Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar Dkt. Aboud S. Jumbe akifafanua jambo kwenye ziara ianayoendelea Jamhuri ya Korea. |
Monday, April 25, 2022
WAZIRI MULAMULA ZIARANI NCHINI KOREA
Thursday, April 21, 2022
Wednesday, April 20, 2022
Saturday, April 16, 2022
Friday, April 15, 2022
DIASPORA AWAVUTIA WATAFITI WA MALIGHAFI ZA UJENZI WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
Mazungumzo yakiendelea |
Thursday, April 14, 2022
Balozi Mbega Awataka Wafanyabiashara wa India kuwekeza Tanzania
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa Mbega ametoa wito kwa wafanyabiashara wa nchi hiyo kuja kuwekeza Tanzania kwenye sekta mbalimbali za uwekezaji.
Alitoa wito huo katika kongamano kubwa la biashara
na uwekezaji (Tanzania India Trade Conference) lililofanyika katika jiji la Chennai, India tarehe 11 na 12 Aprili
2022.
Kongamano hilo lililoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Ubalozi wa Tanzania nchini India na Taasisi ya Uchumi na Biashara ya India (Indian Economic Trade Organization) lilitoa fursa kwa taasisi mbalimbali
zinazohusika na masuala ya uwekezaji na biashara ikiwepo Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE),
na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwasilisha mada
kuhusu fursa za uwekezaji zinazopatikana nchini.
Balozi Mbega alisema licha
ya India kuwekeza nchini mtaji wa kiasi cha Dola za Marekani Bilioni 3.7 na
kuifanya nchi hiyo kuwa ya tano kwa uwekezaji, lakini bado nchi hiyo ina fursa kubwa
ya kuongeza uwekezaji wake nchini.
Kongamano hilo lilihudhuriwa na wafanyabiashara na wawekezaji takribani 110 ambapo
waliweza kufahamishwa fursa za biashara kwa bidhaa za mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi na fursa za uwekezaji katika
sekta za Miundombinu, Madini, Ujenzi wa majumba, viwanda vya madawa, mitambo ya
viwandani, nguo, Elimu na Afya.
Kutokana na kongamano hilo,
tayari wawekezaji mbalimbali wa India wameonesha nia ya kuwekeza nchini
Tanzania ambapo kundi la kwanza la wawekezaji kwenye sekta ya ujenzi wa viwanda
vya madawa ya binadamu na vifaa tiba kutoka India, linatarajiwa kutembelea
Tanzania kuanzia tarehe 19 Aprili 2022 ili kukutana na wadau na kuanza taratibu
za kuwekeza Tanzania.
Wafanyabiashara wengine
walioshiriki Kongamano hilo wameonesha nia ya kushiriki maonesho ya 46 ya biashara
ya kimataifa ya Dar es Salaam ambayo yataanza
tarehe 28 Juni hadi 13 Julai 2022. Ushiriki huo utawawezesha kukutana na wafanyabiashara
na kuona bidhaa zinazozalishwa nchini Tanzania.
Kupitia kongamano hilo, wazalishaji
wa bidhaa za Ngozi na korosho wa Tanzania wameunganishwa na wafanyabiashara wa
India ambapo watapata fursa ya kuuza bidhaa hizo katika soko la India.
Sambamba na kongamano hilo, Ubalozi pia ulishiriki
katika hafla ya uzinduzi wa ofisi ya uhamasishaji na uratibu wa biashara na uwekezaji inayojulikana kwa jina la INDIA TANZANIA TRADE COMMISSION (ITTC) iliyopo katika jengo laJJ Diamonds Mart No. 85,
Barabara ya Gopathi Narayanas wani Chetty Chennai katika eneo la Thyagaraya Nagar ambalo ni kitovu cha biashara jijini Chennai. Ofisi hiyo itaongozwa na kusimamiwa na Dkt. J. Shrenik Naharkama Kamishna wabiashara wa
ITTC.
Uwepo wa ITTC utasaidia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa
haraka wa taarifa sahihi za biashara na uwekezaji zilizopo nchini Tanzania, kwa kuwa ITTC itakuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na taasisi
zinazosimamia masuala ya biashara na uwekezaji za nchini Tanzania.
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe Anisa Mbega akifungua Kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na India Jijini Chennai, India. |
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la biashara na uwekezaji kati ya
Tanzania na India wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa kongamano hilo. |
Balozi
wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa Mbega akikata utepe na kuwasha mshumaa kuashiria
uzinduzi rasmi wa ofisi ya uratibu wabiashara na uwekezaji ITTC.
|
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe Anisa Mbega akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa masuala ya biashara na uwekezaji kutoka Tanzania na India katika hafla ya uzinduzi rasmi wa ofisi ya uratibu wabiashara na uwekezaji ITTC |
Wednesday, April 13, 2022
MHESHIMIWA RAIS SAMIA AELEKEA NCHINI MAREKANI KWA ZIARA YA KIKAZI
TANZANIA, UAE ZASAINI MAKUBALIANO KUIMARISHA USHIRIKIANO
Na Mwandishi Wetu, Dar
Serikali ya Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E), zimesaini Makubaliano ya Tume ya Kudumu ya Pamoja katika nyanja za forodha, elimu, kilimo, nishati, mawasiliano, ulinzi na usalama.
