Thursday, November 17, 2022

WAZIRI SORAGHA: ZANZIBAR NI ENEO BORA KWA UWEKEZAJI

    

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uvuvi na Uchumi wa Buluu, Dkt. Aboud Suleiman Jumbe akitoa neno kuhusu uwekezaji katika sekta ya uchumi wa buluu Zanzibar
Balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Korea, Mhe. Togolany Mavura akichangia jambo kuhusu mada ya uwekezaji katika sekta ya uchumi wa buluu

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Mhe. Abdallah Possi akichangia mada kuhusu uwekezaji katka uchumi wa buluu  Zanzibar.

Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Humphrey Polepole akitoa neno kuhusu uwekezaji katika uchumi wa buluu Zanzibar.



 



WIZARA KUSHIRIKIANA NA SMZ KUTEKELEZA AGENDA ZA KIKANDA, KIMATAIFA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax amesema Wizara anayoiongoza itaendelea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuhakikisha agenda mbalimbali za kikanda na kimataifa zinawanufaisha wananchi wa Tanzania Bara na Zanzibar.

Mhe. Dkt. Tax ametoa kauli hiyo leo tarehe 17 Novemba, 2022 wakati alipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -Ikulu, Mhe. Jamal Kassim Ali, Ikulu Zanzibar.

Mhe. Waziri Tax amemtembelea Mhe. Jamal, Ofisini kwake Ikulu Zanzibar kwa lengo la kumsalimia na kubadilishana naye mawazo ya namna ya kuimarisha ushirkikiano kati ya Wizara na Ofisi yake.

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Tax amemwahidi ushirikiano Waziri Jamal na kumshukuru kwa kupata fursa hiyo muhimu ambayo inalenga kuendelea kuboresha utekelezaji wa majukumu ya Wizara hususan katika masuala ya kikanda na kimataifa kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Waziri Tax ameongeza kuwa Wizara anayoiongoza inaendelea kutekeleza kikamilifu maelekezo yote yaliyotolewa kwao na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kuhusu kuzipa kipaumbele hoja za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye majukwa ya kikanda na kimataifa pamoja na kuwashirikisha Diaspora katika kuchangia maendeleo ya Taifa.

“Mhe. Waziri leo nimekuja kwa ajili ya kukusalimia kwa vile nipo hapa Zanzibar na Mabalozi wa Tanzania wote tukiendelea na Mkutano. Nakuahidi kufanya kazi kwa pamoja kwa nguvu mpya ili kuhakikisha hoja zote za kipaumbele za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinakuwa na tija katika majukwaa ya kikanda na kimataifa kwa manufaa ya pande zote na bila kuwasahau Diaspora wetu” amesema Dkt. Tax.

Kwa upande wake, Mhe. Jamal ambaye Ofisi yake pamoja na mambo mengine, ina jukumu la kusimamia masuala ya kikanda na kimataifa amemshukuru Dkt. Tax kwa kutenga muda na kumtembelea na kwa namna ya pekee alishukuru ushirikiano anaoupata kutoka Ofisi ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ya Zanzibar.

Pia alieleza kuwa, ipo haja ya kuimarisha zaidi ushirikiano ulipo ili kupeleka maazimio ya pamoja kwenye majukwaa ya kikanda na kimataifa na kwamba Ofisi yake ipo tayari kutoa ushirikiano wote utakaohitajika.

Kuhusu Diaspora alisema tayari Ofisi yake imeandaa Sheria na sasa wanaendelea na zoezi la kuwatambua. Hivyo aliomba kuendeleza ushirikiano wa pamoja ili kuendelea kuwatambua, kuwasimamia na kuwaratibu ili kuwawezesha kuchangia kikamilifu maendeleo ya Taifa.

