Baadhi ya washiriki wa mkutano kati ya jumuiya ya wafanyabiashara wa Italia wakifuatilia mkutano huo uliofanyika jijini Roma nchini Italia tarehe 10 Juni,2023 |
Baadhi ya washiriki wa mkutano kati ya jumuiya ya wafanyabiashara wa Italia wakifuatilia mkutano huo uliofanyika jijini Roma nchini Italia tarehe 10 Juni,2023 |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) amekutana na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Italia jijini Roma na kuwaita waje kuwekeza nchini kwa kuwa Serikali ya Tanzania ina dhamira ya dhati kushirikiana nao kukuza uchumi kupitia biashara na uwekezaji .
Amesema ushirikiano huo imara utawezesha pande zote mbili kupata nafasi ya kufahamu fursa mbalimbali zinazopatikana katika nchi hizo, kunufaika nazo na kufanya kazi pamoja.
“Mmesikia mengi yakisemwa hapa, nichukue nafasi hii kuwahakikishia dhamira ya Serikali ya Tanzania ya kutaka kushirikiana na jumuiya yenu katika biashara na uwekezaji, naona kwamba tukishirikiana kwa pamoja tutafahmu fursa zinazopatikana katika nchi zetu na kujua jinsi ya kunufaika nazo, na hivyo kufanya kazi kwa pamoja” alisema.
Alisema mikutano miwili ya jukwaa la biashara iliiyofanyika awali ilikuwa nyenzo za kupatiana taarifa kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kibiashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Italiana kuongeza kuwa jukwaa la tatu litakalofanyika mwezi Julai 2023 litakuwa na manufaa zaidi kwa pande zote mbili.
Amesema Italia imekuwa ni mdau mkubwa wa Tanzania na moja ya nchi zenye biashara na uwekezaji mkubwa nchini na kuipatia misaada ya kimaendeleo japo biashara kati ya nchi hizo imekuwa ikielemea upande mmoja akitolea mfano katika kipindi cha miaka mitano ya 2018 – 2022 na kuongeza ni matumaini yake kuwa mkutano huo utakuwa chachu ya kuweka sawa uwiano huo wa biashara .
Akizungumza katika mkutano huo, hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii nchini Bw. Damas Mfugale alisema Tanzania ina vivutio vingi na vizuri na kuwakaribisha wafanyabiashara ho kuja nchini kuwekeza katika tasnia ya Utalii.
Naye Mkurugenzi wa Mkuu wa Kituo cha uwekezaji nchini Dkt. Gelead Teri alisema Tanzania imeboresha mazingira ya kufanya biashara nchini na kuzingatia garantii inayowekwa ya kupata faida na kurejesha gharama za mtaji pamoja na soko kubwa linaloizunguka nchi la Afrika Mashariki, SADC na sasa AfCFTA.
Alisema hali ya amani na usalama , eneo nchi ilipo, utajiri wa maliasilia ni miongoni mwa sababu kubwa za kuvutia wawekezaji nchini. Amewaita wafanyabiashara hao waje nchini na kwamba hawatajuta kufanya hivyo.
Naye Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) Bw. Khamis Dunia amewakaribisha wafanyabiashara hao kuja Zanzibar kwa kuzingatia uwepo wa miundombinu ya ICT na ujenzi wa bandari kubwa ya Mangapwani. Amewaambia wafanyabiashara hao waje Zanzibar ili wanufaike na kusaidiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika ujenzi wa bandari hiyo
Mkutano huo na jumuiya ya wafanyabiashara Italia uliofanyika jijini Roma uliandaliwa na Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahmoud Thabit Kombo.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.