Friday, June 23, 2023

DR. TAX AFANYA ZIARA CHUO CHA DIPLOMASIA INDONESIA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) akiwa anaendelea na ziara yake nchini Indonesia, ametembelea Chuo Cha Diplomasia cha Indonesia.

Waziri Tax pamoja na ujumbe wake, walipokelewa chuoni hapo na Mkuu wa Chuo hicho, Bw. Mohammad Koba.

Kufuatia ziara hiyo, Tanzania na Indonesia zimekubaliana kuanzisha ushirikiano baina ya Vyuo vya Kidiplomasia, ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu katika maeneo mbalimbali ikiwemo uendeshaji wa chuo na Program za mafunzo kwa Wanadiplomasia, na kubadilishama ujuzi kwa walimu na wanafunzi wa vyuo hivyo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) akisalimiana na viongozi wa Chuo Cha Diplomasia cha Indonesia baada ya kuwasili chuoni hapo kwa ziara


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) akizungumza na uongozi wa Chuo Cha Diplomasia cha Indonesia 
Mkuu wa Chuo cha Diplomasi cha Indonesia, Bw. Mohammad Koba akielezea historia ya chuo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (hayupo pichani)

Mkuu wa Chuo cha Diplomasi cha Indonesia, Bw. Mohammad Koba akimkabidhi zawadi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika picha ya pamoja na ujumbe wake pamoja na Mkuu wa Chuo cha Diplomasia Indonesia Bw. Mohammad Koba pamoja na Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Mhe. Tri Yogo Jatmiko 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akimsikiliza moja kati ya wakufunzi kutoka Chuo cha Diplomasia Indonesia Bibi. Renata Siagian






Thursday, June 22, 2023

TANZANIA YAFUNGUA RASMI UBALOZI WAKE NCHINI INDONESIA

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefungua rasmi Ubalozi wake Jijini Jakarta nchini Indonesia.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Ubalozi huo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amesema kufunguliwa kwa Ubalozi huo kutaziwezesha Serikali ya Tanzania na Serikali ya Indonesia kukuza na kuimarisha uhusiano wake wa kidiplomasia na kukuza uchumi.

“Tanzania imekuwa ikishirikiana kwa karibu na Indonesia hivyo tunaamini kuwa kufunguliwa rasmi kwa ubalozi wetu Jijini hapa kutaongeza ushirikiano zaidi baina ya mataifa yetu mawili hususan katika sekta ya uchumi,” alisema Dkt. Tax

Waziri Tax ameongeza kuwa Indonesia imefika mbali kiuchumi, hivyo ushirikiano wake na Tanzania utatoa fursa kwa Tanzania kupiga hatua na kuhakikisha bidhaa za mazao ya kilimo na madini zinaongezwa thamani na kuuzwa katika masoko mbalimbali ya kimataifa na kuiwezesha Tanzania kukuza uchumi wake.

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Tax ameishukuru Serikali ya Indonesia kwa ushirikiano mkubwa ambao imekua ikiupatia Ubalozi wa Tanzania, Jakarta tangu ubalozi huo ulipoanzishwa nchini humo mwaka 2022 hadi ulipozinduliwa rasmi leo tarehe 22 Juni, 2023.

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia Mhe.  Retno Marsudi amesema, Indonesia na Tanzania zimekuwa na ushirikiano mzuri wa muda mrefu na imara ulioanzishwa na waasisi wa mataifa hayo mawili (Mwl. Julius Nyerere na Rais Sukarno) tangu mkutano wa Bandung uliofanyika mwaka 1955.

Waziri Marsudi alisema kuwa muda wote huo, Serikali hizo mbili zimekuwa zikifanya kazi kwa pamoja na kwa karibu katika maeneno mbalimbali….“Leo najisikia faraja sana kwa Tanzania kufungua rasmi ubalozi wake hapa Jakarta. Hii ni ishara ya kuimarisha zaidi ushirikiano baina ya Indeonesia na Tanzania,” amesema Mhe. Marsudi.

