Tuesday, April 12, 2022

WAZIRI MULAMULA ATETA NA MABALOZI WA UFARANSA, ITALIA NA USWISI

Na Mwandishi wetu, Dar

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) amekutana kwa pamoja na kufanya mazungumzo na mabalozi wa Ufaransa, Italia na Uswisi.

Waziri Mulamula amekutana na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Nabil Hajlaoui, Balozi wa Italia nchini Mhe.  Marco Lombardi pamoja na Balozi wa Uswisi hapa nchini Mhe. Didier Chasot katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili namna ya kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na nchi zao katika kupambana na mabadiliko ya tabia nchi na utunzaji wa mazingira.

Waziri Mulamula amewahakikishia mabalozi hao kuwa Serikali ipo tayari wakati wote kushirikiana na nchi zao katika utunzaji wa mazingira pamoja na mabadiliko ya tabia nchi.

“Serikali ya awamu ya sita imetoa kipaumbele katika utunzaji wa mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi,” amesema Balozi Mulamula.

Nae Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Hajlaoui kwa niaba ya mabalozi wengine, amesema wanafurahishwa na jitihada za Serikali ya Tanzania katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na utunzaji wa mazingira. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Nabil Hajlaoui, Balozi wa Italia nchini Mhe.  Marco Lombardi pamoja na Balozi wa Uswisi hapa nchini Mhe. Didier Chasot katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Nabil Hajlaoui akimueleza jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Balozi wa Uswisi nchini Mhe. Didier Chasot (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Balozi wa Italia nchini Mhe. Marco Lombardi (mwenye suti ya kijivu) akifafanua jambo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula wakati wa mazungumzo yao

Mazungumzo baina ya Waziri Mulalamula na Mabalozi yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam 



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mulamula akiongea na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Nabil Hajlaoui, Balozi wa Italia nchini Mhe.  Marco Lombardi pamoja na Balozi wa Uswisi hapa nchini Mhe. Didier Chasot 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Nabil Hajlaoui, Balozi wa Italia nchini Mhe.  Marco Lombardi pamoja na Balozi wa Uswisi hapa nchini Mhe. Didier Chasot. Wengine ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika Balozi Swahiba Mndeme na Afisa kutoka Wizarani, Bibi Kisa Mwaseba.  



UONGOZI WA WIZARA WAWASISITIZA MABALOZI KUFANYA KAZI KWA BIDII, WELEDI



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara Balozi Joseph Sokoine wakiongea na mabalozi wanne walioapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 10 Aprili 2022, (hawapo pichani) katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Balozi Mindi Kasiga, (wa kwanza kulia) Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa (Multilateral Co-operation) Balozi Macocha Tembele (wa pili kulia), Balozi James Bwana ambaye atakuhudumu katika Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa (Multilateral Co-operation) - (wa tatu kulia) pamoja na Balozi Noel Kaganda ambaye anahudumu katika Chou cha Ulinzi (NDC) wa kwanza kushoto kwa pamoja wakiwasikiliza viongozi wa Wizara (hawapo pichani) katika kikao kilichofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mabalozi wakisikiliza na kufuatilia maelekezo ya Uongozi wa Wizara (hawapo pichani)

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Joseph Sokoine katika picha ya pamoja na Mabalozi mara baada ya kumaliza kikao 

 

Monday, April 11, 2022

TANZANIA, UJERUMANI KUSHIRIKIANA KUBORESHA UTAMADUNI

Na Mwandishi wetu, Dar

Serikali ya Tanzania pamoja na Shirikisho la Ujerumani zimekubaliana kuongeza ushirikiano katika kuboresha Utamaduni na Malikale ili kuendelea kuhifadhi urithi wa historia ya nchi kwa faida ya kizazi kilichopo na kijacho.

Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Shirikisho la Ujerumani Mhe. Katja Keul wakati alipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Balozi Mulamula amesema kuwa Ujerumani imekuwa na msaada mkubwa katika maendeleo ya kijamii, kitamaduni, kielemu na kiuchumi. “Kwa sasa tunaadhimisha miaka 60 ya ushirikiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Ujerumani. ziara ya Mhe. Keul hapa nchini imelenga kuangala namna gani tunaweza kuongeza ushirikiano katika masuala ya utamaduni na malikale ambapo katika kutimiza hilo tayari mkataba wa ushirikiano wa kuendeleza makumbusho yetu ya taifa umesaini jana,” amesema Balozi Mulamula.

