Sunday, May 22, 2022

SEKRETARIETI YA AfCFTA YATOA ELIMU KUHUSU MKATABA WA AfCFTA


Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Omar Said Shabaan akifungua Warsha ya pamoja ya Wabunge na Wajumbe wa Baraza Wawakilishi ili kuwa na uelewa wa pamoja na kutekeleza kwa ufanisi Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) iliyofanyika Zanzibar.   

Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Exaud Kigahe akizungumza katika  Warsha ya pamoja ya Wabunge na Wajumbe wa Baraza Wawakilishi ili kuwa na uelewa wa pamoja na kuutekeleza kwa ufanisi Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) iliyofayika Zanzibar.


Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Omar Said Shabaan (katikati) katka meza kuu wakati wa Warsha ya pamoja ya Wabunge na Wajumbe wa Baraza Wawakilishi kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) iliyofanyika Zanzibar.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Biashara na Utalii katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Yussuf Hassan Iddi (katikati) akiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt. Hashir Abdallah (kulia)  Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Dkt. Aboud S. Jumbe (kushoto) wakifuatilia ufunguzi wa  Warsha ya pamoja ya Wabunge na Wajumbe wa Baraza Wawakilishi kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) iliyofanyika Zanzibar.
Washiriki wa Warsha ya pamoja ya Wabunge na Wajumbe wa Baraza Wawakilishi wakifuatilia ufunguzi wa  warsha kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) iliyofanyika Zanzibar.
Washiriki wa Warsha ya pamoja ya Wabunge na Wajumbe wa Baraza Wawakilishi wakifuatilia ufunguzi wa  warsha kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) iliyofanyika Zanzibar.

Washiriki wa Warsha ya pamoja ya Wabunge na Wajumbe wa Baraza Wawakilishi wakifuatilia ufunguzi wa  warsha kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) iliyofanyika Zanzibar.
Washiriki wa Warsha ya pamoja ya Wabunge na Wajumbe wa Baraza Wawakilishi wakifuatilia ufunguzi wa  warsha kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) iliyofanyika Zanzibar.
Baadhi ya Washiriki wa Warsha ya pamoja ya Wabunge na Wajumbe wa Baraza Wawakilishi katika icha ya pamoja na meza kuu baada ya ufunguzi wa  warsha kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) iliyofanyika Zanzibar.

Baadhi ya Washiriki wa Warsha ya pamoja ya Wabunge na Wajumbe wa Baraza Wawakilishi katika icha ya pamoja na meza kuu baada ya ufunguzi wa  warsha kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) iliyofanyika Zanzibar.

 

Wajumbe wa Sekretarieti ya AfCFTA kutoka Accra, Ghana  katika picha ya pamoja na meza kuu baada ya ufunguzi wa  warsha kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) iliyofanyika Zanzibar.

 

 

Sekretarieti ya Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) limeendesha Warsha ya kujenga uelewa wa pamoja kuhusu Mkataba huo kwa Wabunge na Wajumbe wa Baraza Wawakilishi ili kuwa na uelewa wa pamoja na kuutekeleza kwa ufanisi.

Akifungua warsha hiyo mjini Zanzibar, Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Omar Said Shabaan amesema uelewa wa pamoja kuhusu mkataba huo ni  muhimu kwakuwa utaiwezesha nchi kuutekeleza kwa vitendo na hivyo kunufaika na malengo ya kuanzishwa kwake.

"Kutekeleza mkataba huu lazima kuwe na uelewa wa pamoja, hii itawezesha nchi kujipanga na kwenda pamoja kuutekeleza na hivyo kunufaisha nchi kwa ujumla wake," alisema mhe. Omar

Amesema uelewa wa pamoja wa Mkataba huo wa AfCFTA kutawezesha nchi kupata tija iliyokusudiwa wakati nchi ilipoamua kuuridhia na kusaini na hivyo kuwa miongoni mwa watekelezaji wake.

Amesema Serikali zote mbilii za Muungano na ile ya Mapinduzi Zanzibar zimeufanyia tathmini Mkataba huo na kuja na mkakati maalum wa kusaidia utekelezaji wake

Amezitaka taasisi za uratibu wa mkataba huo kuendeleza juhudi za kuwezesha utekelezaji wa Mkataba huo ili kufahamu na kuzikamata fursa zinazopatikana katika soko la Mkataba huo ili kuutekeleza kwa ufanisi na hivyo kunufaika nao.

Amesema kama nchi haina budi kuangalia fursa za soko la AfCFTA ambalo litakuwa mbadala wa masoko mengine ambayo yana ukomo kutegemeana na nchi inavyokua kiuchumi.

