Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amekutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja
wa Mataifa linalojishughulisha na udhibiti wa biashara haramu ya dawa za kulevya na Uhalifu uliopangwa (UNODC) Mhe. Ghada Fathi Waly jijini Vienna.
Mhe. Dkt. Tax ameelezea kuridhishwa kwake na kupongeza kazi zinazofanywa na Shirika hilo kufuatia jitihada zao za kukabiliana na biashara haramu ya dawa za kulevya , ufisadi na uhalifu wa kupangwa.
Amesema Umoja wa Mataifa na UNODC wanatekeleza jukumu muhimu katika kukabiliana na biashara haramu ya dawa, ambayo inatishia amani, usalama na afya ya watu duniani.
Amesema kupitia mikakati yao kamili, mipango, na ushirikiano, wamekuwa muhimu katika kuongeza uelewa, kutoa msaada wa kiufundi na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa ili kukabiliana na masuala yanayohusiana na dawa kwa ufanisi.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.