“Naomba tuendelee na ushirikiano huu ili tuweze kuwaunganisha pamoja Diaspora wetu pamoja na kuwatambua kwa usahihi ili kuweza kuwasimamia na kuwaratibu katika kuchangia maendeleo ya taifa letu,” amesema Mhe. Jamal

Dkt. Tax yupo Zanzibar kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Sita wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mabalozi wa Tanzania unaofanyika Kisiwani humo kuanzia tarehe 14 hadi 21 Novemba 2022. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -Ikulu, Mhe. Jamal Kassim Ali akimpokea Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax wakati  alipomtembelea Ofisini kwake Ikulu Zanzibar 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -Ikulu, Mhe. Jamal Kassim Ali akieleza jambo wakati wa kikao chake na mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax Ofisini kwake Ikulu Zanzibar 

Kikao baina ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -Ikulu, Mhe. Jamal Kassim Ali na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax kikiendelea 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akieleza jambo wakati wa kikao chake na mwenyeji wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Ikulu, Mhe. Jamal Kassim Ali, Ikulu - Zanzibar 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akieleza jambo wakati wa kikao chake na mwenyeji wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Ikulu - Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Ikulu - Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali akimsindikiza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax baada ya kumaliza kikao chao Ikulu, Zanzibar

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Ikulu - Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali akiagana na mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax baada ya kumaliza kikao chao Ikulu, Zanzibar



DKT. TAX AIPONGEZA SERIKALI YA UAE KWA KUFUNGUA UBALOZI MDOGO ZANZIBAR

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena  Tax amepongeza uamuzi wa Serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) wa kufungua Konseli Kuu (Ubalozi Mdogo) Visiwani Zanzibar na kutoa wito kwa Wananchi kutumia uwepo wa Konseli hiyo kuboresha ushirikiano katika sekta mbalimbali zikiwemo biashara, utalii na masoko kwa bidhaa za Tanzania.

 

Mhe. Dkt. Tax ametoa pongezi hizo hivi karibuni wakati akipokea Hati za Utambulisho za Konseli Mkuu wa UAE, Zanzibar   Mhe. Balozi Saleh Ahmed Alhemeiri katika hafla fupi iliyofanyika katika Ofisi za Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Zanzibar.

 

Amesema hatua hiyo ni muhimu sana katika kuimarisha ushirikiano wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na UAE kwani  sasa fursa nyingi zilizopo Zanzibar ikiwemo utalii, uchumi wa buluu na biashara vitashamiri zaidi na kukua.



Ameongeza kusema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali  ya Awamu ya Nane ya Zanzibar chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  zimeendelea kuimarisha ushirikiano na nchi mbalimbali pamoja na kutafuta fursa za biashara, utalii, uwekezaji  na masoko kwa bidhaa za Tanzania ili kuiwainua kiuchumi watanzania wote.

 

Ameongeza kwamba kufunguliwa kwa Konseli Kuu hiyo ni matokeo ya ziara mbalimbali za viongozi hao nchini humo ikiwemo ile ya Mhe. Rais Samia aliyoifanya nchini UAE mwezi Februari 2022 wakati wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dubai Expo 2020.

 

Pia amesema wakati wa ziara hiyo, pamoja na mambo mengine, Mikataba na Hati za Makubaliano mbalimbali  zilisainiwa kwa ajili ya kuwezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini.

 

"Napongeza kwa dhati uamuzi wa Serikali ya UAE wa kufungua Konseli Kuu au Ubalozi mdogo hapa Zanzibar. Ni imani yangu kuwa, uwepo wa Konseli Kuu hii utasaidia kuharakisha utekelezaji wa masuala mbalimbali ya ushirikiano ambayo tayari yamekubalika kwa manufaa ya pande hizi mbili" alisema Dkt. Tax.

 

Akitaja maeneo ya kipaumbele ya ushirikiano kwa upande wa Zanzibar, Mhe. Waziri Tax amesema ni pamoja na Uchumi wa Buluu hususan katika uvuvi wa bahari kuu, utalii, biashara na uwekezaji kwa ujumla.



Pia Mhe. Dkt Tax amemhakikishia ushirikiano Balozi huyo na kwamba ana imani kuwa kupitia yeye masuala mengi yatakamilika.

 

" Tutashirikiana na wewe kuhakikisha makubaliano yaliyofikiwa kati ya nchi hizi mbili hususan kwa upande wa Zanzibar yanatekelezwa na kama ulivyosema awali kwa kiasi fulani Zanzibar inafanana na Dubai, basi tujielekeze kuigeuza  Zanzibar  kuwa  Dubai ya Afrika" alisema Dkt. Tax.

