Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) akiwa anaendelea na ziara yake nchini Indonesia, ametembelea Chuo Cha Diplomasia cha Indonesia.
Waziri Tax pamoja na ujumbe wake, walipokelewa chuoni hapo na Mkuu wa Chuo hicho, Bw. Mohammad Koba.
Kufuatia ziara hiyo, Tanzania na Indonesia zimekubaliana kuanzisha ushirikiano baina ya Vyuo vya Kidiplomasia, ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu katika maeneo mbalimbali ikiwemo uendeshaji wa chuo na Program za mafunzo kwa Wanadiplomasia, na kubadilishama ujuzi kwa walimu na wanafunzi wa vyuo hivyo.
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) akisalimiana na viongozi wa Chuo Cha Diplomasia cha Indonesia baada ya kuwasili chuoni hapo kwa ziara |
|
|
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) akizungumza na uongozi wa Chuo Cha Diplomasia cha Indonesia |
|
Mkuu wa Chuo cha Diplomasi cha Indonesia, Bw. Mohammad Koba akielezea historia ya chuo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (hayupo pichani) |
|
Mkuu wa Chuo cha Diplomasi cha Indonesia, Bw. Mohammad Koba akimkabidhi zawadi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax |
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika picha ya pamoja na ujumbe wake pamoja na Mkuu wa Chuo cha Diplomasia Indonesia Bw. Mohammad Koba pamoja na Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Mhe. Tri Yogo Jatmiko |
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akimsikiliza moja kati ya wakufunzi kutoka Chuo cha Diplomasia Indonesia Bibi. Renata Siagian |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.