Nae Waziri Keul amesema kuwa Ujerumani na Tanzania zinaadhimisha miaka 60 ya ushirikiano na lengo kuu ni kuongeza ushirikiano katika masuala ya utamaduni na malikale kwa maslahi ya pande zote mbili.

“Katika kuhakikisha tunaongeza na kuboresha ushirikiano katika masuala ya utamaduni na malikale, tumesaini mkataba wa ushirikiano kati ya Makumbusho ya Taifa na Mfuko wa Utamaduni wa Ujerumani lengo kwa lengo la kuhakikisha malikale na uhifadhi wa historia zinalindwa na kusaidia jamii kisayansi, kielimu, kiutamaduni na kiuchumi,” amesema Mhe. Keul 

Kwa mujibu wa Sera ya Malikale ya mwaka 2008, malikale hujumuisha rasilimali za urithi wa utamaduni zinazoshikika na zisizoshikika; zinazohamishika, na zisizohamishika, zilizo nchi kavu na majini ambazo zinadhihirisha mabadiliko ya kimaumbile, kifikra, zana, vyombo na mazingira aliyoishi na kutumia binadamu na zenye umri wa miaka mia moja (100). Malikale hizi zinajumuisha zana za mawe na chuma, vyombo vya usafiri, metali, miti na mifupa; visukuku vya binadamu, mimea na wanyama; michoro ya miambani; miji ya kihistoria, magofu ya majenzi.  

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika mazungumzo na Waziri wa Nchi katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Shirikisho la Ujerumani Mhe. Katja Keul wakati katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Nchi katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Shirikisho la Ujerumani Mhe. Katja Keul akimueleza jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Waziri wa Nchi katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Shirikisho la Ujerumani Mhe. Katja Keul yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Waziri wa Nchi katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Shirikisho la Ujerumani Mhe. Katja Keul yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Waziri wa Nchi katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Shirikisho la Ujerumani Mhe. Katja Keul. Wengine pichani ni Balozi wa Ujerumani nchini Mhe. Regina Hess, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Dkt. Abdalla Possi, Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Balozi Swahiba Mndeme pamoja na Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Maafisa walioambatana na Mhe. Keul katika ziara yake hapa nchini.   



Saturday, April 9, 2022

WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA JAMHURI YA SHIRIKISHO LA UJERUMANI AWASILI NCHINI

Waziri wa Mambo ya Nje wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Mhe.Katja Keul, akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb), mara baada ya kuwasili nchini, kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili. Aliyevaa koti jeusi bila barokoa ni Dkt. Abdallah Possi,Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Mhe. Katja Keul, akisikiliza jambo kwa makini wakati wa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) (hayupo pichani)


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa kwenye mazungumzo na mgeni wake ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Mhe. Katja Keul,muda mfupi baada ya kuwasili nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa kwenye mazungumzo na mgeni wake ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Mhe. Katja Keul,muda mfupi baada ya kuwasili nchini.
Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika (DEA) Balozi Swahiba mdeme akifuatiwa na Balozi wa Tanzania Nchini Ujerumani Dkt. Abdallah Possi na mbali kushoto ni Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Balozi Regina Hess

 

Friday, April 8, 2022

BALOZI MULAMULA AKUTANA NA MWAKILISHI WA HESHIMA WA TANZANIA NCHINI CZECH

Na Mwandishi wetu, Dar

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) amekutana kwa mazungumzo na Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Czech Bw. Roman Grolig katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo yao, viongozi hao wamekubaliana kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Jamhuri ya Czech katika sekta za biashara na uwekezaji, kilimo, elimu na teknolojia.

Balozi Mulamula aliwakaribisha wawekezaji kutoka Czech kuwekeza nchini pamoja na kutia mkazo wa kuimarisha zaidi ushirikiano kati ya Tanzania na Czech. 

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Czech, Bw. Grolig amesema ataendelea kuwahamasisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Czech kuja kuwekeza Tanzania kwani ni sehemu salama ya kuwekeza.