 

Kwa upande wake, Mhe.  Alhemeiri amesema amefarijika kuwepo Zanzibar na kwamba yupo tayari kushirikiana na Serikali hiyo katika kukuza biashara, kilimo, elimu, na uchumi wa buluu kwani zipo fursa lukuki katika Kisiwa hiki zinazohitaji kuendelezwa.

 

"Nia yetu ni kushirikiana na Serikali kukiendeleza Kisiwa kizuri cha  Zanzibar. Nimeona zipo fursa nyingi za kufanyia kazi. Nitajikita zaidi kwenye masuala ya utalii, biashara, elimu, uchumi wa buluu na usafirishaji kwa kuzishawishi mamlaka za UAE kuongeza safari za moja kwa moja za Mashirika ya Ndege ya UAE kuja Zanzibar ili kukuza utalii, alisema Mhe. Alhemeiri. 



Mhe. Dkt. Tax yupo mjini Zanzibar kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Sita wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mabalozi wa Tanzania unaofanyika Kisiwanio humo kuanzia tarehe 14 hadi 21 Novemba 2022. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akipokea hati za utambulisho kutoka kwa Konseli Mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Visiwani Zanzibar, Mhe. Balozi Saleh Ahmed Alhemeiri. Hafla hiyo fupi imefanyika hivi karibuni katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Zanzibar. Mhe. Dkt. Tax yupo mjini Zanzibar kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Sita wa Mabalozi wa Tanzania unaoendelea mjini hapo kuanzia tarehe 14 hadi 21 Novemba 2022

Mhe. Dkt. Tax akizungumza na Mhe. Alhemeiri mara baada ya kupokea hati za utambulisho. Katika mazungumzo hayo, Mhe. Dkt. Tax alipongeza uamuzi wa Serikali wa kufungua Konseli Kuu Zanzibar na kutoa wito kwa watanzania kutumia uwepo wa Ofisi hiyo kuimarisha ushirikiano

Mhe. Dkt. Tax akiagana na Mhe. Alhemeiri mara baada ya kumaliza mazungumzo.

Mhe. Dkt. Tax na Mhe. Alhemeiri wakiwa kati picha ya pamoja
Mhe. Dkt. Tax na Mhe. Alhemeiri wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Hemed Mgaza (kulia) na Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mariam Mrisho (kushoto)

Picha ya pamoja







 

Wednesday, November 16, 2022

MABALOZI WAAINISHA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI





Sehemu ya waheshimiwa mabalozi wakifuatilia majadiliano katika Mkutano wa Mheshimiwa Rais na Mabalozi unaofanyika tarehe 14 – 21 Novemba, 2022 Zanzibar.

Sehemu nyingine ya Waheshimiwa mabalozi wakifuatilia majadiliano katika Mkutano wa Mheshimiwa Rais na Mabalozi unaofanyika tarehe 14 – 21 Novemba, 2022 Zanzibar.

Viongozi Wakuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na mabalozi wakifuatilia kikao katika Mkutano wa Mheshimiwa Rais na Mabalozi unaondelea Zanzibar.

Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ukiongozwa na Waziri Mhe. Dkt. Stergomena Tax, Naibu Waziri Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, Katibu Mkuu Balozi Joseph Sokoine, Naibu Katibu Mkuu, Balozi Fatma Rajab katika picha ya pamoja na mabalozi wa Tanzania Nje ya nchi

Tuesday, November 15, 2022

AFRIKA IJIPANGE KUTUMIA FURSA ZAKE KUKIDHI MAHITAJI YA DUNIA


Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Mhe. Innocent Shiyo akiwasilisha mada kuhusu fursa za biashara na uwekezaji katika kanda ya Afrika katika mkutano wa mabalozi unaoendelea Zanzibar

 

Mkutano wa mabalozi ukiendelea Zanzibar




Monday, November 14, 2022

RAIS SAMIA KUKUTANA NA MABALOZI ZANZIBAR

 



Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akitoa hotuba kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika mkutano wa Mabalozi unaoendelea Zanzibar

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akiwasilisha hotuba yake kwa mabalozi (hawapo pichani). Mkutano huo umeanza leo Zanzzibar na utamalizika tarehe 21 Novemba, 2022. 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab akitoa tathmini ya mkutano wa mabalozi unaoendelea Zanzibar 

