Friday, May 6, 2022

WAZIRI MULAMULA ASHIRIKI MKUTANO WA DHARURA WA BARAZA LA MAWAZIRI WA SADC

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akizungumza katika Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa  SADC uliofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 06 Mei, 2022.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Agnes Kayola (kulia ) wakifuatilia  Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa  SADC uliofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 06 Mei, 2022.

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (wa kwanza kulia) akiwa na washiriki kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakati wa  Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa  SADC uliofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 06 Mei, 2022.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (wa pili kulia) na washiriki kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kikanda wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) baada ya kukamilika kwa  Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa  SADC uliofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 06 Mei, 2022.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) ameshiriki Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 06 Mei, 2022.

Akiongelea mkutano huo Mhe. Waziri amesema Mkutano huo umejadili masuala ya madhara yaliyotokana na mafuriko yaliyozikumba baadhi ya nchi wanachama wa jumuiya hiyo na Mkataba Cotnou ambao unaongelea ushirikiano kati ya nchi za Afrika, Pasifiki na Carebean na Jumuiya ya SADC ili kuhakikisha ushirikiano baina ya nchi unaimarika.

Akizungumza katika kikao hicho, Balozi Mulamula alitoa salamu za pole kwa nchi za Afrika Kusini, Msumbiji, Mauritius na Malawi kufuatia mafuriko makubwa yaliyozikumba nchi hizo na kusababisha vifo vya wananchi wake, hasara ya mali na miundombinu katika nchi  hizo.

‘‘Kupitia Mkutano huu nitoe pole nyingi kwa wananchi wa nchi wanachama wenzetu kutokana na mafuriko yaliyotokea katika nchi za Afrika Kusini, Msumbiji, Madagascar na Malawi, mafuriko ambayo yameziletea nchi hizo madhara makubwa kama vile vifo vya wananchi na uharibifu mkubwa wa mali na miundombinu,’’ alisema Balozi Mulamula.

Katika mkutano huo nchi wanachama kwa ujumla wao waliangalia madhara yaliyotokana na mafuriko hayo na namna ambavyo jumuiya hiyo inaweza kuzisaidia nchi zilizoathirika.

Mkutano huo uliokuwa chini ya uenyekiti wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi Mhe. Nansy Tembo uliridhia utoaji wa fedha kutoka katika Mfuko wa Maafa wa Jumuiya ya SADC kwa ajili ya kusaidia nchi hizo zilizoathiriwa na mafuriko hayo.

 

 

TANZANIA YASHIRIKI MAONESHO YA KILIMO YA MACFRUT 2022 ITALIA

Katika jitihada za kutekeleza Diplomasia ya Uchumi kwa vitendo, Tanzania kwa mara ya kwanza imeshiriki katika maonesho ya kimataifa ya kilimo yanayojulikana kama MACFRUT FIERA yanayoendelea mjini Rimini, nchini Italia.

Maonesho hayo yanawakutanisha wazalishaji, wanunuzi na wauzaji wa bidhaa za kilimo cha mbogamboga na matunda, ufugaji wa kuku na mashine za kisasa zinazotumika katika kilimo. 

Akifungua maonesho hayo, Waziri wa Kilimo wa Italia, Mhe. Stefano Patuanelli, alisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika sekta ya kilimo ikiwa ni pamoja na matumizi ya teknolojia ya kisasa katika kilimo ili kuongeza tija katika uzalishaji na usalama wa chakula. 

Ubalozi wa Tanzania nchini Italia kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo umevutia ushiriki wa sekta binafsi katika maonesho hayo ambayo tunda la mwaka huu ni parachichi. 

Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, aliwasihi wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchini humo kuja kuwekeza Tanzania katika sekta ya kilimo na sekta nyinginezo.

“Nawahakikishia kuwa Tanzania imeboresha mazingira ya uwekezaji kwa kupunguza kero zilizokuwa hapo awali na kwamba, Watanzania wapo tayari kuwapokea,” alisema Balozi Kombo. 

Maonesho ya MACFRUT hufanyika kila mwaka. Awamu inayofuata ya maonesho (MACFRUT FIERA 2023) itafanyika mwezi Mei, 2023 katika mji wa Rimini. 

Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na washiriki kutoka Angola waliotembelea banda la Tanzania katika maonesho ya MACFRUT

Maafisa kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Italia wakizungumza na baadhi ya washiriki waliotembelea banda la Tanzania katika maonesho ya a MACFRUT 

Washiriki kutoka Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja naBalozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo kwenye maonesho ya MACFRUT katika mji wa Rimini, Italia

Naibu Waziri Mkuu wa Uganda na mgeni rasmi katika kongamano maalum kwa ajili ya Afrika, Mhe. Rebecca Kadaga (katikati mwenye barakoa) akiungana na viongozi wengine kukata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa maonesho hayo uliofanyika tarehe 4 Mei 2022


Thursday, May 5, 2022

BALOZI SOKOINE ASHIRIKI MKUTANO WA MAKATIBU WAKUU SADC

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine ameshiriki Mkutano wa Kamati ya Kudumu katika ngazi ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) uliofanyika leo kwa njia ya mtandao.

Balozi Sokoine ameshiriki mkutano huo akiwa katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa SADC unaotarajiwa kufanyika kwa njia ya mtandao tarehe 6 Mei 2022. 