Alisema kufunguliwa kwa ubalozi huo kunaonesha kuimarishwa zaidi kwa uhusiano wa kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na Indonesia na kuahidi kuwa yeye na timu yake wataendelea kushirikiana na Tanzania kukuza na kuimarisha uhusiano uliopo kati ya nchi hizo.

“Kufunguliwa rasmi kwa ubalozi huu leo ni ishara ya kuimarisha zaidi uhusiano wetu wa kidiplomasia kati ya Indonesia na Tanzania, mimi pamoja na timu yangu tunaahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kukuza na kuimarisha uhusiano wetu,” ameongeza Mhe. Marsudi.

Hafla ya uzinduzi wa Ubalozi huo imehudhuriwa na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa waliopo Jakarta, Indonesia.

Tanzania na Indonesia zilianzisha rasmi uhusiano wa kidiplomasia mwaka 1964, ambapo mwaka huo Ubalozi wa Indonesia ulifunguliwa rasmi nchini Tanzania. Aidha, kabla ya kufunguliwa kwa ubalozi wa Tanzania nchini Indonesia, Tanzania imekuwa ikiwakilishwa kutoka ubalozi wa Tanzania uliopo Kuala Lumpur, Malaysia.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akihutubia katika hafla ya ufunguzi rasmi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Jakarta nchini Indonesia

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akihutubia katika hafla ya ufunguzi rasmi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Jakarta nchini Indonesia

Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia Mhe.  Retno Marsudi akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi rasmi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – Jakarta nchini Indonesia

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax na mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia Mhe.  Retno Marsudi wakifungua rasmi Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – Jakarta nchini Indonesia

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax pamoja na mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia, Mhe.  Retno Marsudi wakifurahia baada ya kufungua rasmi Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – Jakarta nchini Indonesia

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax pamoja na mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia, Mhe.  Retno Marsudi wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – Jakarta nchini Indonesia

Balozi wa Tanzania nchini Indonesia, Mhe. Macocha Tembele akitoa salamu za ubalozi wakati wa hafla ya ufunguzi rasmi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – Jakarta nchini Indonesia

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax pamoja na mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia, Mhe.  Retno Marsudi wakigonga glasi kuashiria ufunguzi rasmi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – Jakarta nchini Indonesia


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax pamoja na mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia Mhe.  Retno Marsudi wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali kutoka Tanzania na Indonesia 




Wednesday, June 21, 2023

TANZANIA KUFUNGUA RASMI UBALOZI INDONESIA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amewasili Jakarta nchini Indonesia kwa ajili ya ziara ya kikazi, ikiwa ni pamoja na kufungua rasmi Ofisi za Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini humo hapo Tarehe 22 Juni, 2023.

Mhe. Dkt. Tax baada ya kuwasili Jakarta amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Indonesia, Mhe. Macocha Tembele katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Soekarno-Hatta (CGK).

Akiwa nchini Indonesia Mhe. Dkt. Tax anatarajia pia kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia, Mhe. Retno Marsudi, na kutembelea Chuo cha Diplomasia cha Indonesia.







Monday, June 19, 2023

WAZIRI TAX AWAAGA MABALOZI WA EU, UJERUMANI NA NORWAY

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amekutana na kuwaaga mabalozi watatu waliokuwa wanaziwakilisha nchi zao hapa nchini baada ya kumaliza muda wao wa uwakilishi.

Dkt. Tax amewaaga mabalozi hao katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. Mabalozi walioagwa ni Balozi wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya nchini, Mhe. Manfredo Fanti, Balozi wa Ujerumani nchini Mhe. Regine Hess pamoja na Balozi wa Norway Nchini Mhe.  Elisabeth Jacobsen.

Awali Mhe. Tax alimpongeza Balozi wa Umoja wa Ulaya Nchini, Mhe. Fanti kwa ushirikiano alioutoa kwa Serikali ya Tanzania wakati wa uwakilishi wake na kumuahidi kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Umoja wa Ulaya wakati wote hususani katika sekta ya biashara na uwekezaji.