Sehemu ya mabalozi wakifuatilia kikao

Baadhi ya viongozi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, wakiongozwa na Naibu Waziri, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (wa kwanza kulia), Katibu Mkuu  Balozi Joseph Sokoine (katikati) na Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Amani, Balozi Stephen Mbundi wakifuatilia kikao

Thursday, November 10, 2022

MABALOZI WAFANYA ZIARA HOSPITALI YA CCBRT

Mabalozi wanaoziwakilisha nchi za Palestina, Indonesia na Vietnam hapa nchini wamefanya ziara katika Hospitali ya CCBRT na kujionea utoaji wa huduma za afya na kazi mbalimbali zinazofanywa na Hospitali hiyo pamoja na kuangalia maeneo ya ushirikiano.

Ziara ya mabalozi hao imefanyika leo Jijini Dar es Salaam ambapo mabalozi waliofanya ziara katika hospitaali hiyo ni Balozi wa Palestina nchini, Mhe. Hamdi Mansour AbuAli, Balozi wa Indonesia nchini, Mhe. Triyogo Jatmiko na Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Nguyen Nam Tien.

Akiongea wakati wa ziara hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa CCBT, Bi. Brenda Msangi amesema kuwa ziara ya mabalozi hao imelenga kujifunza na kujionea shughuli mbalimbali zinazotolewa na hospitali hiyo na kwamba CCBRT inaamini kuwa baada ya ziara hiyo mabalozi watapata fursa ya kujionea maeneo ya ushirikiano baina ya nchi zao hospitali hiyo.

“Tunategemea baada ya ziara hii mabalozi wataona maeneo ya ushirikiano, sisi kama CCBRT tuna maeneo matatu ambayo tunapenda kushirikiana nao, eneo la kwanza ni utoaji wa huduma, vifaa na vifaa tiba, na mwisho ni kuwajengea uwezo wataalamu wetu. Maeneo yote haya ni muhimu hasa ukizingatia CCBRT inatoa huduma bobezi na za kibingwa,” amesema Bi. Msangi

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Hemed Mgaza amesema kuwa mabalozi wamefanya ziara katika hospitali hiyo kwa lengo la kujionea utoaji wa huduma mbalimbali zinazotolewa na CCBRT na kupata fursa kuona maeneo ya ushirikiano baina ya nchi zao na CCBRT.

“Katika ziara ya mabalozi hapa CCBRT, mabalozi wameonesha kuridhishwa na shughuli zinazofanywa na hospitali hii, na baada ya ziara hii watawasiliana na nchi zao na kuona maeneo ya ushirikiano katika kuboresha zaidi sekta ya afya,” amesema Balozi Mgaza.  

Naye Balozi wa Palestina nchini, Mhe. Hamdi Mansour AbuAli amesema ameridhishwa na huduma zinazotolewa na CCBRT katika kuboresha afya za watanzania nchini na kuahidi kuwasiliana na serikali ya Palestina kuona ni jinsi gani serikali yake inaweza kushirikiana na hospitali hiyo katika kuboresha sekta ya afya nchini Tanzania. 

“Nimekuwa nikipita maeneo haya mara kwa mara lakini sikujua kuwa huduma nzuri zinatolewa hapa CCBRT, nawapongeza kwa jitihada hizi za kuuelimisha umma kuhusu magonjwa mbalimbali na njia za kuyakabili. Naahidi baada ya ziara hii nitawasiliana na Serikali yangu na kuona ni maeneo gani tunaweza kushirikiana katika kuboresha sekta ya afya,” amesema Balozi AbuAli

Kadhalika, Balozi wa Indonesia nchini, Mhe. Triyogo Jatmiko amesema kazi inayofanywa na hospitali ya CCBRT katika kuwahudumia watanzania hususan akina mama wenye changamoto ya fistula na watu wenye ulemavu wa viungo ni kazi kubwa na inayoigusa jamii.

“Jitihada zinazofanywa na serikali ya Tanzania katika kuboresha vituo vya afya ni nzuri……nimeguswa na jinsi hospitali hii inavyowahudumia wananchi, baada ya ziara hii tutakaa na kuangalia maeneo ya ushirikiano,” amesema Balozi Jatmiko.