Amesema kwa ukubwa wa soko la AfCFTA unaweza kuleta changamoto lna kueleza kuwa Serikali zimejipanga kukabiliana na changamoto za biashara kwa kuboresha mazingira ya kufanya biashara,  kuvutia wawekezaji na kuwafaanya wazalishaji wake wawe na uwezo wa kuzalisha bidhaa zenye viwango ili kufikia mahitaji ya bidhaa katika soko hilo la AfCFTA.

Amesisitiza kuwa utekelezaji wa Mkataba wa AfCFTA utapelekea ukuaji wa biashara, uwekezaji na uzalishaji wa bidhaa bora kwa nchi na hivyo kama nchi lazima itilie mkazo ili kunufaika na soko hilo.

Warsha hiyo inayoendeshwa na Sekretariati ya AfCFTA yenye makao yake makuu mjini Accra ,Ghana ililenga kutoa elimu na mahitaji ya Mkataba wa AfCFTA ambao Tanzania kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliuridhia na kuusaini mwezi Septemba 2021.

Tanzania iliwasilisha Hati ya kuuridhia Mkataba huo kwa Kamisheni ya Afrika jijini Addis Ababa, Ethiopia mwezi Februari ,2022 na hivyo kuwa miongoni mwa mataifa yanayotekeleza mkataba huo.

Mkataba wa AfCFTA ulianzishwa na Wakuu wa Nchi na Serikali za Umoja wa Afrika walipokutana katika kikao kilichofanyika jijiini  Kigali,  Rwanda  mwaka 2018.

 

Saturday, May 21, 2022

WAZIRI MULAMULA AFANYA ZIARA KATIKA MAHAKAMA YA KIMATAIFA YA KESI MASALIA ZA MAUAJI YA KIMBARI (IRMCT)

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula amefanya ziara ya kikazi katika Mahakama ya Kimataifa ya Kesi Masalia za Mauaji ya Kimbari (IRMCT) tarehe 21 Mei 2022 katika eneo la Lakilaki, jijini Arusha.

Pamoja na mambo mengine dhumuni la ziara hiyo lilikuwa kukutana na Uongozi wa IRMCT na kujadili utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya kimsingi unaofanywa na taasisi hiyo sambamba na yale ya kimahakama.

Waziri Mulamula alitumia nafasi hiyo kueleza kuwa Tanzania inathamini imani inayotolewa na mashirika ya kimataifa pamoja na kikanda ya kuifanya kuwa mwenyeji wa mashirika hayo na kutoa nafasi za ajira kwa Watanzania.

‘’ Serikali inafuatilia kwa karibu utendaji kazi wa Mahakama hii, hivyo ni vema mkatekeleza kwa tija malengo mahsusi ya kuanzishwa kwake,” alisema Balozi Mulamula.

Pia akasisitiza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ipo tayari kutoa ushirikiano wa kiutendaji wakati wowote itakapohitajika ili kuiwezesha Mahakama kutekeleza majukumu yake ya msingi ikiwemo kukamilisha taratibu za kesi zilizosalia na lile la kuwa kituo cha kumbukumbu kwa kesi hizo linatekelezwa kwa ufanisi.

Naye Msajili wa Mahakama hiyo Bw. Abubaccar Tambadou amemshukuru Mheshimiwa Waziri Mulamula kwa kuthamini Mahakama hiyo na kutenga muda wake kujadili masuala mbalimbali ya kiutendaji.

Pia akaeleza kuwa kikao hicho kimewezesha kupatikana kwa ufumbuzi wa papo kwa papo katika baadhi ya mambo na kuleta uelewa wa pamoja kati ya uongozi wa Mahakama na Serikali mwenyeji juu ya masuala ya kiutendaji wa taasisi hiyo.

Naye Jaji wa Mahakama hiyo Mheshimiwa William Sekule alifafanua kwa kina juu ya utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya kimahakama na pia akaeleza kuwa kufanikiwa kwa Mahakama hiyo kunahitaji msaada kutoka kwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na nchi mwenyeji katika kutetea maslahi mbalimbali kwa ajili ya kuwezesha uendeshaji wa shughuli za taasisi.

‘’Naipongeza Tanzania kwa kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kupigania upatikanaji wa bajeti ya uendeshaji wa Mahakama, hivyo ni vema tukatambua thamani ya mahakama hii kuendelea kuwepo nchini na kukamilisha majukumu yake,” alisema Jaji Sekule.

Tangu Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa lipitishe Azimio Nambari 1966 mwaka 2010 la kuanzisha Mahakama hiyo nchini, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilisimamia hatua mbalimbali za awali ili kuhakikisha ujenzi wa Mahakama hii unakamilika hususan upatikanaji wa eneo la ujenzi, uwepo wa huduma ya umeme, barabara na maji katika eneo la Lakilaki Jijini Arusha.

