa Mashirika ya Kimataifa kuwa Tanzania chini ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuimarisha uhusiano wake kila wakati.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akitoa hotuba yake wakati wa Sherehe za Mwaka Mpya 2022 kwa Mabalozi (Diplomatic Sherry Party) Ikulu – Dar es Salaam |
Baadhi ya Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa wakiwa katika Sherehe za Mwaka Mpya 2022 kwa Mabalozi (Diplomatic Sherry Party) Ikulu – Dar es Salaam |
Baadhi ya Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa wakiwa katika Sherehe za Mwaka Mpya 2022 kwa Mabalozi (Diplomatic Sherry Party) Ikulu – Dar es Salaam |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi mbalimbali katika Sherehe za Mwaka Mpya 2022 kwa Mabalozi (Diplomatic Sherry Party) |