Ziara hiyo iliratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki iliongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Balozi Hemed Mgaza pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Balozi Ceaser Waitara.

Afisa Mtendaji Mkuu wa CCBT, Bi. Brenda Msangi akizungumza na Balozi wa Palestina nchini, Mhe. Hamdi Mansour AbuAli, Balozi wa Indonesia nchini, Mhe. Triyogo Jatmiko na Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Nguyen Nam Tien. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Balozi Hemed Mgaza pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Balozi Ceaser Waitara pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa CCBRT. 

Mabalozi wakiwa katika kituo cha mabinti cha CCBRT wakati walipofanya zaira hospitalini hapo 

Mabalozi wakiwajulia hali akina mama wanaokabiliwa na changamoto ya Fistula katika hospitali ya CCBRT

Balozi wa Indonesia nchini, Mhe. Triyogo Jatmiko akisalimiana na mtoto anayetumia mguu wa bandia katika karakana ya viungo tiba saidizi na viungo bandia katika hospitali ya CCBRT wakati mabalozi walipofanya ziara hospitalini hapo. Wengine pichani ni Balozi wa Palestina nchini, Mhe. Hamdi Mansour AbuAli, Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Nguyen Nam Tien, Afisa Mtendaji Mkuu wa CCBT, Bi. Brenda Msangi, (Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Balozi Hemed Mgaza pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Balozi Ceaser Waitara) kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Balozi wa Palestina nchini, Mhe. Hamdi Mansour AbuAli akionesha mabalozi wenzake kitu wakati wa ziara ya mabalozi hao katika hospitali ya CCBRT 

Mabalozi wakiwa katika picha ya pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT Bi. Brenda Msangi pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali hiyo 



Tuesday, November 8, 2022

ZANZIBAR WAPIGWA MSASA KUHUSU UZALISHAJI WA MAZAO BORA YA BAHARI

Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Mhe. Suleiman Masoud Makame amesema uzalishaji wa matango bahari na uboreshwaji wa zao la mwani unamanufaa makubwa kwa Zanzibar na Nchi za pembezoni mwa ukanda wa Bahari ya Hidi.

Waziri Suleiman Masoud Makame, ameyasema hayo wakati akifungua semina ya siku 5 kuhusu namna bora ya uzalishaji wa vifaranga vya matango bahari na ukulima bora wa zao la mwani iliyofanyika katika Hoteli ya Verde mjini Zanzibar jana tarehe 07 Novemba 2022.

Mhe. Suleiman ameongeza kuwa kufanyika kwa Mkutano huo mjini hapo kutaleta mafanikio kwa kuwa wajumbe watapata nafasi ya kujadiliana juu ya namna bora ya kuzalisha mazao ya baharini ikiwemo vifaranga vya matango bahari.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Dkt. Aboud Suleiman Jumbe amesema mkutano huo wa watalamu kutoka katika nchi za IORA utafungua milango kwa watalamu na kuona namna gani Zanzibar ilivyojiandaa katika uchumi wa buluu na uvuvi.

"Nchi za ukanda wa pembezoni mwa bahari ya hindi watajifunza mambo mengi hapa Zanzubar kwa vile kuna wizara ya uchumi wa buluu na uvuvi" ameeleza

Nae Mkurugenzi wa Uchumi wa Buluu Bi. Rina Setyawati kutoka ukanda wa Bahari ya Hindi Nchi za IORA zimekuwa na usharikiano wa pamoja katika mambo mbalimbali ikiwemo katika suala zima la kujifunza ubora wa kuzalisha vifaranga vya matango bahari na kilimo bora chenye faida kwa Nchi wanachama.

Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kikanda wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mratibu wa Masuala ya Jumuiya ya Nchi za Mwambao mwa Bahari ya Hindi (IORA) Balozi Agnes Richard Kayola akizungumza katika Mkutano huo ameeleza kuwa IROA inaimani kuwa Mkutano huo utakuwa na tija kubwa kwa wanachama waliotoka nje ya Tanzania kwa vile watapata muda wa kubadilishana uzoefu jinsi ya kufanikiwa katika kilimo cha mwani kwa wananchi.