“Nakupongeza kwa kazi nzuri na kubwa uliyoifanya wakati wa uwakilishi wako hapa nchini, ambapo umefanikiwa kuimarisha uhusiano mzuri baina ya Tanzania na Umoja wa Ulaya katika sekta ya siasa pamoja na uchumi. Kupitia muda wako wa uwakilishi, wote tumeshuhudia mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya yakiimarika. 

Pia tumekuwa na makongamano kadhaa ya biashara yaliyowakutanisha wafanyabishara wa mataifa yetu na kujadili fursa za biashara baina ya mataifa yetu,” alisema Dkt. Tax

Naye Balozi Fanti ameishukuru Tanzania kwa ushirikiano iliompatia wakati wote wa uwakilishi na kuahidi kuwa ataendelea kuwa Balozi bora wa Tanzania.

Kadhalika, Dkt. Tax amemuaga Balozi wa Ujerumani nchini hapa nchini Mhe. Regine Hess. Waziri Tax alimshukuru kwa ushirikiano aliouonesha kwa Serikali ya Tanzania wakati wa uwakilishi wake hapa nchini.

“Tanzania tunakushukuru kwa ushirikiano wako wakati wote wa uwakilishi wako hapa nchini, ushirikiano wetu (Tanzania na Ujerumani) umekuwa imara na bora wakati wote na tunaamini utaendelea kuimarika,” alisema Dkt. Tax

Naye Balozi Hess alisema kuwa anaondoka akiwa na faraja ya kuona masuala ya utawala bora, haki za binadamu pamoja na amani na usalama yakiwa yameboreshwa kwa kiasi kikubwa. 

Katika tukio jingine, Dkt. Tax amekutana na kumuaga Balozi wa Norway nchini, Mhe. Elisabeth Jacobsen ambapo ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kumpa ushirikiano wakati wa kipindi chake cha uwakilishi hapa nchini.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Balozi wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya nchini, Mhe. Manfredo Fanti baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi nchini. Dkt. Tax amemuaga Balozi Fanti katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akimkabidhi zawadi ya picha na Balozi wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya nchini, Mhe. Manfredo Fanti baada ya kumaliza muda wao wa uwakilishi nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akimsikiliza Balozi wa Ujerumani nchini Mhe. Regine Hess baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi nchini. Dkt. Tax amemuaga Balozi Hess katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akiagana akizungumza na Balozi wa Norway Nchini Mhe.  Elisabeth Jacobsen katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. Balozi Elisabeth amemaliza muda wake wa uwakilishi nchini.  

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika picha ya pamoja na Balozi wa Norway Nchini Mhe.  Elisabeth Jacobsen katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Idaya ya Ulaya na Amerika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Swahiba Mndeme (mwenye koti jeupe) pamoja na maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Ubalozi wa Norway.  





Saturday, June 17, 2023

WATUMISHI WA MAMBO YA NJE WAFANYA USAFI HOSPITALI YA MKOA WA DODOMA KUADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki itaendelea kuratibu upatikanaji wa madaktari bingwa, vifaa tiba na misaada mingine kutoka kwa wahisani kwa ajili ya kuboresha sekta ya Afya nchini.

 

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 17 Juni 2023 na Mkurugenzi wa Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen P. Mbundi wakati wa zoezi la watumishi wa Wizara hiyo kufanya usafi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya sherehe za kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma.

 

Balozi Mbundi ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu, Balozi Samwel Shelukindo, alisema kuwa Wizara kwa nafasi yake inaendelea na mkakati wa kutangaza utalii tiba hasa kwa nchi jirani, na mafanikio yamenza kuonekana kutokana na sekta ya afya nchini kuimarika na kuwa na uwezo wa kutoa huduma za kibingwa kwa gharama nafuu ukilinganisha na maeneo mengine duniani.

