Tuesday, June 13, 2023

KONSELI KUU YA LUBUMBASHI YAKUTANA NA MADEREVA

Kaimu Konseli Mkuu katika Konseli Kuu ya Tanzania, Lubumbashi, Bi. Asha Mlekwa akiwa na ujumbe wa wataalam kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama wa Jimbo la Haut-Katanga, Mhe. Erick Muta Ndala walifanya ziara ya kutembelea madereva wa malori ya Tanzania  yanayofanya safari kati ya Tanzania na DRC upande wa Jimbo la Haut-Katanga na Jimbo la Lualaba. Ujumbe huo uliofika maeneo hayo tarehe 12 Juni 2023 ulisikiliza changamoto za kiusalama zinazowakabili madereva wa malori wanaosafirisha mizigo kati ya DRC na Tanzania inayopita katika Bandari ya Dar es Salaam. Mhe. Ndala aliahidi kuendelea kuboresha hali ya usalama wa madereva na mizigo akitoa mfano wa mafanikio yaliyofikiwa katika kupunguza vitendo vya utekaji wa malori yanayobeba madini ya shaba.

Madereva wa Malori wakielezea changamoto wanazokutana nazo na kupewa majibu kutoka kwa Wahusika.
Kaimu Konseli Mkuu katika Konseli Kuu ya Tanzania, Lubumbashi, Bi. Asha Mlekwa  na Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama wa Jimbo la Haut-Katanga, Mhe. Erick Muta Ndala na ujumbe wa wataalam kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wakiwasili eneo la kuegesha malori kwa ajili ya kujadili  utatuzi wa changamoto wanazokabiliana nazo madereva wa Tanzania wanaofanya safari kati ya Tanzania na DRC.




No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.