Makubaliano hayo yamesainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula na Waziri wa Nchi wa UAE, Shakhbout bin Nahyan Al Nahyan katika Mkutano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja kati ya Tanzania na UAE leo Jijini Dar es Salaam
Akizungumza katika hafla hiyo iliyotanguliwa na kikao cha Makatibu Wakuu, Waziri Mulamula amesema kusainiwa kwa makubaliano hayo ni ishara tosha ya kunaimarika zaidi kwa ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili.
"Kusainiwa kwa makubaliano hayo kunatoa fursa kati ya Serikali ya Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu kuendeleza biashara na uwekezaji ,” amesema Balozi Mulamula
Kwa upande wake Waziri wa nchi wa UAE Mhe. Sheikh Shakhboot Nahyan Al Nahyan amesema ni faraja kwa kwa kusainiwa kwa makubaliano hayo kwani wamesubiri kwa muda, na kilicho bakia ni utekelezaji wa maeneo waliyokubaliana kwa maslahi ya mataifa yote.
“Natumaini yale tuliyozielekeza chemba za biashara za pande zote mbili kuhakikisha kuwa zinashirikiana zaidi katika kuboresha zaidi mazingira ya bishara na uwekezaji kwa maslahi ya pande zote mbili,” amesema Mhe. Al Nahyan
"Baada ya kusainiwa kwa makubaliano haya tumedhamiria kuanza kuongeza maeneo ya ushirikiano baina yetu katika sekta za elimu, nishati, kilimo, biashara na mawasiliano,"amesema Al Nahyan.
Awali, akiwasilisha hotuba yeke, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab amesema kusainiwa kwa makubaliano ya Tume ya Kudumu ya pamoja kati ya Tanzania na UAE ni wazi kuwa ushirikiano baina ya Tanzania na UAE utazidi kuimarika zaidi.
“Pamoja na mambo mengine, kikao cha Makatibu Wakuu tumejadili na kukubaliana kuongeza ushirikiano katika nyanja za biashara na uwekezaji, mawasiliano, usafirishaji pamoja na ulinzi na usalama……kusainiwa kwa makubaliano haya kunaakisi ishara nzuri ya kuendeleza ushirikiano baina yetu,” amesema Balozi Fatma
Naye Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu (UAE) Balozi Mohammed Mtonga amebainisha fursa mbalimbali zinazopatika katika Falme za Kiarabu ikiwa ni pamoja na masoko ya matunda, nyama na korosho.
Mkutano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja kati ya Tanzania na UAE ulifanyika mwaka 2016.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwasilisha hotuba yake katika Mkutano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja kati ya Tanzania na UAE leo Jijini Dar es Salaam |
Waziri wa Nchi wa UAE, Shakhbout bin Nahyan Al Nahyan akiwasilisha hotuba yake katika Mkutano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja kati ya Tanzania na UAE uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akibadilisha mkataba wa makubaliano na Waziri wa Nchi wa UAE, Shakhbout bin Nahyan Al Nahyan mara baaya ya wawili hao kumaliza kusaini mikataba hiyo |
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab akibadilisha mkataba wa makubaliano na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu nchini Mhe. Khalifa Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi mara baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo katika kikao cha ngazi ya Makatibu Wakuu uliofanyika Jijini Dar es Salaam |
Mawaziri, Mabalozi na Makatibu wakuu wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mkutano |
TANZANIA NA MOROCCO KUFUNGUA MILANGO YA USHIRIKIANO KATIKA MASUALA YA DIASPORA
Bi. Tagie Daisy Mwakawago, Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akisalimiana na Mhe. Zakaria El Guomiri Balozi wa Ufalme wa Morocco nchini Tanzania walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam |
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Tagie Daisy Mwakawago akielezea jambo wakati wa mazungumzo na Balozi wa Ufalme wa Morocco nchini Tanzania Mhe. Zakaria El Guomiri yaliyofanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam. |
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Tagie Daisy Mwakawago akisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Balozi wa Ufalme wa Morocco nchini Tanzania Mhe. Zakaria El Guomiri yaliyofanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam. |
Balozi wa Ufalme wa Morocco nchini Tanzania Mhe. Zakaria El Guomir akifafanua jambo wakati wa mazungumzo na Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Tagie Daisy Mwakawago yaliyofanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam. |
Mazungumzo yakiendelea |
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Tagie Daisy Mwakawago (watatu kulia) na Balozi wa Ufalme wa Morocco nchini Tanzania Mhe. Zakaria El Guomir (watatu kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa wa Ubalozi wa Morocco na Kitengo cha Diaspora. |
BALOZI KATTANGA AKUTANA NA WAZIRI WA NCHI WA U.A.E
Na Mwandishi Wetu, Dar
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa nchi Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) Mhe. Sheikh Shakhboot Nahyan Al Nahyan, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Balozi Kattanga amekutana na ugeni huo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Sulluhu Hassan. Viongozi hao pamoja na mambo mengine, wamejadili masuala mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) katika nyanja za biashara na uwekezaji pamoja na Ulinzi na Usalama.
