Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax amekutana na kuzungumza na Waziri anayeshughulikia masuala ya Ulaya na Uhusiano wa Kimataifa wa Austria Mhe. Alexander Schallenberg ofisini kwake jijini Vienna, Austria
Viongozi hao wamena kujadili masuala mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Austria.
Dkt. Tax alielezea kufurahishwa kwake na jinsi uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Austria ulivyo imara na hatua za kuhakikisha unaendelea kuimarika zinachukuliwa na pande zote mbili.
Waziri Dkt. Tax ameishukuru Serikali ya Austria hasa Wizara inayoshughulikia masuala ya Ulaya na uhusiano wa Kimataifa kwa ushirikiano mkubwa ambao imekua ikiupatia Ubalozi wa Tanzania Vienna tangu ulipoanzishwa mwaka 2021 na kuahidi kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Austria kama mdau wake mkubwa wa maendeleo.
Naye Waziri anayeshughulikia masuala ya Ulaya na Uhusiano wa Kimataifa wa Austria Mhe. Alexander Schallenberg alisema Austria inaupongeza uamuzi wa Serikali ya Tanzania wa kufungua Ubalozi wake nchini humo na hivyo kuwa na uwakilishi kamili.
Alisema Austria itaendelea kushirikiana na Tanzania katika maeneo mbalimbali ya ushirikiano kama vile elimu, afya, miundombinu na kubadilishana watalaamu ili kuwezesha nchi zote mbili kunufaika na uhusiano huo.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.