“Jamhuri ya Czech imedhamiria kuongeza ushirikiano na Tanzania na katika kutimiza azma hiyo, wafanyabiashara na wawekezaji wameonesha nia ya kuwekeza katika viwanda vya kutengeneza ndege ndogondogo Pamoja na magari makubwa hapa Tanzania,” amesema Bw. Grolig

Pia ameongeza kuwa kwa sasa Czech ipo katika mchakato wa kuanzisha safari za ndege za moja kwa moja hapa nchini Tanzania  ili kuwawezesha wawekezaji na wafanyabiashara kusafiri kwa urahisi kuja Tanzania kutafuta fursa za uwekezaji,” amesema Bw. Grolig.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiongea na Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Czech Bw. Roman Grolig katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Czech Bw. Roman Grolig akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Czech Bw. Roman Grolig yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Czech Bw. Roman Grolig yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Czech Bw. Roman Grolig  

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Czech Bw. Roman Grolig katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Dkt. Abdallah Possi, Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika Balozi Swahiba Mndeme na Afisa mambo ya Nje kutoka Wizarani, Bibi Kisa Mwaseba. Kushoto mwa Bw. Grolig ni maafisa alioambatana nao kutoka Jamhuri ya Czech



Thursday, April 7, 2022

BALOZI MULAMULA AZISIHI NCHI ZA EAC KUISHI KWA AMANI

Na Mwandishi wetu, Dar

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amezisihi nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuishi  kwa amani ili kuepukana na mauaji kama ya kimbari dhidi ya Watutsi yaliyotokea nchini Rwanda 1994.

Waziri Mulamula ametoa wito huo leo jijini Dar es Salaam katika kumbukizi ya miaka 28 ya mauaji ya Kimbari.

Balozi Mulamula ameongeza kuwa Tanzania inaungana na Rwanda kukumbuka tukio hilo baya lililoacha makovu kwa rai wa Rwanda.

"Tunashukuru na tunathamini hatua zilizochukuliwa na Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mhe. Paul Kagame kuijenga nchi na kuponya majeraha na makovu ya mauaji yale, ni tukio baya lilitokea, tunaomba lisijirudie tena katika nchi zetu,” amesema Balozi Mulamula.

Aidha balozi Mulamula ameongeza kuwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zina mikataba inayotuongoza kuzuia mauaji na kuishi kwa amani. 

Kwa upande wake Balozi wa Rwanda nchini Tanzania Mhe. Meja Jenerali Charles Karamba amesema wananchi wa Rwanda wanakumbuka tukio baya la kuuawa kwa ndugu zao lakini wanajivunia hatua zilizochukuliwa na viongozi wao na mafanikio yaliyopo leo nchini humo.

"Mauaji ya Kimbari yalituumiza sana kwa kupoteza ndugu zetu wasio na hatia lakini leo hii tunajivunia hapa tulipofika, kama taifa tumeendelea kujenga uzalendo na umoja,"amesema Balozi Karamba.

Nae Mratibu Mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN), nchini Tanzania, Zlatan Millisic alisema shirika hilo linatoa pole kwa kumbukizi hiyo mbaya katika historia ya Rwanda na kusema leo kumbukizi hiyo imetumika kuelimisha dunia kuwa chuki ni mbaya.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwasilisha hotuba yake katika kumbukizi ya mauaji ya Kimbari, leo Jijini Dar es Salaam

Balozi wa Rwanda nchini Tanzania Mhe. Meja Jenerali Charles Karamba akihutubia Wanyarwanda paomja na wageni mbalimbali waliojitokeza katika kumbukizi ya miaka 28 ya mauaji ya Kimbari

Balozi wa Comoro nchini, Mhe. Ahmed El Badaoui Mohamed Fakih akitoa hotuba yake katika kumbukizi ya miaka 28 ya mauaji ya Kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994

Mratibu Mkazi wa Shughuli za Umoja wa Mataifa (UN) Bw. Zlatan MiliÅ¡ić akitoa salamu za UN katika kumbukimbizi ya miaka 28 ya mauaji ya Kimbari 











Tuesday, April 5, 2022

MKUU WA MAJESHI YA ULINZI ATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI AFRIKA KUSINI

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo amewataka Watumishi wa Serikali wanaopata fursa ya kuiwakilisha nchi nje kuwa wazalendo na kufanya kazi kwa bidii huku wakijua wao ni wawakilishi wa nchi kwenye maeneo waliyopangiwa.


Jenerali Mabeyo ametoa rai hiyo hivi karibuni alipotembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini kwa lengo la kuwasalimia Watumishi wa Ubalozi huo.