Pamoja na masuala mengine, Makatibu Wakuu wamejadili athari za mafuriko yaliyotokea katika Ukanda wa SADC kwa kipindi cha Januari hadi Aprili 2022.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akishiriki Mkutano wa Kamati ya Kudumu katika ngazi ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) uliofanyika leo kwa njia ya mtandao katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akishiriki Mkutano wa Kamati ya Kudumu katika ngazi ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) uliofanyika leo kwa njia ya mtandao katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo  ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Balozi Agnes Kayola.  



BALOZI MUSHY AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO KWA RAIS AUSTRIA

Balozi wa Tanzania nchini Austria, Mhe. Celestine Joseph Mushy, amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Austria, Mhe. Alexander Van der Bellen, leo tarehe 05 Mei 2022

Januari 2022, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan alimteua Balozi Mushy kuwa Balozi wa Tanzania nchini Austria. 

Balozi wa Tanzania nchini Austria, Mhe. Celestine Joseph Mushy akiwasilisha  Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Austria, Mhe. Alexander Van der Bellen

Balozi wa Tanzania nchini Austria, Mhe. Celestine Joseph Mushy akiwasilisha  Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Austria, Mhe. Alexander Van der Bellen

Rais wa Jamhuri ya Austria, Mhe. Alexander Van der Bellen akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Austria, Mhe. Celestine Joseph Mushy 

Rais wa Jamhuri ya Austria, Mhe. Alexander Van der Bellen akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Austria, Mhe. Celestine Joseph Mushy mara baada ya kupokea Hati za Utambulisho za Balozi Mushy



WAZIRI MULAMULA APOKEA NAKALA ZA HATI YA UTAMBULISHO YA BALOZI WA MTEULE WA ETHIOPIA NCHINI

 

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akipokea Nakala ya Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Ethiopia nchini Mhe. Sibru Mamo Kedida alipofika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam  kujitambulisha baada ya kuwasili nchini  

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akionesha Nakala ya Hati za Utambulisho alizopokea kutoka kwa Balozi Mteule wa Ethiopia nchini Mhe. Sibru Mamo Kedida alipofika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam  kujitambulisha baada ya kuwasili  nchini

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiangalia Nakala ya Hati za Utambulisho alizopokea kutoka kwa Balozi Mteule wa Ethiopia nchini Mhe. Sibru Mamo Kedida alipofika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam  kujitambulisha baada ya kuwasili nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Balozi Mteule wa Ethiopia nchini Mhe. Sibru Mamo Kedida alipofika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam  kujitambulisha baada ya kuwasili nchini

Balozi Mteule wa Ethiopia nchini Mhe. Sibru Mamo Kedida akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula alipofika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam  kujitambulisha baada ya kuwasili nchini

Mazungumzo yakiendelea

Mazungumzo yakiendelea

Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiongozwa na Mkuu wa Itifaki nchini Balozi Yusuph Mndolwa (wa kwanza kushoto) ulioambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula  hayupo pichani ukifuatilia mazungumzo kati wa Balozi Mulamula na Balozi Mteule wa Ethiopia nchini alipofika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kuwasilisha nakala ya Hati za Utambulisho

Balozi Mteule wa Ethiopia nchini Mhe. Sibru Mamo Kedida akimkabidhi zawadi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula alipofika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kukabidhi nkala ya Hti za Utambulisho baada ya kuwasili nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (wa pili kulia) akiwa na Balozi Mteule wa Ethiopia nchini Mhe. Sibru Mamo Kedida (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja baada ya kukabidhi Nakala ya Hati za Utambulisho alipofika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam  kujitambulisha baada ya kuwasili nchini. wa kwanza kulia ni Mkuu wa Itifaki nchini Balozi Yusuph Mndolwa na wa kwanza kushoto ni ofisa Ubalozi wa Ethiopiaa nchini Bw. Mulato.




Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) amepokea nakala ya Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Ethiopia nchini Mhe. Shibru Mamo Kedida leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Baada ya kupokea nakala ya hati hizo viongozi hao walipata fursa ya kuzungumza ambapo Balozi Mulamula alimhakikishia Balozi Mteule ushirikiano wa hali ya juu kumuwezesha Balozi huyo kutekeleza majukumu yake ya kibalozi hapa nchini na kuhakikisha uhusiano kati ya Tanzania na Ethiopia unaendelea kuimarika.

‘‘Unaona timu yangu niliyoambatana nayo hapa, nichukue nafasi hii kukuhakikishia kuwa Wizara itakupa ushirikiano wote utakaouhitaji katika kutekeleza majukumu yako, saa 24 milango yetu iko wazi, tunataka uhusiano kati ya nchi zetu uzidi kuimarika,’’ alisema Balozi Mulamula.

Balozi Mulamula amesema Tanzania imefarijika kupata balozi mpya baada ya Balozi wa awali kumaliza muda wake wa uwakilishi, na kuongeza kuwa kitendo hicho ni ishara ya uhusiano mzuri na urafiki uliopo baina ya Tanzania na Ethiopia.

Naye Balozi Mteule wa Ethiopia Mhe. Sibru Mamo Kedida amemshukuru Waziri Mulamula  kwa jinsi alivyompokea na kuelezea uhusiano kati ya Tanzania na Ethiopia ulivo mzuri na kuahidi kuwa atahakikisha uhusiano huo unazidi kukua na kuimarika.

“Ethiopia na Tanzania zimekuwa katika uhusiano mzuri sana  kidiplomasia, nchi zzetu zimekuwa na lengo moja, nitahakikisha uhusiano kati ya nchi hizi unaimarika na hata kufikia nchi hizi Tanzania na Ethiopia zinashirikiana kufanya biashara na uwekezaji kwa maslahi ya pande mbili,” amesema Mhe. Balozi Kedida