Saturday, June 10, 2023

WAZIRI TAX AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI WA FAO JIJINI ROMA, ITALIA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula Duniani (FAO) Dkt. Qu Dongyu walipokutana kwa mazungumzo jijini Roma, Italia

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax amekutana na kufanya mazungumzo na  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula Duniani  (FAO) Dkt. Qu Dongyu. Katika mazungumzo yao Dkt. Tax amepongeza FAO kwa jitihada zake za kutafuta na kukusanya rasilimali kwa ajili ya jamii mbalimbali ili ziweze kunufaika na  maendeleo ya kilimo ambazo amesema Watanzania wengi pia wanazitegemea.

Dkt. Tax yuko nchini Italia kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine anatarajiwa kuzungumza na jumuiya ya wafanyabiashara wa nchini Italia.

Mkutano ukiendelea
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula Duniani (FAO) Dkt. Qu Dongyu wakiwa katika mazungumzo yaliyofanyika makao makuu ya FAO jijini Roma, Italy
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula Duniani (FAO) Dkt. Qu Dongyu katika picha ya pamoja
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula Duniani (FAO) Dkt. Qu Dongyu wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa FAO, Ubalozi wa Tanzania nchini Italia na wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.