Balozi Kattanga amemhakikishia Waziri huyo kuwa Tanzania inayo mazingira mazuri ya biashara na salama kuwekeza.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Mhe. Sheikh Shakhboot Nahyan Al Nahyan ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano ambao imekuwa ikiutoka kwa Umoja huo wakati wote.
Waziri wa Nchi wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Mhe. Sheikh Shakhboot Nahyan Al Nahyan amewasili nchini leo kuja kushiriki Mkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu kati ya Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga akimsikiliza Waziri wa nchi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) Mhe. Sheikh Shakhboot Nahyan Al Nahyan, wakiwa katika mazungomzo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam |
Waziri wa nchi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) Mhe. Sheikh Shakhboot Nahyan Al Nahyan, akieleza jambo wakati wa mazungumzo baina yake na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Kattanga, Ikulu Jijini Dar es Salaam |
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga akimueleza jambo Waziri wa nchi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) Mhe. Sheikh Shakhboot Nahyan Al Nahyan (hayupo pichani), wakati wa mazungomzo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam |
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga katika picha ya pamoja na Waziri wa nchi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) Mhe. Sheikh Shakhboot Nahyan Al Nahyan na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula mara baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam |
Tuesday, April 12, 2022
WAZIRI MULAMULA ATETA NA MABALOZI WA UFARANSA, ITALIA NA USWISI
Na Mwandishi wetu, Dar
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) amekutana kwa pamoja na kufanya mazungumzo na mabalozi wa Ufaransa, Italia na Uswisi.
Waziri Mulamula amekutana na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Nabil Hajlaoui, Balozi wa Italia nchini Mhe. Marco Lombardi pamoja na Balozi wa Uswisi hapa nchini Mhe. Didier Chasot katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili namna ya kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na nchi zao katika kupambana na mabadiliko ya tabia nchi na utunzaji wa mazingira.
Waziri Mulamula amewahakikishia mabalozi hao kuwa Serikali ipo tayari wakati wote kushirikiana na nchi zao katika utunzaji wa mazingira pamoja na mabadiliko ya tabia nchi.
“Serikali ya awamu ya sita imetoa kipaumbele katika utunzaji wa mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi,” amesema Balozi Mulamula.
Nae Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Hajlaoui kwa niaba ya mabalozi wengine, amesema wanafurahishwa na jitihada za Serikali ya Tanzania katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na utunzaji wa mazingira.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Nabil Hajlaoui, Balozi wa Italia nchini Mhe. Marco Lombardi pamoja na Balozi wa Uswisi hapa nchini Mhe. Didier Chasot katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam |
Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Nabil Hajlaoui akimueleza jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam |
Balozi wa Uswisi nchini Mhe. Didier Chasot (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam |
Balozi wa Italia nchini Mhe. Marco Lombardi (mwenye suti ya kijivu) akifafanua jambo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula wakati wa mazungumzo yao |
Mazungumzo baina ya Waziri Mulalamula na Mabalozi yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mulamula akiongea na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Nabil Hajlaoui, Balozi wa Italia nchini Mhe. Marco Lombardi pamoja na Balozi wa Uswisi hapa nchini Mhe. Didier Chasot |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Nabil Hajlaoui, Balozi wa Italia nchini Mhe. Marco Lombardi pamoja na Balozi wa Uswisi hapa nchini Mhe. Didier Chasot. Wengine ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika Balozi Swahiba Mndeme na Afisa kutoka Wizarani, Bibi Kisa Mwaseba. |
UONGOZI WA WIZARA WAWASISITIZA MABALOZI KUFANYA KAZI KWA BIDII, WELEDI
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara Balozi Joseph Sokoine wakiongea na mabalozi wanne walioapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 10 Aprili 2022, (hawapo pichani) katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam |
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Balozi Mindi Kasiga, (wa kwanza kulia) Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa (Multilateral Co-operation) Balozi Macocha Tembele (wa pili kulia), Balozi James Bwana ambaye atakuhudumu katika Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa (Multilateral Co-operation) - (wa tatu kulia) pamoja na Balozi Noel Kaganda ambaye anahudumu katika Chou cha Ulinzi (NDC) wa kwanza kushoto kwa pamoja wakiwasikiliza viongozi wa Wizara (hawapo pichani) katika kikao kilichofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam |
Mabalozi wakisikiliza na kufuatilia maelekezo ya Uongozi wa Wizara (hawapo pichani) |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Joseph Sokoine katika picha ya pamoja na Mabalozi mara baada ya kumaliza kikao |