 ================================================


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kulia) akifafanua jambo wakati wa kikao na Uongozi wa Mahakama ya Kimataifa ya  Kesi Masalia za Mauaji ya Kimbari  kilichofanyika tarehe 21 Mei 2022 katika eneo la Lakilaki, jijini Arusha. Pembeni ya Mhe. Waziri ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Caroline Chipeta.

Kutoka kushoto ni Msajili wa Mahakama ya Kimataifa ya Kesi Masalia za Mauaji ya Kimbari (IRMCT) Bw. Abubaccar Tambadou na Jaji wa Mahakama hiyo Mheshimiwa William Sekule akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mahakama kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula.

Ujumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ulioambatana na Mhe. Waziri katika ziara hiyo ukifatilia majadiliano katika kikao hicho. Kushoto ni Msaidizi wa Mhe. Waziri, Bw. Seif Kamtunda na Kulia ni Afisa Mambo ya Nje, Bi. Laila Kagombora.

Uongozi wa Mahakama ya Kimataifa ya Kesi Masalia za Mauaji ya Kimbari (IRMCT) ukifatilia majadiliano ya kikao.

Kikao kikiendelea

Picha ya Pamoja Waziri Mulamula na Msajili wa Mahakama Bw. Tambadou na Mhe. Jaji Sekule.

Picha ya pamoja ujumbe wa Wizara ya Mambo ya Nje  na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ukiongozwa na Mhe. Waziri Mulamula na Uongozi wa IRMCT.

Waziri Mulamula akipata maelezo katika chumba cha Mahakama na taratibu nyingine za uendeshaji wa kesi katika mahakama hiyo.

Muonekano wa chumba cha Mahakama.

Waziri Mulamula akipata maelezo kutoka kwa afisa anayesimamia Makavazi (Archieve) ya mahakama hiyo.

Waziri Mulamula akipata ufafanuzi juu ya uendeshaji na usimamizi wa Makataba inayosimamiwa IRMCT ambapo alielezwa kuwa hadi sasa Makataba hiyo inashirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Makumila kutoka Tanzania na Chuo  Kikuu cha Makelele kutoka Uganda.

Picha ya pamoja Mheshimiwa Waziri na Watanzania wanaofanya kazi IRMCT


TANZANIA YAFUNGUA KONSELI KUU GUANGZHOU, CHINA


Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 20 Mei 2022 imefungua Konseli Kuu mjini Guangzhou China. Uwepo wa Konseli Kuu katika mji huo kuta iwezesha Tanzania kutumia vyema fursa za biashara na uchumi na kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa Watanzania wanaoishi na kufanya shughuli mbalimbali katika mji huo. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akihutubia kwenye hafla ya ufunguzi wa Konseli Kuu hiyo kwa njia ya mtandao alisema kufungua ubalozi huo sambamba na kuendeleza uhusiano mzuri wa kidiplomasia na biashara katika ya Tanzania na China , Konseli Kuu hiyo ni muhimu katika kuhudumia Jumuiya ya Watanzania ambapo ndio idadi kubwa zaidi kuliko miji yote ya China.

"Guangzhou imekuwa mshirika mkubwa wa kibiashara kati ya China na Tanzania ambapo kwa mwaka 2020/2021 kupitia mji huu biashara kati ya Tanzania na China ilifukia shilingi dola za Marekani 6.74. Hivyo ni matumaini yetu kwa kuwa na Konseli Kuu hapa biashara kati ya Tanzania na China itakuwa maradufu” alisema Mhe. Balozi Liberata Mulamula

Konseli Mkuu wa Konseli Kuu ya Tanzania mjini Guangzhou Bw. Khatibu Makenga, akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi alisema Konseli hiyo italeta msukumo mpya wa biashara, uwekezaji na mahusiano ya kiutamaduni baina ya Tanzania na China.

Kwa upande wake Bw. Luo Jun, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Mambo ya Nje ya jimbo la Guangdong, akizungumza katika halfa ya ufunguzi alisema mji wa Guanzhou licha ya kuwa ni lango kubwa la biashara kati ya China na Mataifa mengine duniani una historia ya kipekee kwenye historia ya ushirikiano baina ya Tanzania na China. Aliongeza kusema Guangzhou ni kielelezo cha ushirikiano na urafiki baina ya Tanzania na China. 
Konseli Mkuu wa Konseli Kuu ya Tanzania mjini Guangzhou Bw. Khatibu Makenga na Viongozi wa Mamlaka mbalimbali kutoka mji wa Guangzhou na Guangdong wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa Konseli Kuu ya Guangzhou, China.
Hafla ufunguzi ikiendelea


Konseli Mkuu wa Konseli Kuu ya Tanzania mjini Guangzhou Bw. Khatibu Makenga akihutubia wakati wa hafla ya ufunguzi wa Konseli Kukuu hiyo