Mkuu huyo wa Majeshi amesema kuwa, watumishi wa kada mbalimbali wanaopangiwa kufanya kazi kwenye Balozi za Tanzania au Mashirika ya Kikanda na Kimataifa wanatakiwa kutumia fursa hiyo kuiwakilisha nchi vizuri kwa kufanya kazi kwa bidii na kuendelea kuwa wazalendo kwa nchi yao kwa maslahi mapana ya Taifa.


“Nawapongeza kwa kuendelea kuiwakilisha nchi yetu vizuri hapa Afrika Kusini lakini nawahimiza mchape kazi kwa bidii na kuwa wazalendo kwa nchi yenu wakati wote”, alisisitiza Jenerali Mabeyo.


Kuhusu hali ya nchi, Jenerali Mabeyo amewaeleza Watumishi hao kwamba, hali ya nchi na mipaka yote ni salama na kuwahimiza kuendelea kuiombea nchi na Viongozi wote akiwemo Mhe. Rais ili hali ya amani na utulivu iliyopo iendelee kuwepo.


Kwa upande wake, Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Meja Jenerali Mstaafu Gaudence Milanzi amemshukuru Jenerali Mabeyo kwa kutenga muda wake na kuutembelea Ubalozi huo na kuielezea hatua hiyo kuwa ni heshima kubwa kwake binafsi na Watumishi wote wa Ubalozi.


Kadhalika, alimweleza kuwa hali ya ushirikiano wa Tanzania na Afrika Kusini ni nzuri ambapo nchi hizi zinaendelea kushirikiana kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo biashara, utalii, elimu, uwekezaji na ushirikiano katika kukuza lugha ya kiswahiili. 


Aliongeza kusema moja ya jukumu kubwa la Ubalozi ni kutekeleza Diplomasia ya Uchumi. Hivyo, Ubalozi unaendelea kukamilisha mpango mkakati wa kutekeleza dhana hiyo ili kuiwezesha Tanzania kunufaika na fursa mbalimbali zilizopo nchini humo zikiwemo za biashara, uwekezaji na masoko kwa bidhaa za Tanzania.


Mhe. Jenerali Mabeyo alikuwa nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Dharura wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ambao ulihusisha pia Jamhuri ya Msumbiji na Nchi Zinazochangia Vikosi katika Misheni ya SADC iliyopo Msumbiji (SAMIM) ambao ulifanyika jijini Pretoria kuanzia tarehe 01 hadi 03 Aprili 2022.

Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Mhe. Meja Jenerali Mstaafu Gaudence Milanzi akimpokea Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo alipotembelea Ubalozi huo hivi karibuni. Jenerali Mabeyo alikuwa nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Dharura wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ambao ulihusisha pia Jamhuri ya Msumbiji na Nchi Zinazochangia Vikosi katika Misheni ya SADC iliyopo Msumbiji (SAMIM) ambao ulifanyika jijini Pretoria kuanzia tarehe 01 hadi 03 Aprili 2022. 

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini.

Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Mhe. Meja Jenerali Mstaafu Gaudence Milanzi akizungumza kumkaribisha Jenerali Mabeyo (hayupo pichani) Ubalozini.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Mhe. Jenerali Venance Mabeyo akizungumza na Watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini (hawapo pichani) alipoutembelea Ubalozi huo hivi karibuni. Kushoto ni ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Agnes Kayola. Jenerali Mabeyo na wajumbe wengine kutoka Tanzania walikuwa nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Dharura wa Kamati ya Mawaziri wa SADC
Mhe. Jenerali Mabeyo akizungumza
Mkutano kati ya Jenerali Mabeyo na Watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini ukiendelea
Sehemu ya Watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini wakimsikiliza Jenerali Mabeyo (hayupo pichani) alipowatembelea Ubalozini hapo
Sehemu nyingine ya Watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini
Mhe. Balozi Milanzi akimkabidhi Jenerali Mabeyo zawadi ya saa kama ukumbusho kwa kutembelea Ubalozini hapo
Mhe. Jenerali Mabeyo akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Milanzi
Mhe. Jenerali Mabeyo akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Milanzi na Mhe. Balozi Kayola
Mhe. Jenerali Mabeyo akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini
Mhe. Jenerali Mabeyo akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Tanzania ulioshiriki Mkutano wa Dharura wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC uliofanyika nchini humo hivi karibuni