Aidha, katika kipindi cha siku 5 cha semina hiyo wakulima wa mazao mbalimbali ya bahari watapata fursa ya kuonesha bidhaa zao sambamba na utaalam wanaoutumia kuzalisha mazao hayo. Hatua hiyo itawapa wakulima hao nafasi ya kujifunza zaidi kuhusu uchumi wa buluu, sambamba na kujipatia fursa za makoso mapya ya mazao yao.

Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Mhe. Suleiman Masoud Makame akihutubia wakati wa ufunguzi wa semina ya siku 5 kuhusu namna bora ya uzalishaji wa vifaranga vya matango bahari na ukulima bora wa zao la mwani uliofanyika katika Hoteli ya Verde mjini Zanzibar 

Semina ya namna bora ya uzalishaji wa vifaranga vya matango bahari na ukulima bora wa zao la mwani uliofanyika katika Hoteli ya Verde mjini Zanzibar 
Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kikanda wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mratibu wa Masuala ya Jumuiya ya Nchi za Mwambao mwa Bahari ya Hindi (IORA) Balozi Agnes Richard Kayola akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya namna bora ya uzalishaji wa vifaranga vya matango bahari na ukulima bora wa zao la mwani uliofanyika katika Hoteli ya Verde mjini Zanzibar 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Dkt. Aboud Suleiman Jumbe akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa semina ya namna bora ya uzalishaji wa vifaranga vya matango bahari na ukulima bora wa zao la mwani uliofanyika katika Hoteli ya Verde mjini Zanzibar 
Picha ya pamoja

Saturday, November 5, 2022

WIZARA KUSHIRIKIANA NA VYUO VIKUU KUONGEZA WIGO WA ELIMU

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeahidi kuendelea kushirikiana na vyuo vikuu nchini ili kupanua wigo wa kutoa elimu kwa wanafunzi kuhusu fursa mbalimbali zinazotolewa na wahisani yakiwemo mashirika ya Kikanda, Kimataifa na nchi marafiki.

Ahadi hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga alipokutana na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Henry James na baadhi ya Viongozi wa Serikali za wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) jana katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Ubungo.

“Fursa za Masomo Nje ya Nchi na ajira zimekuwa zikitangazwa na kuratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje kwa kushirikiana na wadau wengine ili kuendelea kupanua wigo wa kutoa elimu kwa wanafunzi kuhusu fursa mbalimbali zinazotolewa na Wizara Kikanda na Kimataifa.,” Alisema Balozi Mindi

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Bw. Kheri James amepongeza jitihada zinazotekelezwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika kuhakikisha watanzania wanapata fursa mbalimbali za masomo na kazi Nje ya nchi kwani jambo hilo ni la kizalendo.

“Wizara ina fursa ya ziada ya kuviunganisha vyuo vikuu nchini na Vyuo Vikuu Nje ya nchi kwa ufadhili wa masomo, mahusiano kati ya vyuo vya Tanzania na vya Nje na kubadilishana wanafunzi katika taaluma mbalimbali ili kuwajengea uwezo na ufanisi katika masomo,”Alisema Bw. James.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Rais wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bw. Spencer Minja na Rais wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji Bw. Mark Makaranga ambapo pamoja na mambo mengine wanafunzi hao wameipongeza na kuiomba Wizara kuandaa Kongamano la wanafunzi wa Elimu ya Juu kuhusu Mtangamano wa Jumuiya ya Kikanda na Kimataifa. 

Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo ina vyuo vitano ambavyo ni, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Shule Kuu ya Sheria, Chuo cha Maji na Chuo cha Mtakatifu Joseph.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga akieleza jambo wakati wa kikao na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Henry James na baadhi ya Viongozi wa Serikali za wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) jana katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Ubungo

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Henry James akimsikiliza Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga wakati wa kikao na baadhi ya Viongozi wa Serikali za wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) jana katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Ubungo

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga akifafanua jambo wakati wa kikao na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Henry James na baadhi ya Viongozi wa Serikali za wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) jana katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Ubungo

Rais wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji Bw. Mark Makaranga akieleza jambo wakati wa kikao

Kikao kikiendelea 

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Henry James katika pichaa ya pamoja na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga, Rais wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (kulia), Bw. Spencer Minja na Rais wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji Bw. Mark Makaranga (kushoto)