 

Aliendelea kueleza kuwa watumishi wa Wizara ni sehemu ya jamii ya Watanzania na uamuzi wa kufanya usafi katika hospitali hiyo ni moja ya jukumu lao la kuhudumia jamii, kwa sababu usafi ni tiba ya magojwa.

 

Kwa upande wake, Daktari Bingwa wa Magonjwa Hatarishi, Dkt. Paul Julius Mageni ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo ameishukuru Wizara kwa uamuzi wake huo wa kizalendo. Alisema kitendo kilichofanywa na watumishi wa Wizara ni ibada kubwa na kina lenga kuzuia maambukizi ya magonjwa. “Njia nzuri na rahisi ya kutibu ugonjwa ni kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo na usafi ni moja ya njia za kuzuia magonjwa kusambaa”, Dkt. Mageni alisema.

 

Wizara inaendelea kuadimisha Wiki ya Utumishi wa Umma kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujadili na kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazowakabili watumishi ili kuchagiza ari na motisha kwa watumishi kufanya kazi kwa juhudi na maarifa.

Mkurugenzi wa Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen P. Mbundi (mwenye barakoa) akishiriki zoezi la kufanya usafi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya sherehe za kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma. Balozi Mbundi  alimwakilisha Katibu Mkuu, Balozi Samwel Shelukindo. Mwenye miwani ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt. Paul Mageni. Zoezi hilo limefanyika kwenye Hospitali hiyo tarehe 17 Juni 2023. Kaulimbiu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi mwaka huu ni "Kufanikiwa kwa Eneo Huru la Biashara Barani Afrika kunahitaji usimamizi wa Utumishi wa Umma wenye Mtazamo wa Kikanda".

Balozi Mbundi akiwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Salifius Mligo (kushoto) wakiendelea na zoezi la usafi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma.
Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bw. Kawina Kawina naye akiendelea na zoezi la usafi
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi, Bw. Magabilo Murobi (kushoto) akiwa na Afisa Usafirishaji  wa Wizara Bw. Maulid Mkenda wakishiriki zoezi la usafi
Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji,  Bw. Athuman Nkungu akiendelea na zoezi la usafi 
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiendelea na zoezi la usafi
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiendelea na zoezi la usafi kwa kuchoma takataka
Zoezi la usafi likiendelea
Watumishi wa Wizara wakijituma katika zoezi la usafi
Zoezi la usafi likiendelea 
Zoezi la usafi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma likiendelea
Zoezi la usafi likiendelea
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje wakiendelea na zoezi la usafi
Zoezi la Usafi likiendelea
Zoezi la usafi likiendelea
Zoezi la usafi likiendelea
Usafi ukiendelea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma
Zoezi la usafi likiendelea
Watumishi wa Wizara wakishiriki zoezi la usafi
Usafi ukiendelea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masahariki wakiwa katika eneo la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kwa zoezi la usafi

Balozi Mbundi (kushoto) akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu mara baada ya Wizara kukamilisha zoezi la usafi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma Bw. Mageni akitoa neno la shukrani kwa Wizara kwa kutembelea Hospitali hiyo
Picha ya pamoja

....Ushiriki wa Wiki ya Utumishi katika Ofisi Ndogo za Wizara-Dar es Salaam

Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambao wapo katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam nao wakishiriki zoezi la usafi katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma. Zoezi hilo limefanyika tarehe 17 Juni 2023

Sehemu nyingine ya Watumishi wa Wizara waliopo Dar es Salaam wakiendelea na zoezi la usafi katika Taasisi ya Sratani ya Ocean Road kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma

........Ushiriki wa Wiki ya Utumishi wa Umma katika Ofisi ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Zanzibar 

Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambao wapo katika Ofisi ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Zanzibar wakishiriki zoezi la usafi katika Hospitali ya Rahaleo kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma. Zoezi hilo limefanyika tarehe 17 Juni 2023
Usafi ukiendelea katika Hospitali ya Rahaleo Zanzibar kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma